Mimi naitwa Tenisha-(si jina langu halisi) nimekuwa nafuatilia blog yako kwa muda mrefu na nimeona jinsi unavyosaidia watu kwa ushauri wako ,na mimi pia nikaona niseme yaliyoko moyoni kwangu.
Kwa kuanzia mimi nina miaka 25, niliolewa miaka miaka 4 iliyopita na sina mtoto (bado tulikuwa hatujapanga kufanya hivyo kwa wakati huo),ndoa yenye furaha na amani tele, mpaka mwaka 2008 mwezi April mambo yalipobadilika.
Mume wangu alipata ugonjwa kama unaofanana kabisa na Herpeszoster japo Doctor alisema huo ni mbaya zaidi , mimi nilikuwepo na nilimuuguza mpaka alipopona. Baada ya hapo Doctor alisema ingekuwa vizuri kama tungepima HIV, lakini kabla ya ndoa tulikuwa tumepima na wote tulikuwa negative.Lakini mimi nilikuwa na utaratibu wangu wa kupima mara kwa mara ninapopata nafasi ya kufanya hivyo.
Majibu yalipotoka yalikuwa ya kusikitisha, mimi nilikuwa na negative na mume wangu mpendwa alikuwa positive, nilillia sana sana (namaanisha hivyo ) lakini pia sikuweza kubadilisha ukweli.
Ikabaki hivyo tukaenda tena kupima Angaza na hospital tofauti majibu yakabaki hivyo kuwa mimi ni negative na mume wangu ni positive . Tokea hapo mpaka leo nimeshapima sehemu nyingi tofauti na majibu ni hayajabadilika.
Mume wangu namjua tokea tuko wachumba tabia yake naijua sio mtu wa kuhangaika na wanawake, nimekuwa namfuatilia sana nikawa najichosha mwenyewe (lakini ukweli zaidi anao mwenyewe kama ana nyumba ndogo mimi sijui).
Alikoupata sijui hata yeye mwenyewe alikiri hafahamu, ikabidi tukubaliane na ukweli, Sikutaka kumuuuliza sana kama alikuwa na mwanamke mwingine au la ! kwa sababu pia sikutaka akose amani na hali aliyonayo.
Basi ikabadi aanze dawa za kurefusha maisha (sio ARV)ambazo tulipewa na Doctor wetu. Wakati amepata huo ugonjwa tayari CD4 zilikuwa 200. Tuliongea na Doctor sana kuhusu maisha yetu na tulipenda sana kuwa na mtoto mwaka huu 2009, japo haiwezekani, njia aliyotuambia ni fertilization (nadhani wengine wanaijua)ambayo pia sio 100% .
Niliongea nae sana kuhusu mtoto yeye akasema alivyofikiria yeye nizae na kaka yake damu isiende mbali ,nilikataa hapo hapo nikamuambia sitaweza (never happen). Pia tulishauriwa asifanye mapenzi sana kwa mwezi kama mara 2 hivi au 3 asizidishe kwa ajili ya kulinda afya yake na huwa tunatumia condom na tuko makini sana kwa hilo.
Jamani kama nilivyosema hapo juu nina miaka 25, ninapata majaribu sana (kwa muonekano naonekana kama mdogo zaidi ya hiyo miaka na ni mzuri hilo nalifahamu hata mimi mwenyewe-hehe he hehe .) Kufanya mapenzi mara 3 kwa mwezi hakunitoshelezi pia nilizoea sana kufanya romace na deep kiss ila sasa hatuwezi kufanya hivyo ili kunilinda mimi asiniambukize.
Nampenda kumuacha naona siwezi, pia naona anahitaji mtu wa kumfariji kwa sababu bado anaona kama ni ndoto kwake. Na hatujawahi kumuambia mtu yoyote zaidi ya madoctor wanaotupima.
Naomba ushauri .
1.Nitafanyaje kuhusu mtoto , namhitaji sana mpaka huwa nakosa usingizi nikifikiria juu ya kupata mtoto wa njia ambayo hata mume wangu ataridhika na yeye na huyo mtoto (hataki nizae na mtu mwingine )
Jawabu: Hili linawezekana kabisa ila itabidi mchukue tahadhali sana na ni "risk" kwa mtoto. Kama mnaishi nchi zilizoendelea Mf-UK au US mnaweza kuliweka wazi hili suala la kuwa na mtoto huku mmoja wenua na VVU na wao watawaweka kwenye uangalifu mkubwa na kukukufanyia wewe mama (ukishika mimba) vipimo vya mara kwa mara ili kuhakikisha mtoto anakua vema tumboni bila hatari yakupata VVU, Mara nyingi mwanamke hupewa "course" ya madawa fulani kabla hamjanzakujaribu ili "kumimbana".
Kwa "case" yako ni rahasi zaidi kwa vile wewe huna VVU (japokuwa utakwenda through vipimo vingi na vya mara kwa mara kuhakikisha hilo, kuwa kweli huna kabisa-kabisa VVU), mwanamke akiwa hana VVU anaweza kuzaa mtoto ambae hana VVU tena bila kutumia madawa yeyote ya kumzuia mtoto kulikwaa gonjwa hilo kwa vile inasemekana kuwa mbegu za kiume hazibebi vijidudu vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuliko mwanamke mwenye VVU.....tafadhali bonyeza link hapo pembeni kulia mwa blog hii kwenye maandishi yakijanani chini ya Profile yangu kuna maelezo ya kutosha kutoka kwa madaktari na pia unapata nasafi yakuwauliza maswali moja kwa moja, tafadhali jiweke karibu nao kwa ushauri zaidi wa kitibabu.
Kitu kingine unapaswa kufahami ni kuwa HIV Virus ziko za aina 3 tofauti. Aina mbili ambazo ni hatari zadi zinanawiri nchi za joto hasa Afrika na aina ya nyingine inastawi zaidi nchi za Baridi. Inasemekana kuwa ukiwa na VVU aina ya tatu na unaishi nchi za joto kuonekana sio rahisi ukilinganisha na zile mbili za "kiafrika".
Ndio maana nikasema kabla ya kuambiewa wendelea na suala la kumimbwa huwa wanakupa vipimo vingine lukuki ili kuwa na uhakika....tafadhali soma Tovuti nyingine inayojihusisha na kuzuia VVU kwa watoto....bonyeza hapo kulia kwenye Logo ya mtoto kwa maelezo zaidi ya kitaalamu.
2.Mimi jamani bado mdogo nina mihemuko ya ujana nahitaji kufanya mapenzi nifurahie pia sitaki kutoka nje ya ndoa.
Jawabu:Kutokana nakilichotokea kwenye ndoa yako na kama ulivyodai kuwa unampenda mume wako na nyote mnaonekana ni waelevu basi sio mbaya kama utashauriana na mume wako na kukubaliana kuwa wewe uwe ukitumia "sanamu" kujiridhsiha pale unapohitaji zaidi. Matumizi ya sanamu za ngono sio kitu ambacho mimi binafsi huwa nashauri wapenzi kutumia kwavile naamini katika uumbaji wake Mungu, lakini kama "issue" ndio hii ya VVU ninafuraha kabisa kusema....tafadhali kanunueni sanamu ili wewe uweze kukabiliana na mihamko yako.
Utakachotakiwa kufanya hapa ni kuwa "mbinafsi" kidogo ili kuzuia kumtamanisha mumeo ambae kutoka na ushauri wa Daktari hapaswi kufanya ngono mara nyingi kama ilivyokuwa hapo awali kabla hajajua kuwa anaishi na VVU.*****
Nitashukuru wa ushauri /maoni kutoka kwako Dinah na wengineo. Nimejieleza kwa kifupi ila nina imani nitakuwa nimeeleweka na nitapata ushauri mzuri.
Tenisha"
Jawabu:Tenisha, asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mahali hapa, shukurani kwa mail yako na kwa uwazi wako.
Pamoja na kuwa nimekujibu moja kwa moja ningependa nitoe maelezo kwa ujumla ili kuweka sawa au kujazilizia mengi na mazuri yaliyosemwa na wachangiaji. Inasikitisha wengi wamekushauri uachane na mumeo (kitu ambacho mwanaume actually angekifanya kama wewe ungekuwa na VVU).
Kuna wachangiaji wamgehusia suala la "rushwa", ni kweli kabisa watu wengi wanatoa "kitu kidogo" kwa madaktari ili wapatie majibu ya uongo (hawana HIV) lakini ktk hali halisi wanakuwa navyo na wanajua kuwa alikwisha vikwaa miaka ya nyuma, lakini kwa vile CD4 ziko juu, wanaendelea na maisha kama kawaida na zitakapo pungua na kudaka maambukizo wakati tayari yuko kwenye ndoa unaweza kusukumiwa wewe lawama kuwa ulikuwa "kicheche" ndani ya ndoa.
Kama ulivyosema ulijitahidi kumchunguza na kuhakikisha kuwa hana tabia ya "kuchomoka" nje ya ndoa yenu, inawezekana ni kweli kabisa hajaupata baada ya kutoka nje ya ndoa, kuna uwezekano mkubwa aliupata kabla ya ndoa na akafanya "makaratee" na Dk ili kupata majibu kama yako.
Kuna njia nyingine za mtu kupata VVU ambavyo sio lazima iwe Ngono (inategemea na shughuli zake) kama Nesi au Daktari anaefanya kazi na waathirika wa VVU. Vilevile kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuishi na watu wenye VVU ambao tayari wanaugua....kutokana na utu au ukaribu wa wahusika au ukosefu wa vifaa hapo nyumbani mtu anaweza kujisikia vibaya kuosha kidonda/kinywa kwa kuvaa mpira na badala yake akatumia mikono mitupu ambayo huenda ilikuwa na mkato/mchubuko ndani ya ukucha n.k.
Pia wapo watu ambao wanaambukiza wenzao kwa makusudi kwa kujichoma sindano kisha kuwachoma wenzao na sindano za kushonea, pini, kitu chochote chenye ncha kali au hata kuweka vifaa vya kunyolea walivyovitumia karibu au hata kuvibadilisha(kuonda visafi na kuweka vyao walivyotumia).
Njia nyingine ambayo mtu anaweza kupata VVU ni kunyoa, tengeneza nywele Salon, sio wahudumu wote wa sehemu hizo wanatumia bidhaa maalumu iliyothibitishwa kitaalamu ili kuuwa vijidudu vinavyosababisha UKIMWI na wanapofanyia kazi nywele zako sio wakati wote wanaikwepa ngozi, wakati mwingine inatokea bahati mbaya ngozi naguswa, sasa kama kifaa hicho kilimnyoa mtu mwenye VVU ni wazi unakuwa hatarini (Inashauriwa kwenda na mashine/vifaa vyako mwenyewe just incase)
Kutokana na maelezo yako nahisi mumeo alijua alichonacho mwilini mwake (VVU) na akawa muangalifu sana kila anapofanya mapenzi na wewe ili asije kukuambukiza, lazima alihakikisha unakuwa tayari kabla ya tendo na hakuwa akilazimisha ikiwa hauko kwenye "mood".
Ni vema jamii ikabadilika jinsi inavyolichukulia suala la VVU. UKIMWI ni gonjwa hatari kama yalivyo magonjwa mengine mengi ambayo hayana tiba bali dawa ya kupunguza makali yake Mf ni Pumu, Moyo, Kisukari, Saratani mbali mbali, Matatizo ya akili n.k tofauti yake ni kuwa UKIMWI unaambukiza wakati hayo mengine hayaambukizi lakini yote yanaua na ktk hali halisi baadhi yake yanakuondoa haraka kuliko yule mwenye VVU.
Tukumbuke kuwa hivi sasa tunamezunguukwa na jamii kubwa inayoishi na VVU, na kuwa na vijidudu hivyo haina maana kuwa wewe ni mgonjwa japokuwa unatakiwa kuwa muangalifu na kumuona Daktari wako mara tu unapojisikia tofauti (maumivu au kujisikia ovyo/vibaya), hii inasaidia wao kukufanyia vipimo na kujua tatizo ni nini....huenda umekumbana na maambukizo fulani na hivyo inakuwa vema kulitibu tatizo hilo kabla halijawa sugu kwani mwili wa mtu mwenye VVU hauna kinga za kutosha za kupigana na magonjwa/maambukizo mbali(sote tunalijua hili).
Elimu kuhusu UKIMWI in terms of kujilinda, unavyoambukiza na kujizuia imetosha lakini sasa inahitajika elimu kuhusu namna ya kuishi na VVU na kuishi na watu wenye VVU.
Kidokezo:Napenda kuwakumbusha rafiki zangu. Condom ni asilimia 100 lakini kutokanana sababu za kisheria hiyo asilimia moja ambayo inafanya bidhaa hii kuwa 99% inalinda Kampuni husika kwa utengenezaji wa bidhaa hiyo, ikiwa wewe utaitumia vibaya na kupata maambukizo ya VVU.
Unapoamua kutumia Condom, mnapaswa kuwa waangalifu kama sio kuziruka harakati nyingine za kuandaana kuelekea kwenye safari yenu kabla ya kuvalia vazi hilo maalumu. Kushikana nyeti, kugusisha nyeti zenu, kubusu, kunyonyana huko chini n.k....huwezi kufanya vyote hivyo kisha ukadai "nilivaa Condom au alivaa Condom hivyo sina HIV", kama ndio katabia kako ka kutumia condom baada ya kufanya yote hayo bila Condom......kapime!
Wapo wanandoa kama huyu Mdada (nawafahamu) ila wao walifunga ndoa wakijua kabisa mmoja wao ana VVU baada ya mkewe kufariki, pia ilithibitishwa baada ya Njemba kupima. Siku zote wanadai kutumia Condom na walipokuwa wanataka "mimba" ndio walikuwa wanakwenda nyama 2 nyama lakini kwa uangalifu na kwa kuzingatia lengo moja tu ambalo ni kusababisha mimba na sio mambo ya utamu au kwenda mwendo mrefu. Sasa wanawatoto wawili wenye afya na mkewe hana VVU huyo bwana yuko chini ya matumizi ya madawa.
Fafadhali mpenzi msomaji ukipata nafasi tembelea Tovuti husika kuhusu HIV ili kujifuza zaidi mabadiliko ya wadudu hao, kuishi navyo, kuishi na walionavyo, ngono na mpenzi mwenye VVU na mambo mengine mengi kwa faida yako, huenda sio wewe leo lakini kesho ikawa mdogo wako au hata rafiki yako kama sio mtoto wako.
Kila la kheri Tenisha, na hongera sana kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa mumeo. Mungu akubariki na nawatakia maisha marefu ya ndoa.