Mimi nimeolewa miaka 25 iliyopita na nina watoto wakubwa tu, lakini kutokana na shughuli zangu nyingi za kikazi sikuwa na muda wa kuipa Ndoa yetu attention na matokeo yake tukawa tunaishi kama mtu na flatmate wake.
Mimi nikienda kulala mume wangu anaendelea kufanya shughuli zake kwenye Comptuter au kuangalia TV, yeye akiwa amelala mie nakuwa macho nikifanya shughuli zangu. Maisha yetu yakawa hivyo kwa muda mrefu sana.
Ikafikia wakati nikawa nakosa the attention kutoka kwa mume wangu lakini yeye akawa hajali kabisa, mwishowe nikaamua kujiunga na dating site ya wanandoa ambao wako bored (nilipewa habari na co-worker hapa kazini). Huko nilikutana na wake kwa waume na wote ni wanaume na wake zao nyumbani.
Nilikuwa muoga lakini baadae nikawa nafurahia attention kutoka kwa wanaume hao kupitia emails na hatimae nikaamua kukutana nao moja baada ya mwingine na nilikuwa nafurahia sana jinsi walivyokuwa wakinijali na kunipa the attention na sifa lukuki nyingine hata mume wangu hakuwahi kuniambia.
Kwakweli nilibadilika na kuwa mwanamke mwenye furaha sana na nikabadilika kimavazi kwani zile sifa zilinilevya ukizingatia wengine walikuwa wakiniambia nikivaa magauni ya hivi napendeza zaidi na umbile langu linaonekana vizuri zaidi, basi mie nikawa nanunua nguo kwa mitindo hiyo ili kupendeza zaidi kwa nje na kujisikia vizuri kwa ndani.
Pamoja na kukutana nao hao wanaume kwenye dates sikuwahi kushawishika kufanya nao ngono, siku zote niliishia kuongea kuhusu maswala ya kimaisha, matatizo ya ndoa zetu, wale wanaume waliokuwa wakijaribu kutaka kwenda zaidi ya maongezi mara nyingi nilikuwa siwapi nafasi ya kukutana na mimi tena na wala sikuwa nikiwajibu.
Kwa bahati mbaya Rafiki wa Mume wangu alijiunga kule na ndio ukawa mwisho wa maisha yangu ya ndotoni kwani aliliona profile langu na moja kwa moja akaenda kumueleza mume wangu. Mume wangu alikasirika sana na tukagombana sana siku hiyo, lakini mie nikamuambia mume wangu kuwa yeye ndio chanzo kwani alikuwa akiniona kama vile fenicha ndani ya nyumba, nimpikie, nimfulie, nimuandalie mahali pa kulala na yeye anachofanya ni kula, kulala, kwenda kazini nakurudi.
Mume wangu akaondoka kwa hasira huku akisema tunahitaji kupeana nafasi na atakuwa Hotelini, mume wangu tangu atoweke hapa nyumbani hajaongea na mimi bali watoto wake wetu tu ndio anaongea nao na huenda kumtembelea huko hotelini. Watoto wetu hunipa habari baba yao anaendeleaje.
Dinah mdogo wangu, mume wangu nampenda sana japokuwa alikuwa nakasoro zake na kweli nilijibu kwa hasira nikidhani kuwa atakubali kosa na kunipa nafasi nimueleze ukweli wa ile dating site, lakini hakunipa nafasi hiyo.
Namtaka mume wangu kuliko nilivyokuwa nikimtaka mwanzo, sasa ni heri niwe nae nyumbani na sipati attention kuliko kukosa vyote. Yeye simuoni na attention haipo mara saba zaidi.
Naomba wanablog na Dinah mnipe ushauri ili mume wangu arudi nyumbani."
Dinah anasema: Habari ni njema tu Mama Samirah, asante kwa mail yako. Natambua pea nyingi sana hujisahau au niseme husahau kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi ndani ya ndoa yao mara wanapozingwa na shughuli nyingi za kikazi.
Kutokana na maelezo yako nimegundua makosa mawili, Mosi ni uamuzi wako wa kumsaliti mumeo na kwenda kukutana na wanaume wengine, haijalishi kama uliwapa mwili (ngonoana) au la! Muda ulioutumia kwenda kutafuta, kujiandikisha na hatimae kuwa unakutana na hao wanaume nje ya ndoa yako ndio muda ambao ulipaswa kuutumia kurudisha romance ambayo ingeokoa ndoa yako.
Pili ni kumsukumuzia mzigo wa lawama yeye mumeo wakati unajua kabisa kuwa wote wawili mlijisahau au mlikuwa mnategeana au oengine mlikuwa mnadhani kuwa mmekuwa wazee kupeana attention kama wapenzi.
Badala ya kumuambia kuwa yeye ndio chanzo ulitakiwa kumuomba msamaha kwani wewe ndio uliyemtenda mwenzio, hata kama alikuwa hakupi attention bado alikuwa anakuheshimu na kukuthamini na kutumia muda wake nyumbani.
Ni wazi kuwa Mumeo amehama hapo nyumbani baada ya kugundua kitendo chako ili kupata nafasi ya kufukiri kabla hajafanya uamuzi kwa faida yake na watoto wenu, sasa unachotakiwa kufanya ni kama ifuatavyo:-
Mosi, ni kuomba msamaha kwa kumsingizia kuwa yeye ndiye aliyesababisha wewe kuibua tabia chafu na kumsaliti. Kama alivyoshauri mmoja kati ya wachangiaji, unaweza kutumia Kadi, Emails au barua (kizamani) ambayo actually siku hizi ni more romantic kuliko emails na Kadi. Hakikisha unaandika maneno yako kutoka moyoni na sio kuCopy na kuPaste kisha unaPrint.
Pili, kubali kuwa ulikuwa mjinga, mbinafsi na mwepezi kushawishika kirahisi na kufanya ulichokifanya, jutia kosa lako na kubali lawama zote ikiwa atazitoa juu yako (kumbuka you want him back ukianza ubishi utakuwa unamuongezea hasira)
Tatu, wakati unakili kuwa wewe ndio wa kulaumiwa, tumia nafasi hiyo kusema ukweli kuhusu kile ulichokuwa unakikosa lakini pangilia maneno ambayo hayatamfanya ajisikie alikuwa kajisahau (again, kumbuka wewe ndio unamtaka Mume asikutaliki hivyo kuwa mwangalifu), Mf: badala ya kusema kuanzia sasa tupeane attention.....unaweza kugeuza kibao na kuahidi kuwa utajitahidi kugawa majukumu na muda wako kati ya kazi na yeye n.k
Nne, kamwe usizungumzie wanaume wangapi umekutana nao na wapi mlikuwa mkikutana au nini walikuwa wakikuambia. Lakini ikiwa atataka kujua kama ulifanya ngono nje ya ndoa yenu basi sema ukweli (hapa umesema hukukutana nao kimwili) mhakikishie hilo kwa kusema wazi hisia zako juu yake, namna unavyomthamini kiasi kwamba huwezi kutoa mwili wako kwa mwanaume mwingine yeyote, sema hakuna mwanaume yeyote anaestahili mwili wako bali ni yeye mumeo na mengine yote ujuayo kuhusu kumfanya mwaname ajisikie Safiii!
Tano, mpe muda wa kufikiri mara baada ya kumuomba msamaha na kumueleza ukweli. Usilazimishe aje nyumbani haraka na badala yake muonyeshe namna unavyompenda kwa vitendo zaidi (kumbuka ahadi ulizompa), hakikisha yote uliyosema unayafanya kwa vitendo.
Kuwa mvumilivu kwani haweza akaamua kukusamehe na kusahau hapo hapo, atahitaji muda. Pia kumbuka kuna mtu wa tatu hapo anahusika ambae ni rafiki yake. Huyu rafiki (inategemeana na urafiki wao) anaweza akajenga au kubomoa ndoa ambayo tayari inaufa.Hivyo basi, kama unauhakika kuwa huyu rafiki ni wa Damu basi unaweza kumtafuta huyu Bwana na kumueleza ni jinsi gani unampenda mumeo na watoto, ni namna gani ungepeda ndoa yenu iendelee kuwepo. Mwambie ni vipi unajisikia vibaya kwa kitendo ulichokifanya kwa rafiki yake ambaye ni mumeo, Weka wazi hisia zako za kimapenzi kwa mumeo mbele ya huyu bwana.
Hii itasaidia sana kufikisha ujumbe kwa mumeo ambao utajazaia yale uliyokwisha mueleza mumeo, hasa ukizingatia yeye ndiye aliyepeleka ujumbe wa dating site.
Baada ya hapa, watumie watoto ili kupata date ya familia ikiwa ni pamoja na baba yao, watoto siku zote wanapenda baba na mama kuwa pamoja hivyo haijalishi ni uchafu gani umefanya na utawaumiza lakini kama nia ni kurudiana watoto watasaidia kwa kiasi kikubwa sana kufanikisha hilo.
Kwa sasa nikuachie hapa ili ufanyie kazi Ushauri wa wachangiaji wengine na ule kiasi niliokupatia live kwenye radio siku ya Kipindi.
Kila la kheri.