" Hello Dinah,
Tatizo ni kwamba nina girlfriend ambae alikuwa ni wa mchizi wangu wakaachana, baada ya muda mdada akawa ananizimia mimi sana sana alivyoshoboka mie nikatoka nae kingono.
Sasa naona dizaini mdada ananipenda na anataka uhusiano ila mchizi wangu hajui kama mimi nipo nae huyo dem, hapa nifanye nini?
Dinah anasema: Heyaa! Well sio kwamba umemuimba huyo Dem hivyo mimi sioni kama wewe una makosa, makosa ni ya huyo Dem ambae inaonyesha hakuheshimu urafiki kati yako wewe na ex wake ambae ni mchizi wako.
Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Mchizi wako atakuwa cool akijua kuwa unatoka na Ex wake.
Kitu muhimu cha kuzingatia kabla rafiki yako hajajua ni hisia na mpango wako juu ya binti huyo. Je nawe unampenda? Je ukotayari kuanzisha uhusiano na kutetea penzi lenu?
Ikiwa jibu ni ndio kwa maswali hayo basi taratibu anza kutoka na binti huyo bila kutangaza kuwa ni mpenzi wako kwa kusema wala kuonyesha....Mchizi anaweza kukuuliza au akamuuliza ex wake kama ninyi ni pea.
Hilo likitokea tafuteni njia nzuri ya maelewano na kesi itakuwa imekwisha na hivyo mtakuwa huru na uhusiano wenu.
Ikiwa majibu ni hapana basi achana na huyo Binti na uendeleze urafiki na Mchizi wako.
Wachangiaji wengine wataongezea.
Kila la kheri!
------------------