Monday

Condoms au Dawa za kuzuia Mimba

"Mke wangu anataka tutumie kondom, hiyo ni kweli? Nimeoa miaka 6 iliyopita, tumejaliwa watoto wawili wa miaka 4.5 na mwingine ni mwaka Mmoja.

Tangu tumepa mtoto wa pili, Mke wangu alianza visingizio kuwa yeye hatatumia njia nyingine za Uzazi tofauti na Condom kwani njia zingine zinamsababishia kuumwa Mgongo, Joto kali na mengine mengi.


Mie kutumia Condom najiona kana kwamba nipo na Changudoa, sipati raha hata tone, nimemueleza haelewi, nishauri nifanyeje?"

***********


Dinah anasema: Hello there! Ahsante kwa Ushirikiano.


Kabla ya yote unapaswa kutambua kuwa Raha/Utamu wa Ngono upo Akili(kichwani) na sio kwenye Uume, Uume ni kitendea kazi.


Suala la kuona kama upo na Changudoa kwasababu ya kutumia Condom ni Dharau kuu kwa Mkeo! Inamaana ukivaa Condom unapoteza mapenzi na hisia zote za Huba kwa Mkeo na hivyo unafanya tu ili kuji-relief?

Ikiwa Mkeo anasumbuliwa na Dawa za kuzia Mimba na kumfanya aumwe kama alivyokuambia hakika hawezi kukuelewa. Wewe kama mumewe ulipaswa kumuelewa na kumpa-support na kwa pamoja ama kukubaliana na matumzi ya Condom au kutafuta/jaribu aina nyingine ya Dawa za kuzuia Mimba.


Ikiwa kila dawa anazojaribu zinamsababishia matati kiafya ni vema kutotumia na badala yake mtumie Condom kama alivyo-suggest, kama hutaki na Nyama to Nyama ni muhimu kuliko Afya ya Mkeo basi kazibwe Mirija ili usiwezi kumtia Mimba.

Unapaswa kutambua Dawa hizo (baadhi) zinahomono na huwafanya wanawake wengi wapate "side effects" mbaya sana.

Wengine huwa wakali, wakatili, wazembe/wachafu, wanapoteza hamu ya kufanya mapenzi, wanapoteza hali ya kukupenda wewe, kujipenda wao au watoto, maumivu ya Kichwa yasiyoisha, kupata Hedhi kwa muda mrefu (miezi 3-9), Unene/Kujaa maji, Mapigo ya Moyo kuwa juu n.k.


Wanaume wengi (hasa Waafrika) mpo nyuma sana kwenye ku-support Wake zao kwenye matumizi ya Condom kwa kuamini kuwa Condom inazuia raha na "nimemuoa hivyo hakuna kutumia Condom"...Condom ni njia nzuri sana ya Kuzuia Mimba ikiwa njia nyingine zinasumbua.

Techology ya Condom imekuwa sana na mengi yamebadilika, kuna Condom nyepesi kama ngozi lakini Imara(hazipasuki)....explore aina za Condom Mwanaume, za bure waachie Wanafunzi na watu wasio na Uwezo.

Condom za leo haziwashi, sio nzito(lakini Imara), hazinukii kama mpira....nunua kulingana na mahitaji yako.

Wekeza kwenye Condom Mwanaume sio unashupalia Nyama to Nyama na kutojali matatizo ya Kiafya ya Mkeo utadhali Uhai wapo depends on Nyama to Nyama!



Mapendo tele kwako...

Friday

Mapenzi na Kazi, unakabiliana vipi?

"Mimi ni msichana wa miaka 24, nimekua na mahusiano na boyfriend wangu miaka mitatu sasa mwaka wa kwanza tulikua na matatizo kutokana na Ex wake aliyekua anamng'ang'ania na kuwashirikisha ndugu wa mwanaume ili wamsaidie arudiane nae.


Bahati nzuri mpenzi wangu ni mtu mwenye msimamo kidogo haku-fall kwa hilo na yote niliyavumilia..kama wapenzi tumekua na ups and down na tumevumiliana nimeshafanya makosa sana lakini bado ameendelea kuwa na mimi.

Tatizo linapokuja hapa, mpenzi wangu ameajiriwa na mimi bado nipo Chuo ila Ofisi yao ilitangaza nafasi za kazi za muda mfupi akani recomend nikapata kazi ila akasema tuseme sisi ni marafiki maanake Ofisi itaona amemtafutia kazi mpenzi wake kitu ambacho sio kizuri.


Nikakubali manake kazi yenyewe ilikua ya muda, kuanza kazi pale nikakutana ma mdada ambaye anampenda boyfriend wangu though my boyfriend anamchukulia kama rafiki. Yupo nae close and all that.


Siku moja tukatoka Out kama Ofisi, kwa vile tumeamua kufanya mahusiano yetu yawe siri hata siku hiyo tukashindwa kuwa pamoja matokeo yake akawa karibu na wadada wengne wa Ofisini mmoja wapo akiwa huyo anayempenda my bf.

Kwa hasira nikaishia kunywa pombe hadi nikapoteza kumbukumbu kabisa nikarudishwa nyumbani na my bf na he took care of me. Nikajisikia vibaya mno kwa nilichokifanya.


Kesho yake akanambia nililewa nikafanya ujinga kitu ambacho sikumbuki, akasema nimemuumiza sana na kwa mara ya kwanza akalia. Najua nilifanya makosa na hiyo ikawa mwisho wa kunywa pombe!


Siku hiyo tukaamua kuachana ila tukawa tunaendelea na mawasiliano, ikapita kama Mwenzi tukaanza tena kulala pamoja but kipindi hiko haikua serious sana.

Nikawaza vile mimi ndio nilikua responsible kwa uhusiano wetu kuvunjika basi ntavumilia tu ikapita kama three months tukawa sawa and tokea hiyo incident ni mwaka sasa.


Tatizo ni lile lile hataki watu wa ofisini wajue uhusiano wetu japo ndugu zake wote na marafiki zake wote wanajua uhusiano wetu. Kipindi hiki nimerudi tena kufanya hapo kazi anadai wanawake wa pale Ofisini anawajua vizuri wakijua sisi ni wapenzi sitafanya kazi kwa amani, kwamba kutakua na maneno sana ila siku itafika watajua tu ukweli.

Nampenda mno namuamini pia ila kwenye hilo suala linakua chanzo cha ugomvi kati yetu wakati mwingine. Nakua njia panda

Nishauri dada yangu. And sorry kwa maelezo marefu."


*******

Hello there, usijali maelezo marefu yaliyokamilika nayapenda na ndio huyafanyia kazi. Shukurani sana kwa ushirikiano.

Hapo kuna mawili-matatu! Moja inawezekana Mpenzi wako alikuwa na Uhusiano na mtu ambae bado yupo hapo Ofisini au Mkubwa wake wa Kazi hapendi wafanya kazi wawe na wapenzi wao mahali pa kazi(kuepusha uzembe na kupendeleana) na mpenzi wako hataki upoteze kazi.....(Fanya uchunguzi hapa, usikurupuke ukakosa vyote).

Pili, Mpenzi wako hataki ijulikane kuwa wewe ni mpenzi wake na hivyo kasaidia au alisaidia wewe kupata kazi pale ofisini kwake....kasema ni marafiki na labda baadae ukipata ajira ya moja kwa moja atajifanya amekudondokea na hapo kuanzisha uhusiano(wakati ukweli mnaujua wenyewe).

Ni vema mpenzi wako atambue kuwa kufanya uhusiano Siri wakati yeye anakuwa karibu na Wanawake wengine huku wewe ukishuhudia ni ngumu na inaumiza sana (anakunyanyasa Kiakili na Kihisia).


Kufanya kazi hapo ni muhimu kwako kwa ajili ya uzoefu na pengine ajira ya kudumu hapo baadae hivyo usilazimishe sana kujulikana na watu wengine hapo Ofisini (hawana umuhimu sana kama Ndugu zake) na hakika unaweza kupewa Ukweli(umbea) wa nini mpenzi wako alikuwa akifanya na mtu fulani hapo ofisini(tuseme ni Ex) na hapo kukawa na ugomvi au makundi na kufanya maisha ya kikazi Jehanam.


Muhimu ni kuzungumza na mpenzio na kumueleza unavyojisikia bila hasira, kisha wote kwa pamoja muelewane kuwa yeye apunguze au aache kabisa ukaribu na wanawake wote hasa yule ambae unadhani kuwa anampenda mpenzi wako.

Kama yupo serious na uhusiano wenu na mnapendana (mwambie) basi ni vema tukaweka Mipaka dhidi ya watu wa jinsia tofauti wanaotukaribia ili kusiwe na maumivu Kihisia na Kiakili.

Inawezekana kabisa kuwa na uhusiano Kazini kama Wafanyakazi na Wapenzi mkiwa nje ya Kazi ikiwa mtafuata hayo hapo juu.

Hili likishindikana basi ni vema mmoja wenu aombe uhamisho au abadilishe kazi.


Kila lililo Jema.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Mzee aniharibia Nyumba!

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28, mpenzi wangu ana Ishirini na Tisa na tumeishi nyumba moja yapata mwaka.











Kwa sasa tunatofauti kidogo. Mpenzi wangu alianzisha uhusiano na Mzee ambaye ni mkubwa kwetu. Baada ya muda niligundua kuwa kabla ya uhusiano wao huyo Mzee alikua karibu na familia yake.











Hivyo tuligombana na ugomvi ulikuwa wa muda mnamo /11/2014 niliamua kumpigia simu huyo mzee na alikua mstaarabu na kuahidi kuachana na huyu Msichana.











Alipojua nimefanya hivyo tuligombana kwa maneno mpaka ikafikia hatua ya kupigana, nilimuumiza na yeye akaamua kwenda kwao.









Kwa sasa ninajaribu kurudisha penzi letu lakini napata shida sana nifanye nini ikiwa bado namuhitaji?"





*************





Dinah anasema: Habari gani? Ahsante kwa ushirikiano.







Ikiwa Mpenzi wako amekusaliti kwa kutoka na mzee huyo na ukajaribu kukomesha uhusiano wao kwa kuzungumza na Mzee husika ili akuachie Mpenzio. Lakini Mpenzi wako akakasirika na kugombana kutokana na kitendo cha wewe kupigania penzi lenu unadhani Mwanamke kama huyo anakupenda au kukuthamini?











Mtu anapofikia mahali anatetea Kosa lake au kutafuta sababu ku-justify anachokifanya au mtu anaetenda nae kosa ni wazi kuwa huna umuhimu kwake.









Kitendo cha wewe kumpiga na kumuumiza sio kizuri(ni Kosa Kisheria), pamoja na kumpenda kwako sidhani kama ni sahihi kuendelea kupigania Penzi ambalo ni la upande mmoja tu (wako), angekuwa anakupenda kwa dhati msingefikia mlipofikia.









Jitahidi kusahau na utafute namna ya kusonga mbele na maisha yako bila yeye.





Nakutakia kila lililo jema.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Mbinu za Kupendwa Ukweni!

"Dinah habari, nilikuwa nataka kujua jinsi ya kuelewana na kupendana na ndugu wa Mume wangu katika kutafuta google ndio nikakutana na Blog hii.

Mie na Mume wangu tumefunga Ndoa miaka kadhaa na tumejaaliwa watoto Watatu. Mwanzoni hatukuwa na matatizo yeyote kati ya Shemeji na Wifi zangu.

Matatizo yameanza hivi karibuni na chanzo sikijui. Nimejitahidi sana kuwapenda ndugu wa Mume wangu lakini hawapendeki. Kila wakija kwangu ni maneno, imefikia hatua wanasema nimembadilisha Kaka yao.


Nikiongea na Mume wangu kuhusu habari hizi, yeye anaishia kusema niwadharau.

Je, nifanye nini ili kuwe na Amani miongoni mwetu? Naomba ushauri au kama kuna hatua, mbinu zozote za kuwafanya ndugu wa mume wangu wanipende, wanikubali. Ahsante".


**************


Dinah nasema: Nakumbuka nilikwisha zungumzia kuhusu hili ila kwa namna nyingine kati ya mwaka 2007 na 2008 (angalia kwenye Topic zilizopita hapo Kulia).

Niligusia kuwa wakati unaandaliwa(Fundwa) ili uende kuishi na mtu mwingine(Mume) na watu wengine (ndugu zake), unaonywa wazi kabisa kuwa uwaheshimu ila usilazimishe wakupende na kamwe usijipendekeze kuwapenda!

Kibinaadamu huwa inatokea una-click na baadhi ya watu na mnakuwa na mahusiano mazuri kama Wifi/Shemeji na wakati mwingine unachukiwa kabla hata hawajakufahamu.


Kosa Kuu ni kuwa tunaaminishwa kuwa ni "lazima" uwapende ndugu wa mwanaume na matokeo yake unasahau kuwa hao "ndugu" ni Binadamu na Binadamu anahisia na hisia hizo sio lazima ziwe za upendo kwako.....sasa ukienda Ukweni full force "nawapenda ndugu zake" hakika itakuumiza.

Pia wakati mwingine wewe mwenyewe inatokea tu unampenda "Wifi" yako na unatamani mngekuwa "marafiki" ukidhani atasaidia kulinda Ndoa yako in case ikabuma.

Ninachojaribu kukuambia hapa ni kuwa, ni muhimu kumchukulia kila mtu kama alivyo na kumheshimu (so long anakuheshimu pia), kama hawakuheshimu basi achana nao (wadharau).

Kumbuka Upendo haulazimishwi. Kama ilivyo Shuleni au Kazini, unakutana na watu ambao huwajui, hujawahi kuwaona maishani mwako lakini inatokea unapatana na baadhi na wengine inakuwa Hola(huwapendi au hawakupendi).

Na pengine unawachukulia kama walivyo tu bila kuwa na hisia ya chuki au upendo kwao hivyo wanakuwa Wanafunzi wenzio au Wafanyakazi wenzio na sio Rafiki zako.

Hakuna mbinu zitakazowafanya ndugu wa Mumeo wawe kama unavyotaka au ulivyotegemea. Wanamaisha yao na familia zao (Wake/Waume na watoto wao).....usipoteze muda na nguvu kulazimisha Upendo ambao haupo, Wekeza Muda na Nguvu zako kwenye zingatia maisha yako, ya wanao na Mumeo.

Likitokea jambo la kuwakutanisha kama Ukoo(tangu umeolewa na Kaka yao) shiriki bila kinyongo, ongea nao kama watu tu (sio Wifi-Shemeji).

Kila lililo jema.

Mapendo tele kwako...

Kumuendekeza mwenza(wa Kiume)!

Unajua tunapoanza mahusiano huwa tunajitahidi kufahamiana na kujuana zaidi kabla hatujaamua kuwa -serious(Ku-ndoa-na).











Baadhi yetu hujitolea "Mhanga" na kwenda kujuana na kufahamiana baada ya kuwa serious(Ndoa-na kwanza mengine yanafuata).











Wachache huamua kuichukulia kila siku kama inavyokuja(hawa bado wanakua au wanaogopa kuji-commite baada ya kutendwa).











Jinsi siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo kila mmoja wenu anajifunza jambo au mambo kuhusu mwenzie. Ukigundua kuwa mambo au jambo fulani linaweza kuwa Mzigo huko mbeleni ni vema kuliweka wazi na kulizungumzia kisha kutafuta Mbadala.











Baadhi huamua kuendekeza tabia za mwenza wakitegemea kuwa watabadilika....bila kujua huko mbeleni inaweza kuwa Mzigo. Mfano Uvivu ambao hupelekea mtu kuwa tegemezi, Ulevi au Uchafu n.k.











Baadae mnapokuwa na familia utajikuta unakuwa Single-mother with a husband, kwamba unafanya kila kitu kuanzia kazi za ndani mpaka kutafuta pesa ya Chakula na Matumizi mengine kwa Familia......ukidhani kuwa huko ndio kuwa "independent".











Nimelenga wanaume kwasababu ndio ambao huwa wagumu "kubadilika" kutokana na ile imani kuwa "mwanamke hawezi kunibadilisha" au "usikubali kubadilishwa na mwanamke".









Hakikisha unakuwa Msaada kwa mwenza wako ili awe kwenye mstari na msaidiane, kama hakueleweki....Mpige Mkwara.







Feels great to be Back!

Mapendo tele kwako...

Friday

Samahani Nipo Likizo!

Habari gani?



Samahani kwa kutokukutonya kwani sikuona umuhimu wa kufanya hivo (Mie sio Celeb bana).









Nachukua nafasi hii kukufahamisha kuwa nilikuwa na bado nipo Likizo (napumzika na Blog hii) kwa Muda.









Ahsanteni wote kwa kuonyesha kujali kwa kunijulia hali/ulizia kama nipo salama.







Nitakuona nikimaliza Mapumziko.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Mume Mbishi au apenda Changamoto?

Hongera kwa kuokoa Ndoa za walio wengi mimi ni mfuatiliaji wa blog yako kwa muda sasa na ninapenda saaana kazi zako. 

Kiufupi mimi ni mwanamke nimeolewa miaka miwili iliyopita na nimebahatika kuwa na mtoto mmoja. Naomba ushauri ambapo sijui tatizo ni la kwangu au ni la mume wangu au ndio kukosa hisia!

Ni kwamba nahisi Mume wangu hana hisia nami kwa sababu zifuatazo;

1. Huwa hanisikilizi kama zamani na amekuwa mbishi kupindukia anaweza kubishana na hata mtu mzima kumzidi, mimi ndio usiseme.

***********

Dinah anasema: Mumeo amekuwa na huenda Upeo wake umepanuka kwamba anauelewa wa mambo mengi kwa undani kuliko ilivyokuwa awali (mlipokutana).


Kubishana sio tatizo kwani inakusaidia kuweka wazi Mawazo yako wazi kuhusu issue inayozungumziwa, muhimu ni yeye kutoa nafasi ya kukusikiliza na wewe umpe nafasi ya kujieleza(weka mawazo yako wazi).

Kuhusu kubishana na mtu mzima kuliko yeye ni dalili kuwa anajitegemea kiakili na anajua kuwa anahaki ya kusikilizwa na kuweka maoni yake wazi....kuna watu wanapenda "debate"....ni sehemu ya "character" yake kama yeye.

Jaribu kuzungumza nae na kumuambia tabia yake ya kubishana kuhusu kila jambo haikupendezi na inakunyima amani, ni vema mjifunze kuzungumza (kuwasiliana) kama Wenza.
*************

Anaweza kuondoka na asiseme anakwenda wapi kwa kweli mimi huwa ananiudhi inafikia hata kipindi namchukia.

**********


Dinah anasema: Hili pia ni suala la kuzungumza na Mumeo na kumuambia kuwa ni muhimu kuanga na kukuambia anakwenda wapi na kwasababu gani ili kukuondolea hofu na usumbufu wa akili kwani Dunia inamengi na lolote linaweza kutokea muda wowote na wewe usijue kama Victim ni Mumeo au la!
***********


2. Hana shukrani hata upike vizuri kiasi gani, upambe chumba au hata nijipambe mwenyewe hawezi kunisifia sasa huwa sijisikii vizuri pale ninaposifiwa na watu wengine wakati wa kunipa faraja ni yeye....ila utamsikia mmh leo mmmh leo. 

*********

Dinah anasema: Huenda alipata Malezi mabaya, hakufundishwa manners nzuri(na muhimu Maishani) ambazo kila Mzazi anapaswa kumfunza mwanae tangu akiwa Mdogo nazo ni Kushukuru, Kuomba, Kusalimia, Kuaga, Kubisha(Hodi) n.k.


Kwenye kukusifia kuhusu Muonekano wako sio muhimu ailimradi tu mwenyewe unajijua umependeza, lakini kama kwako ni Muhimu na inakufanya ujisikie vizuri au kukufanya ujiamini basi weka wazi kwake mnapozungumza au mkumbushe(kama anajua anapaswa kukusifia ukipendeza).

**************


3. Hanifikishi kama zamani, siku hizi akipiga kimoja hoi ndio nitolee hiyo wakati mwanzo alikua anaenda hata round nne kwa siku na si za masihara ni za ukweli!


**********


Dinah anasema: Jinsi siku zinavyokwenda Mwili wa mwanadamu hubadilika! Hivyo inawezekana mwili wake hauwezi tena au anahitaji "kuhamasishwa" zaidi baada ya hicho kimoja. 

Halafu pia Wanaume wengine huwa Hodari wa Mizunguuko pale mwanzo wa uhusiano ili mwanamke usikimbie....na vile mnaonana mara chache basi "anajitunza" mwenyewe ili akija au ukienda mfanye mapenzi kufidia siku Saba zijazo na Saba zilizopita!

Lakini baada ya ndoa anakuwa na uhakika wa kukupata muda wowote hivyo haitaji ku-show off "uhodari" wake ana-relax a bit. AGAIN....zungumzeni kuhusu hili pia na mkubaliane kurudisha "moto" kwenye uhusiano wenu.
************

4. K yangu ni ndogo sana inanifanya hadi niumie kila wakati hata kama mume wangu ataniandaa kwa masaa matano mwisho wa mchezo naambulia maumivi sasa tatizo sijui nini? 


***********

Dinah anasema: Sasa mrembo walalama Mizunguuko Michache, hapa unasema unaambulia Kuumia, huoni hicho kimoja ni afadhali kuliko viTano eti?!!


Hakuna Uke Mdogo linapokuja suala la kufanya Ngono ailimdari kuna Ute wa kutosha Nje (mwanzo wa Uke) na ndani kusaidia Uume kuingia na Misuli ya Uke ku-relax jinsi anavyoingia taratibu(hatua kwa hatua).

Lakini kutokana na yote uliyoelezea hapo juu ni wazi kuwa unapoteza hamu ya Tendo hivyo hata akikuandaa kwa muda mrefu Misuli ya Uke wako inashindwa ku-relax kwasababu wewe huja-relax akilini kutokana na maudhi ya Mumeo.

Kumbuka kupata Ute sio kielelezo kwamba upo tayari kwa Tendo (kuingiliwa)....jaribu kumaliza issues zenu kwa kuzungumza na kuelewana ili wote kwa pamoja muweze kufurahia Ndoa yenu.
**************

Kiufupi da dinah nampenda sana mume wangu na sitamani kumkosa ila kwa tabia sijui hata nitamrekebisha vipi.

Na nikimkubaria kila kitu anasema simpendi kwa nini niwe namkubalia kila nachosema na nikimkatalia pia  ni hivyo hivyo nifanye nini jamani au mimi ndio namkosea sijui jinsi ya kuishi nae?!!

**********

Dinah anasema: Ahsante Mrembo, shukurani sana kwa ushirikiano.


Nimejitahidi kujibu kila swali papo kwa hapo ili nisikuchanganye.


Hilo la mwisho nitalijibu hivi:- Wanaume wa Kisasa wanapenda Changamoto, hawapendi ile "ndio bwana" kwenye kila jambo kwani haiwasaidiii.


Kama nilivyogusia awali, inaonyesha Mumeo amepanuka kiupeo na ana-enjoy changamoto au anataka kupata Maoni yako kuhusu jambo analokuambia.

Hategemei kukubaliwa au kataliwa moja kwa moja/haraka hali ambayo wewe unadhani ni "umbishi".


Ndoa yenu haina Mawasiliano na inaelekea hamkujipa nafasi ya kujuana zaidi kabla ya Ndoa, matokeo yake kila jambo unaona "jipya".

Kuwa pamoja kwa Muda mrefu kabla ya Ndoa sio kithibitisho cha kujuana zaidi (usichanganye), bali Uwazi kwenye kujieleza kuhusu Malezi yenu, Wepesi wa kuhoji, Uhuru wa kuweka wazi au kuonyesha "good manners" n.k.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Ushauri wa Kimaisha

Dada Dinah Habari za Kazi? Mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 35 nina watoto wawili wenye baba tofauti. Wa kwanza ana miaka 16 na wa pili ana 12.


Hapo nyuma nilikuwa sipo vizuri kimaisha kwani nilikuwa sina kazi. Baada muda nikapata kazi Mkoani, nikafanya kama miaka miwili hivi.


Then nikapata kazi yenye maslahi zaidi ya kule kwa mwanzo Mkoa mwingine, ambako ndio nyumbani kwetu kabisa kwa wazazi wangu.

Nilipokuja kuripoti nikafikia nyumbani hadi hii leo, kwani toka nianze nina
kama miezi sita hivi.

Tangu watoto wamezaliwa wamekuwa hapa kwa wazazi hadi hivi leo hii kwani  wazazi wangu hawataki niwachukue
nikakae nao mwenyewe.


Kwa hiyo hadi hii leo wote tupo hapa nyumbani ila najipanga
kuhama.

Swali: kuna vitu viwili ,vinanichanganya nina kahela kangu nawaza je nifungue biashara au nirekebishe nyumba ya wazazi wangu?

Yaani najiuliza sipati jibu kwani nyumba nayo ni ya kizamani sana naomba unishauri dada Dinah nijiongezee kipato kwa kufungua biashara
au nianze na ukarabati wa nyumba yetu?

Yote ni muhimu kwani napenda wazazi wangu wakae kwenye nyumba nzuri, nianze kwanza kukarabati nyumba then biashara ifuate au?


Kumbuka hao watoto mimi ndio baba na ndio mama maana sijaolewa na umri umeenda. Ningependa ufiche email yangu. Asante.

**********


Dinah anasema: Habari ni njema, shukurani kwa ushirikiano.

Najua kuna hisia ya Hatia inakusukuma au kukufanya utake kuanza kukarabati nyumba ya wazazi wako kama shukurani!

Lakini kumbuka ilikuwa chaguo lao kuwachukua watoto, hukuwalazimisha au kuwaomba wakusaidie hivyo huna haja ya kurekebisha nyumba kwasababu ya kuhisi "guilt" na badala yake fanya kitu ambacho una uhakika kitazalisha Pesa ulizonazo.


Biashara itakuwezesha kurekebisha Nyumba yenu, kuwasaidia kujikimu na wakati huohuo kutakuwa na muendelezo wa kipato cha pili kuingia.


Lakini pia, unaweza kufanya yote kwa wakati mmoja, endelea kubaki hapo kwa wazazi ili senti za kulipia Nyumba ya kupanga (kutoka kwenye Mshahara wako) ndio uitumie kurekebisha Nyumba ya Wazazi wako taratibu(kila mwezi). Na hizo pesa za pembeni zikafanye Biashara unayotaka kuifanya.


Nina Imani kuwa maelezo haya yatakupa mwanga zaidi, nafurahi kuwa sehemu ya Maamuzi yako Muhimu ya Kimaisha.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Mchumba Hanipendezeshi...

Shikamoo da Dinah.
Asante kwa kutuelimisha na mungu akubariki sana.

Da dinah naomba ushauri wako kwa hali na mali maana nipo njia panda. Mimi ni mwanamke 27yrs nipo kwenye mahusiano miaka 4 sasa na tumebarikiwa kuwa na mtoto mmoja.

Tunatarajia kufunga ndoa miezi mitatu ijayo na tunaishi pamoja. Tatizo langu ni kwamba mimi nina mpenzi binafsi sana yeye hanifikilii kabisa anajipenda yeye tu.

Mimi nimemaliza Chuo na sina kazi kwa sasa, kwa kipindi cha nyuma kidogo nikiwa mwanafunzi nilikuwa nikijishughulisha na vibiashara vyangu ambavyo vilinisaidia kufanya mambo mengi pamoja na kujiendeleza kielimu na maisha kwa ujumla.


Nilikuwa simwombi huyo mpenzi kitu chochote, lakini mimi kama mwanamke siku zote nimekuwa nikimtekelezea mpenzi wangu anachohitaji kutoka kwangu na kujaribu kuremba penzi letu.

Katika suala la kunipenda naona ananipenda na hawezi kukaa mbali nami hata akisafiri kikazi basi atajitahidi kutekeleza majukumu arudi kabla ya siku  alizotakiwa kukaa huko.

Mawasiliano ni mazuri akiwa hayupo nyumbani hawezi kupitisha masaa mawili bila kunipigia LAKINI akiwa nyumbani ndiyo tunawasiliana vizuri but kuna wakati ana majibu mabaya sana kiasi kwamba hunifanya nipoteze mapenzi kwake.


Nashindwa kumwelewa huyu mpenzi wangu, tangu tumekuwa wapenzi hanijali mimi kama mwanamke wake haninunulii nguo, hanipi pesa ya Saloon hanifanyii kitu chochote kinachonihusu mimi binafsi.

Mimi ni mwanamke ninaejipenda kweli kwa kipindi cha nyuma nilijimudu mwenyewe kama nilivyoeleza hapo mwanzo lakini niliacha kila kitu baada ya kuwa Mjamzito, maana niliumwa sana. Hata baada ya kujifungua afya yangu haikuwa stable mpaka sasa.


Nikimwambia baby naomba pesa nikanunue nguo hizi zimechoka, nguo navaa miaka mitatu hizo hizo out of fashion kama unavyojua sisi wanawake inatakiwa tuwe nadhifu!


Lakini nitaambiwa nitakupa basi inaishia hapo. Cha ajabu yeye binafsi anajipenda sana ni kawaida kununua vitu vyake binafsi kama nguo au viatu kila mwezi tena vya bei ghali laki ngapi huko na saa zingine ataniita dukani mzigo mpya umeingia nimchagulie vitu vizuri lakini mimi mpenzi wake hanifikilii hata siku moja!

Kipato sio tatizo ana huo uwezo nikimwambia ataniahidi tu itaishia hapo nasindwa kuelewa tatizo nini?


Da dinah kuna wakati nahisi hanipendi labda yupo na mimi kwa sababu anajua nitamsaidia kujenga family basi, natamani hata siku moja mpenzi wangu anipe zawadi lakini hakuna!

Mpaka kuna wakati anasema "najinunulia mimi tu ngoja mke wangu usijali nitakupendezesha tu subiri" hapo unakuta anapima nguo kaniona mie mnyonge.

Najisikia vibaya na nahisi kama hana mapenzi ya dhati kwangu sababu tofauti na hayo kuna mambo mengi anayostahili kunisaidia ktk future yangu ( kusaidiana) lakini hakuna kitu.

Mimi nimekuwa nikimpa support kwa kila kitu niwezavyo lakini mwenzangu hapana. Nahisi  sina furaha na nimemchoka sasa natamani hata niachane nae na vikao vya harusi ndio vimeanza naona kama ananitumia kujifurahisha tu.

Niliona aibu siku nimeenda nyumbani kwetu Mama yangu amechukua pesa zake akaenda kuninunulia nguo, pochi na viatu ananiambia mbona nimevaa vitu vya zamani nami ni mke wa mtu hivi they expect to see me shining nilishindwa kumweleza ukweli.

Naomba ushauri wako da dinah nipo taabani.

************


Dinah anasema: Marhabaa Mrembo, shukurani kwa Ushirikiano.


Sasa siku ya Ndoa utavaa nini Mrembo? Usijejikuta unavaa gauni lako la mwaka juzi ambalo haliendani na sherehe husika na yeye anawaka na Suti Mpya!

Kabla sijaingia ndani! Makubaliano yenu yalikuaje? Malezi? Uchumi? Mipango na je mlikubaliana kuzaa au ilikuwa "bahati mbaya"?

Kwasababu mtu huwezi tu kuacha shughuli zako/Elimu ili uzae wakati hujui utakaezaa nae atakuangalia au mtasaidiana vipi (kama ni Mchumba/Mume)?


Mambo ya kushika Mimba kiholela ukitegemea Mwenye Mtoto atakutunza bila mipango ya mbeleni ni Uzamani na husababisha matatizo makuu kwa mwanamke, moja ni kama hili ulilonalo wewe.

Huyu mtarajiwa(mume) sio mbinafsi, angekuwa mbinafsi asingekuwa akiijali familia yake kwa mawasiliano na kukatisha safari zake ili awahi kurudi Nyumbani.

Kwani nani huwa ananunua mahitaji muhimu ya hapo nyumbani? Je huwa Mpenzi wako anakupatia Senti za manunuzi ya kila Siku/Wiki.....je huwezi kuwa unabajeti na ku-save kwa ajili yako?!!

Nadhani ama ulimzoesha kwa kujifanyia kila kitu mwenyewe bila kumshirikisha(ile twende shopping na kununua vitu pamoja) pale uhusiano wenu ulipoanza na wewe ukiwa unajitegemea Kiuchumi.

Wengi wainachanga hii "kujitegemea kiuchumi"....mwanamke kujitegemea kiuchumi haina maana anachukua "jukumu la mwanaume" kwenye familia/uhusiano au Jamii!

Au Mbahili....maana kuna aina mbili za Wabahili....(1)-Hawataki kutumia pesa zao kabisa (2) wana-prefer kuzitumia kwa ajili yao kuliko wenzao.


Pamoja na kusema hivyo inaonyesha wazi uhusiano wenu unakosa Nguzo kuu mbili ambazo ni Mawasiliano(sio kupigiana simu na kujuliana hali) bali kuzungumza kama Wenza na Ushirikiano.

Wenza huzungumzia mengi kuhusu maisha yaliyopo na yale yajayo, kupanga Mipango....Mipango ikiwa ni pamoja na "shopping" ya chakula na Mavazi sio kujenga na kufanya miradi.

Wenza hushirikiana kwenye kila kitu bila kujali nani anaingiza Pesa na nani hana Kipato.


Kabla hujakubali kuzaa nae au kufanya mapenzi bila KUJIKINGA dhidi ya Mimba ulipaswa kuzungumzia na kukubaliana "future" yenu kama wapenzi.....mtafanya nini kuhusu malezi ya Mtoto ikiwa mtazaa?.....utakapojifungua hutorudi kwenye shughuli zako, je mtasaidiana vipi mpaka utakapo kuwa tayari kurudi "job"? N.k.

Hii ni 2000s sio 80s Mrembo, hakuna kuacha kazi inayokuingizia Kipato na kuchanua Miguu bila Kinga wakati hujui kilicho mbele!!

Sasa fanya hivi; Mkiwa mmekaa vizuri na hakikisha anakusikiliza, anza....Mpenzi (Tumuite Paul) Paul hivi unajua kabla sijakutana na wewe/sijazaa nilikuwa najipenda sana?!! Ningewa kama nilivyo hivi sasa walahi usingevutiwa na mimi na tusingekuwa pamoja!

Mwanamke nimechakaa mpaka najichukia....navaa nguo za Miaka 3 iliyopita lakini Mume wangu unag'aa mpaka napata aibu!

Kila nikiomba senti za Shopping, mwenzangu unanipa ahadi zisizotekelezwa.....sasa mpenzi kama hutaki kunipendezesha Mkeo basi naomba Mtaji ili nifanye Biashara na ikilipa nitakurudishia.

Pia inabidi tutafute Msaidizi (Nanny) au tumpeleke mtoto Chekechea maana sitokuwa na Muda wa Kumuangalia hapa Nyumani.


Msikilize atakujibu nini?.....akikupa ahadi! Demand muda maalum kwani hutaki kupoteza muda!


Akilalama kuwa mtoto bado ni Mdogo na anahitaji Mama zaidi ya Msaidizi (kama mtoto ni chini ya miaka 4) basi Jaribu kumuelewesha(wanaume wengine hawajui) na mkumkumbushe jukumu lake kama Mumeo na Baba bila kufoka wala hasira ila kuwa firm(serious)!

Wanaume wengine walilelewa ovyo, kwamba wao ni majina na Maumbile tu, lakini hawajui majukumu yao mpaka wakumbushwe au kushikwa mkono na kuelekezwa.

Suala la yeye kuwa na majibu ya hovyo ambayo yanakufanya upoteze "mapenzi" itakuwa ngumu kwangu kusema lolote kwani hukuwa wazi kwa kueleza Majibu yake hayo hutokana na maswali ya aina gani kutoka kwako?

Siku nyingine (baada ya hili la kurembwa kupita na kufanikiwa)....rudini kwenye Nguzo ya mawasiliano tena, na mzungumze kuhusu hilo.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Friday

Chuki ya Mzazi kwa Mpenzi...

Dada habari za wakati huu mimi ni kijana wa kati nina mpenzi wangu ambae tunapendana sana pia tumefikia hatua ya kukubaliana kuoana.











Uhusiano wetu sasa una mwaka na nusu tatizo limetokea upande wangu ambapo mzazi wangu anaonesha hali ya kutompenda huyu nimpendae.











Halafu mara nyingi humuonesha Mpenzi wangu na sio mimi yaani hajaniambia hamtaki sasa mpenzi wangu anaumia coz tunapendana kweli nae anaogopa baadae inaweza kutokea akajateseka.











Sasa hii imeleta hofu ya kuishi na mimi na sijui nifanye nini maana amekata tamaa kiukweli, naumia sababu sihitaji kumkosa kwani nampenda sana.







***********



Dinah anasema: Habari ni nzuri kabisa, ahsante na shukurani kwa ushirikiano.









Issue yako ni ngumu kuhakiki na sio vema kwenda kumuuliza Mzazi wako kwanini anaonyesha kumchukia mpenzi wako wakati huna uhakika.









Pia huwezi kumkatalia Mpenzio kuwa anachosema au kukiona kutoka kwa Mzazi wako ni Uogo!











Mapenzi ni ya wawili hivyo mwambie mpenzio kuwa wewe ndio umechagua kuishi nae na unampenda. Kuwa na wewe sio kuwa/kuishi na Mzazi wako kwazi Mzazi wako alikuwa na maisha ya yake ya Ujana na mpenzi wake na yamepita, haya ya sasa ni yako wewe na yeye.









Baada ya kumhakikishia mpenzi wako Msimamo wako na hisia zako kwake, anza kuweka "ukuta" baina yao....yaani Mpenzio na Mzazi wako.











Hakuna haja ya Mpenzi wako kwenda kwa Mzazi wako.....yeye anakupenda wewe na sio lazima ampende Mzazi wako au Mzazi wako ampende huyo Binti(Upendo haulazimishwi).











Suala muhimu kwao hao wawili ni heshima, so long mpenzi wako anamuheshimu Mazazi wako na Mzazi wako anamheshimu mpenzio inatosha.











Ni kawaida kwa Wake(hasa wanawake) kudhani kuwa wana nguvu sana kwenye maamuzi ya kimapenzi ya watoto wao kwa sababu tu waliwazaa.











Baada ya kuweka "ukuta" kati yao(hawaonani) fanya uchunguzi kivyako ili ugundue ukweli kuhusu Chuki ya Mzazi wako kwa Mpenzio au Mpenzio kwa Mzazi wako....maana baadhi ya wanawake huwa na yao!





Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Hanitaki kwake kisa Ex ni rafiki wa Dada'ke!

Habari za kazi pia pole na majukumu, hongera kwa kazi nzuri ya kutushauri wadau, mimi nikiwa mmoja wao!

Dada dinahicious mimi ni mwanamke umri wangu ni miaka 30 kwanza napenda kukufahamisha kuwa nimepitia mahusiano kadhaa ingawa sio mengi kihivo!

Tatizo langu linalo nisumbua sasa kwa huyu bwana niliyenae ni hili, nimeanza mahusiano nae ya kimapenzi mwezi wa Kwanza mwaka huu 2014 hadi leo hii tarehe 18.8.2014 ninavyoandika mail hii tuna miezi 7 na wiki kadhaa ingawa tumefahamiana tangu mwaka 2009.


Mwenzangu ana umri wa miaka 38, wakati tunaanza mahusiano alinieleza kuwa alikua na mke na akabahatika kuzaa nae watoto 2. Waliacha kutokana na sababu zao ambazo alinieleza nikaridhia ingawa kwa maelezo yake ni kwamba sababu za kuachana ni Usaliti wa mkewe.

Kabla ya kuanzisha mahusiano na mimi tulika tukiheshimiana sana mwisho wa siku tukaamua kuwa wapenzi kwa kifupi historia yake ni hiyo na hakunieleza kitu kingine zaidi ya suala la kuachana na aliyekua mke na mama wa watoto wake.


Nami pia nilikua nimeachana na mpenzi wangu takribani mwaka na miezi kadhaa nilikua naishi mwenyewe, ila tatizo linalonisumbua ni kutopajua anapoishi hadi hivi ninavyo andika email hii kwako!

Tulienda na hali hiyo baada kufikisha miezi 2 nilishindwa kuvumilia maana nilistaajabu kuona hakuna siku aliyoniambia karibu nyumbani kwangu na hali yeye anafika nyumbani kwangu na yupo huru sana.


Nikamwambia naomba nipajue unapoishi akasema utapajua usiwe na shaka na akaniambia kupajua anapoishi sio defence ya mahusiano yetu natakiwa kuangalia moyo wangu unasema nini kwake na moyo wake unasema nini kwangu na kusisitiza kua ananipenda na anamalengo.


Baada ya hapo alinifahamisha jambo linalomfanya ashindwe kunipeleka kuwa baada ya kuachana na mkewe alijikuta anaanzisha mahusiano na msichana ambaye hakutaraji pia hakua na malengo nae msichana huyo.

Aliniomba msamaha kwa kutonifahamisha hilo, alinisihi sana nisimwache pia akaniomba nitulie anitengenezee mazingira salama na akadai pale nyumbani anaishi yeye na wadogo zake 2 moja wa kiume na mwingine ni wakike hivyo binti aliyeanzisha mahusiano nae anaurafiki sana na mdogo wake wa kike hivyo mara nyingi huyo binti amekua akipendelea kwenda pale nyumbani kwa sababu hawakai mbali sana.

Yeye kuishi na wadogo zake aliniambia mapema pia akasema anawaheshimu wadogo zake hivyo nimpe muda asitishe mahusiano na yule bila kutumia nguvu nyingi.


Kiukweli nilimwelewa sikuendelea tena kumuhoji kuhusu hilo, tumeendelea na mapenzi hadi mwanzoni mwa mwezi wa 8 mwaka huu nikaona suala hili linaniumiza sana kichwa pia nimejikuta natawaliwa na hasira sana wakati mwingine.


Nikamkumbushia tena kuhusu kupajua anapoishi bado akanisihi niwe na subra na kwamba amejitolea kua nami hakuisha maneno akaniambia mapenzi ni ghalama na amejitoa sadaka kwangu na kauli hiyo alikua anapenda kuitumia toka tunaanza mahusiano mara ya kwanza nilikua simwelewi mara nyingi alikua akiniambia unajua nimejitoa sadaka kwako kwa lolote.


Wakati mwingine ananiambia unajua mapenzi ni ghalama sana kwa siku hizo nilikua simuelewi ila nikaja kumuelewa alichokua akimaanisha kiukweli inaniuma sana na nimekua nikitawaliwa na hasira kila ninapolifikiria suala hili. Nimekua nikijiuliza maswali mengi sipati majibu.


Ingawa nakiri kwa kipindi chooote ambacho nipo nae kama mpenzi wangu amekua karibu na mimi sana ananijali na haijawahi pita siku bila kuonana usiku kabla ya kulala tunawasiliana.

Yeye ni mtu ambae amejiari anaofisi yake na mimi pia ninafanya kazi katika kampuni moja ambayo haipo mbali sana na ofisi yake hivyo kwa kipindi chote hicho nimekua nikitoka ofisini kwangu napitia ofisini kwake nakaa then naondoka zangu pia huwa hasiti kunitambulisha kwa watu wake wa karibu hususani marafiki zake.


Huwa tunatoka mara nyingi hasa siku za Jumamosi na Jumapili baada ya kutoka Ibadani kuanzia saa 3 huwa tunakua pamoja hadi usiku saa 5 ndio ananiaga anaenda zake kwake.

Ananipa treatment kama mke na kila anaponiona nimebadilika na kua na hasira hua haishi kunisihi nimvumilie hatanitenda kama nilivyo kueleza hapo juu kua suala la kutopajua anapoishi linaniuma hivyo nimejikuta nikiwa mtu wa kutawaliwa na hasira hasira hasa nikikumbuka.


Tafadhali naomba ushauri wako dada dinahicious pamoja na wadau kulingana na jinsi nilivyo jieleza kichwa kinaniuma stress tupuuu,


Samahani kwa maelezo marefu.


***********


Dinah anasema: Habari ni njema, ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.


Ni rahisi sana kwa mwanaume (mume) kusema "nimeachana na mke wangu kwasababu alinitenda" lakini ukweli ukawa yeye ndio Msaliti mkuu na wewe ndio unaefanikisha Usaliti huo....Kwamba hajaachana na mkewe as in kupeana Talaka.

Ndoa yake ni ya Kikristo? Ndoa za Kikristo huwa hazivunjiki kutokana na "Maandiko" yao hivyo utakuta Mke/Mume anaendelea kuishi tu na Mume/Mke ambaye ni Msaliti.

Sioni umuhimu wala sababu ya wewe kupata hasira kwasababu hukujui nyumbani kwake....,adhani ungepata hasira kwanini yule binti (ex) bado anauhusiano na Jamaa na anaendelea kwenda kwake kwa kisingizio cha Urafiki na Mdogo wake!!

Tena kakuambia kabisa anataka "kumalizana" nae taratibu na wewe ukamuelewa REALLY?!!! Moja haku-declare kuwa na ka-ex (baada ya Mke) THEN I mean pili anakuambia "anataka kumuacha tataribu" kwa kigezo cha " "uwifi" kati ya mdogo wake na ex.


Kuna mawili nayaona hapa: Mosi, hajaachana na Mkewe ila anampango huo(wana issues zao kwenye Ndoa yao). Anashindwa kukupeleka kwake kwasababu hataki Ugomvi na Mkewe na hataki kuwachanganya na kuwaumiza watoto wake kihisia.


Hivyo anatafuta visingizio kila leo kwani hataki kuwa mkweli kuhusu familia yake, hasa watoto wake kwako kwasababu anahofia kuachwa. Ukimuacha wakati hana maelewano na Mkewe atakuwa kakosa kote.

Ujue, kuna baadhi ya wanaume waoga sana kuachwa hivyo akiona dalili za kuachwa na Mke, huwa anatafuta mtu pembeni just in case..... Ndoa ikibuma anaendeleza huko nje bila ku experience upweke(sijui unanielewa?).

Pili, anauhusiano na huyo Binti rafiki wa dada yake na wakati huohuo anauhusiano na wewe.....aka Malaya!


Suala la kukaa na wewe mpaka Late usiku na kuondoka sio kielelezo cha Upendo au Uaminifu! Anaweza kutoka kwako muda huo na kwenda kwa Mkewe au yule rafiki wa dada yake pale Nyumbani kwake.


Kuwa treated kama Mke ndio kukoje kwani? Ikiwa Mkewe anam-treat kwa kutokuwa nae muda wote anapokuwa na wewe....utasemaje anaku-treat kama Mke?

Sasa Mwanamke, ili kujua ukweli wa nini ni nini hasa ni vema kufanya Uchunguzi bila yeye kujua.

Mfuatilie nyendo zake anapokwenda kwake ili ujue nyumbani kwake ni wapi hasa, kisha kuwa Detective.... Siku nenda pale kwako ukijua hayupo na ukajitambulishe kama Mfanya biashara mwenzie au rafiki yake na una-deals au mmepanga kukutana hapo kwake!

Ukipata nafasi (ukikaribishwa ndani) au hata kwa nje, jaribu kuwa Mcheshi na kuhoji uliowakuta kiujanja....Mf: kama kuna binti na kijana unaweza kusema "wewe na huyu nani Mkubwa?"...."Baba yenu anapenda sana kuwazungumzia, anajivunia sana watoto wake"

Maelezo hayo (sio lazima yale kama yalivyo, tafuta ujanja wako mwenyewe wa kupata ukweli) yatawafanya au kumfanya mwenyeji wako kuwa comfortable na wewe.


Ana/wanaweza kusema Fulani(mpenzi wako) hana watoto au sisi sio watoto wake au watoto wake wapo blablah...


Kumbuka unachokifanya kinaweza kumpunguzia mpenzi wako Uaminifu kwako lakini unaweza kujitetea kwa kitendo chako (ikitokea umebambwa na alikuwa Mkweli).


Wewe ndio mwenye Mamlaka na furaha yako, mwenye uwezo wa kuchagua aina gani ya maisha unataka kuishi.....kama mtu mwingine anakusababishia usumbufu wa akili na haonyeshi kukuelewa au hamuelewani basi huna haja ya kupoteza Muda.

Wengine wataongezea....
Kila la kheli.

Mapendo tele kwako...

Monday

Nilimuacha, sasa namtaka tena...

Natumaini umzima bukheri wa afya, dada Dinah mimi ni kijana ambae

nilikua na mpenzi na tulipendana sana ila nilimuacha kutokana na

Wivu wangu wa kijinga.













Sasa nina mawazo sana kwasababu bado nampenda kiasi cha kunifanya nisongwe na mawazo mpaka kufikia kuumwa.











Bado namuhitaji mpenzi wangu ila sijui nianzie wapi maana alinivumilia

kwa visa vingi nilivyomtendea na sasa ameamua kunisahau kabisa.









Tafadhali dada dinah naomba unishauri nifanyaje maana naumia sana na

nahitaji turudiane.





***********





Dinah anasema: Namshukuru Mungu, ansante kwa ushirikiano.







Kuna msemo huku unaenda hivi "She will love you, she will cry, she will ask why, she will hate you, she will forgive you, she will love you again.....but one day she'll go and never come back".











Mtu anaweza kuvumilia visa na vituko lakini ipo siku moja akipata "akili" ya kuondoka au kwa bahati nzuri akaachwa kama ulivyofanya wewe inakuwa ngumu sana kurudi(anagundua kuwa alivaba/kosea).....inakuwa lucky escape!











Kwasababu sijui nini hasa kilipelekea wivu wako wa kijinga na hata kumfanyia visa na hatimae kumpiga buti itakuwa ngumu sana kukupa ushauri wa nini cha "kujaribu" kufanya ili umshawishi akubali kurudi kwako.









Kabla hujaanza harakati za kuenda "kumuimbia" misamaha ya kamosa(vile Visa) ni vema kuhakikisha kuwa umebadilika na kujiamini moyoni(na akilini) kuwa hutorudia tena makosa yako kwake (akikubali) au mwanamke mwingine hapo baadae(akikukataa).











Kama unampenda kweli basi pigania penzi lako kwake haraka kabla mwingine hajawahi akamsahaulisha wewe.









Akikataa kubali kuwa sio mwisho wa Maisha yako(huitaji mtu, unahitaji hewa/chakula na maji), ipo siku nyingine utakutana na mwingine na kutokana na ulichojifunza huenda utam-treat vema zaidi huyo Mpenzi Mpya mtarajiwa.







Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Nimesamehe vya kutosha, sasa simuamini tena

Shikamoo dada dinah, pole kwa kazi.
Dada  nahitaji ushauri wako
Nina mpenzi wangu nampenda sana na yeye anaonyesha kama ananijali.

Tangu tuanze mahusiano ni miaka mitatu sasa. Kipindi tunaanza mahusiano aliniambia hana mpenzi na mimi nikamuamini, ila baada ya Wiki kadhaa mwanamke mmoja akanipigia na kudai kuwa huyo niliyenaye ni mpenzi wake!


Nilimuuliza yule mwanaume kuhusu mwanamke yule lakini yeye alikataa ila mwisho wa siku akaadmit kama alikuwa na mahusiano naye ila hamtaki tena akaniomba msamahi basi nikamsamehe.

Mwaka jana nikakuta msg kwenye simu yake anachati na mdada na huyo dada kamtumia picha za uchi nilipomuuliza alidai huyo ni rafiki yake tu, nilimuelewa na kumsamehe.

Ila kama mwezi hivi hatukuwa kwenye mawasiliano mazuri yaani ni ugomvi tu bila sababu. Siku moja nikakuta tena msg anachat na mwanamke na anamahusiano naye nilipomuuliza akasema kweli alianzisha mahusiano naye kutokana na kutoelewana kwetu na akaomba msamah nikamsamehe.


Ila  dada dinah yaani simuamini tena na nahisi bado ana mahusiano na huyo mwanamke. Nampenda sana ila simuamini kabisa na kila nikifikiria aliyonifanyia nakosa hata hamu ya kula.


Dada dinah naomba ushauri wako je nifanyeje??? Nampenda sana ila tabia yake naona inanishinda.


*************

Dinah anasema: Marhabaa mrembo, shukurani kwa ushirikiano.

Mtu kakudanganya mwanzoni kabisa mwa uhusiano utamuamini vipi? Ile ilikuwa dalili ya kwanza kuwa jamaa ni Muongo.....ona sasa umesamehe mpaka kusamehe inapoteza maana eti!

Unahitaji kusamehe mara moja na msamehewa(Mkosaji) kubadilika na kuacha uchafu wake wa tabia....akirudia kosa unanawa Mikono, unaenda kutafuta furaha bila yeye!


Kutokana na maelezo yako ni wazi huyo bwana ni Malaya na ni muoga kuachwa hivyo akiishagundua kuwa mwanamke kajua tabia yake chafu na kuna hatari ya kuachwa....anaanzisha uhusiano mpya wakati bado yupo kwenye uhusiano mwingine uliopo "hati hati".

Sasa akiachwa kwenye uhusiano "hati-hati" anaendeleza ule uhusiano mpya hivyo hatokaa bila mpenzi.

Ndio maana alikuambia kuwa yule alikuwa mpenzi wake lakini hamtaki, hakisema SINA UHUSIANO NAE....."Simataki" ilikupa matumaini na uhakika kuwa wewe ndio unatakiwa na upo peke yako(Kisaikolojia).

Wewe huku unashindwa kula wakati yeye yupo sehemu amekumbatia mwanamke mwingine na anafurahi kama hakuna Kesho!! Bibie umeangushwa, inuka jifute vumbi na uanze kusonga mbele taratibu.

Umevumilia visivyovumilika kwa Miaka mitatu na ameshindwa kukuheshimu wala kukuthamini, haitaji uwepo wako kwenye maisha yake Machafu.


Achana nae, unastahili mwanaume mwema, muaminifu,mwenye mapenzi ya kweli na mwenye kuthamini utu wa mwanamke.

Kumpenda mtu sana sio kigezo wala sababu ya kuendelea kuishi na mwanaume mjinga-mjinga hasa ikiwa anaweka Maisha yako hatarini.

Utaumia, Utajiuliza kwanini? Utalia, Utajutia muda uliopoteza, Utachukia kisha Utakubali kuwa uhusiano haukufai na utasonga mbele kirahisi bila yeye.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Mimi;Nakupena..Yeye;Usijali

Shikamoo dada dinah! Mimi ni mwanamke na nilikuwa ktk mahusiano for 4years but nikaachana na ex wangu sababu alikuwa ananicheat sana.

Sasa kuna mkaka ambaye nilikuwa namjua na tulikuwa tunasoma Chuo kimoja japo yeye alikuwa amenizidi na alikuwa anachukua Masters.


Alikuwa ananifatilia wakati wote huo lakini mimi sikuwahi mkubalia kwasababu nilikuwa kwenye mahusiano na yule Ex, baada ya kuachana nae tukaanza kuwasiliana serious kama mwezi mmoja hivi.


Siku moja akaniambia niende kwake, nilipofka akataka tufanye mapenzi mimi nikamwambia nahitaji kumjua zaidi na japo kucheck afya! Akataka tufanye kwa kutumia Condom but mimi nilikataa.


Sina nia mbaya na yeye ni kweli nampenda halafu dada mimi ni muaminifu sana kwenye mahusiano. Nilivyokataa ku do naye akasema sawa, tulikiss na kunishika shika.

Toka siku ile hapokei simu zangu na msg hajibu. Kuna siku nikamtext kumueleza kuwa nampenda sana akajibu in short akasema usijali!

Kiukweli naumia sana na mimi nampenda huyu kijana sasa simuelewi nimemuomba tuonane tuongee hajajibu chochote.

Dada chonde nisaidie nimekosa raha kabisa sielewi nia yake ni kunichezea au? Na mimi sio kwamba siko tayari kushiriki penzi naye but nahitaji nimjue vizuri then mengine yafuate.
Asante.


******

Dinah anasema: Marhabaa mrembo, ahsante kwa ushirikiano.


Mmeanza kuwasiliana kwa umakini kwa mwezi mmoja....unauhakika kweli unampenda huyo Mr Masters au ume-miss tu kuwa na mpenzi baada ya kuachana na Ex na huyo jamaa akawa easy target kwasababu alionyesha kukutaka?


Miaka minne ni mingi sana kuwa kwenye uhusiano wa Kimapenzi na ku-get over uhusiano wa muda mrefu hivyo huchukua Muda zaidi ya mwaka! Haya ni muda gani umepita tangu umeachana na the cheater one?


Pamoja na kuwa unasababu nzuri sana ya kukataa Ngono (hongera kwa Msimamo Mzuri) bado inaonyesha upo needy na unaharaka ya commitment kwa sababu umemwambia unampenda mapema sana, huwezi mpenda mtu ndani ya mwezi mmoja tena baada ya kutoka kwenye uhusiano wa muda mrefu.


Sio tu inauma kumwambia mtu unampenda alafu yeye anakujibu "usijali" au "ahsante" inakufanya ujihisi aibu mbele yake na pengine kujiamini kunaweza kupungua kimtindo!


Ni wazi kuwa jamaa hajaanza kujisikia "anakupenda" as in "I love you" yaani penzi halijamvaa kama unavyodhani ila anapendezwa au kuvutiwa na wewe as in "I like you a lot".


Kiswahili hakina maneno mbadala ya kuwakilisha hisia kabla, labda napendezwa nawe ilikuwa sahihi zaidi ya "nakupenda".

Tangu kaamua kukuchunia basi ni vema na wewe kuuchuna na kuangalia ustaarabu mwingine.

Kuwa cheated on alafu kujibiwa hivyo hakika inaweza kukukatisha tamaa kabisa na suala zima la Wanaume au unaweza kuamua "liwalo na liwe" kwamba unakubali mwanume yeyote atakaejitokeza ili kujihisi vema moyoni na kujirudishia kujiamini.....(Utajiumiza zaidi).


Unahitaji muda kupumzika kabla ya kuingia tena kwenye mahusiano ya Kimapenzi. Achana na huyo Mr masters.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Mume kapitiliza kwa Kudeka!

Natumaini wewe ni mzima wa afya na family yako pia. Nakushukuru kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuelimisha kwani tunapata vitu vingi sana vya kutujenga kutoka kwako. Ubarikiwe sana.
      


Mimi ni mwanamke wa miaka 25 sasa, Ni mara yangu ya pili kuomba ushauri kwako mara ya kwanza ulinipa ushauri mzuri sana na umenijenga vilivyo na ndio maana nimeamua nirudi tena kwa jambo jingine.


Nimeolewa na mwisho wa mwaka nitatimiza mwaka mmoja wa Ndoa. Mume wangu amenizidi sana kiumri kwani ana miaka 44.

Kutokana na umri wake kunipita watu wanaona nimeolewa na mwanaume aliyenizidi sana wananisema kichinichini nami nazipata habari zao.

Mume wangu mzuri ana mapenzi kwangu na ananiheshimu sana mimi pamoja na familia yangu. Ananipa matunzo vizuri  kwani sijafanikiwa kupata kazi bado na hiyo ni kutokana na kuishi mbali mimi na yeye kwa sababu nitakozokueleza.

Mume wangu na familia yake wanakaa nje ya nchi(Marekani)  ila ni Watanzania waliondoka kitambo kidogo baada ya baba yake kupata uamisho wa kikazi. Aliondoka akiwa mdogo hivyo ana miaka zaidi ya thelathini anaishi huko hivyo ana tabia za kizungu na mambo yake kama wazungu.

Alikuja Tanzania tukakutana tukapendana tukafikia uamuzi wa kuoana. Wazazi wake walikuja ikawa harusi nzuri kweli. Ila mimi bado nipo Tanzania kaniacha huku tukishughulikia mambo ya Visa, ikitick niende.


Anajitahidi kuja mara tatu kwa mwaka  akipata likizo tu anakuja kwani anafanya kazi huko. Mume wangu bado anakaa na wazazi wake huko.

Nawapenda sana wakwe zangu ni watu wazuri, ila kuna tabia siipendi kutoka kwa mume wangu ni mtu flani anapenda kuwataja taja Baba na Mama yake muda mwingi yaani anawataja mno kama mtoto mdogo.

Haiwezi kupita siku bila kuwataja baba yake na mama yake hadi kwenye chakula anacompare akimaanisha cha mama yake kitamu kuliko tunachopika sisi.
      

Muda mwingine tupo na watu tunapiga story yaani lazima atafute sehemu achomekee kitu kuhusu baba na mama yake kama mtoto mdogo na huku kiumri ni mkubwa. Sasa sijui ni sababu ya kukaa na wazazi wake mpaka umri huu.

Nawapenda sana wazazi wake lakini kwa hili sipendi, naona anazidi mpaka sometimes naona kama angeendelea tu kukaa na wazazi wake maana kukaa na mke hakumfai.


Yaani hata akija Tanzania akiongea na wazazi wake kwa simu akimaliza atasema nimewamiss sana wazazi wangu mpaka namuhesabiaga siku ziishe aondoke aende kwa wazazi wake mie nibaki zangu peke yangu.


Unakuta roho hainiumi yeye akiondoka maana naona anapapenda huko zaidi. Kuna muda natamani nisipate Visa mapema maana nikienda huko nitajisikia vibaya zaidi.


Naomba ushauri wako dada yangu kama ni kawaida na nifanyaje ili nizoee hii hali maana naona kama naanza kumchukia na kumuona kama anadeka yaani upendo unaisha kabisa.


Na kumwambia siwezi maana sitaki kuingilia chochote na familia yake. Ahsante sana.
    


**********


Dinah anasema: Mie na familia yangu afya tele, mbio-mbio tu. Ahasnte kwa kujali na shukurani kwa ushirikiano.


Unajua kila Binadamu anamapungufu yake (kasoro), kuna mapungufu ya kimwili (nje au ndani), kitabia, n.k.....Baadhi ya mapungufu huonekana na mengine hayaonekani(utayaona ukianza kuishi na mhusika).

Unapompenda mtu kwa penzi la kweli, mapungufu hayo huwa hayaonekani.....yapo lakini penzi linayaziba hivyo unamchukulia Mpenzi wako kama alivyo.

Unapoyaona mapungufu hayo na ukahisi hayakupendezi na ukahisi unaweza kumsaidia mwenza wako kuacha au "kupona" basi unajitahidi na kujitolea kumsaidia.

Inawezekana Mumeo alidekezwa sana na wazazi wake na hivyo kumfanya ashindwe kujiamini kufanya mambo peke yake kama Mwanaume na hivyo wazazi wakawa tegemezi kuu kwake.

Pia inategemea na alivyokua kimazingira, ujue mtoto kuhamia na kuishi Nchi za Magharibi unakumbana na mengi Hasi ambayo kwa kawaida watu waishio huko huwa hawayasemi na badala yake wanasema yale Chanya tu.

Sasa huwezijua Mumeo alipitia nini Miaka yote 30na alipokuwa huko hali iliyomfanya ahisi kuwa Baba na Mama yake ndio kila kitu kwake(zaidi ya Wazazi).

Kingine ni kuwa Maisha ya Kimagharibi wakati mwingine yanaweza kuwa ni ya Upweke sana.....hasa kama umetoka kuishi "kiafrika" halafu ukaenda mahali ambapo kila mtu anajifungia kwake (unaita kizungu, mie naita Kimagharibi), utajikuta Mnyonge na watu pekee ni wazazi wako na ndugu zako.

Nadhani hata wazazi wake wanatamani sana Mtoto wao aanze "kujitegemea" wakihofia siku wakifa basi Kijana wao anaweza kuwa Mwehu au hata kujiua na yeye.

Ni mumeo na mnapendana, sasa penye hasi weka Chanya na ujichukulie kuwa wewe ndio muongozo wake, chukulia wewe ndio utamsaidia aanze kujitegemea "kiakili" na "kisosho" (baadhi ya wanaume huchelewa ku-mature).

Anza kumuandaa taratibu kuwa ungependa kuishi mbali na wazazi ila tafuta namna ya kufikisha ujumbe wako ili asijisikie vibaya(usiumize hisia zake).

Unapozungumza nae kuhusu maisha yenu pamoja huko US, jaribu kumuuliza mtakaa wapi kama mke na Mume....akisema kwetu as in kwa Baba na Mama, uliza mtakaa hapo kwa muda gani kabla hamjatafuta kwenu?.

Kumbuka utafika US hautokuwa na Kazi hivyo itakubidi utafute kazi (kama una ujuzi tayari) ama urudi Shule kuongeza/kupata Ujuzi ili uweze kuajiriwa kirahisi huko US.....vinginevyo itakuwa rahisi kwenu kama Pea kujibanza kwao mpaka mtakapojiweka sawa kiuchumi.

Kukutumia senti za matumizi Tz inaweza kukufanya udhani jamaa anamahela....Tsh haina thamani hivyo Dola inalipa (ukibadilisha) lakini utakapokuwa huko US hali inaweza kubadilika kiasi, kwamba matumizi yatakuwa ghali....usilishau hili!


Akiuliza kwanini unahofia kuishi na wazazi wake nyumba Moja....Weka wazi kuwa haupo comfortable kuishi na Wakwe nyumba moja....weka sababu zako za ki-romantic zaidi na kwamba hautokuwa huru ku-romantic-a na yeye (Mumeo).


Wanaume wote wanapenda kufananisha/linganisha Wake zao na Mama zao kwenye Mapishi!

Ni wanawake waliowalea na kuwapikia maisha yao yote ya mwanzo hivyo huwachukua Muda mpaka waje kuzoea mapishi ya watu wengine.

Muhimu ni wewe kuongeza mautundu kwenye kupika na ataanza kusahau ya Mama yake na kusifia ya mkewe kwa Wifi zako (watanuna hao) na marafiki.

Nadhani maelezo haya yatasaidia kukupa mwanga na kutuliza hofu yako.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Nimpendae anamtoto (Ready made Family)

Habari dada, pole na kazi na asante kwa msaada wa kimawazo ambao
umekua ukitusaidi kuhusiana na mahusiano ya kimahaba.

Nimekuandikia
ili unishauri juu ya tatizo langu kama ifuatavyo. Baada ya kumaliza masomo nilipata Kazi hivyo nikaona ni vyema nitafute mwenzangu.

Nilikumbuka enzi zile nikiwa shule kuna mdada nilimwacha kama madarasa mawili nyuma kwa sasa yupo Chuo, nilimkazia fikra zangu zote
nilikumbuka jinsi alivyokuaga mwema mtulivu.


Tulikua marafiki wa kawaida nilimheshimu sana nikaona she is the best. Nilitafuta mawasiliano yake nikapata tukawa tunaongea na kuchat sana kupitia Simu.


Nilimweleza hisia zangu akakubali akasema hata yeye alikua
akinipenda sana. Tuliendelea kuchat na kupeana ahadi nyingi.


Akasema wakifunga Chuo wakati anaelekea nyumbani atapitia kwangu kuna jambo la kuzunguma na ni vizuri tuonane.

Walipofunga chuo akaja, nilienda kumpokea kwa furaha coz ni muda wa kama 5yrs hutujaonana. Alizidi kuwa mrembo ila mkononi alikua amepakata
katoto kama kamiezi mitano doh!

Tulipo pata nafasi ya kuzungumza alisema tatizo ndio hilo ana mtoto
amezaa na Mume wa mtu na huyo jamaa ni baba wa watoto watatu na walikutana huko Chuoni.


Kwa mujibu wa maelezo yake Jamaa anatoa ushirikiano mzuri tu katika
malezi ya mtoto, matumizi na wanawasiliana.

Nikamuuliza ilikuaje mpaka mimba inamaana walikua hawatumii kinga! akadai ni utoto alikua hajui mambo ya uzazi.

Kweli nampenda natamani tuoane ila hili linakua zito, ahadi na viapo vyangu vinanisuta kumwacha, nifanyeje?

Kinacho niuma zaidi siwezi
kuzuia mawasiliano yao coz ni baba wa mtoto japo anasema hana uhusiano
naye tena. Kiukweli najenga picha mbaya kichwani akiwa huko Chuoni sijui
kinachoendelea.


Naomba msaada wa kimawazo nifanyeje. ASANTE!


************


Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, ahsante na shukurani kwa ushirikiano.


Anasingizia utoto, angekuwa mtoto asingechanua miguu kwa Mume wa mtu na Baba wa watoto 3, angelala na kijana mwenye umri unaofanana na wake. Alijua alichokuwa akikifanya. Tangu hukuwa nae kipindi hicho, achana na hilo!

Natambua itakuwa ngumu sana kwako kuwa na amani Moyoni kila wakati Mwanamama huyo anapokuwa Chuoni na "baba mtoto" wake. Watu waliokwisha onana wakiwa Uchi (Exes) achilia mbali ku-share mtoto ni ngumu kuaminika wakiwa peke yao.


Mbaya zaidi huna nguvu kwenye maisha ya huyo Mdada kwasababu uhusiano wenu sio rasmi hivyo huwezi kumshauri/shawishi ahame Chuo ili awe mbali na Baba mtoto wake wala ku-demand mipaka kati yake na Ex wake.


Kama kweli unampenda na unataka ku-share maisha yako nae + mwanae basi anza kuweka "msingi" serious wa uhusiano wenu sasa huku ukiungulia maumivu ya kutomuamini anapokuwa na Ex wake na mtoto wao mbali ya macho yako.


Uhusiano ukikomaa angalau utakuwa na sauti au nguvu ya kumuwekea Mipaka mpenzi wako kuhusu Mawasiliano na Ex wake.


Kwasasa huyo Mdada anasoma which means hana kipato na hivyo hawezi kumtunza mtoto hali inayopelekea yeye kumtegemea huyo Mume wa mtu.

Usijemharibia "utaratibu" wa kujikimu alafu ukaja muacha huko baadae ateseke na mwanae akiwa mwanafunzi (hana kipato).

Kwenye Matunzo ya mtoto kunaweza kukatwa ikiwa wewe utakubali kumhudumia mtoto kipindi ambacho mama yake hana kazi....utakuwa umejipatia "ready made family"


Kwa upande mwingine itakuwa nzuri kipindi hiki mtoto bado mdogo sana so utakuwa kama umemuasili mwanae na hivyo kum-cut off baba yake (akikua mtamwambia ukweli).

Ila kumbuka kuwa kufanya uhusiano na mwanamke mwenye mtoto na mwenye connection ya karibu na Ex wake kama huyo wako ni ngumu sana, maisha yako yote yatakuwa ya wasiwasi na hofu kila wakati Baba mtoto anapotaka kumuona mwanae au mtoto (akikua) anataka kumuona Baba yake.

Weka "nampenda sana" na "viapo na ahadi zako kukusuta" pembeni kwanza halafu kaa chini na jiulize tena, katika umri wako ambao ni chini ya miaka 35, upo tayari kweli kulea mtoto wa mwanaume mwenzio?


Je, kweli gharama hizo za maisha (mtoto ni gharama) ndizo ulizokuwa ukizihitaji mara tu baada ya kuanza kazi au ni muhimu kujipa Muda, kujijenga alafu ndio Utafute Mwenza?


Fanya uamuzi kulingana na majibu yako.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Pale Mume anapoweka Password kwenye Simu yake....

Hi Dinah,
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kazi nzuri. Mie binafsi blog yako imenibamba kweli na imenitowa kimasomaso kwa mambo mengi.


Nimepata elimu na nimnefurahia sana.
Mpendwa naomba kuuliza! Mie ni mwanamke mwenye Ndoa ya miaka Sita. Tulipo oana na mume wangu mwaka wa kwanza wa Ndoa yetu tulikuwa tunakaa Mikoa mbalimbali, yeye akikaa Lindi na mie Dar kwa sababu za kikazi.

Mungu alijalia mwaka wa pili akapata kazi Dar akahamia Dar, tuliishi vizuri na sikuwa na wasiwasi naye maanake niliona kama mwanzo wa maisha mapya kwa pamoja tukiwa chini ya dali moja.

Baada ya miezi kama Sita hivi mume wangu alibadilika na style yake ya maisha ikabadilika ikiwa hata marafiki. Hapo ndipo nilipo anza kutafuta kushika simu yake ili kujua kinachoendelea.

Duh amakweli usilolijua nikama usiku wa giza, nilipoanza kushika simu yake nilikuta ni kiwembe cha kutupa! Alikuwa na mademu wasiopungua 10 wengine amewasave kwa majina ya magari, hotels na kwa majina ya marafiki zake wa kiume.


Dinah niliunia sana nikakaa chini nikaongea naye nikamwambia madhara ya Umalaya ni nini? athali zake kwa watoto wetu akasema atajirekebisha.

Nikampatia muda akabadilisha namba kwa malengo ya kupoteza mawasiliano na wao, ila baada ya muda mfupi hali ile ilijirudia.

Kweli nilipitia kipindi kigumu sana kwa miaka yote hiyo. Mwaka jana nikamwambia kama simfai mie naondika na watoto wetu 2 ili yeye afaidi maisha anayoyataka .

Akapiga magoti akalia akaomba msamaha akasema ni company mbaya za shetani akaahidi ku cut-off marafiki na kubadilika kwa mambo yote niliyo mweleza.

Nikampatia nafasi aniambie kama kuna mapungufu kwangu aniambie nijirekebishe akasema tatizo ni yeye na nimpe muda.


Hivi sasa simu zake zote ameweka password, Airtel na Tigo na ameongeza line nyingine ya Airtel sasa dinah sina amani na simuamini kwani amekosa uaminifu kwa muda mlefu.


Nashindwa elewa kama ana-improve makosa yake kwa sababu ya password kwenye simu na naomba nielimishwe kuhusu matumizi ya simu ya mwenza ni mwiko kushika?


Au anafanya hivyo ili nisione kinachoendelea? Naipenda Ndoa yangu na na muomba sana Mungu anisaidie. Sipendi Talaka na kuachana imani yangu ya Dini hainiruhusu.

Nahitaji elimu jinsi ya ku- overcome haya maumivu na stress.
Natanguliza shukrani.

************


Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.


Sometimes watu wanamsingizia Shetani! Hapo Shetani hausiki kabisa ni yeye mwenyewe amejiachia kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe.


Sasa hapa mie ndio huwa napata Hasira!!! Mumeo ni Malaya na umethibitisha lakini hutaki kuachana nae bali unataka to overcome Maumivu na stress za Umalaya wake. MWANAMKE mwenzangu!!!! Kweli?!! Kivipi(maana mie sijui)?


Kama Dini yako hairuhusu basi Sheria inaruhusu mkimama....Miaka Sita ya Kunyanyaswa Kihisia, Kimapenzi, Kimwili na Kisaikolojia juu ya Umalaya wa Mumeo kwenye ndoa haijakutosha tu....usije zeeka au kufa bila kujua nini raha ya Maisha.


Huwezi ku-overcome Umalaya wa mtu kwa kuendelea kuishi nae na kumuacha aendeleze Umalaya wake na kum-treat as if wewe ndio mwenye Makosa!


Huyo ni mumeo, sio boyfriend....baada ya kugundua Usaliti wake ungemuweka Chini ukiwa firm (sio unalia-lia), ungempa msimamo wako kwenye Ndoa yenu na unge-Demand kupima afya zenu na mabadiliko ya kudumu haraka sana or else!! Hakuna kumpa Muda.


Kama kweli anakupenda na anaitaka Ndoa basi angekuomba msamaha na angebadilisha tabia yake, SIO kubadilisha namba ya Simu na kuweka password.

Huyo mumeo hafai, hakuheshimu, hakuthamini na wala hakupendi.....yupo na wewe possibly kwasababu ya watoto au mambo mengine lakini sio Mapenzi.


Watu wanakaa kwenye Ndoa kwa sababu za Kikazi (status), wengine kwasaabu ya Miradi n.k.


Sasa usijedhania unapendwa sana na mumeo pale anaposhupaa na kulia kabisa usimuache....usikute analilia "mkate" kwamba Kazi yake inamlazimisha awe na Mke (kazi nyingi za serikalini).


Kuhusu Mumeo kuwa na line nyingi za Simu na kuweka "kiingilio" cha siri ni wazi kuwa anakuficha Mengi ambayo anajua ukiyajua basi utamkimbia.


Unapaswa kuhoji kwanini hasa anakuwa na line nyingi za Simu na kwanini anaweka "neno la siri"?....ni mumeo na unahaki ya kujua kila akifanyacho....hii ni 2014 sio 1994!!


Wengine huweka "neno la Siri" ili simu zao zisitumiwe na watu wengine hasa Makazini, wanaweza kuiba details za kibiashara au hata Picha binafsi na kuzisambaza Mitandaoni.


Hii isikupe matumaini, tayari unajua Mumeo ni Mshenzi hivyo uaminifu haupo so ni vema kupata ukweli kutoka kwake.

Kwa kawaida hakuna mipaka kati ya Mume na Mke linapokuja suala la simu ya Mkononi, kama mna-share kila kitu kama familia kwanini simu ya Mkononi iwe tofauti?!!

Tatizo lako ni kwamba humuamini tena Mumeo na kama hakuna Uaminifu kwenye Ndoa ni wazi hakutakuwa na Amani.

Mumeo anahitaji kubadilika na kukuhakikishia kuwa kabadilika kwa vitendo ili akusaidie kurudisha hali ya kumuamini tena.

Lakini Mumeo hawezi kubadilika ikiwa unam-treat unavyom-treat sasa(kutokana na maelezo yako).....anafanya atakavyo kisha anaomba msamaha....anapewa muda....anarudia tena mzunguuko uleule.

Nasikitika kuwa sina mbinu ya kukushauri ili ku-overcome Umalaya ya mumeo ambao ni very active.....kwamba sio alifanya miaka 2 iliyopita bali nafanya sasa hivi.
Labda wasomaji wasaidie.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Mwaka kama wapenzi(online) ila hataki tuonane.

Am sorry dada dinah nina mpenzi kwa mwaka na nusu tangu tuwe kwenye mahusiano lakini hatujawahi kuonana.







Mpenzi huyu nilimpata kwenye Mtandao flani. Shida inakuja kwenye kuonana, hivi kwanini hataki niende kwake kwa suprise.





Hebu nisaidie je ni mtu mwema kweli?







Dinah anasema: no bother Mrembo, ahsante kwa Ushirikiano.





Sasa mdogo wangu humjui huyo mtu, hujawahi kumuona zaidi ya maandishi, simu na labda Picha....Kitu gani kinakufanya utake kum surprise nyumbani kwake? Akikubaka au kukuchinja je??!!







Mtu wa mtandaoni anaweza kuwa anybody kuanzia mtu genuine mwema tu Muuaji sugu.









Logically unapokutana na mtu Mtandaoni na kuanzisha uhusiano au kudhani mnauhusiano na kuitana majina matamu (ya kimapenzi) unashauriwa kuonana nae ana kwa ana mahali ambapo kuna kadamnasi ya Watu.











Hupaswi kukubali kwenda nae hotelini, guest au kwako/kwake ukiwa peke yako. Hakikisha unapokwenda kukutana nae watu wako wanajua na kama inawezekana wajue ni wapi hasa unaenda ili kuepusha Mauaji au Ubakaji.









Watu wa Mtandaoni wengi wao (Wake kwa Waume) huwa ama waongo au kuna walakini kwenye Utambulisho wao, kwamba maisha yao ya "online" ni tofauti na maisha yao halisia.







Siwezi kusema huyo bwana ni Muuaji au Mbakaji, ila nadhani atakuwa ama kwenye uhusiano au hataki kuwa na wewe kama mpenzi ila anafurahia ku-flirt tu na wewe.







Mapenzi ya Mtandaoni ku- pass time hasa kama ana issue na Mpenzi wake.







Kuna wengine hu-pretend kuwa wanaume/wanawake ili kuendesha maisha yao ya Mtandaoni.....ni tatizo la akili na linajina lake (nimelisahau).







Sasa mtu kama huyo hatokubali uonane nae, achilia mbali kum-surprise nyumbani kwake!!!









Nikijibu swali lako: Siwezi sema kama ni mwema au sio Mwema, ila nadhani hana mpango na wewe in real life, anafurahi na wewe kimtandaoni tu.









Natumai maelezo yangu ambayo hujayaomba(nimehisi kuwa responsible kukueleza) yatakusaidia kupanua upeo wako kuhusu Maisha ya Mtandaoni.



Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Haonyeshi kuumia baada ya kumuacha...

Habari dada dinah, pole na kazi pia hongera kwa kuelimisha
jamii.


Nimekua nikifatilia sana blog hii na kujifunza mengi, ila leo na
mie yamenikuta
(kabla ya yote kwanza naomba ulihifadhi jina langu).

Mimi ni Kijana wa Kiume mwenye miaka 22 nilivyoanza
chuo mwaka jana nilikutana na Msichana ambaye sijawahi ona!! inshort
nikampenda na nilichukua muda kumchunguza kama anatabia nzuri na
nikagundua kua anatabia nzuri na anafaa.


Tukaanza mahusiano ya kimapenzi na huu ni mwezi wa Sita ila
hatujawahi kufanya Ngono kwa sababu huwa anaogopa sana kwasababu hajawahi kuguswa.

Nimevumilia yote lakini sasa akaanza kuonyesha kutokunijali kama
mwanzo na hanitreat kama mpenzi ila kama rafiki nimemwambia
abadilike mara nyingi lakini hanielewi.


Mara ya mwisho wiki iliyopta
nikamuuliza mbona unanipa mapenzi nusu nusu akanambia kwasababu
haniamini! Nilishangaa coz najua anauhakika asilimia mia kua yupo peke
yake akaongea na mengine mengi yakuniudhi.

Some time anaenda kwa marafiki
zangu anakaa mpaka masaa mawili huko...pia fb na whatsapp
anachat muda mwingi na hufanya hivyo wakati nikiwa nae.

Kiukweli heshima yangu hanipi kama
mwanzo tena, sasa nimeamua kumuacha ili nipunguze hizi stress na maumivu coz nampenda mpaka nimepitiliza.

Tangu nimemuacha haonyeshi dalili za
kuumia wala kujali wakati mimi nazidi kuumia. Hii ni mara ya pili kumbuka niliamua kumwacha baada ya kuchoshwa na stress zake ila nampenda na natamani
hata arudi tena tuendelee na mapenzi. Nifanyaje???


Dinah anasema: Salama kabisan ahsante na shukurani kwa ushirikiano.

Dogo una asili ya u control freak eti! Kabla hujaanza uhusiano ukamchunguza kwanza, uliporidhika ndio ukaanzisha uhusiano nae.....ndani ya Miezi sita una demand msichana afanye mambo ka' Mkeo na umemuacha mara Mbili in 6months kwasababu hafanyi utakayo.

Unataka akuheshimu vipi? Ikiwa hakutukani mbele za watu au kukukebehi mbele ya ndugu, jamaa na marafiki as Gf atakuwa anakuheshimu....au unataka asikae na rafiki zako au asi-chat na rafiki zake kwenye Mitandao?


Ikiwa wewe unamiaka 22 ni wazi yeye ataluwa hivyo au mdogo zaidi, katika hali halisi Wasichana wadogo ndivyo walivyo....bado anajitambua, anajifunza mambo kama Binti anaeelekea kuwa Mwanamke, anapenda kuzungumza na marafiki na kujenga uzoefu na watu mbali mbali.


Nadhani ama umeaninishwa mambo kuhusu mahusiano ya kimapenzi ambayo ni tofauti na hali halisi ya Maisha au umejiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi bila kujua uhusiano wa kimapenzi ni nini hasa!


Huwezi kumtawala Binti wa watu kwa jinsi ulivyoelezea na yeye kuendelea kutaka kuwa na wewe kama Mpenzi wake.....inawezekana hapendezwi na tabia yako ndio maana ameamua akufanye uwe rafiki tu.

Nadhani timing ya wewe kumuacha ilikuwa mbaya, umemuacha wakati yeye tayari alikuwa kakuweka kwenye "friends zone" hivyo hakupata au hapati maumivu ya kuachwa kama mpenzi(hana habari).


Kama kweli unampenda na unapenda akurudie basi ni vema kubadilika kwanza halafu ndio ujaribu kumshawishi tena kwa kuomba msamaha na kumhakikishia kuwa hutokuwa ukimtawala.

Akikubali kurudiana na wewe unatakiwa ku-relax na kumuacha awe huru kuzungumza na wenzake iwe mitandaoni au vinginevyo ailimradi tu havuki mipaka.

Akikataa basi nadhani ni vema umuache aendelee kuwa yeye na kujifunza who she is kama msichana na wewe zingatia Masomo na huko Mbele utakutana na mwingine na kuanzisha uhusiano mwingine.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Mpenzi haniamini, nifanyeje....

Habari Dada Dinah,

Naomba ushauri wako nifanye nini katika hili! Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 na nina mpenzi ambae tumetokea kupendana sana kwa muda wa mwaka mmoja sasa.


Niseme tu ananipenda nami nampenda sana katika swala la tabia sio muhuni kabisa! Niko free na simu yake muda wote ni msikivu na tumepanga kufanya mambo mengi sana.


Tatizo kubwa lililopo hajiamini hata kidogo kutokana na historia ya
mahusiano aliyokuwa nayo huko nyuma kwani alitendwa sana.

Nimejaribu kumuweka chini na kumuelewesha na kujaribu njia mbali mbali za kumfanya awe na amani na mimi lakini naona bado tatizo liko pale pale, kiasi kwamba nakosa raha kabisa.

Mfano naweza chukua simu yangu labda nikamjibu Dada angu msg yeye anakasirika kiasi cha kupoteza maelewano kwa muda wa dakika kadhaa! Hili linanifanya mpaka nikiwa nae niweke simu mbali kwa kuhofia kutoelewana.

Dada Dinah tafadhali nisaidie katika hili sitamani kumpoteza na mimi
wala sio muhuni kabisa, akitaka simu yangu anapata muda wote tatizo bado
haniamini.


Anasema hawezi muamini mwanamke katika maisha yake! kauli hii huwa inanisononesha sana mpaka kuna muda nafikiria kuachana nae.


**********

Dinah anasema: Habari ni nzuri sana, ahsante na shukurani kwa ushirikiano.


Bila shaka kutendwa huwa kunampotezea mtu hali ya kuamini tena na humchukua mhusika muda mrefu sana (inategemea na mtu).

Wengi huwa hawajiingizi kwenye Mahusiano ya kimapenzi mpaka watakaporudisha hali ya kuamini mwanamke/mwanaume tena.

Baadhi hujiingiza kwenye mahusiano tena wakitegemea wapenzi wao kuwarudishia hali ya kuamini kwavile wanahisi wao peke yao hawawezi. Huyu mpenzi wako inawezekana kabisa ni mmoja wao.


Ni vema amekuwa wazi kwako kwa kusema kuwa hatomuamini tena mwanamke hivyo kama unampenda kweli na hutaki kumpoteza basi ajira ndio hiyo, fanya yote ambayo unadhani yatamrudishia hali ya kuamini tena, na zaidi kukuamini wewe.

Unajua unapokuwa na Mpenzi mpya mara zote unakuwa hujui Uzoefu wake hivyo unajaribu "kumfanya" asahau alikotoka incase aliepita alikuwa "Mkali" kwa kuwa mbunifu au kufanya mambo ambayo unadhani hajawahi kufanyiwa au kama aliwahi kufanyiwa basi sio kama unavyofanya wewe....yaani unaweka "Ustadi" wa hali ya juu ili apagawe!

Unabadilisha ufanyaji mpaka siku aseme "sijawahi kupata uzoefu huu" au "ktk maisha yangu hakuna aliewahi kunifanyia hivi" au "duh wee ni kiboko".....ukipata hiyo ndio unaanza kupunguza speed na kumpa mambo makali once a week au mwezi(inategemea na ujisikiavyo)....


Sasa basi hata kwenye kumrudishia mwanaume hali ya kuamini na kukuamini wewe unapaswa kutumia mbinu kama hivyo.....badala ya matendo kingono, fanya kitabia, onyesha kumjali, mshirikishe, onyesha kuwa unajivunia yeye unapokuwa na watu wengine, toka nae na uonyeshe affection kwake....sio lambanana ndimi na sura bali unaweza tu kumshika mkono, bega au kumpa nusu kumbato huku mnatembea, kaa nae 0-destance mnapokuwa nje n.k.


Punguza au acha mazoea yasiyo ya lazima na Wanaume(rafiki zake wakiwemo) via Simu au Mitandao ya Kijamii.


Pia tambua kuwa baadhi ya wanaume ni sensitive na wanaweza kuwa emotional at times(sio Ushoga) ndivyo walivyo tu. Wanaume kama hawa wakitendwa huwa wanahitaji kuhakikishiwa kuwa unawapenda, hutowatenda kamwe, uaminifu wako kwao n.k.

Yaani mara kwa mara wanahitaji kuwa reassured japo hawasemi, sasa tangu unajua tatizo liko wapi Mrembo jaribu niliyosema alafu uone kama kutakuwa na mabadiliko.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Penzi kwa Simu, Nikimuona Penzi Nywiii...

Habari dada dinah, natumai umzima na pole na kazi. Kwanza napenda kukupongeza kwa hii blog yako kwa kweli tunafaidika sana na tunajifunza mengi kutoka kwako nakupenda sana.


Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 naishi Dubai. Nimepata Mchumba ana umri wa miaka 37 na kakubalika nyumbani na tuko kwenye harakati za kufunga Ndoa.


Kwakweli huyu bwana ananipenda sana kupita kiasi . Ananijali na kunithamini na kuniongoza katika kila jambo na kunishauri mambo yake yote kuhusu maisha yake na kwa kila kitu kiasi ambacho kanisubiri muda wa Miaka mitano ili nimalize masomo ili anioe.

Kwakweli miaka yote hatuna tabia ya kutoka pamoja wala kuonana ila nimazungumzo kwenye simu tu kwa muda wa miaka miwili.

Anakuja kwetu kawaida na mie kwakweli namempenda huyu kwa jinsi anavyonipenda na kunijali na navutiwa naye sana nikiwa naongea kwa simu kiasi ambacho siwezi kukaa siku bila kuongea nae na siwezi kufanya jambo bila kumshauri yeye tu.


Lakini cha kunishangaza akija kwetu kuonana na mie Moyo wangu unabadilika nahisi kuwa kama sijampendaa huyu mtu!

Naomba usinielewe vibaya dada dinah kusema kweli dada dinah nikikaa nikifikiria kiakili nahisi  sijaimpenda sura yake kwakweli na kwajinsi nilivyo huwa inanijia kama tukitoka wote itakuwa vipi?


Ila moyoni nampenda sana na siwezi kumkosa kabisa. Kwakweli dada dinah nahisi nachanganyikiwa sijui nijiamulie vipi niufate moyo wangu au akili yangu?

Naogopa sana ikaja ikawa tatizo kwenye ndoa yangu na kutompa furaha anayoitarajia au je hili halitokuwa tatizo nikioana nae kwa vile Moyoni nampenda ntakuja kumpenda na kutojali sura yake.


Naombaa unisaidie dadaa dinah, nakupenda sana. Asante sana.


*********


Dinah anasema: Habari ni njema tu Mrembo, ahsante. Aah! Nakupenda pia kwa kunipenda sana.....shukurani kwa ushirikiano.

Hapo ni Je, kufuata Moyo wako au Macho yako?....Akili haihusiki.


Binaadamu tupo tofauti na tunapendezwa na mambo tofauti na wakati mwingine pia umuhimu wa vitu/mambo maishani ni tofauti.

Kuna ambao hawajali sura ya mtu bali tabia, wapo wanajali Mali/Pesa tu....wengine hujali Umbo zuri sio sura wala tabia, wachache hujali Umaarufu/mtindo wa Maisha....alafu kuna wengine ka' Dinah hapa ambapo vyote ni muhimu isipokuwa Umaarufu/Pesa/Mali!


Kama unahisi Sura yake inabadilisha upendo ulionao kutoka Mpenzi kuwa jamaa tu wa kushauriana nae basi ni vema kutafuta namna ya Kuizoea sura yake.

Kwa maana kwamba tumia muda wako mwingi kuongea nae ana kwa ana, tokeni pamoja na mfanye mambo pamoja mara kadhaa kwa Wiki halafu uone kama utaendelea kumuona "mbaya".

Kama baada ya mwezi, miezi 3 bado unajisikia kutokumpenda kila unapomuona basi ujue kuwa humpendi kweli bali unapenda Msimamo wake kimaisha, unapenda anavyozungumza na wewe, unapenda anavyoshauriana na wewe, unavutiwa na sauti yake n.k.


Yeye kukusubiri wewe kwa Miaka Mitano ili umalize Masomo ilikuwa Choice yake wala usihisi Hatia kabisa na wala isikusukume kwenda kufunga Ndoa nae ambapo unajua wazi hautokuwa na furaha kila ukimuona (yeye na sura yake).


Ndoa sio "kitu" cha kuingia na kutoka kama unavyotaka.....kama haupo tayari ni vema kusubiri kuliko kuingia kwa ajili ya sababu nyingine na sio Mapenzi.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Sina raha na Ndoa Yangu!

Hi, dada Dinah,
Hongera kwa kazi nzuri ya kuelimisha watu mbalimbali hususani juu ya suala la mahusiano au love affairs.


Mimi ni mmoja kati ya wadau wa blogu yako. Nimekuwa nikisoma na kujielimisha mengi yahusuyo love na relations kupitia ushauri unaotoa kwa wengine.


Unfortunately, leo nami nimejikuta naingia katika orodha ya watu uliowashauri kutokana na ishu ambayo imekuwa ikiniumiza kichwa katika ndoa yangu. Ishu yenyewe iko hivi:


Umri wangu ni 26 years, niimeoa mwaka mmoja na miezi nane iliyopita, Mwaka wa kwanza wa masomo yangu ya Chuo. Mke wangu ana miaka 24 sasa.


Kabla ya kuoana, tulikuwa tukifanya mawasiliano nae tangu niko form 5 na tukakubaliana ya kwamba tusubiri mpaka nimalize masomo yangu. Kutokana na utaratibu wa Dini, hatukuweza kuingiliana kimwili ingawa na admit kwamba mara kadhaa tumewahi kufanya romance ambayo ni kutokana na msimamo wake tuliweza kutoingiliana.

Nilikubali matokeo na kuvumilia. Sometimes she used to call me na kuniambia anahitaji tukutane kimwili but when tukiwa wawili tu akawa anataka tufanye tu romance kwani anaogopa kupoteza Usichana wake kabla ya ndoa. I agreed with her and let things go.

Hali yangu ya kiuchumi haiko sawa coz i had no Kipato cha maana sana kama Mwanafunzi wa Chuo, ishu ya Ndoa ilileta hali ya kutoelewana katika familia yao lakini akashikiria msimamo wake kwa kuwa alinipenda mno. Upande wa familia yangu was ready to support me mpaka namaliza Chuo.

Siku ya kwanza tukiwa katika honeymoon. Akaanza kulia na kunambia hayupo tayari kukutana nami kimwili. Niliumia mno. Mara akadai anaogopa kuitoa Bikra yake. Mara akadai kuwa dada yake hajaridhika na Ndoa yake.


Nikajitahidi kumliwaza na kumbembeleza sana asiwaze kuhusu ndugu zake coz maisha yashakuwa ni yetu wawili sasa hivyo ajali maisha yetu tu. Hakunielewa. Nilihisi ni njozi tu. Nikajipa moyo na kujaribu kumsahaulisha.


Nilipoona kaanza kuwa normal tukaendelea, mara baada ya tendo lile nikawa na kibarua cha kumliwaza tena.

Kwa ajabu akaanza kunambia kuwa haitaji tena kuwa nami na akawa anadai Talaka yake. Nilidhani ni masihara tu, kumbe she was seriuos. Akawa anajibu ovyo na kwa mkato. I was geting hungry. I slaped her once.

Toka siku hiyo Ndoa yangu ikaanza kupoteza mvuto na thamani. Hakutaka tukutane kimwili akidai anajiskia maumivu. Nikakubali kuvumilia but life yangu ilianza kuyumba slowly chuoni.


I decided to pospone my studies without informing my guardians. She did not want to hear kila ninachomuelekeza. Ujeuri ukawa ndio silaha yake kubwa. Niliumia mno.

Sometimes nilijaribu kuwaeleza ndugu zake ambao pamoja na kumkanya lakini niliona dalili za kumsapoti kwa kile anachokifanya. Nilizidi kuumia.


Mpaka hivi sasa, maelewano yetu si mazuri ingawa tukiwa nje watu wanaweza kusema tunapendana. Imefikia wakati hatuongei siku nzima. Dah!


Sawa na kipato changu cha Uanafunzi bado nimekuwa nikiacha pesa ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya ziada coz mahitaji muhimu yote yapo, but wakati mwingine nakuta pesa imetumika kwa jambo lisilo na maana. Nikiuliza naamiwa 'mwanaume nina gubu unaulizia hadi chenji?' Sipaswi kuuliza pesa imetumikaje.


Maisha yamekuwa ni ya kununiana, kujibiana mkato mpaka inafikia muda sioni mapenzi kabisa. Sioni faida ya Ndoa tena.


Nikimuelekeza asifanye jambo fulani baya leo, kesho anarudia. Anaomba samahani then anaendelea kulifanya. Hana heshima kwangu kama mumewe no matter what i am trying to be.


Hivi sasa nimepanga nihamie hosteli za Chuo mara baada ya Masomo kuanza then nimrudishe kwao akapumzike au nimpeleke kijijini kwetu akakae mpaka nimalize masomo kwanza.


Nahisi ataniharibia future yangu na ya familia yangu ingawa bado hatujafanikiwa kupata mtoto.Nahitaji kuwa free ili nipange life yangu upya.


Nahitaji ushauri wako juu ya nini cha kufanya kabla sijachukua maamuzi mengine ambayo yanaweza kumkwaza yeye na famila yao.

Nimechoka kuishi maisha yasiyo na muelekeo mzuri. Please, dada ushauri wako ni muhimu mno kwangu.

************


Dinah anasema: Hello! Ahsante sana na shukurani kwa ushirikiano.


Muhimu: Kutokana na tabia za kitoto na kibinafsi za Mkeo usifikirie kabisa kuahirisha (tena) au kuacha Masomo kwa ajili yake. Unaweza kuacha mengine kwa ajili yake lakini sio hilo.

Hapo ulipompiga kibao Mkeo pameniudhi kweli, najua kuna maudhi yanakufanya utake kumdunda mtu(mke/mume).....sipendi watu wanaopiga wenzao bila kujali Kosa ni kubwa kiasi gani! Ni vema kujifunza kuzuia hasira zako Kichwani, usiziache zishuke "mikononi" na kufanya uharibifu!!

Kutokana na maelezo yako inaonyesha ama Mkeo hakuwa tayari kuolewa na wewe ukiwa Mwanafunzi, labda alitegemea mkifunga Ndoa utaacha Masomo na ufanye kazi (uwe na Kipato Kizuri)....possibility ni kubwa anafanya Visa na Vituko akitaka kufikisha ujumbe. Hilo moja.

Pili, inaonyesha ama huko kwao wanapenda kuolewa na watu wa "aina na kipato fulani" na Dada mtu ndio kinara (tumuite Control freak) anatumiwa "kuharibu".


Pia huyo Dada mtu(shemeji yako)inawezekana ama ana wivu (kama hajaolewa/kaachika).....maana wakati mwingine Adui mkuu anaweza kabisa akawa Ndugu yako wa Damu.....sema ile "sisi damu moja hatuwezi gombana" huwa inaficha ukweli wa mambo kuonekana.

Hapo kwenye "uaduia wa ndugu" hata wewe Mume hutokuwa na namna ya kumfanya mkeo aone Uadui wa ndugu yake kwake kwasababu utaonekana wewe "mtu wa nje" unataka kuwaharibia Undugu wao, wanajuana na wameishi wote kwa miaka!, wewe umeishi na Mkeo kwa Mwaka na Nusu tu(vichwani mwao)....MUHIMU ni kumuacha yeye mwenyewe aje kugundua with time.(Usiwaingilie).


Nini cha kufanya:

1-Acha tabia ya kumuambia au kumueleza, kumbuka huyo sio Mtoto, sio Mdogo wako na sio Mwanao!


Jaribu kuwasiliana nae kwa kuzungumza nae. Mpe nafasi ya kujieleza na wewe usikilize....hoji kwa upendo nini hasa tatizo linalipolekea yeye kununa na kususa?


Mjipe nafasi ya kila mmoja wenu kumueleza mwenzio jinsi anavyojisikia....kwa mabaya na mazuri. Kitu gani kifanyike ili wote kwa pamoja muishi maisha ya amani na furaha bila mikwaruzano ya mara kwa mara kama Wanandoa?

Zungumzeni kama ninyi na sio "wewe", "mimi"......kumbuka kutokurudia issue ya Fungate na yeye kuomba Talaka (nadhani alilopoka tu kutokana na maumivu).

Zingatia issues za kununiana, kutowasiliana, kujibizana kwa ujeuri, kuitana majina mabaya...(wacha kuulizia pesa zimetumikaje....unless ulikuwa na shida nazo).


Vyovyote utakavyoongea na mkeo kumbuka kusisitiza Mapenzi yako kwake, umuhimu wake kwako na kwenye Ndoa yenu kama Familia.


2-Usihamie Hostel kwani kutakuongezea gharama, huyo ni Mkeo na kama huna mpango wa kumtaliki basi mpeleke kwenu (umemuoa ni wa kwenu sio kwao....."Mke ataacha kwao aende kwa Mumewe").

Lakini kama umefanya yote na hakuna mabadiliko na unadhani mapumziko a.k.a "trial" Talaka au "separation" itamfanya abadilike au ku-rethink basi mrudishe kwako kwa muda maalum.

Nadhani kabla ya yote niliyoyasema kuna taratibu Kidini na Kisheria(mmefunga Bomani), inategemea Mmefunga Ndoa wapi au chini ya Imani gani?.....sio lazima kuyafuata kwa mtiririko lakini ni vema kuzingatia kulingana na Maagizo ya Ndoa yenu chini ya Imani zenu.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

"Hanitamani" sababu ya ku-Flirt Mitandaoni...

Habari dada, mimi ni kijana wa kiume na nina umri wa miaka 30 nina mke wa miaka 28 na mtoto wa miaka 3.


Kwenye ndoa yetu na Mke wangu kuna vitu vya hapa na pale ambavyo vinaniumiza kichwa kutoka kwa mwenzangu ambavyo ni; mara nyingi sana mimi ndiye naomba kufanya nae mapenzi sikumbuki mara ya mwisho ni lini yeye amenianza.

Mara nyingine tunakaa mpaka mwezi mzima kila nikimwomba anasema hajisikii, pia mara nyingi sana tukifanya mapenzi Uke unakuwa mkavu matayarisho tunayafanya ya kutosha tu.

Mke wangu anapenda sana kuchat kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba nishawahi kufumania mpaka chat za kimapenzi akaniomba msamaha!!

Nina mpenda Mke wangu naomba msaada kutatua hayo mambo.


***********


Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, ahsante! Shukurani kwa ushirikiano.


Hivi mpaka karne hii mtu na mkewe wanaombana kufanya mapenzi? Kumuomba mpenzi wako kufanya mapenzi huoni inaweza kukata "stimu" eti? (Labda ni mimi tu).

Si wanawake wote wanapenda kuombwa tendo, wengi hupenda iwe spontaneously....kwamba yupo jikoni, unamnyemelea kwa nyuma kisha unaaza kunshika maeneo apendayo ambayo yatamfanya ajisikie kupendwa na nyege at the same time...kwa mfano:

Au mpo chumbani kisha unamnyanyua na kumuweka kitandani kisha unaufanyia mwili wake "shughuli" ili ajihisi kupendwa, kuvutia na wakati huohuo Nyege na mengineyo....sio "mama Kadala nipe haki yangu"....au "mke wangu naomba basi leo" n.k.

Pia ni vema utambue kuwa sio wote wenye kupenda "kulianzisha", hii ni kutokana na kuaminishwa kuwa mwanamke kumuanza mwanaume kitandani ni Umalaya* lazma Mwanaume akuanze kisha mwanamke kutoa ushirikiano (inategemea na Mazingira aliyokulia).

Ikiwa unapenda Mkeo "alianzishe" basi ni vema kuzungumza nae na kumwambia "najisikia kupendwa ikiwa mke wangu unaonyesha kunitaka kingono, unanipa dalili kuwa unanihitaji kimwili"....kwa mfano!

Nadhani kuna uwezekano Mkeo alikuwa ana-cheat kihisia (hashiriki kimwili) na hao anaochat nao lakini kitendo cha kuchat maswala ya kimapenzi/ngono (flirtation) kunaweza kumfanya Mtu akose hamu na Mume/Mke wake kwani yule au wale anaochat nao wanaonyesha kujua kumridhisha mwanamke/mwanaume kuliko Mume/Mke wake.

Hali hiyo hupelekea mhusika kutaka kufanyiwa yale anayoambiwa au chat about na watu hao lakini anashindwa kumuambia mwenza wake na hivyo anaishia kukukwepa.


Hali hiyo ikiendelea basi Mume/Mke hupoteza kabisa hamu/matamanio na mwenza wake na hivyo kutegemea kuridhika na chat za hao anao-flirt nao kwenye mitandao.

Baada ya kugundua kuwa ana-cheat (flirting online/via texts IS CHEATING) na yeye kuomba radhi, wewe kama Mumewe ulipaswa kuweka "rules" kwenye Uhusiano wenu au kumpiga marufuku kabisa kujihusisha na Mitandoa na aweke muda wake na attention yake kwenye maisha yake halisia ambayo ni familia yake(wewe na Mtoto).


Badilisha au boresha namna ya kumtaka mkeo kingono, badala ya kuomba....tumia vitendo kama nilivyogusia hapo awali.


Pia ni vema wewe na mkeo mkawa wazi kingono ili kila mmoja wenu aweze kumridhisha mwenzio bila kujali nani "kalianzisha"


Kufanya ampenzi sio Mshindano, sio Kazi, hivyo sio lazima yeye afanye jambo kwa vile wewe unafanya kila siku.....ukianza kulinganisha ni wazi utakuwa unachukulia suala zima la kufanya mapenzi kama Kazi au Mashindano.


Kwenye Ndoa/Uhusiano wenu kuna ukosefu wa Uaminifu, Ushirikiano na Mawasiliano.....ili msipoteze Ndoa yeni ni Muhimu mkaboresha hayo mapema.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Friday

Mimba ya Mume wa Mtu, Mama hanielewi.

Shikamoo Dada, pole na majukumu. Mimi in msichana mwenye umri wa miaka 22, naishi marekani na familia yangu nikimaanisha mama na ndugu Dada yangu. Nafanya kazi kama server kwenye restaurant maarufu hapa nchini.

Tatizo langu nilijishirikisha kwenye mapenzi na Boss wangu ambae pia ni mume wa MTU ni baba mwenye umri sawa na baba yangu japo muonekano wake na umri ni tofauti anaonekana mdogo.

Tokea tumeanza mapenzi ni muda usiopungua  miezi minane.  Familia hawakumkubali lakini kutokana na kuona ni furaha yangu ikabidi wajilazimishe hivyo hivyo. 

Wiki iliyopita nilikuwa naumwa hali iliyofika hadi kuhisi kizungu zungu na kutaka kuanguka kazini ndipo boyfriend wangu aliponipeleka Hospital, baada ya siku tatu nikaambiawa nina matatizo ya upungufu wa damu  nisipokuwa makini Anaemia inaninyemelea na kingine ni kwamba nina Ujauzito.

Hapo ndio nilipochanganyikiwa zaidi. Maana Mimba ni ya mume wa mtu japo mwenye yupo willing kuilea ila anahofia mkewe akijua sitakuwa na amani. Pili kuitoa huku inaruhusiwa kisheria ila anahofia nitaharibikiwa Kisaikolojia.


Ukija kwetu mama hajafurahia hata kidogo kwani miezi mitatu iliyopita Dada yangu alipata mimba hali iliofikia kutibuana na mama na kuamua kuhama nyumbani kwenda kwa bwana wake kwa maana alikataa kuitoa.

Sababu ikiwa ameshatoa mimba mbili kabla hivyo kuitoa ya sasa hataki kabisa. Hivyo kahama in kufanya mama kuchanganyikiwa na kunionya Mimi nisije nikafanya kama Dada yangu.


Hapa sasa hivi niko na mawazo mpaka nawaza mabaya. Kuitoa naogopa nitakufa ama kitu kibaya kitatokea. Pia nawaza kama nikiitoa Dada yangu akizaa nitazidi kuumia maana mtoto wake atakuwa ukumbusho wa kwangu.

Pia naanza Chuo Fall (September ) so kusoma na Ujauzito sijui kama nitaweza. Kiufupi Dada yangu nipo kwenye dimbwi la mawazo.

Dada yangu kaniambia nitulie kwanza na kufikiri nini nataka. Lakini still naona wazimu unataka kunijia. Silali vizuri, mama yangu haongei na Mimi. Ndipo nimeona  nikwandikie wewe labda msaada wako wa mawazo  unaweza kunikwamua katika hili dimbwi la mawazo.

nitafurahi kusikia majibu yako either kwa email au blog yako.

Ahsante.


************


Dinah anasema: Marhaba mrembo, pole kwa yote ila ungekuwa karibu ningekusema mpaka Mimba itoke....(Natania)! Ila kwanini? Jamani kwanini at 22 unachanyanga maisha yako kizembe hivyo?!!!

As if mume wa mtu haikutosha ku-mess up maisha yako, ukaamua kujiachia kabisa na kushika Mimba!! Mama hakukufundisha namna ya kujikinga dhidi ya Mimba?

Haijalishi muonekano wake wala umri wake, Mume wa mtu ni Mume wa mtu tu hukupaswa kumpanulia Miguu...end OFF!....well limetokea, let's deal with it.

Wewe sio Dada yako so option ya kutoa Mimba achana nayo na mimi sikushauri uitoe kwasababu siamini katika kutoa Mimba bali naamini katika kuzuia kushika Mimba.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa ulikuwa unataka kuzaa na mume wa mtu alikuwa easy target, hivyo hakuna cha "tulia uangalie unachokitaka".....unamtaka mtoto then keep him/her....utamtunzaje? Ulipaswa kujiuliza kabla hujafanya Ngono bila Kinga.

Kuna uwezekano mkubwa huyo Boss Mume wa Mtu boyfriend wako ama akakuachisha kazi ili kulinda Ndoa yake, kama alivyokuonya kuwa Mkewe akijua utakiona cha MTEMA KUNI. Hilo moja.

Pili, akasema yupo willing kumtunza mtoto, hiyo sio guarantee ya yeye kufanya hivyo bila mkewe kujua hivyo anaweza kuamua kukuchunia tu ili aendelee kulea familia yake.

Muhimu ni wewe mwenyewe ku-sort things out na Mama yako ili angalau uwe na mahali pa kuishi kwa Muda na ujiandae kuwa a single mother (kwa UK is a bonus maana single mother wanamisaada kibao kifedha hihihihihi sorry).

Kama nia ipo na umekamia unaweza kabisa kusoma ukiwa Mjamzito(kama mimba haitosumbua), lakini kama hujiamini kuweza kufanya hivo basi badilisha mipango na uanze shule Next Sept utakapo kuwa umejifungua (Mungu akijaalia).


Sasa mrembo fanya hivi; Umekwisha haribu na matokeo unayo, hakuna haja ya kuwaza na kuwazua ufanye nini (too late), Simama kama mwanamke na angalia mipango ya Chuoni ili ubadilishe mwaka/tarehe ya kuanza.

Angalia Mkataba wako wa kazi unakulinda vipi au unalinda vipi Wajawazito na Wazazi (waliojifungua)....soma Sheria za Kazi za hapo ulipo ili ukifukuzwa kazi uweze ku-sue Boss wako(sio bf) kuwa kakufukuza kazi kwa sababu ya Ujauzito....sijui US sheria zilivyo ila nadhani hazitofautiani sana na za hapa (UK).


Usimwambie mtu yeyote kuhusu mipango yako ya ku-sue ikitokea umefukuzwa kazi(iwe between mimi Dinah na wewe).

Nimejaribu kuwa mpole ili nisikufanye ujione mpweke, lakini nina hasira sana na wewe, zaidi ya Mama yako.


Kua mwanamke Imara, Soma, piga kazi, lea mwanao.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Nahisi Mume wangu ni Shoga...

Habari dada Dinah, hongera sana kwa kazi yako nzuri mno! nimekuwa nikisoma Blog yako siku zote na kuifurahia sana.


Leo nami naomba ushauri dada yangu.Mimi ni mama wa watoto watatu, nimefunga ndoa ya Kikatoliki mwaka wa 11 sasa.


Siku zote tumeishi vizuri na Mume wangu, makwaruzano ndani ya Ndoa hayakosekani ila siku hizi Mume wangu amebadilika sana kiasi cha kunifanya nipate mawazo mabaya juu yake.

Hakuwa na kawaida ya kujipulizia pafume ila ghafla ameanza kijipulizia hadi sehemu za siri!!Inaniogopesha sana.

Anatumia muda mwingi kwenye kioo! anavaa Macheni na Mapete makubwa makubwa! Nimejaribu kumuuliza sababu ya kufanya hivyo kawa mkali kama pilipili.


Dada yangu inawezekana akawa amejitumbukiza kwenye masuala ya Ushoga?


Na mwanaume akiwa Shoga anaweza ngonoka na Mkewe kama kawaida? nifanyeje kukomesha tabia hii ambayo inaninyima raha katika Ndoa yangu?


Pole kwa maswali marefu naomba unisaidie dada-Asante(tafadhali hifadhi jina langu).

**********

Dinah anasema: Habari ni njema, ahsante sana kwa ushirikiano.


Ulivyo-panic umenifanya nicheke ghafla!....Miaka 11 ni mingi kiasi. Je mnampeana attention ya kutosha kama wapenzi au mnamchukuliana kama Wazazi tu?

Mumeo ana umri gani kwani? Maana kuna baadhi ya wanaume wakifikia umri fulani 49+ huwa wanabadilika ghafla.

Kuna Makala moja ya Uchunguzi nilisoma mwaka jana wakazungumzia hilo na hitimisho lao lilikuwa sio Ushoga bali Mwanaume kuelekea kwenye "kikomo cha Hedhi" usishituke, sina neno lingine la kiswahili la "Menopause".

Mie nikabisha(as usual) kwa kusema kuwa mbona wanaume hawana Hedhi sasa "kikomo" kinaibukia wapi? Mpaka leo sijui na sikufuatilia tena.


Kuna umri fulani hufikia na watu kutamani au kutaka kujiamini tena kama walivyokuwa enzi zile kabla ya Ndoa na watoto, kwasababu walikuwa busy sana na majukumu ya "uzazi" sasa watoto wamekua na wao wanaamua kufurahia maisha yao.

Sasa mume wako kaamua kubadili Mtindo wa mavazi.....wengine huamua kufunga ndoa na mabinti wadogo, wengine kupunguza mwili, kurudi shule n.k ili kujiongozea hali ya kujiamini.

Mumeo ama hataki kuzeeka, kachoka kuonekana vilevile kwa miaka yote 11 au ame-miss attention aliyokuwa akiipata alipokuwa Kijana hivyo akivaa anavyovaa anazipata au alitegemea kupata....mf: wewe mwenyewe unampa attention japo sio nzuri (aliyotegemea ndio maana akawa mkali).


Nadhani ni vema kubadilisha uulizaji wako....badala ya kumkalipia, kumuita Shoga au kumkataza asivae anavyovaa kwavile anaonekana Fala. Pia ni vema kujipanga kwenye suala la Mavazi ambayo unadhani yatampa akitakacho lakini atapendeza na kutavutia kuliko sasa.

...mwambie kwa upole na kujali, "Mume wangu najua unapenda kuvaa unavyovaa, lakini uvaaji huo wala hauendani na wewe,.....jaribu kuvaa hivi".....onyesha mavazi ambayo unadhani yatamfanya Mumeo aonekane kijana na kuvutia na sio "Pimp"....Mvishe Mumeo.

Ushoga sio kitu/tabia za kujiingiza bali ni "ujinsia" ambao mtu anakuwa nao....kwamba anavutiwa na watu wa jinsia yake kingono/mapenzi.

Inategemea na jamii inayomzunguuka au "utayari" wake kuishi kama Shoga....wengi huishia kuoa na kuzaa ili kuficha "Ujinsia"....nikijibu swali lako ni kuwa sio lazima Shoga ashindwe kufanya Ngono/Mapenzi na Mkewe.


Mashoga huwa hawavai kama ulivyoelezea, Pimps ndio huvaa hivyo. Suala la kujipulizia Manukato sio tatizo, katika kujipenda na kujijali kunukia nayo imo!


Ila kujipulizia Manukato sirini mwambie aache kwani Manukato yana "alcohol" ambayo hukausha ngozi na hata kusabbaisha muwasho na maamukizi mengine ya Ngozi kutokana na joto la mahali huko(sirini).


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Sitaki kufika 30yrs nikiwa Bikira

Habari dada, Natumaini hujambo. Naomba ushauri wako kwa hili. Mimi ni msichana soon will turn 26. Nilikua na bf lakini tuliachana miaka 2 iliyopita na tulikaa kwa miezi ka 6 tu kabla hajaniacha.


Alikuja niambia baada ya muda bila mimi kumuuliza sababu ya kuachana na mimi ni alirudiana na Ex wake.

Kipindi tulichokua pamoja kama couple hatukufanya sex wala hakuniforce kufanya coz alikua anajua sijawahi kufanya sex before.


Baadaa breakup tukawa friends tu though deep down ile breakup iliniuma sana na ilichukua muda kumove on, karibu mwaka.

Mwaka huu tumekutana kwenye course fulani tunafanya wote, dada naona bado yupo moyoni.

Tatizo niliambiwa ni player lakini nampenda bado, naona awe tu my first guy kwenye sex coz sioni mwanaume mwingine wa kufanya nae na umri ndio hivyo unakwenda na sina boyfriend.


Sijatokea kumpenda mtu tena baada yake nisije nikafika 30's na bikira yangu. Naweza sema he is my first love coz sijawahi kumpenda mwanaume yeyote na mapungufu yake kama yeye!


*******

Dinah anasema: Mie sijambo, ahsante kwa ushirikiano.

Sasa Mrembo, kama umeamua na unataka (unaona) awe tu wa kwanza kwako, mimi nishauri nini hapo wajameni? Ila kama unataka niseme on that here we go;


Yack! Katoka kwa mtu kaja kwako, karudi kule tena yamemshinda (au bado anae) bila kinyaa wala second thought upo radhi kujiachia kwake for the name of first love? what is the 1st/childhood love do to people's lives? NOTHING so it is NOT that important/special. Mwanamke labda hupendi kuwa Bkira basi angalau jithamini.


Sio kwamba hakuna mtu uliempenda kama yeye bali hukujipa muda wa kumsahau huyo Ex au hukutoa nafasi ili kupendwa/kupenda kwa sababu ya kushikilia hisia zako kwa mtu ambae alikuwa bado na hisia kwa Ex wake.


Kitendo cha yeye kutotaka Ngono na wewe kwa miezi Sita haina maana kuwa alikupenda, was more to do with his feelings to his Ex.....alimheshimu Ex wake na sio wewe, nadhani alikutumia kupitisha muda au kumtia Wive Ex aliemrudia.


Usikate tamaa na kujishusha kiasi hicho! Hata kama hutaki kuwa Bikira by the age of 30 na hakuna mwanaume "msafi" umpendae basi bora u-pretend not to be Virgin (in your Head) uendelee na maisha mpaka utakapopenda na kupendwa ila sio huyo.


Usikimbilie kujitoa kingono kwa kuhofia kufika miaka 30 na Bikira, fanya ngono kwa sababu unataka na upo tayari, Likitokea la kutokea ni your responsibility.


Mwanamke usikate tamaa na kujitoa utu wako kwa huyo Ex, toka nje ya mzunguuko wako eeh! Tanzania kubwa sana na inawanaume wengi tu ambao hawana Mizigo ya madeni ya hisia Exes (wasafi).


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Pages