Tuesday

Msabato na Ex...

Mpendwa dada Dinah. Pole sana na kazi nyingi na kutoa ushauri kwa watu wenye ishu mbalimbali kama sisi.


Niliandika muda mrefu kumbe attachment kwako ikawa ngumu kufunguka. Huwa napenda kuingia katika page yako mara kwa mara kusoma mambo mbalimbali na  kupata mawili matatu.

Nilishawahi kuandika kwenye page hii na ukanishauri vyema, narudi tena nikiwa na tatizo jingine kabisa.


Mimi ni mdada nina miaka 28 sasa mwaka huu. Nimemaliza Chuo na nimebahatika kupata kazi nzuri kabisa.

Nilishawahi kudate mkaka enzi hizo nasoma Degree chuoni na tulikuwa na uhusiano kwa miaka mitano na tukabahatika kupata mtoto wa kike ambae kwa sasa ana miaka 3 na zaidi.


Niliposhika mimba ya mtoto huyo mwanaume alishauri sana kuitoa lakini mimi nikagoma kufanya hivyo, na hapo ndipo matatizo yalipoanza kwani penzi lilianza kupungua.

Ila kwa msaada wa wazazi na ndugu zangu nilibahatika kujifungua salama. Tangu nijifungue hakuwa mtu wa kujali sana kuhusu mtoto. Awe mzima au mgonjwa na hakuwahi hata kuja kumwona mtoto hata mara moja.


Nilikuwa bado nambembeleza akae sawa, ikafika kipindi mtoto akiwa na miezi tisa nikasikia anatoka na mtu mwingine na anaishi nae.

Nikabeba mwanangu nikaenda hadi kwake Mwanza kuhakikisha hilo kwani mie naishi Mbeya. Sikubahatika kumfumania na nilikaa kwake kwa muda wa siku tatu.

Sikutaka kuamini kuwa ni yule mwanaume ambae mie niliwahi kudate nae kwani namfahamu jinsi gani alikuwa anapenda na kubembeleza ngono hadi analia.


Lakini kwa siku tatu nilizokaa kwake hakunigusa wala hakuomba ngono na kwa kuwa nilikuwa nishasikia mengi sikuhangaika nae kutaka mapenzi.

Hapo nikajua kweli hana hisia tena kwangu, siku ya 3 nikijua kesho yake ndio naondoka niliamua kumuuliza juu ya jambo nililosikia la kuwa anadate mtu mwingine, alikuwa muwazi kusema kweli anadate mtu na kuwa mimi na yeye basi.


Niliichukulia kiume japo ni mwanamke niliondoka nikaenda kulala Hotel na kesho yake kugeuza safari. Nami mahusiano yakaishia hapo.


Nikaanza maisha mapya yangu na mtoto japo kwa tabu ila nikaja kuzoea. Cha kushangaza hata ndugu zake wakajitenga si Mama, Madada, wala Kaka zake hamna aneuliza hadi leo mtoto anaendeleaje tangu kipindi hicho akiwa na miezi tisa hadi sasa miaka mitatu na kashaanza na shule hamna anejua mtoto anafanana vipi.

Maisha yangu yaliendelea huku nikiwa sina mawasiliano nae. Baada ya mwaka hivi akaanza kupiga simu. Mwanzoni nikawa sipokei ila baada ya muda nikawa napokea na kumuuliza shida nini akawa anasema anataka kuongea na mwanae.


Nikawa nampa simu mwanae aongee makorokocho yake kwa sababu bado alikuwa haongei vizuri sana alichelewa kupanga maneno.

Akawa anapiga simu hivyo hivyo siku ananiomba tuzungumze na ukiongea nae anakuambia nimekumis, namis kila kitu kwako mara hiki hiki anaanza kutaja vitu tulivyofanya pamoja enzi hizo.

Sikutaka kumweka akilini sana na nikaacha kupokea simu zake maana akawa akipiga simu ni kuongea habari za kumisiana tu.


Maisha yakaendelea hatimae nikaamua kumove on kimahusiano baada ya miaka 2 ya kukaa single nikilea mtoto wangu kwanza.

Nikampata mkaka mwingine ambae tulianza mahusiano  na sasa tuna mwaka mzima na zaidi katika mahusiano.

Nakumbuka tulianza mahusiano hata mie sikuwa sawa kiakili, kihisia kwa kuwa bado nilikuwa nawaza sana Ex wangu na kila kitu nilichozoea kufanya nae.

Kiukweli nilimpenda sana na huyu Mkaka wa pili nae alikuwa katoka kusalitiwa na mpenzie ikawa tumekutana Ofisini kama marafiki hadi tukaanza kudate.

Tatizo lililopo sasa ni kuwa huyu mpenzi mpya ni Msabato na mimi ni Mkatoliki. Yeye ana ishu nyingi za kidini ambazo anadai zinamrudisha nyuma katika kuamini kuwa nitakuja kuwa mke mzuri kwake kama unavyojua sheria za Kisabato.

Pia tuna interests tofauti mwenzangu anapenda kuimba miziki ya dini mimi si sana japo siichukii. Mwenzangu mchamungu zaidi yangu.


Tumekuwa tukiishi hivyo kwa mwaka na zaidi sasa bila sex ila romance na tunaishia hapo. Jambo ambalo mie naliona sawa tu ukizingatia nilishaharibu nyuma.


Kila kitu kinaenda sawa sasa hivi japo nilipata tabu sana mwanzoni kumzoea kwani hata hiyo kiss tu ilikuwa tabu kwa kuwaza Ex wangu kila nikiwa nae.

Ila nikaanza kuzoea na alijitahidi sana kwa kuwa nilimweleza ukweli nae alinieleza kuwa pia anajifunza kuwa sawa kwani aliumizwa vibaya na akasema hatopenda tena na kajikuta katika mahusiano.

Wote tuliingia katika mahusiano bila kupendana tofauti tu ni kuwa sasa nampenda kupita kiasi baada ya kuona ni mwanaume mzuri sana, ana moyo mzuri na anatoa nafasi ya mwanamke kuzungumza na kuchangia mambo.

Ni mkweli hanaga longolongo kitu kipo hivi anasema direct hata kama anajua kitakuumiza. Yaani dada dinah kama mume yeye ni zaidi ya mume anafaa.


Tatizo lipo kwake kwa sasa kuwa upendo wake kwangu unakuwa taratibu sana hadi napata wasiwasi na tushakaa tukazungumza na kuangalia possibility za kutengana ila wote tunaishia kulia na kubembelezana kuwa tuendelee kujipa muda.


Mie niko sawa sasa nampenda kiukweli baada ya kuhangaika kujifunza tatizo lipo kwake kwani anasema tusiachane atajifunza kunipenda ili afikie level ya kama nimpendavyo mimi.

Sio kwamba hanipendi kabisa ila anakuwa muwazi kusema upendo upo ila mdogo ukiringanisha na wangu kwake.

Kiukweli nampenda ndio na natamani kuwa na mume kama yeye mwenye hofu ya Mungu hasa kwa baada ya kuumizwa vibaya.

Upande mwingine Ex baba wa mtoto  nae anakuja kasi kwa kudai mimi simweshimu kwa kuwa simpi nafasi ya yeye kama baba wa mtoto. Kisa alisikia mtoto nimempeleka shule fulani bila kumtaharifu.

Kiukweli sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kama hata centi hatumi na anaweza kukaa miezi hata 4 kimya hajui mtoto anakula nini, analala wapi na ada sh ngapi, anaumwa au mzima.


Anadai tukutane aniambie matatizo yangu kwani analaumu kuwa namtreat vibaya na simpi nafasi kama mwanaume na pia siwi kama wanawake wengine wanaoheshimu wanaume zao.


Nani mwenye matatizo kati yetu? maana ananilaumu kuwa si mama mzuri pia sasa sijui anataka niact vipi? na je kuhusu Msabato unaweza kuniambia kama dini ni kikwazo cha hayo yote?

Naomba pia nifahamu kwa mwanaume anaweza kujifunza kumpenda mwanamke na akaweza?

Na je muda gani anaweza kuchukua kujifunza? nifanyaje kwenye situation hii niendelee kuvumilia au nirudi nyuma?


NB:Kama ni kuchagua mwanaume ningemchagua Msabato ila tu simwelewi anaposema anahitaji kujifunza zaidi kupenda.

NAHITAJI MSAADAWAKO DADA DINAH KWANI NAONA UMRI WANGU UNASOGEA NAZEEKA SASA NA SINA MWELEKEO WA MWANAUME GANI SAHIHI KWANGU…

Wako katika mawazo.

*********

Dinah anasema: Salama kabisa Mpendwa na shukurani kwa kurudi tena baada ya Miaka.


Tuanze na huyo Ex king'ang'anizi asie na utu, heshima, adabu, haya wala aibu.

Fanya yote lakini usirudi kwa Ex, sana sana utakuwa "second best" na utaishia kujilaumu au kuumia zaidi. Kashindwa huko alikokuwa ndio anataka kurudi leo? Tena kwa lawama na kukufananisha....hana heshima kwako in what so ever!

Hana aibu wala haya kukulaumu kuwa wewe sio Mama mzuri wakati umelea Mimba peke yako, Umejifungua peke yako na unamelea mtoto mwenyewe.

Ukampa nafasi ya kuwa karibu na mtoto wake lakini hakuijali kwani alichokitaka yeye ni "kuipoteza" Mimba ili aendelee kula ujana......


Mtoto akikua na kusikia kuwa baba yake hakutaka azaliwe (alimkana alipokuwa Embryo) ndio atakapo jua nani Mzazi mzuri na nani useless.


Mbaya zaidi anakulinganisha na wanawake wengine, jinga kabisa na hafai kuwa baba wala mume....he's an example of a man. The shenzi kabisa tena akafie mbele kwa mbele huko na ukoo wake.(Huh! I hate Exes that's all)

Sasa onto Msabato Guy: Wasabato sana (Level ya Ulokole) nao bana, wengi wanapenda kuoa Bikira ka' Waarabu wakisha Oa wanaanza "kutumbukiza" nje ya ndoa ka' wameioa Dunia....

Pamoja na kuumizwa sana na Ex wake hali inayoweza kumfanya ashindwe kuamini mwanamke yeyote pia nadhani huyu Msabato wetu kashikiliwa zaidi na Jamii ya Kisabato (wanakaubaguzi fulani hivi ka Dini)....sasa nadhani hilo linaweza kuwa tatizo kuu.

Je, anachukuliaje suala zima la wewe kuwa na Mtoto kabla ya ndoa? Je umewahi kuhoji kama mtoto anaweza kuwa tatizo kwenye Usabato wake?

Kama mmewahi kujadili au "kutishia" kuachana na mkaishia kulia ni wazi kuwa mnapendana na mnahisi hamuwezi kuishi bila each other(how sweet).


Hakuna muda wa kujifunza kumpenda mtu, ni unampenda au humpendi....hisia za mapenzi huongezeka/hupungua jinsi mnavyozidi kuzoeana na kugundua kasoro, habits n.k....lakini kama umependa kiukweli utajifunza kuishi na Kasoro zake kwani hakuna aliekamilika.


Hawezi kukupenda wewe kama unavyompenda yeye kwasababu ninyi ni watu tofauti kwa kila kitu....kuanzia Jinsia mpaka interests.

Kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi lazima kuna mmoja atampenda mwezie zaidi....kamwe hamuwezi kupendana kwa level sawa, ila naweza kupenda idea, vitu au jambo kwa kiwango sawa.


Inaonyesha pia Msabato wetu bado hajamaliza hisia za maumivu aliyopata kutoka kwa Ex, hali hiyo inamfanya ashindwe kuendelea.


Wanaume wengi hawapendi kuachwa na wakiachwa huamua kwenda kulala na wanawake tofauti tofauti na baadhi huchagua mmoja ili kujipoozea mpaka machungu yamuishe.


Sasa kwa vile Msabato wetu Usabato unamzuia kufanya kama wanavyofanya wanaume wengine inamchukua muda mrefu kupata "uponyevu". Kumbuka Mwaka mmoja sio muda mrefu kihivyo.


Hamuwezi kuwa na interest zinazofanana kwani ninyi ni watu tofauti muhimu ni kila mmoja wene ku-support interest za mwezie au ukishindwa basi unamuacha na interests zake na wee endeleza zako.


Mimi nakushauri uendelee na huyo Msabato, kwa vile ni muwazi basi ni vema na wewe kuwa wazi kwake....kama issue ni mtoto, wewe kubadili Dini, Mawasiliano na Ex, Jumuiya ya Wasabato kanisani kwake, Wazazi wake(wasabato) n.k.


Kumbuka wanaume hawapendi mwanamke aendeleze mawasiliano na Ex hata kama mtoto anahusika....hebu tafuta ukweli na ikitokea Ex anamkwaza (anahofia kuwa na wewe ni kuwa na Ex pia) basi "ua" mawasiliano nae.

Since Ex hakuwepo tangu mtoto kazaliwa na mtoto hamjui kama Baba yake huna haja ya kuwasiliana nae. Mtoto akikua atamtafuta baba yake (akitaka).

This is 2014, at 28 wee bado katoto kabisa....Uzee ni jinsi unavyojichukulia sio miaka (namba)....

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Hatukuzaliwa waaminifu, tumejifunza...

Umewahi kusikia mtu akimtetea "rafiki" au mtu anaefahamiana nae wa jinsia tofauti kuwa anamke/mume/Mpenzi hawezi kufanya chochote?


Walio kwenye Ndoa/Uhusiano ndio washenzi wa tabia kuliko wale ambao ni "single"....labda kwa vile mara nyingi (tumeaminishwa) kuwa mwanandoa/uhusiano akitoka nje ya ndoa yake na "m-single" mwenye kosa ni yule aliekuwa "single".

Wakati mwingine wanandoa kwa wanandoa wanakubaliana ku-switch "mahusiano" illegally....kwamba wote wanawatenda wenza wao.


Walio kwenye ndoa/uhusiano ndio mwenye jukumu la kulinda ndoa/uhusiano na sio yule aliekutokea/kubali ambae ni single, kataa kama kielelezo cha Heshima kwa Mwenza wako na Watoto.


Mimi binafsi siamini mtu yeyote iwe kaoa au kaolewa, haina maana kuwa simuamini Mume wangu la hasha, namuamini sana tu ila sio kwa asilimia zote(hihihihi Mjini hapa + hizi sosho media hizi, akuu...).


Hakuna mwanadamu kazaliwa na Tabia njema (Uaminifu unatokana na tabia njema ya mtu), sote tunajifunza/tumejifunza kutokana na mazingira tuliyokulia na Malezi kutoka kwa wazazi wetu.

Since hatukulelewa pamoja na hujui mwenzio alikulia mazingira gani, huna sababu ya kumuamini kwa asilimia zote....


Wale waliooa au kuolewa na hao ni wake/waume wao wa kwanza ndio huwa hatari zaidi baada ya miaka kadhaa ya Ndoa, maana hawajui "mwingine" zaidi ya huyo alienae.


Sina maana watu muanze Umalaya au u-Serial dating wa kutosha kabla ya ku-settle, hapana. Najaribu kusema pitisha angalau mmoja, kula nae maisha (ujue mwili wako) kabla hujafunga ndoa....kwa mfano.


Na huyo mmoja ujitahidi kujaribu nae as mambo mengi as possible ili ukijaku-settle usidhani wanaume/wanawake wote wako hivyo au hawako hivyo na huyo ulie nae ndio funga kazi.


Kumbe waaapi bana....siku ya siku unakutana na Blog hii(mfano tu, usipaniC) then unahisi "umepitwa" kweli....ukaanza kutamani kutoka ili "ujionee" na kuumiza mwenza wako na watoto.


Ni vema itambulike kuwa ili kuwa na uzoefu huitaji kuwa foleni ya Exes, Mmoja tu in your life anatosha...yaani wa Kwanza na atakaefuata (wa pili) ni Mumeo.


Muhimu ni kuwa makini kabla "hujajikita" kwenye uhusiano na mtu(ili kuepusha namba kubwa ya Exes....!


Sasa huyo wa kwanza jaribu yote ambayo unadhani ni muhimu (kuchelewa kuanza nako kunasaidia), jifunze as much as unaweza kabla hujaingia kwenye uhusiano (na kushiriki Ngono).

Hapo mwisho nimelenga zaidi wadogo zangu waliopo Early 20s....


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Kwanini Wajua Mapenzi huachwa?

Habari Da Dinah, Mimi ni Mwanamke mwenye umri wa kati wa Miaka 30, nimeolewa na nina watoto Wawili. Naishi Dar lakini kikabila ni Mnyamwezi.

Hivi kwanini Makungwi wengi wameachika ikiwa wao ni mabingwa wa mambo ya Ndoa?


************


Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, nashukuru.

Kusema ukweli sijui(inabidi tuwatafute tuwaswalike) ila nitasema ninachodhania.

Kwenye suala la kuachika/acha/achwa haliegemei sana kwenye kuyajua mambo kitandani, kwani Ndoa au Mahusiano sio Ngono pekee.


Natambua kuwa Makungwi wengi wa "Kizazi Kipya" wanafunza mwanamke kuonyesha mapenzi na mavituzi ili asiachwe....na sio Maisha ya Ndoa, Uzazi n.k.


Nadhani "ukitaka usiachwe" ni "Brand" inayouza sana....kwasababu kila mtu hataki kuachwa au hataki Ndoa yake "ifeli" ndani ya miaka michache....wote wanataka Ndoa zao zidumu muda mrefu.


Lakini wanasahau kuwa umri mkubwa wa Ndoa au Uhusiano sio kielelezo cha furaha au mafanikio kwenye Ndoa husika.


Baadhi huendelea kubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine na sio Mapenzi, wengine huendelea kubaki kwenye ndoa kwa vile wanadhani umri mfupi wa Ndoa zao ni aibu kwenye jamii n.k.


Ili Uhusiano au Ndoa iwe yenye furaha inahitaji Nguzo kuu 5 ambazo ni Maelewano/Makubaliano, Mawasiliano, Heshima, Uvumilivu na Ushirikiano....Mengine yote hujitokeza humo.


Nguzo moja kati ya hizo ikikosekana hakika Ndoa au Uhusiano utayumba. Sasa mmoja asipotoa Ushirikiano kwenye Mawasiliano ili kuwe na Maelewano, amani na furaha hutoweka.


Hata kama unayajua sana Mambo kitandani, huwezi kuendelea kuishi na mtu asiekupa ushirikiano, asie kuheshimu, kukupenda n.k.

Kama umejitahidi kufanya yote au mengi uliyofundwa kama mke lakini Mume haonyeshi kuelewa au kutaka kubadilika ili muendelee kufurahia Muungano wenu then ni bora kutoka Ndoani.

Hivyo nadhani hao Makungwi ndoa zao zimefeli kwa sababu nyingi tofauti lakini wapo ni kutokupata ushirikiano kutoka upande wa pili.

Kwasababu mwanamke kafundwa haina maana ndio awe mtekerezaji wa mahitaji yote muhimu kwenye Ndoa. Ndoa ni umoja, Ndoa ni Timu....ndoa ni kuwa tayari kujifunza na kubadilika inapobidi ili muendane.


Natumaini utaridhia majibu yangu....


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Nifanye nini Mke wangu awe Msafi!

Dada Dinah vipi mambo. Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 25, nimeoa na nina mtoto Mmoja.

Mke wangu ananiboa yaani ni mchafu aoshi uke akikojoa, akioga asubuhi mpaka asubuhi. Nikimwambia hanielewi yaani mpaka nafikiria kumuacha hebu naomba ushauri wako dada.

*******

Dinah anasema: Poa!


Swali lako ka' la kutunga vile. Si umshukuru Mungu angalau anaoga mara moja kwa siku? Watu wanaoga mara Moja kwa wiki siku nyingine wafanya ku-wash/refresh/jifuta kutokana na shida ya Maji.


Hiyo tabia mkeo ameianza hivi karibuni au alikuwa hivyo kabla hamjafunga ndoa? Maana kwenye kila ndoa inayofungwa Binti hupewa "darasa" na usafi ni moja ya somo linalosisitizwa au ilikuwa ndoa ya Mkeka?!!


Wataka kumuacha mkeo na kuumiza hisia za mtoto wako kwa sababu/tabia ambayo inarekebishika.


Kuna tofauti ya kuongea na mtu(upendo na heshima) na kumwambia (dharau na command).....watu wengi huchanganya au hawajui tofauti yake.


Kutokana na maelezo yako na jinsi ulivyoandika inaonyesha wazi huna mapenzi ya dhati kwake, huna heshima kwake na unamchukulia kama "chombo" au kitu.


Nikionacho hapa ni kuwa Ndoa yenu inakosa Nguzo muhimu 4 za uhusiano wa Kimapenzi/Ndoa.

1-Mawasiliano: Zungumza nae kwa mapenzi, muelekeze na kumfundisha (labda hajui) faida ya usafi, muonyeshe "topic ya jinsi ya kujiswafi" ipo kwenye topics za 2007.


2-Ushirikiano: Kila unapoenda kuonga nenda nae na muogeshane so kama unaoga x3 kwa siku nae atakuwa anaoga mara tatu kwasababu unaoga nae.


3-Usaidizi:Msaidie shughuli za kulea na nyingine za ndani au mtafutie msaidizi, sometimes mtoto anaweza mfanya mama ajisahau(akose muda/kuchoka).


Kwasababu yupo nyumbani na wewe unakwenda kazini, haina maana yeye wa nyumbani hafanyi kazi au hachoki. Wote mnafanya kazi katika Mazingira tofauti na kazi zote zinachosha....pengine ya kulea mtoto inachosha zaidi.

4-Heshima: Mheshimu kama yeye na ukubali kuwa yupo tofauti, kalelewa tofauti na mazingira aliokulia na tamaduni pia ni tofauti hivyo m-treat ipasavyo bila dharau au kum-bully kwa vile tu ni mwanamke(Mfumo Dume).


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Nimechoka Kugombana...

Za majukumu dada natumai hujambo na unaendelea na majukumu ya kila siku. Dada dinah niko kwenye mahusiano ambayo mpaka sasa naona hakuna ukweli maana kila wakati ni ugomvi.


Mimi na mpenzi wangu ambae kiumri amenizidi kama miaka 5 na yeye ndio mwanaume wa kwanza kwangu kuwa nae.

Mara nyingi tunagombana ikiwa yeye anataka tufanye mapenzi na mimi nikikataa tu atasusa hata siku tatu hataki mawasiliano na mimi.


Mpaka nimmbembeleze ndio awe tena kawaida na kuna wakati ananiambia maneno makali mno kuna siku dada dinah aliniambia "kwani mimi kaka yako unakataa kunipa penzi" seriously nilikaa nikafikiria hiyo kauli nikaona nafanya vibaya nikamwambia sawa ila itakuwaje nikapata mimba?


Akaniambia yeye sio mtoto mdogo awezi kufanya ujinga huo, nikamwambia sawa ila twende tukapime basi hapo tena ikawa ni shida tulikaa wiki bila kuongea akanitafuta akaniambia niende nikapime yeye tayari kapima.


Nikamwambia nataka nirudi Dar tukapime wote, kweli nilirudi Dar tukaenda kupima na Majibu yakaja wote tupo salama sasa ikawa bado kutimiza alichotaka.


Siku ilifika tukawa tumekutana ilikuwa mara ya kwanza dada dinah na sikujua naanza vipi na nilitetemeka mwili mzima ila siku hiyo alishindwa kuingia hadi ndani.


Dada dinah sikukaa muda sana akataka tena turudie ili apite mpaka ndani but hiyo siku ilifika tuko Lodge akaniudhi kweli nikamuuliza kwanini anakuwa mkorofi muda wote?

Akasusa kwanini nimemuuliza vile, akaniacha mule chumbani mwenyewe akaondoka zake. Nililia sana nikaamua niachane nae.

Kila siku matatizo, nilikaa peke yangu muda mrefu bila kumtafuta na yeye hakunitafuta mpaka Christmas mwaka jana ndio akanitafuta, nikamchunia.


Mwaka mpya pia akaniambia tuwe tunawasiliana kwanini nakataa kuwasiliana nae au kwasababu nishapata bwana mwingine? nikamwambia sawa tutawasiliana.


Usiku akawa akituma msg ya usiku mwema anaanza nakupenda sijui nini mambo mengi tu. Kuna siku nyingine ananiambia Leo nimekuota mara nimekumiss, nashidwa kumuelewa analengo gani na mimi.


Maana tumekaa miezi mingi hajanitafuta wala kuuliza siku alivyoniacha Lodge kama nilifika nyumbani salama au laa.


Mwezi wa tatu ameniaga anaenda jeshini na atarudi mwezi wa 9 na siku ananiambia anaondoka eti alikuwa anataka nikamuage nyumbani kwake.


Kanilazimisha kweli ila mpaka sasa hivi simuelewi yuko vipi dada dinah nisaidieni kumuelewa napata shida nimempenda ila nashindwa kumuamini ..kazi njema


**********

Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa ushirikiano.

Huyo Kijana inaonyesha akili yake bado haijakua, yote anayoyafanya ni kama Mtoto wa miaka 20.


Muache aende Jeshini salama, na wewe focus kwenye issue nyingine za kujikomboa kama mwanamke.


Bado Binti mdogo, huitaji kupewa hekaheka za akili mtu asiejielewa kama huyo....umri wako (ulionitajia) ndio pekee wa kuanza kujiweka sawa ama kielimu au kikazi/kibiashara/kimaendeleo.


Kwavile tu alikuwa wa kwanza sio sababu ya wewe kuendelea kuwa nae hata kama inaonyesha wazi anachokitaka kwako ni Ngono.


Mwanaume huyo hana Utu na wala hajali Hisia na Matakwa yako....alikuacha peke yako mahali pageni (Lodge) kwasababu hukutaka Ngono au hukuwa tayari.


Mwanaume mwenye Utu, Heshima na kujali Hisia zako angetaka kujua kwanini hutaki na ange heshimu matwaka yako au angekubembeleza ili ukubali lakini sio kususa na kukuacha peke yako.


Huyo Kijana hakufai, inaonyesha hana mapenzi na anakutumia kwavile anauhakika huna maambukizo kwa sababu yeye ni wa kwanza kwako.


Uamuzi wako wa kumchunia ulikuwa sahihi na sioni sababu ya wewe kwenda kumuaga(atataka Ngono) kabla hajaenda Jeshini.


Najua (kutokana na umri wako) huelewi au umechanganyikiwa as hujui nini hasa ni Mapenzi au Uhusiano wa Kimapenzi.....je Mapenzi ni Ngono kama atakavyo yeye au Mapenzi ni kumpenda mtu na kuwa nae karibu kwa ajili ya maongezi na romance kama unavyotaka wewe?


The "wangu wa kwanza" thing haina maana yeyote kwa mwanaume bali kumuongezea "Ego" kuwa hakuna mwingine kabla yake....Haina guarantee kuwa atakupenda, atakuheshimu au atakuwa mwaminifu kwako.


Bikira inamaana kwa mwanamke husika, ni sifa kwako kuwa umejitahidi kushinda vishawishi kwa muda wote huo uliokuwa Bikira.....


Kwa mabinti wengine ambao bado Bikira, tafadhali itunze kwa ajili yako na sio kwa ajili ya kupata heshima au kupendwa au kuolewa na atakaekua wa kwanza.

Na ikitokea umeolewa ukiwa Bikira usitegemee sana kuwa Mumeo atakuwa mwaminifu kwa ajili hiyo, kama sio mwaminifu atabaki kuwa hivyo daima milele hata kama yeye ni wa kwanza kwako.

Furahia maisha yako bila stress na ukiwa tayari utafurahia uhusiano na Mkaka mwingine na hakika utafurahia Ngono kwenye umri mkubwa zaidi ya ulionitajia.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Tarehe za kuzuia Mimba

Dinah! Mambo? I hope mzima wa afya, unaendelea na majukumu ya hapa na pale.


Mimi mmoja wa fans wako katika blog yako. Samahani, na swali moja nahitaji kufahamu. Nilikutana na mpenzi wangu kimwili na siku hiyo nakutana nae kama tarehe 15.


Yeye alikuwa anaingia Hedhi tarehe 24, na hatukutumia kinga. Then kuna siku nilikuwa napitia blogs nikakutana na kitu kuhusu mwanamke anaweza kutambua siku zake na kujikinga na Mimba.

Ilikuw hivi; kabla ya mwanamke hajaingia hedhi kuna siku 8 za hatari kabla ya tarehe yake ya kuiona hedhi, na kuna siku 8 baada ya hedhi ni za hatari.

Basi nilivyo soma hivyo nikamtext na akanielewa kuwa ni kwel ikabidi tusubiri tuone kama ataingia hedhi tena coz alikuwa anaelekea kuingia tena.

Ilipofika tarehe 24 hakuiona hedhi kwamba atakuwa amepata ujauzito, nilimwambia akapime na jibu aliloniletea aliniambia kuwa ni mjamzito.

Sorry Dinah kuna ukweli wowote juu ya hili? Au ananidanganya coz siko nae karibu.

Thanks.


**************

Dinah anasema: Namshukuru Mungu, ahsante kwa ushirikiano.

Asa wewe sijui nikucheke au nikutukane? Hakika atakuwa na Mimba.....unafanya bila kinga then unaenda kusoma maelezo kwenye blog kisha unajipa Moyo kuwa hatoshika mimba! Who does that?!!....Only Dumbs...KINGA 1st mengine yanafuata dogo!


Huyo alieandika siku 8 kabla na siku 8 baada ya Hedhi bila shaka atakuwa Mwanaume.....ndio hao hao wanaodai kilele kwa mwanamke ni kama kutaka kukojoa mkojo wa kawaida!!!

Ndio, ni kweli kuna siku kwenye mzunguuko wa hedhi ambazo ni Salama (Humimbiki) na Hatari (Unamimbika) lakini tarehe hizi hutoa matokeo yenye uhakika kama Mzunguuko wa mhusika ni wa siku 28 kwamba haubadiliki.

Mzunguuko wa Hedhi wa kawaida wa siku 28 ndio pekee (nadhani) unaaminika(kwasababu ni rahisi kukumbuka).

Siku ya kwanza ya Hedhi ndio siku ya kwanza ya Mzunguuko na Yai hupevuka siku ya 14 tangu Hedhi kuanza.



Siku ya kushika Mimba(Hatari) ni siku ya 10, 11, 12, 13, 14, 15 na 16 tangu Hedhi kuanza(sio tarehe kwani hubadilika).....siku Salama na zenye uhakika ni Siku ya kwanza ya Hedhi mpaka ya siku ya 7 ambapo kwa baadhi ya wanawake bado yuwa Hedhini....Siku zilizobaki sio Salama kivile.


Sitopiga mahesabu hapa (sina maelezo ya kutosha kuhusu mzunguuko wa huyo Binti) ila nitakupa maelezo ambayo yatasaidia ili wewe mwenyewe ufanye mahesabu.


Mwanamke anapoamua kutumia tarehe kama Kinga ya Mimba anatakiwa kufuatilia kwa karibu "mahesabu" ya tarehe zake angalau kwa miezi 3 kabla ya kuanza kungonoka bila Kinga.


Kutokana na uzoefu wangu siku kabla ya Hedhi huwa ni hatari kwasababu hakuna anaejua Manii husika zitakuwa hai ndani ya mwanamke kwa muda gani.

Inategemea na afya Manii hubaki hai kuanzia siku 3-7 hivyo unaweza ukapata Hedhi na ile umemaliza tu Mimba ikaingia.....


.....sidhani kama Hedhi inasafisha Manii na pia inategemea Upevukaji wa Yai linalofuata(sometimes hupevuka mapema).

Pole kwa kushtukiziwa Mimba, next time weka tumia Condom kama hutaki mtoto....

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Mke ana Wivu, je nimtaliki?-Ushauri

Habari za kazi sister? Mie nina miaka sawa sawa na Chama Tawala. Nimeoa nimebahatika kupata watoto wawili, wa kwanza miaka minne na wapili Miezi Mitatu.

Mke wangu amekuwa na Wivu kupita kiasi, nimejaribu kumueleza anakokwenda siko lakini haelewi.

Nimemgawia nyumba 3, moja ya kuishi, gest na nyumba ya wapangaji na kumpatia Lorry Scania ajitegemee kwani nimechoshwa na tabia za wivu lakini hataki.


Ukweli mie sina mchepuko, nataka niachane nae niendelee na biashara zangu. Naomba ushauri wako nifanyeje? naomba usitoe jina langu.


****************


Dinah anasema: Njema kabisa Brother, nashukuru.


Sasa ndugu yangu biashara na familia si ndio zinapaswa kwenda sambamba....kwamba unatafuta kwa ajili ya familia yako eti?!!


Ukimuacha mkeo kwa sababu inayorekebishika(au ya muda) huoni kuwa utakuwa unawaonea yeye na kuwaumiza watoto wako pia? Umri wa watoto wako ndio umri ambao wanahitaji upendo na uwepo wa Baba na Mama.

Huo wivu wake umeanza au kuongezeka lini? Ni baada ya kushika mimba ya 2 au baada ya kujifungua?

Maana wakati mwingine Mabadiliko ya Homono wakati wa Mimba na baada ya Mimba yanaweza kusababisha makanganyiko wa hisia na tabia kwa ujumla.


Inawezekana sio Wivu bali ni uoga wa kuwa peke yake na watoto wawili, usikute anakuwa paranoid akiwa peke yake (Usiseme umemuwekea msaidizi, msaidizi sio mumewe....hana connection nae kama mpenzi).


Pia kuna Ugonjwa wa Akili unaowapata Wazazi baada ya kujifungua (Post-natal Depression)....isije kuwa mkeo anaugua bila yeye/wewe kujua.


Ni Ugonjwa unaowapata wanawake wengi (mimi mwenyewe mmoja wapo) na dalili zake wakati mwingine sio zile ambazo zinajulikana na kila mtu kwani watu tunatofautiana.


Siku mkeo ataja kujiua na pengine kuua watoto na wewe utasema "wivu ulimzidi" lakini ukweli sio Wivu bali ni tatizo la akili.


Mkeo bado ni Mama mpya, amejifungua miezi 3 iliyopita bado mwili na akili havijakaa vizuri then boom unatishia kumpa Talaka.


Haitaji stress zaidi kwenye akili na mwili ambao tayari umechoka. Kama mume wake Unahitaji kumuelewa (hata kama huelewi jifanye unamuelewa), kumuonyesha mapenzi na kumhakikishia kuwa unampenda.


Badilisha ratiba ya Shughuli zako ili utoe attention kwa mkeo, sio kila leo unarudi usiku wa manane.....tafuta siku 3 tofauti katika wiki ambapo unarudi mapema na kuwa pamoja kama familia.


Tatizo la mkeo linarekebishika/tibika kama mtashirikiana na kuboresha mawasiliano yenu kama wapenzi na sio Baba na Mama.

Pia ni vema kwa wote ku-share hofu zenu kwenye uhusiano wenu kwa mtu wa tatu ambae sio ndugu wala rafiki bali aliewafungisha ndoa au Mtaalam wa masuala ya Familia na Ndoa (sina hakika kama Tz wanapatikana), wao watawasaidia kwa ukaribu na ulevu kutoka pande zote mbili.

Mali na Pesa hazina maana kwake bali kuwa na wewe na kama ana Ugonjwa wa PD Mali na Pesa ndio hazionekani kabisa(haoni umuhimu wake)!


Ikiwa hana PD (Daktari wa Magonjwa ya Akili kathibitisha) then Mali na Pesa havina nafasi linapokuja Penzi lake kwako.


Sidhani kama Mkeo ana Wivu ule wa "kuchosha" nadhani huwa Paranoid (moja ya dalili ya PD) unapokuwa mbali....


Nashauri muende kumuona Daktari wa Magonjwa ya Akili ili kuwa na uhakika kuwa yupo salama (hii hali inaweza kujirudia au kujitokeza baada ya miezi michache hadi mwaka baada ya kujifungua).


Kama hana PD then kwa pamoja mfanyie kazi uhusiano wenu na mjaribu ku-compromise.


Kama Biashara zako haziruhusu kuwa na muda wa kuwa na mkeo kipindi hiki ambacho mimi nadhani ana issues kiakili ni vema kuomba msaada kutoka kwa Mkwe (mama yake) au ndugu yake ambae wanaelewana na aje hapo kuwa nae karibu.


Mtoto wa miezi 3 akifikisha Mwaka na mmefanya niliyogusia hapo juu lakini bado Mkeo ana "wivu wa kuchosha"...then err Vumilia....fanya uamuzi ambao hautoumiza hisia za watoto wako wala Mkeo.


Kwa umri wako huoni kuwa unakila sababu ya kuwa karibu na Familia yako? Jiulize ni Legacy gani utawaachia wanao? "Chuki" kwa kumuacha Mama yao bila kosa (Wivu sio kosa)....kuwapa mafunzo mema na mifano mizuri Kama baba?


Mali na Pesa haviwezi kuziba muda waliokosa kucheza na kujifunza kutoka kwako.


Mali na Pesa hazitojibu maswali yao na hazitoondoa "Chuki" watakayoijenga kwako kutokana na Sababu ya uliyoitaja ya kumuacha Mama yao.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Simuelewi

Pole na kazi, nina mchumba anamiaka 35, ananipenda kwa dhati na anatabia nzuri, mcha mungu, mpole na ananiheshimu. Tumekuwa kwenye Uhusiano kwa miaka 6.


Tatizo lake hana future, hana malengo na hajishughulishi walau kuweka Miradi. Anategemea Mshahara ambao haukidhi mahitaji tangu tumejuana mpaka leo hana hata Kiwanja na soon tutaoana.


Nipo njia panda je anafaa? Nahisi tutaishi maisha magumu kutokana na yeye kutojishughulisha.

Nimejaribu kumsihi mara kadhaa anasema ataanza kwani bado anajiimarisha. Namuonea huruma kumuacha ila tatizo ndio hilo.


Kazi njema


**************

Dinah anasema: Nashukuru ahsante.

Tangu mmekuwa pamoja kwa miaka hiyo sita ni yeye ndio aliekuwa akitumia Mshahara wake kukuhudumia wewe sio?

Kama sasa anamiaka 35 ni wazi mmeanza uhusiano akiwa na miaka 28 which means ulikuwa mdogo kwake kwa miaka kadhaa na ni wazi kuwa alikuwa akitumia senti zake kwako.


Kama alikuwa akitumia Laki kwa mwaka(mfano tu) hivi sasa angekuwa na Laki Sita Bank kama angeamua kutunza....sasa calculate pesa zote he gave you for the past 6yrs.


Huoni wewe ni mchango mkubwa wa yeye kutokuwa na Kiwanja....Eti Mrembo?!!


Je, wewe una mchango gani kwenye uhusiano huo zaidi ya Ngono? Je, unafanya Kazi/Biashara/upo nyumbani unalea watoto wenu?


Kingine unachopaswa kujiuliza ni kuhusu familia yake, Je anategemewa kwenye familia yake?(Hasa kama yeye ni Mkubwa au mwanaume Pekee).


Mchumba wako anafanya kazi, huko ni kujishughulisha, anakwenda kazini kila siku...huko ni kujituma.


Atafunguaje mradi au kwa pesa/Mtaji gani ikiwa Mshahara wake kwa sasa hautoshi kukidhi mahitaji?

Hofu yako ni kuishi maisha magumu ikiwa mtafunga ndoa kitu ambacho nakielewa....lakini pia ukumbuke kwenye ndoa kuna mabadiliko je, mkifanikiwa sasa na kuishi maisha mazuri bila tatizo la pesa na mara pesa zikaisha(miradi hailipi) utamuacha?


Kwenye maelezo yako huonyeshi Mapenzi kwake na wala huonyeshi (hujasema) mchango wako kiuchumi.

Uhusiano sio kupokea tu, uhusiano ni kutoa pia. Kabla hujaanza kulalamika na kuweka hofu mbele na kumshutumu mwenzio kuwa "hajitumi" au "mzembe" wakati tayari anakazi.....unatakiwa kujiuliza maswali niliouliza hapo juu.


Kama yeye "hajitumi" lakini kila mwezi anakupa senti za Salon, Simu, Pombe na Nyama choma au kufanya manunuzi yako binafsi au chakula then bana matumizi na senti za salon na Pombe(kwa mfano) uzitunze ili zikitimia ufungue Mradi.


Kama umeweka mezani na yeye anakuambia bado hajakaa vizuri basi muonyeshe kwa vitendo. Mpenzi mwema hutumia akili na kujituma ili kusaidiana na mwenzie....


Mchumba wako inaonyesha kuwa anafaa na ni mwanaume mwema mwenye mapenzi kwako(kutokana na maelezo yako)....hastahili kuachwa kwasababu mshara wake hautoshi.


Anakwenda kazini na kufanya kazi zake peke yake na mwisho wa mwezi mnatumia Mshahara wake kwa pamoja kurekebisha mambo.

Tatizo sio yeye bali ni wewe kuwa tegemezi (unaweza kuwa na shughuli na bado ukawa tegemezi) kwasababu tayari anajituma.


Hakuna kanuni ya kufanikiwa maishani. Wengine hufanikiwa mapema na wengine hufanikiwa in their 50s, hivyo miaka 35 sio Tija.

Jitume kama mwanamke, piga kazi/buni na endeleza mradi/biashara na weka mchango wako Kiuchumi kwenye uhusiano wenu, mfunge Ndoa na kwa pamoja mshirikiane kununua Kiwanja na kuanza kujenga.


Kuna mchangiaji mmoja aliwahigusia "Heri pesa za kutafuta pamoja, kuliko zile unazozikuta".....mie naongezea....Heri kujenga pamoja kuliko nyumba uliyoikuta.


Kama nia yako ni kuachana nae basi tafuta sababu nyingine lakini sio hiyo ya "kutojituma".


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Friday

Social Net na Mahusiano!

Social Network hazina tofauti na kuangalia Tv.....Unapokuwa mfuatiliaji wa karibu wa Tv programs na kuhisi umekuwa addicted nazo ndivyo ambavyo huwa kwenye "Shosho Netiwoku"....







.....Unajikuta unakolea huko mpaka unasahau kama una familia achilia mbali Mpenzi.









Miaka ya nyuma (Mwaka nilioanza kublog) niliandika kuhusu Technology na sikwenda moja kwa moja kwenye Sosho Media/Netiwoku kwani enzi hizo hazikuwa nyingi nadhani zilikuwa ni blogs, forums na facebook....









Soma topic hiyo http://dinahicious.blogspot.co.uk/2007/09/vishawishi-vinavyosababishwa-na.html?m=1







Miaka mitatu baadae nikakutana na topic kama yangu kwenye Magazines na Magazeti ya huku nikasema "heko to me, niliona mbele kabla yao".







Ingekuwa ni Magazine na Magazeti ya Tz ningesema wameiba sehemu ya maelezo yangu hihihihihi lakini ilikuwa ni Media za UK ambazo nina uhakika Waandishi wao hawasomi wala kupitia Blog yangu.







Anyway, sina mengi ya kusema zaidi ya kukumbushia tu kuwa hizi Technolojia za mawasiliano zimeanza kuchangia sana tena sana Uvunjikaji wa Ndoa na Mahusiano mengi kitambo.







Ukiachilia mbali ongezeko la matatizo ya Kisaikolojia na maovu mengine ya kutisha, Teknolojia imeingilia na kuharibu heshima miongoni mwetu na kuua Uoga wa kuumiza hisia za wenzetu tunaowapenda, pengine kwa makusudi au bila kujua.









Kuna faida gani kuwepo nyumbani mapema au kutoka na mwenza wako huku attention yote ipo kwenye Tv au Simu?!!!





Kama ilivyo kwenye kila kitu, moderation na kujua limit ni muhimu.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Muda wa Kawaida..

Dada dinah pole na majukumu. mi naitwa J na ninaomba kujua muda wa kawaida ambao Uume unatakiwa kusimama tena baada ya  kupiga bao la kwanza ili kuendelea na round nyingine. je ni dakika ngapi?





********************





Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.







Nadhani inategemea na mwanaume in terms of umri, afya, anavutiwa vipi na mwanamke anaefanya nae mapenzi, anasisimuliwa kwa njia zipi na maeneo gani? Ukame (amekaa muda gani bila tendo), Uwezo wake wa kingono (sex drive), Uchovu au Uvivu.







Inaweza kuwa kati ya Dakika 5 mpaka saa nzima na wengine huenda mpaka kesho yake au wiki ijayo na huo wote ni muda wa kawaida kwa mwanaume husika.







Nikijibu swali lako, sijui kwa uhakika, labda wanaume wenzio wasaidie kwenye Comments.





Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Tuesday

1st Love, Unasahau vipi ili Usonge...

Pole na kazi dada. Mimi ni mwanaume nina miaka 25 nimewahi kuwa na mpenzi mmoja ambae nilianza nae mapenzi nikiwa Mwaka wa kwanza Chuoni.


Nilikuwa nakutana nae kila ninaporudi likizo tu nyumbani Morogoro maana yeye alikuwa Form 4 katika shule ya Wasichana hapa Morogoro.

Tulipendana sana kama hatutakuja achana.Tulikuja achana mwaka jana mwezi wa tatu wakati mimi namalizia Chuo nae anamaliza Form 6 sababu alidai kuwa tumezidi gombana.

Mimi huwa napenda tukubaliane kitu na tuishi kadri ya makubaliano yetu. Tuliacha kuwasiliana kabisa kama miezi 3 hivi. Nikiwa nyumbani baada ya kumaliza chuo, nawaza ntapata kazi lini na wapi nikaona sms yake ananisalimu. Kwavile nilikuwa na hasira nae sana niliishia kumtukana.


Alipo kuwa anakwenda Chuo Mwanza, tukawa tunawasiliana ambapo yeye ndio alikuwa akinitafuta. Kwasababu nampenda sana nikawa nami namtafuta. Tukawa kama tumerudiana maana alikubali kuja kunitembelea ninakofanyia kazi.

Alikuwa amenitambulisha na kwao japo sio rasmi ila nilikuwa nafahamika. Anadai hana mpenzi ila baadhi ya siku simu yake bisy sana nikimuuliza anasema anaongea na rafikize.

Nikiwasiliana nae akirespondi vibaya naumia hadi najilaumu kwanini nimemtafuta lakini kuacha nisimtafute kabisa nashindwa.

Nikiwaza kuwa na mwanamke mwingine nafsi inaniuma nashindwa kuwa na mahusiano na msichana mwingine.

Dada nisaidie, nifanyaje niweze kumsahau na niwe huru kupenda msichana mwingine? Maana nikiacha kuwasiliana nae kwa muda yeye hunitafuta.

Yaani dada dinah mimi hata simuelewi. Je alianza kuwasiliana nami kwa lengo la kifuta soo kwangu maana aliniacha kwa maneno mengi. Nilimtumia hadi watu wa kumbembeleza hakutaka kuwa nami.

Au ni kweli anataka turudiane harafu anakuwa muoga?

Au ananizugisha tu pengine kwa kuwa baada ya mimi kaona alikosea kwa maamuzi yake kwamba mimi ni bora kwake?


**************

Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.


Aah! Mambo ya 1st love halisahauliki, haliishi nini na nini....eti! Katika hali halisi uzoefu wowote unaupata kwa mara ya kwanza huwa hausahauliki....

....ilikuwa ni mara ya kwanza kupata au kuhisi hisia za kimapenzi....was magical.....tendo likawa very special (not really, it's because hatujui kitu kwa mara ya kwanza).

Utaendelea kukumbuka uzoefu huo kwa muda mrefu sana katika Maisha yako mpaka siku utakapokutana na mpenzi mwenye kukupenda kweli na mwenye kauzoefu....hiyo ndio itakuwa mwisho wa "first love never ends/dies".

Utamkubuka kama wa kwanza na atabaki kuwa hivyo, hakuna zaidi na hautokuwa na hisia nae na badala yake utatambua kuwa "ngono ya kwanza" ndio haisahauliki na sio Penzi.

Humuelewi: Nadhani utoto unamsumbua na bado hajui akitakacho kutoka kwa mwanaume, uhusiano au maisha yake kwa ujumla.

Kwasababu alikwisha kuacha hapo awali nadhani huwa anakutumia kama "kipoza Moyo" ikiwa kakorofishana na Boyfriend au kashindwa kukutana nae kwa mfano. Au anapokuwa Mpweke au down kwa sababu nyingine na anataka kuwa cheered up.


Hii huwa ni solution ya muda mfupi kwa wanawake wengi in 20s ambao hawawaelewi wapenzi wao, wapenzi hawatoi commitment kwenye uhusiano, hawana wapenzi lakini hawataki kuwa na an Ex wanasubiri Mr Right n.k....hukimbilia kwa an ex waliowaacha for comfort.....


Kwa kawaida huwa wanakeep mawasiliano au kusema bado wanaurafiki na Ex kwa sababu hiyo....kuwatumia in the future.


Wakati mwingine hali ikiwa mbaya na upo karibu basi na Ngono utapewa ilimradi tu ajisikie "kutakwa" tena...."Kutamaniwa" au "kujaaliwa" lakini hakuna mapenzi.


Nimejuaje? Well sikuzaliwa tu nikawa in my 30s....nimepita humo.

Kujaribu kutowasiliana nae kwa muda ni hatua nzuri lakini unashindwa kusonga mbele kwa vile yeye bado anawasiliana na wewe(hajafuta mawasiliano yako).


Badilisha namba au m-block kisha futa mawasiliano yake. Anza kufurahia company za wadada wengine kikawaida au kirafiki tu sio kimapenzi.

Taratibu utaanza kupata hali ya kujiamini tena na hisia kwa mwanamke mwingine kwenye mzunguuko wako au mbali zitajitokeza.

Just go out there....have fun, enjoy your life kwa uangalifu though maana Mjini kuna mengi.


Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Monday

Umri gani sahihi kupishana kati ya Mume na Mke?

Salaam dada dinah, pole kwa shuhuli za kuelimisha jamii. Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32, nimeolewa miaka kumi iliyopita na nimebarikiwa kupata  watoto wawili. Mume wangu ana umri wa miaka 48.

Naomba unisaidie suala moja, je ni umri gani sahihi wa  kupishana kati ya Mke na Mume?


Nauliza hivyo kwa sababu mimi na mume wangu tumepishana miaka 16. Hapo mwanzo sikuwahi kufikiria kuwa issue ya umri itakuja kuwa tatizo kwenye ndoa yangu ila kwa sasa ndio naona mapungufu mengi sana tena sana dada dinah.


*************


Dinah anasema: Kupishana miaka sio Tija na sidhani kuna umri sahihi as long as hakuna mtoto kati yenu(chini ya Miaka 18).

Pamoja na kusema hivyo ni vema kuepuka gap kubwa sana...Maana mnaweza kugongana kwenye kufanya maamuzi ndani ya uhusiano au ndoa. Mmoja akiwa mdogo sana (hajamaliza Ujana) mwingine Mkubwa sana (kamaliza ujana).

**************


Kwanza kabisa kwenye suala la mapenzi kifupi ni kwamba perfomance ya Mr imepungua sana, mpaka huwa namuonea yeye huruma na mimi pia najionea huruma sana.

Yaani sijui hata nisemeje, dada dinah si unajua umri wangu ndio kwanza nina moto wa hatari, mwanzoni  Mr alikua moto wa kuotea mbali ila kwa sasa  hakuna kitu.

Sasa sijui ni umri, sijui ni stress, sijui ni majukumu au ni nini? ila hakuna kilichobalika ktk suala zima la kazi zake za kila siku.

**************

Dinah anasema: Point hiyo, "hakuna kilichobadilika ktk suala zima la kazi zake za kila siku". Mumeo anakaribia kugonga Nusu Karne maisha yake kikazi hayajabadilika....hata mie ningepata stress na depression kabisa!!


Maisha yake yamebadilika, sasa ana mke na watoto ambao wanakua na mahitaji yao yanavyoongezeka lakini Kazi zake ni zilezile tangu mmefunga ndoa....huoni hii ni sababu kuu ya Mawazo, Hofu na Mashaka?

Pia, inawezekana ni uoga wa utu uzima, Miaka 50 inatisha ujue?!! inaweza kumtisha hasa kama hajafanikisha alichotaka kufanikisha kabla ya umri huo.

Kama issue ni hiyo basi utendaji wake kitandani na afya yake kwa ujumla inaweza kuathirika.

****************


Tulishawahi kulizungumzia hili suala na yeye anasema hajui kwa nini? ila hatujawahi kusema twende kwa Daktari au kusema atumie dawa.

Mwanzoni ilikuwa tunasex karibu mara nne kwa wiki na hapo unapata kitombo cha hatari mpaka K inawaka moto ila kwa sasa maskini sipati hata miezi miwili.


Hata haijaingia vizuri wakati huo mimi ndio naisubiri kuipokea daaah  tayari ameshapiz. Inaniumaga lakini ndio ivyo tena sina jinsi.

Namwambia asante, nampa pole basi!!! hapo ndio basi tena hata uimbe nyimbo zote haisimami tena!!! naomba unisaidie kwa hili kwani napata shida sana na minyege.

***************


Dinah anasema: Kwavile umesema wakati mwingine mnakaa hata miezi 2 bila Ngono huenda "ukame" ndio unamfanya acheke mapema.

Kama ilivyo kwa Wanawake, wanaume pia wanamatatizo yao ya afya. Yanaayosababisha mabadiliko ya huko "sirini"....yaweza kuwa mf: Kisukari, Saratani, n.k

Mimi kama mwanamke siwezi kukusaidia kwa kukupa jibu lenye uhakika kwasababu sijawahi kuwa na uzoefu huo (umri wa Mume wangu haujafika huko).

Nadhani wanaume wanaweza kukusaidia zaidi kama wamewahi kuwa na tatizo linalofanana na hilo.

Suala la kuzidiwa na Nyege unapaswa kulijadili na Mumeo na kwa pamoja mkubaliane namna ya kusaidiana...maana kuna njia nyingi za kufurahia na kupunguza Nyege bila kuingiliwa.

*******************


Isitoshe alikua ameshanizoesha kufurahia Ngono kisawasawa,halafu hali inachange ghafla, naniuma sana.


****************

Dinah anasema: Maisha ya Ndoa hubadilika kama yalivyo maisha yetu sisi kama wanadamu, inabidi mmoja au wote m-adopt mabadiliko ili kufurahia ndoa yenu.

Hamuwezi kuishi maisha yale yale kwa miaka kumi na yaendelee kuwa hivyo kwa miaka mingine kumi.

*******************


Kwa ujumla hali hiyo imeanza kama miaka miwili iliyopita, kuna mabadiliko mengi sana achilia mbali hayo ya kitandani.


Hobbies zimechange, caring, outings hakuna tena na many many things. Hata suala la kushauriana kimaendeleo hakuna tena yeye anafanya mwenyewe bila hata kunishirikisha.

Nikimwambia vipi? anasema anafanya anachoweza yeye. Nimekaa nikajiuliza maswali bila majibu.

*************

Dinah anasema: Mdada mbona hapo hali inajieleza wazi! Ikiwa anafanya anachoweza ni ama hana pesa za outings au kuendeleza Hobi zenu za zamani.


Kama hayo mambo ni muhimu sana kwenye uhusiano wenu lakini yeye hawezi basi fanya wewe(kama una kipato), book mahali, toka na mumeo kwa ajili ya Mlo au kinywaji.

....kama huna kipato basi vumilia na utoe mawazo ya kuongeza kipato nje ya kazi zake ili maisha yawe vile upendavyo.


Kumbuka pamoja na mengine, maisha ya ndoa yanahitaji ushirikiano na kusaidiana.

************


Je ni kweli umri wake umeenda sana na haya yote yanaweza sababishwa na  umri huo?? au ni nini nisaidieni kuhusu hilo na pia unishauri kama anaweza tumia dawa.
Asante,


Kila jema kwako  dada dinah
naomba mobile namba yako dada dinah please, nitumie kwenye mail yangu.


***********


Dinah anasema: Sidhani kama ni Umri, miaka 48 mbona bado sana. Nadhani kuna issues nyingine zinamsumbua ama kichwani (hofu, mawazo) au mwilini(afya).


Ushauri wangu ni kumpa ushirikiano na support ya kutosha, zungumza nae kuhusu afya yake (kufuatia mabadiliko)....


Punguza ku-demand outings, shopping sijui Hobbies na badala yake toa ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa chanzo cha mabadiliko unayoyaona kwa mumeo.

Kuna wanaume hutoa maelezo mazuri sana, natumaini wataliona hili na kutoa ushauri kama wanaume.

Nasikitika kuwa sina namba ya simu kwa ajili ya ninachokifanya hapa.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Saturday

Anajua nina Familia lakini anataka nimuoe.

Pole na majukumu ya kazi Dinah
Mm ni kijana wa miaka 33 na nimeoa na nina mtoto mmoja

Awali nilikuwa na msichana kama friend chat wa kwenye mtandao na baadae tukapanga tuwe wapenzi but mwemzangu alikuwa bado anasoma. Kwahiyo kwa kipindi chote hatukuwahi kukutana kimwili.


Mwaka 2010 tulipoteza mawasiliano, mwaka jana alinipigia simu na kunieleza kwamba amesha maliza masomo na yupo tayari kuoana na mimi.


Ndipo nilimwambia ukweli kuwa mimi nina familia lakini yeye aliomba tuonane. Kusema kweli nampenda but ni Mkristo na siwezi kuvunja kanuni ya mke zaidi ya mmoja.

Yeye amekubali kuwa hata mke wa pili maana ananipenda je? nifanyeje na bado tunapendana?


***********


Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.


Watu kwa ku-complicate maisha ya wenzenu khaaa! Kama kweli mlikuwa mnapendana kitu gani kilikufanya uendelee na maisha mengine na hata kuanzisha familia?

Si ungesubiri "sikumoja atarudi", actually ungemtafuta kwa hali na mali huyo mwanamke wa mtandaoni na kurudisha mawasiliano kabla hujaongeza another life(mtoto) Duniani.


Umewahi kusikia kitu inaitwa "second best"...nitakupa a little real story ili yakuingie vema.

Kuna mdada alikuwa na bf Tz, yeye alikuwa akiishi Ulaya. Huko Ulaya akawa anakula maisha na wanaumbe mbalimbali yaani alikuwa akifanya umalaya.

Jamaa wa bongo akachumbia, Mdada akakataa kuolewa nae akidai bado yupo shule hivyo bora waendelee tu kuwa wapenzi wa mbali, mwanamke akapunguza mawasiliano na baadae kukata kabisa.

Jamaa kwavile alikuwa akimpenda aliendelea kuvumilia akiamini siku akirudi watafunga ndoa.

Miaka ikapita, umri wa mdada ukaenda akaanza kuwa desperate kuolewa lakini mwanaume aliekuwa nae Ulaya hakutaka kumuoa kutokana na sifa mbaya alizozisikia kuhusu huyo Mdada.

With desperation ya kuolewa na aibu ya wanaume wa Ulaya kumgwaya...akakumbuka kuna Bwege linampenda Bongo Tanzania.

Akarudisha na kukoleza mawasiliano na ku declare mapenzi kwa yule wa Bongo, akarudi Tz wakafunga ndoa na kwenda Ulaya kuanzisha familia.

Hana mapenzi na yule mwanaume lakini kwa vile alitaka kuolewa na kuzaa akaamua kuolewa na mwanaume ambae awali alimkataa na kukata mawasiliano.

Faida kwake ni kuwa Mwanaume hajui maisha ya yakimalaya aliyokuwa akiishi Ulaya na hafahamiani na watu wa huko hivyo chance ya kuyajua ni ndogo na hata akija kuyajua baadae atakuwa tayari kaolewa na anawatoto so itakuwa win win situation.


Miaka 12 baadae ndoa imekuwa ndoano, Mume keshajuana na watu na wanampa stori kuhusu Mkewe....jamaa kuuliza mkewe...mke akakubali kwa dharau na kumwambia ukweli kuwa ulikuwa "Second best"

.....mwanamke kabadilika (well karudia tabia yake), sasa wanaishi nyumba moja ili kukuza watoto wao lakini hawana mapenzi hata yale ya awali ya kuigiza kutoka kwa Mke mtu.

The end.****

Kama ungekuwa unamapenzi ya dhati kwa mkeo na mwanao usingeenda kukutana na huyo mwanamke pale alipoomba mkutane.

Baada ya kumuambia hali halisi ya maisha yako ya sasa na kuweka Msimamo wako wazi kuwa huna mpango wa kuwa nae achilia mbali kumuoa asingeshupalia kuwa Mke wa pili.

Inaonyesha ulitoa mwanya wa yeye kuolewa na wewe, maana umesema "amekubali kuwa mke wa pili", hukupaswa kutoa mwanya wowote wa kutaka uhusiano na huyo Mwanamke.


Nia yake hapo sio kuwa mke wa pili kwani anajua haiwezekani, "anachomaanisha ni kuwa iterekeze familia yako unioe mimi".


Wanaume mjifunze kuwa na msimamo, sidhani kama kuna mapenzi hapo kama kungekuwa na mapenzi juu ya huyo mwanamke ungepigana na kufanya lolote ili "asipotee" kwenye 18 zako, ungeenda hata kwao.... lakini you moved on quiet kirahisi na kuanzisha familia.


Futa mawasiliano na huyo mharibifu wa familia za watu (wapo wengi kama yeye) focus kwenye familia yako, ipende, itunze, ithamini na kuijali ili uishi maisha marefu.


Fainali uzeeni, unamiaka 33, mke na mtoto bado unahaha na kupoteza muda na hizi mambo za "mapenzi ya mtandaoni" hebu piga kazi ili kuwekeza kwenye Elimu ya mwanao.


Kesho-keshokutwa umerudisha namba, nani atamsomesha mwanao? Ona mbele sio umbali wa Miguu yako ukiwa umesimama.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Uhusiano wa Kimapenzi na Binamu...

Hi dinah natumai umzima na unaendelea vyema na majukumu ya kazi.

Mimi ni msichana ambae nilijikuta nime fall in love na Binamu yangu ambae kiukweli ni wa mbali kidogo ktk ukoo wetu hivyo sikuwa na mjua kwa sura ila kwa jina tu.


Ikatokea kama bahati tukawa na mawasiliano as sister and brother at the end tukajifunika shuka moja baada ya miezi sita ya uhusiano wetu.

Yeye ndio wa kwanza kwangu nami kwake ni wa kwanza. Tukawa tunaendelea na maisha kama kawaida lakini ikatokea Udhuru na akateuliwa yeye kuendesha familia.


Mwanzo alikua anaiendesha sawa lakini mwisho akawa anafanya ilimradi tu. Katika kuchunguza kwangu nikagundua kuwa ana msichana ambae alikua anauhusiano nae kwasababu alikuwa anaongea nae maneno ya sita kwa sita.


Baada ya kugundua hilo nikamueleza na yeye kunijibu kuwa hana uhusiano nae ila anafanya hivyo kuficha uhusiano wetu wa miaka minne sasa ambao bado hatujauweka wazi.

Cha kushangaza sasa akawa kila akirudi kutoka kazini anakuwa kakasirika, mfano nikiingia chumbani kwake anakasirika kiufupi akawa kabadili tabia tukawa hatuna mapenzi kama yale ya awali ya kusaidiana kazi za ndani.

Yeye anadai hakuwahi sex nae lakini mwanamke alimtumia mpenzi wangu (Binamu) picha zake kwa whatsap.

Hivi sasa yupo mbali nami anasema eti ananipenda na hajawahi nisaliti huko alipo. Anasema kuwa anapanga maisha vyema hivyo nijichunge kwasababu mimi ndio nitakaekuwa mke wake.


Je? ananipenda kweli au he wants to waste my time?


*************

Dinah anasema: Ah! Mie bukheri wa afya namshukuru Mungu.


Atakupotezeaje muda wakati ni Binamu yako tena kapewa jukumu la kuendesha familia eti....hihihihi natania mwaya.


Hata kama angekuwa Binamu wa karibu upande wa Mama au Mjomba nisingeshangaa maana Chemistry inaweza unganisha mambo ukashindwa kuelewa (kwa vile huwa hakuna strong connection kama Ndugu) sema Waafrika tunapenda kulazimisha tu Undugu.


Siwezi kusema au kumdhania kuwa anakupotezea muda kwasababu uhusiano wenu ni wa kuibia kwa Miaka minne.

Kwenye kuongea masuala ya mapenzi na kupokea/tunza picha za mwanamke husika kunatia mashaka kiasi.


Mwanaume mwaminifu na committed kwa mpenzi wake hapaswi kuwa na picha za mwanamke mwingine ambae sio ndugu yake wa karibu au kuongea masuala ya kimapenzi na mwanamke mwingine....hakuna kisingizio.


Kwasababu wewe ulikuwa wa kwanza kwake ni wazi hukuwa na uzoefu na hakupata uzoefu wowote kutoka kwako.

Nasema hivyo kwa sababu wanaume wengi hupenda kupata uzoefu kabla hawaja-settle(kuoa) so kwa dunia ilivyo sasa mmmmh! sidhani kuwa ni mkweli au muaminifu kwako.


Kama mpo serious na uhusiano wenu basi wote kwa pamoja mliweke hilo wazi kwenye familia zenu ili mjue nini mtakabiliana nacho huko mbeleni.

Mf: Kususwa na familia zenu, kuachanishwa kwa lazima, kuondolewa kwenye Mirathi au mmoja wenu kuozwa kwa lazima ili kutunza "siri ya familia".

Msimamo wake kwenye hayo niliyogusia ungeninifanya nijaji kuwa hakupotezei muda na yupo serious na committed kwako na uhusiano wenu.


Miaka minne ni mingi sana, zungumza nae na useme yaliyoujaza moyo wako na kuwa upo tayari kwenda hatua ya mbele kwenye uhusiano wenu.


Mwambie ungependa na upo tayari kuweka wazi uhusiano wenu ujulikane kwenye familia zenu.

Majibu yake ndio yatakayokufanya ujue msimamo wake kwako au kwenye uhusiano wenu kwa ujumla.

Akisita kutoa jibu au kuomba muda zaidi basi ujue kuwa ni mpitaji tu huyo.....sababu kama ni muda wa kufikiria mwisho Miaka miwili.


Kwa miaka minne amekuwa akijua kuwa analala na "Binamu yake" kwa maana hiyo alikuwa anajua kama ni kosa au si kosa mbele ya Familia/Ukoo wenu.


Huombi kuolewa au Mahari bali unaomba uhusioano ujulikane so hakuna cha kusita hapo ni NDIO au HAPANA! hilo moja.

Pili, akikataa na kusema familia ita-whatever then mnapotezeana mida.

Tatu, akikubali lakini kudai muda zaidi wa kusubiri basi rudisha muda nyuma kwamba akisema msubiri hadi July, mwambie unataka May. Jibu lake hapa litakufanya ujue msimamo wake.

Ukiona anakuyeyusha, sahau miaka minne, sahau tena tupa kule "mie wa kwanza kwake".....

Toka nje ya "Ukoo" ili uone zaidi ya "Binamu" namaanisha usafishe macho kwa ku-date sio ukafanye ngono ovyo-ovyo.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Nifanye nini ili harufu iishe...

Pole na kazi za kuelimisha jamii na hongera pia. Mimi ni mfuatiliaji
mzuri wa uelimishaji wako kwenye mtandao na ninatatzo ambalo
linanikosesha raha na marafik.


Ninaumri wa miaka 19 toka nizaliwe sijawahi kufanya mapenzi ila tatizo langu ni huwa natoa harufu sana sehemu za siri.

Nimeenda Hospitali mpaka nimechoka, na kujisafisha najisafisha kila siku
sijui tatizo ni nini?

Nakosa raha na marafki wananikimbia na kunisema, hata wanaume wanaponitaka kimapenzi nawakatalia kukwepa aibu.

Natamani kuwa na mpenzi ila
nashindwa, dada natumai utanisaidia kwa ushauri kuhusu tatizo langu ili niwe na furaha kama wenzangu.


Asante


*********

Dinah anasema: Shukurani kwa ushirikiano na ahsante sana.

Pole sana Mrembo, hao marafiki gani wanakukimbia na kukusema badala ya kukusaidia angalau hata kwa ushauri au kutafuta ushauri kwa niaba yako?!! The shenzi type.

Kwenda hospitali na kupewa dawa au ushauri na Daktari wa Jumla (GP) haisaidii sio Daktari Maalum kwa ajili ya tatizo lako.

Unapaswa kwenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kike/Wanawake ili ufanyiwe uchunguzi yakinifu na kupatiwa matibabu.

Magonjwa ya sirini (wengi huita zinaa) kwa wanawake sio lazima yasababishwe na kufanya Zinaa au kufanya Ngono.

Kutokana na maumbile yetu yalivyo, kutokuvaa Chupi tu kunaweza kukusababishia maradhi Ukeni.

Kuvaa chupi kunasaidia lakini ni muhimu kujua aina au material ya Chupi husika, ni vema uvae za Pamba au zenye kijitambaa cha pamba pale kati (panapoziba uke).

Kuchangia kamba ya kuanikia nguo, vifaa unavyotumia bafuni/chooni, sabuni unayotumia wakati wa kuoga n.k. pia inaweza kukusababishia maradhi ya Zinaa kutoka kwa watu wengine.

Wakati mwingine mabadiliko ya Homono wakati wa Ukuaji (Kubalehe) kwa wanawake kunaweza kusababisha maambukizo...."Vimelea" rafiki vinavyotunza Uke hu-attack mwili kwamba vinakuwa adui.

Ukipatiwa matibabu anza kuwa muangalifu sana, hakikisha unanawa na safi na kujikausha kila unapokwenda kukojoa.

Tumia maji yaliyochemshwa vema na kupoa/mji ya kunywa kunawa kila unapomaliza kukojoa.

Kama unachangia kamba ya kuanikia nguo hakikisha unazipiga pasi ili kuua wadudu.

Hata kama unaochangia nao ni ndugu zako wa damu, hakikisha unachukua hatua mbili mbele ili kujilinda.

Undugu/Ujirani mwema sio sababu ya wao kuwa salama na sio lazima wakuambie kuwa wanagonjwa au walikuwa na gonjwa la zinaa.

Tafuta kifaa chako pekeyako kwa ajili ya matumizi ya kuoga au kujisafisha baada ya kutumia Choo.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Ma' mtoto wa Pembeni Msumbufu, nifanyeje?

Mambo dada dinah,



Mimi ni kijana wa umri wa miaka 28 nina mke na mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 3 sasa lakini pia nilizaa na mwanamke mwingine ambaye mwanae ni mwenye miaka 3 pia.









Huyu wa pili tuliiba tu na bahati nzuri akapata mimba ya mtoto huyo ila mimi

nimemwambia sipo tayari kuoa wanawake wawili na yeye ilikuwa si ahadi tuoane.









Nikimwambia aolewe anipe mwanangu hataki anataka aolewe na mimi. Mimi siwezi naomba ushauri nifanyaje? Kama matumizi natoa.





*************



Dinah anasema: Mambo poa kabisa, vipi wewe?





Uliibia na mwanamke mwingine nje ya ndoa bila Kinga alafu kashika Mimba unasema bahati nzuri?! Hiyo ni bahati mbaya tena MBAYA sana.









Bora Mkeo angekukuta na mtoto kuliko kumpelekea mtoto mwenye umri sawa na mwanae....! Wanaume Weusi kwa kusambaza umasikini (kuzaa ovyo) tu mnaongoza!!







Ni rahisi kusema nipe mwanangu nawe uende kuolewa, lakini ukiweka hayo katika vitendo ni ngumu sana.









Sio rahisi kwa mama kuacha mtoto wake mdogo aende kulelewa na mama mwingine(subiri afikishe miaka 15 labda) ambapo mtoto ataamua mwenyewe kukaa na Baba yake au Mama yake.









Pia sio wanaume wengi ambao wanapenda kuoa wanawake ambao tayari wana mtoto/watoto. Most wanaume huwa abuse watoto husika kijinsia.







Nenda Ustawi wa Jamii na ukaelezee issue yako nadhani wao wana-refer kesi yako Mahakamni kwa ajili ya Uamuzi kisheria kuwa utamtunza mwanao kwa kiasi cha pesa watakchokupangia kutokana na kipato chako(hakikisha mkeo anajua kama alikuwa hajui na uwe tayari kwa Vita).









Huyo mwanamke hawezi kukulazimisha umuoe ikiwa wewe mwenyewe hutaki kufanya hivyo kwa vile tayari umeoa.









Ikiwa anatumia mtoto kukutishia kuwa usipofunga ndoa nae atatoa siri au atakuharibia kazi....then itabidi ukamripoti Polisi.









Jifunze kumheshimu na kumthamini Mkeo. Unapotoka nje ya ndoa unaumiza Mkeo, mtoto/watoto wako na mtoto atakaezaliwa nje ya ndoa yenu.





Acha ubinafsi, Uzizi na kusambaza Umasikini.



Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Pages