Habari yako dada dinah!! pole kwa majukumu, dada mimi ni msichana wa miaka 27 nina mpenzi wangu ambaye tupo kwenye mahusiano kwa muda wa miaka sita sasa na tuna mtoto wa miaka mitatu.
Bado hatujaoana kwani tunasoma na tulianza mahusiano wakati mimi nipo mwaka wa kwanza chuo na yeye mwaka wa pili.Tunasoma nje ya nchi ila mtoto yupo Tanzania analelewa na wazazi wangu.
Dada tangu tumeanza mahusiano mpenzi wangu alikuwa ananipenda saana na kunijali na nilivyojifungua pia aliendelea kunipenda.
Tulikuwa tukifanya kila kitu pamoja na tulishirikishana kila jambo,tulishea pass words za kila kitu,fecbuk,emails nk!!
Mwaka jana akapeleka barua ya Posa kwetu! TatIzo langu ni kuwa mimi ni mkorofi halafu nina wivu mnoo...yani kipindi chote hiko cha mahusiano yetu siku akichelewa kurudi tuu(maana tuna appartment huwa tunakaa pamoja kwa baadhi ya siku kwasababu tunaishi mikoa tofauti) hata simuulizi namvamia na maneno na some times nafanya fujo kabisa!
Nikiona kawasiliana na mwanamke zaidi ya mara mbili nafanya fujo! Yaan kanivumilia mnoo!ila nampenda na baada ya kufanya hivyo huwa najirudi nayeye ananieleza ukweli basi najiona mjinga then tunaendelea na maisha.
Ila tabia yangu siachi akifanya kingine naarudia!! yaani huwa nafanya fujo,nampiga na glass, navunja simu zake n.k ila ananibembeleza tunakaa sawa.
Sasa this time naona amechoka wa na visa vyangu maana december niligundua ananichit, ikaniuma sana na nikampigia huyo msichana akaniambia kweli yupo na mahusiano na mpenzi wangu na wana kama mwezi mmoja!(na huyo msichana ni malaya sana na yasemekana ameathirika sema mpenzi wangu hajui hizo story maana mpenzi wangu sio mtu wa kujichanganya na watu hivyo habari nyingi za mtaani mpaka mi nimpe).
Then nikarudi kwa mpenzi nikafanya fujo kama kawaida but akanituliza na kuniomba msamaha, akasema ananipenda na hana fyucha na huyo dada sema alifanya hivyo maana nimezidi visa na ujeuri na imefika kipindi simpi mapenzi.
Akachukua simu akamcall yule dada kumwambia its over na akamtext whatsup kumueleza kuwa ana mpenzi wake anaomba waachane!
Alifanya yote hayo mbele yangu na akambock koote! ila pamoja na yote hayo mimi nikawa nasindwa kumuamini kama kamuacha japo nikishika simu zake sioni kitu.
Alijitahidi kunionyesha ameacha but mimi wapi, nilimwambia nilimsamehe but moyoni nilikuwa naumia. Ikawa nikipiga simu asipo pokea on time naanza ugomvi, nikienda apartment akachelewa kurudi nafanya fujo tena za ajabu!
Akaniambia sasa hivi tusikutane nikae kwangu mpaka hasira ziishe ila bado nikawa nampigia kelele hunipendi ndomana waniambia nikae kwangu.
Nikakaa kwangu kama wiki huku twawasiliana na kugombana! juzi kanambia niende kule tumefurahi but usiku alilala nikashika simu yake ili nione kama anaendelea na yule dada. Sikukuta vya yule dada bali nilukuta meseji ya mwanamke mwingine akimlalamikia mpenzi wangu kuwa ahamini kama anampenda maana hakuna kitu chochote wanachofanya pamoja!(mesej ni ya tar 19 januar na yule dada wa kwanza tulisolve 23 dec) nikapiga ile namba kwa simu ya mpenzi wangu, akapokea huyo dada mwingine.
Yaani nilichanganyikiwa!! nikamwambia mpenzi wangu akasema hakuna chochote bali panic zangu tuu, nikaanza kumfokea akaniambia this time ananipiga maana nimezidi ujinga!!
Tukapigana hadi basi, mpenzi wangu akaondoka akaniacha appartment na hatukutafutana but usiku nilimcall akasema hawezi rudi mpaka mimi niondoke maana yeye ana mitihani(anafanya medicine huku ni miaka 7) amechoka fujo zangu anataka asome maana mimi sijielewi!!
Na kuhusu matatizo yetu akipata muda huko mbele atakuja mkoani kwangu tuongee kwa sasa anaomba asome!!
Kwahiyo dada nahisi mpenzi kanichoka na mimi nampenda saaana na yeye ananipenda ila ndio tumefikia hapo, je nifanyeje?
Amenichit kwa wanawake wawili ndani ya muda mfupi!!na huko nyuma hakuwa hivyo kabisaa!!
Tafadhali nishauri cha kufanya!! tulipanga ndoa tufunge mwaka huu, maana mimi ndo namaliza masters yangu mwezi wa pili.
Ahsante sana, nasubiri ushauri wako wako maana nahisi kuchanganyikiwa.
***************
Dinah anasema: Habari ni njema mrembo, shukurani kwa ushirikiano
Tabia yako ni mbaya na ulipaswa kuachana au kujirwkebisha kitambo. Unaweza kuwa na wivu sawa kwani ni suna lakini kuwa agressive na violent sio vema.
Pamoja na tabia yako mbaya bado sio sababu ya mpenzi wako kutereza nje ya uhusiano wenu mara zote hizo.
Mpenzi wako anatumia ''kasoro yako '' kitabia ku justify Umalaya wake na kwasababu anajua kuwa unajua kuwa Unatatizo hilo basi inakufanya rahisi kwake kufanya makosa na kukusukumia wewe kuwa ndio umesababisha awe hivyo.
Mtu chake, hata mimi huoji mume wangu kwanini anaongea na baadhi ya wanawake au wanaume.(si wameoa au wapenzi ambayo ni wanawake eti hihihi) Bibi alinambiaaaa usiamini mwezi wako kwa asilimia zote Mia, achia nafasi ya Wivu kwani bila wivu hakuna mapenzi.
Moving on.........Acha kuomba msamaha na kujiona mkosaji, mchumba wako ndio mkosaji mkuu na ameonyesha kiburi na kutojali kwa kusema atakuja huko kwako kuzungumzia issue iliyojitokeza.....basala ya ku sort out kabla ukweli haujapindishwa na kupoteza makali ya issue husika.
Angekuwa anajali na kujutia makosa yake ya kuku cheat na kukupiga( hakupaswa kukupiga au kupigana na wewe bali kukuzuia usiwe too agressive na kupiga).
Huyu mpezi wako huenda amekuzoea, anapenda the idea of ''nina uhusisno mzuri na mama mtoto wangu'' lakini hana mapenzi kwako na ikiwa yapo mapenzi basi haoni thamani yako kwake na inamuhuwia vigumu kukuheshimu.
Pia uhusiano wenu unamapungufu ya mawasiliano, hamzungumzii uhusiano wenu ikiwa ni pamoja na mawazo ya kila siku mpaka mmoja afanye kosa ndio mmoja wenu a nazungumzia kuhusu kinachomkwaza.
Uhusiano ni kama kazi ofisini, kuna issue basi unaitwa na kuambiwa umekosea wapi na ujorekebishe vipi......boss akikaa kimya mpaka mteja aje kulalamika ni wazima unaweza kupoteza kazi.....sijui naeleweka?
Ushauri wangu kwako ni kuachana nae kwa muda alioomba kujiandaa na mitihani na akimaliza angalia kama atakuja kama alivyoahidi.
Tumia muda huu kujifunza namna ya kuzuia unapohisi hasira. Unaweza ku soma dua/sala kila unapojisikia ku exprode pia omba msaada professionally kuhusu tatizo lako. Inategemea upo nchi gani ila natambua Ulaya inapatikana widely.
Oh nenda kaangalie afya ili kujua kama hujakopeswa HIV......hili lilikuwa la kwanza sema nimeputiwa.
Wengine wataongezea, kila la kheri.