Dada Dinah habari yako, Mimi naitwa G nina umri wa miaka 25, Tumeachana na mke wangu sasa yapata mwezi mmoja na tuna mtoto mmoja wa kiume ana umri wa mwaka na miezi mitatu.
Kutokana na tabia yake ya ukorofi, ubinafsi na ujeuri na akapata mashoga majirani ambao tabia zao sio nzuri, ilifuka kipindi akabadilika.
Akawa hataki hata kunifulia nguo zangu ila alikua anapenda sana kufanya mapenzi yaani ana nyege sijawahi kuona kila siku tulikua tunafanya mapenzi hata mara nne.
Tabia yake ikanishinda alivyoanza kubadilika na ikabidi nimwache akaenda kwa dada yake Morogoro sasa naskia anafanya kazi bar huko Morogoro.
Nampenda ila moyo wangu umekua mgumu kwake yaani hata sijui nifanyaje na maisha ya kule magumu na kwenda kwao hataki.
Naomba ushauri dada yangu.Mimi naishi Dar es salaam.
************
Dinah anasema: Habari ni njema mkibaba. Shukurani kwa ushirikiano.
Unaacha mke kwa sababu zinazorekebishika(za kizembe)......halafu utamuachaje mke kimtaani hivyo. Au ulimfukuza bila Talaka?
Kama ulivyokwenda kwao na kumposa na ukakubaliwa na hatimae kumuoa.....ndivyo ulivyotakiwa kufanya ila tofauti this time ungekuwa unamrudisha KWAO.
Binti wa watu akipatwa na la kupatwa huko kwa dada yake ambako sio kwao utashitakiwa na Wazazi wake kwa kosa la kumterekeza mtoto wao na kusababisha usumbufu na maisha ya taabu au hata kifo ikitokea bahati mbaya.
Mtu hawezi tu kukurupuka na kuanza kuwa mkorofi au mjeuri......lazima kuna kitu kinasababisha mkeo kuwa na tabia hizo kama kisasi kwavile hawezi kukupiga na hajui kuwakilisha issues zinazomkera kwao.
Baadhi ya wanawake huamua kuwa kama mkeo ili kufikisha ujumbe kwasababu sio kila mwanamke anajua namna ya kuwakilisha kero kwa mumewe.
So atakuwa mjeuri au mkorofi akitarajia wewe mumewe kumuweja chini na kwa panoja mzungumze na pengine wewe kujirekebisha ili yeye asiwe na tabia hizo.
Ikiwa wewe unaumri huo ni wazi mkeo ni mdogo zaidi.....yupo kwenye stage ya kujitambua na kutengeneza marafiki ni sehemu ya kujifunza na kujitambua.
Ikiwa majirani wanatabia mbaya ambazo wewe huzipendi hilo litakuwa tatizo lako. Huenda mkeo alirafikiana nao kwa sababu za kufahamiana na kuongea kama majirani na sio kuiga tabia zao.
Suala la yeye kugoma kukugulia nguo sio sababu kuu ya yeye kuwa mkeo. Yeye alikubali kuwa mkeo kwasababu anakupenda na alitaka penzi lenu linawiri mkiwa pamoja kila siku.
Kwenye ndoa kuna mengi muhimu na kufuliwa nguo sio muhimu. Akiona kuwa ni muhimh kukufulia anapofua zake au za mtoto sawa.....vinginevyo fua mwenyewe.
Kulea mtoto 24hr sio kazi rahisi na juu ya hilo bado kuna shughuli nyingine zinahitaji nguvu na focus ya mkeo.....bila kupewa ushirikiano mkeo atahisi kutokujaaliwa, kutengwa, kutokupendwa au kulemewa na kazi zote za nyumbani plus mtoto.
Mwanamke anapoanza kuhisi hivyo huwa mkali au mjeuri kwa sababu akilini mwake anahisi kuwa humpendi na humjali kwasababu tu kazaa.....pia huoni au kuthamini chochote anachokifanya incl kukugulia.....huonyeshi shukurani.
Mkeo alihitaji ushirikiano na wewe kumuelewa lakini badala yale umemtimua......unadhani nani mbinafsi?
Kungonoana ni afya.....yeye kuhitaji ngono zaidi hakuna uhusiano na urafiki wake na majirani wenye tabia mbaya. Ni muda tu umefika baada ya kuvuka mwaka tangu ajifungue.
Umesema unampenda....hilo ndio muhimu. Angekuwa katoka nje ya ndoa yenu na kumuacha chap chap ningekuunga mkono.
Sasa fanya mpango wa kuwasiliana nae na kutafuta uwezekano wa kuzungumzia issue yenu na kutafuta muafaka.
Kilichotokea kati yenu sio kikuu cha kukufanya umuache mkeo haraka hivyo bila hata kujaribu mazungumzo kwa kujali mahitaji ya mtoto kihisia.
Kila la kheri.