Thursday

Kanisaliti na kuzaa x2 na vibaba 2 tofauti....ataka tufunge Ndoa


Habari za siku nyingi Dada mpendwa. Natumaini Mungu bado anakulinda. Na afya yako inazidi imarika kwa neema ya Mungu.

Dada mpendwa mimi niko katika hali ya sintofahamu, naamini kwako ntapata uvumbuzi.

Miaka ya nyuma nilikuwa naishi Bujumbura, nikaanza kupendana na Binti flani. Kwa vile nilikuwa na soma ilinibidi nitoke kidogo ili kujianda kwa ajili ya Mtihani mkuu. Nilipo rudi nikakuta yule Binti ana Mimba ya mwanaume mwingine!

Tangu apo mawasiliano yakakoma. Alipo jifunguwa baadaye akaniomba msamaha nakuhitaji turudiliane tena, nikamsamehe nakurudiliana naye kimapenzi!

Baada ya muda Binti uyo akaitwa na kakaye huko Afrika ya kusini(South Africa) ili aende kusoma na kuniacha Bujumbura!

Alivyofika huko mawasiliano yetu yakaendelea lakini baada ya muda yakazimika kwamba simu yake ikawa haipatikani!


Jinsi muda ulivyokuwa unakwenda na mimi nikajaaliwa kwenda Africa ya Kusini(South Africa). Siku moja nilipokea simu ya yule mwana dada niliyekuwa napendana naye bila kujuwa amepata wapi namba yangu ya Simu!


Huku akiniomba turudiane tena wakati alishazaa mtoto mwingine na mwanaume mwingine Afrika ya Kusini(South Africa)!
Na amewahi ishi na huyo Baba mtoto kama mumewe. Ila kwa bahati mbaya hawakuweza elewana wakaachana.

Mimi binafsi sikuwa namfikiria tena na nilikuwa tayari nilisha pendana na Binti mwinhine ambaye nilikuwa na tarajia kuowa tangu nilipofika Afrika ya Kusini(South Africa). Ila bahati mbaya huyo Binti nilie tarajia kuowa naye kaniotea meno ya juu na mapenzi ya mimi naye yakaisha!

Kwavile nilikuwa katika mahitaji ya kuowa ukizingatia nilie tarajia kuoana naye kaniotea meno ya juu, basi nilikuwa sina jinsi, nilikubali kumsamehe nakurudiliana na yule mpenzi wangu wa zamani ambaye kwa sasa ana watoto wa wili.

Mwana dada huyo ameniomba tuwe mke na mume (tuowane) tusameheane na kusahau yalio pita.

Kwa kweli na mimi najihisi kumpenda, licha ya disappointments. Pia amekubali kunisaidia katika mpango wangu wakusoma kwavile yeye anafanya byashara na anauwezo kunizidi.

Sasa mimi nina wasiwasi kwa sababu amesha nisaliti mara mbili na kuzaa watoto wawili na wanaume tofauti! Huwa nahisi huenda akajakunisaliti tena baada ya kumpa moyo wangu na kumchukua kama mke wangu.

Kwa kweli Dada mpendwa nahisi kumpenda nakuwa tayari kumuowa huyo mwana dada licha ya disappointments zilizo tokea na watoto wawili anao sasa!

Ila nazungumuza na nafsi yangu ya kwamba nisisubutu kumkabidhi moyo wangu hadi pale ntakapo ona mapenzi ya dhati kwake.

Mimi sina mtoto wala sijawahi kucheat. Dada mpendwa je ni busara kwangu kuowa huyo mwana dada?

Nini hasa kinaweza nipata kwa siku za usoni? Tafadhali Dada yangu mpendwa naitaji ushauri kwa hali na mali ili nisije kujutia baadaye. Asante kwa msaada wako Mungu akujali.

*********

Dinah anasema: Ni njema kabisa kaka Mpendwa, ahsante kwa ushirikiano.

Huyo mkimama ni mapepe. Sio mwanamke wa kuishi nae kwa kumuamini kama mkeo sio tu kwa vile anawatoto wawili bali jinsi alivyowapata hao watoto wake.


Mara zote anakuterekeza halafu anaenda na mkibaba mwingine na kuzaa.....logically unadhani anafaa kuwa mkeo?



Mke/Mume ni mshiriki wako wa kudumu anaepaswa kukuoenda, kukuheshimu na kukuthamini, kuku-support na kukushauri sio kukimbi kwa wanaume/ wanawake wengine kila unapokuwa mbali au kila likapotokea tatizo.



Anatumia "mali" ili akupate kirahisi.....anajua unahitaji la kusimama huko SA pia anajua unahitaji la kuoa baada ya kutolea nje last minute na Moyo wako bado haujapona vema hivyo Kisaikolojia na Kihisia haupo sawa.


Hali hiyo inaweza kukufanya uingie kwenye ndoa au uhusiano ili kujirudishia ile hali ya kujiamini tena baada ya kuachwa. Hali ya kuhisi kuwa unapendwa baada ya uliempenda kuingia mtini.



Ukiachilia mbali hali yako Kihisia na Kisaikolojia.....je ni kweli kabisaaaaa upo tayari kuishi ukiwa unasikia kuhusu Exes na kuona (watoto) wao waliozaliwa baada ya huyo mkimama kukusaliti?


Ingeleta unafuu kwa mbali kama aliwazaa hao watoto kabla hamjakutana japo sio rahisi kuishi na mtu ambae ex zake wanahusika kwenye mahusiano na maamuzi yenu kwenye maisha yenu yote yaliyobaki.



Mf: Ex kamuudhi mkeo kutokana na mtoto wao.....mkeo anakununia au kukufokea wewe na mengine mengi.....trust me ni mzigo.


Fact of life(usinihukumu Maisha magumu bana): Sasa kama upo Single Kaka yangu na unahitaji msaada alioku-offer chukua lakini hakikisha humpi Mimba na wala hakutegeshei kushika Mimba na usionyeshe kuwa unataka sana mtoto(jifanye 2 alionao wanatosha) na kubwa lao USIFUNGE NAE NDOA.


Jiwekee mipango inayokwenda na muda kwamba ndani ya miaka miwili nitakuwa nimemaliza Masomo au nimesimama Kibiashara (hakikisha haimuhisishi yeye) Ukikamilisha mipango yako achana nae.


Ni vema kumwambia ukweli kuwa 2 kids ni hell of Mzingo na huwezi kuwa wanakupa kumbukumbu mbaya kila ukifikiria walivyopatikana.



Atakulaumu umemtumia nakadhalika.....ungekuwa kwenye Uhusiano ningekushauri vinginevyo.

Kila la kheri.

Monday

Utajuaje kama unadanganywa?


Kiufupi nilikuwa ktk mahusiano na mdada mwanzoni tulipendana sana nilijitolea kwa mengi katika umoja wetu.


Sasa alianza kubadilika kitabia kiujumla akawa hanijali, msili, hana muda na mimi, ahitaji ushirikiano na mimi.



Ikafika kipindi nikaanza kuhisi nasalitiwa lakiji nilimvumilia. Sasa nahitaji kujua je huyu Dada ni mkweli kwangu na ananipenda au? maana kuwa karibu na mimi imekuwa shida au tunakuwa tunagombna sana.




Nikiwa nahitaji kujua kitu kuhusu yeye lazima tuishie kugombana. Sasa hivi imefika mwaka tupo kwenye mahusiano lakini simuelewi.

Sijawahi kufanya nae mapenzi nae nahisi hiyo ndio sababu ya kufanya haya yote na aliniambia yeye ni Bikra.


Pia napenda kujua sifa za Bikra au utatambuaje msichana ulienae ni Bikra au la! na utajuaje kuwa unadanganywa au la!

***********

Dinah anasema: Hello there. Ahante kwa ushirikiano.

Umri wa uhusiano wenu ni mdogo sana kujua kama mtu kabadilika. Nadhani hajabadilika isipokuwa hana hisia alizokuwa nazo kwako mlipoamua kuwa pamoja.


Nimeondoa sehemu ya maelezo yako ili kukuachia a bit of privacy. Umri wa binti huyo ni mdogo kwa yeye kujua atakacho kutokankwenye uhusiano. Bado yupo kwenye kipindi cha mpito cha kujifunza ujinsia wake.

Anapata hisia za kutaka kuwa karibu na mwanaume na kuna kuwa na wengi wanavutiwa nae na hivyo anashindwa kujua wapjnpa kwenda na ku commite......hii haina maana kuwa analala nao la hasha....bali wanakuwa kichwani na hivyo kumhuia vigumu kufanya uamuzi.

Wanaume wengi kumtaka inampa hali ya kujiamini na haoni tatizo kuachana na wewe kwani kuna foleni.


Sasa unapokuwa too demanding na kuanza ku act as if umemuoa au kama Baba au Kaka yake ndio matatizo yanapoibuka.

Anahitaji kuwa huru anapokuwa nje ya nyumbani ambako kuna wafuatiliaji (Baba na Kaka)......sasa kama hapati uhuru kutoka kwako ni wazi atatafuta namna ya kuachana na wewe.

Kama bado unataka kuwa na uhusiano huu basi unahitaji kubadilika......badilisha tabia yako ya kuwa too demanding na ku act kama mume kwake wakati sio mume na pengine hutokuwa mume wake.


Sidhani kama kuyofanya nae mapenzi ndio sababu ya yeye kuwa hivyo alivyo. Nadhani tabia zako kwake ndio zinamsogeza mbali nawe. Kuwa mpenzi na sio Baba au kaka.....punguza maswali na upunguze kumfuatilia.


Kujua kama mtu anakudanganya ni rahisi ikiwa unajua kuitumia sixth sense yako. Pia kama umeishi na mtu huyo kwa muda ambao ni zaidi ya miaka 2. Hii ni kwasababu mtu unaeishi nae hawezi kuigiza kwa miaka 3.....lazima atachoka na kuvua Wasifu.


Baadhi ya watu huingiza kwa muda mrefu ili kupata watakacho au zaidi mpaka wakaipate.



Utamjuaje kama ni Bikira? Well hakuna njia zaidi ya kumuamijk kuwa hajawahi kushiriki tendo. Siku ya siku ikifika rudi kwangu uniamjie ilivyokuwa then nitakuambia kama ni mara ya kwanza kwake au siku ya kwanza na wewe.


Nia na madhumuni ya Uhusiano wa kimapenzi ni kukubalibali kuwa na mtu umpendae na kufurahia umoja wenu.



Ikiwa kwenye umoja huo hakuna furaha na unadhani hakuna namna ya kuipata furaha baada ya mazunhumzo na mabadilikonkadhaa basi ni vema kutoka na kuanza upya.

Kila la kheri.

Tuesday

Kazaa na kuolewa kisa Umbali.....nipo radhi kurudiana.

Nimatumaini yangu humzima dada dinah pole na kazi unayoifanya ya kutuelimisha.
Mm nikijana ninae ishi Mbeya.


Nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda kidogo. Nilikuwa ninampenzi wangu ambaye nimekuwa nae zaidi ya miaka 2 huyu mpenzi wangu alikuwaga rafiki yangu toka utotoni na ukweli tulikuwa tunapendana sana.



Na tulikuwa tunamipango mizuri kama wapenzi na nilikuwa kwenye mipango ya kumtambulisha nyumbani kwetu kwa wazazi wangu japo nyumbani wazazi walikuwa wakimfahamu.



Sasa huyu mwenzangu alihitaji kujiendeleza kimasomo na kweli alipata Chuo, kwenda kusoma kwa mwaka mmoja kwahiyo Morogoro ambapo alikuwa anaishi na nduguzake.


Mahusiano yetu yaliendelea vizuri huku tukiwa tunawasiliana na tulikaa mwaka mzima bila yakuonana. Tulijitahidi kuonana lakini fedha ilikuwa kikwazo kwasababu ya umbali hivyo tukakubaliana amalize masomo yake atakapo rudi tutaonana.




Kama unavyojua mkisha kuwa mbali na hasa wapenzi kukorofishana kupo. Kuna kipindi tulipishana na hatukuwasiliana ndani ya mwezi mmoja ila tulikuja kupatana tukaendelea kama kawaida.



Kumbe ktk kipindi ambacho tulipishana na mwenzangu yeye alipata mwanaume mwingine ambaye alimpa Mimba na kipindi tunasameehana alikuwa tayari ana Mimba na ukweli alinieleza



Sasa huyo jamaa aliye mpa Mimba alikuja akamuoa huyo binti na mpaka sasa amejifungua mtoto. Lakini tatizo lililopo kwangu huyu mwanamke muda wote amekuwa akiwasiliana na mimi na amekuwa akiniambia bado ananipenda na hata mimi moyo wangu bado unamuhitaji.



Alikubali kuolewa kwasababu ya ile Mimba maana kuna kipindi alitaka kuitoa ili aendelee kuwa na mimi ila mimi nilimsihi asifanye hivyo.

Naomba ushauri wako dada dinah mimi bado na mpenda huyu mwanamke hata yeye ananipenda na yupo tayari kumuacha huyo mumewe.

************

Dinah anasema: Mungu anabariki na ahsante kwa ushirikiano.

Kwanza napenda ufahamu kuwa mwanamke hapewi Mimba bali anashiriki kwa hiari yake tendo ambalo matokeo yake ni mimba.


Sio kama mwanamke alimfuata na Mimba kisha akambebesha bali mbegu za jamaa na yai lake ndio Mimba so hakupewa Mimba na bali kashika Mimba. Hilo moja.



Pili....kuna uwezekano mkubwa kuwa aliahidiwa kwenda huko ili akasomeshwe na huyo mkibaba.....kumbuka umesema hukuwa na pesa hata za kufanya mawasiliano.



Kutokana na mahesabu yangu ya ghafla hapa sio rahisi kwa mtu kwenda mahali kusoma na ndani ya mwaka mmoja kushika mimba na kuolewa....ni wazi kulikuwa na kauhusiano kasiko rasmi lakini serious na huyo mjamaa hata kama ulikuwa ule wa Internet sijui whasaap bin facebook na walipokutana ikawa kama wamejuana kwa miaka kadhaa.....uaicheze na Power of mawasiliano ya Kimtandao.



Huyo mwanamke hakuolewa kwa sababu ya Mimba.....alishika mimba kwa vile hakutumia Kinga na ameolewa kwasababu alitaka hiyo Ndoa.



Maana kama kweli Mimba ilimfanya aolewe ni wazi hakutaka kulea mtoto bila baba yake.....sasa jiulize kwanini leo akuambie kuwa yupo tayari kuiacha ndoa ili aje kuwa na wewe halafu na wewe uamini?



Najua unampenda au unahisi kuwa unampenda kwasababu katika umri wako niliouficha ni wazi kuwa unahitaji kusafisha macho a bit more kabla haujajua kama ulipenda huyo Binti au unadhani kuwa ulimpenda.


Umekwisha sema pesa ilikuwa kikwazo sasa je ukirudiana na huyo mwanamke na mzigo wake ambao ni mtoto utakuwa tayari kumsaidia kumlea mtoto huyo in terms of pesa? Au utakuwa fine mwanaume mwenzio kukusaidia kumtunza mpenzio.....Maana watoto ni gharama.


Je? Unampango gani na huyo mwanamke.....unataka tu uhusiano wa nakupenda tangu enzi au unamalengo mengine huko mbele Ndoa ikiwa moja wapo.



Usijekubali aache ndoa aje kwako kisha siku yakimshinda kwako au usipomtimizia mahitaji ya mwanae akulaumu kwa kumharibia maisha yake na mwanae.



Nadhani ni vema kukubali tu kuwa hakuna future kati yako na huyo mkimama.

Poteza mawasiliano yale na wewe go out a bit more ukapate penzi la kweli kutoka kwa mtu mwenye kukuthamini jila kujali umbali au kipato.




Akiendelea kukufuatafuata mwambie ungependa kuanza fresh bila kuhofia mtoto wa mwanaume mwingine ulietereza nae nje ya uhusiano wetu.


Ka cheat.....kashika Mimba na kaolewa na huyo alieCheat nae bado unataka kurudiana nae?

Wacha kujishusha chini zaidi ya tumbo la Nyoka......jirudishie heshima na kujiamino kwa KUSONGA MBELE BILA YEYE.

Kila la kheri.

Pages