Wednesday

Hivi Limbwata kweli Ipo?

"Mimi dada Dinah, leo nataka kuja na mpya, huenda ikawa ni kero au nikuomba msaada. Si mpya kwamba ni jambo ambalo halipo, ni mpya katika uwanja huu wetu. Na huenda si mpya, umeshaligusia, ila hatukulipa kipaumbele kwasababu ni jambo lakukosa `elimu’. Na huenda sio kukosa elimu tu kwani wapo wenye elimu zao wanaliendekeza.


Tuliite ni Imani za watu fulafulani.Yupo jirani yetu ambaye tunaweza kumuita `womenizer’ au mhuni au mume mwenye pepo wa ngono. Jamaa huyu hakikatizi kitu, kila amuonaye kwake ni mzuri, na alivyo na kisimite, huwa akiomba hakosi.


Alikuwa akitamba kuwa wake kwake ni kama shati, hataki wamtawale milele ingawaje kaoa. Na cha ajabu alienda kupima ngoma hana! Mke wake ni mpole, mke toka kijijini, katulia home, kimya (kaziba masikio kwa pamba). Sasa mke wake akawa analalamika, baada ya mambo kumzidi na bahati alikuja hadi kwa my wife kuomba ushauri.


Kabla hajapewa ushauri alishakuwa na nia moja ya kwenda kutafuta `dawa ya mapenzi’-limbwata au love potion, alimwambia mke wangu ana nia hiyo.Hutaamini, kumbe licha ya mke wangu kumshauri vinginevyo, kuwa `ndoa’ ni kuvumiliana na hakuna dawa ya mapenzi inayoweza kusaidia, na huenda ikaharibu kuliko kusaidia.


Alipewa mifano ya watu mbalimbali ambao inasemekana waliwafanyia waume zao na matokeo yake yakawa kinyume chake. Lakini hakuelewa, alienda kwao mikoani na aliporudi, ndipo tulipoona mabadailiko. Hutaamini lakini ndivyo ilivyotokea.

Yule bwana akawa habanduki nyumbani, yule jamaa akawa hazungumzi na watu hasa wanawake. Hata marafiki zake ambao walikuwa wakikesha naye kwenye bar wakaanza kutilia mashaka. Kulikoni mwenzetu huyu vipi! Jamaa hutaamini hata kazi yake ya udereva wa masafa marefu akaamua kuiacha na alinzisha biashara ndogondogo karibu na nyumba yake.


Wengine waliofika kwake wanasema kawa mume-bwege. Jaribu kufikiria mtu alivyokuwa awali na sasa utafikiri ni watu wawili tofauti.Sasa dada Dinah, sio vizuri kuchimba sana undani wa huyu jamaa na mkewe, ila ndio nimekuja na hili swali jipya, huenda kuna watu wana uzoefu nalo. Huenda kuna watu ya mewakuta au jamaa zao.


Huenda hata wewe mwenyewe umeshawahi kuona, kukuta, hatuwezi kupata maoni ya jambo hili ili kuboreshana kimahusiano, kuonya au kupeana ushauri?What is `love potion’ Limbwata au neneo gani jingine sijui. Hiki ni kitu gani hasa, je kipo,? Je kinasaidia, je nini madhara yake kwa wanandoa au wapenzi? Je kinafanywaje kwa wale wanaojua, na wengi wanaoendekeza hili ni akina mama, twaomba msaada jamani." Mimi Emu-three

Jawabu: Well, mimi sina uzoefu na hili ila nimesikia na hata kuulizwa dawa ya mapenzi na nini na siku zote jibu langu ni kuwa mapenzi hayana dawa ni hisia za mtu juu yako, hazilazimishwi.

Limbwata kwa ufahamu wangu ni ushirikina na inafanyakazai kama ambavyo nguvu za giza/ushirikina unavyofanya kazi inategemea zaidi umenuia vipi (nia yako ni nini hasa when doing it).


Sasa unapomwendea mpenzi wako kwa mtoa Limbwata ni wazi kuwa humpendi na unataka kumbadilisha utakavyo wewe kwani atakapofanyiwa Limbwata atakuwa na "characture" nyingine kabisa na hatoonyesha mapenzi kwako bali atakuwa mjinga kwa kutofanya vitu ambavyo "real man does" hachezi mbali na wewe/nyumbani, haishi kukuzungumzia na kukusiafia mbele ya watu wengine, kulia nakuomba msamaha kila manapozozana, kufanya kila unachoamuru afanye n.k.


Hayo sio mapenzi kwa vile sio hisia zake juu yako na anafanya vitu sio kutoka moyoni kutokana na hisia zake ju yako bali kichwani kutoakana na ulivyo/alivochezewa/changanywa/blackmailed.
Mara nyingi hali hii inapomuishia mtu aliye-Limbwatika huwa hana mapenzi kabisa na mpenzi wake, yaani hali inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa awali.


Wanawake wengi wanaofanya hivi ni ama waliolewa kwa vile wanatabia njema kama wake lakini waume zao hawakuwapenda, wanawake ambao hawajiamini kiuchumi au kuendesha maisha bila mume/mwanaume, wanawake wanao Imini kuachika au kuomba Talaka ni aibu kwa jamii hivyo anaamua ku-stick kwenye ndoa yake n.k.


Hili lipo, linafanya kazi kama nguvu nyingine za giza na hufikia muda nguvu hizo zinaisha.Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu ni kujiamini na kutolazimisha penzi, kwani hata ukim-limbwata mwenzio atafanya utakavyo lakini wewe unajua moyoni kuwa hakupendi.


Vilevile ni vema kuzingatia msemao wa kale usemao "mpende akupendae na asie kupenda achana nae".Hata kama uko kwenye ndoa na unaona wazi kuwa ndoa yako doesnt work pamoja na kujaribu kwako kote, usilazimishe omba Talaka endelea na maisha yako ukiwa huru.....mambo ya kung'ang'ania penzi wakati unajua hupendwi ni uzamani. Kunafaida gani ya kuwa mpweke ndani ya uhusiano/ndoa?

Wengine wataendelea.....Asante M3

No comments:

Pages