Thursday

Mke wangu akerwa na Kitumbo......Ushauri!


"Dada Dinah. Naomba niweke swali langu tena hapa.Mimi nina tatizo kidogo nahitaji kusikia ushauri wako na wa wasomaji wote wa ukumbi huu mzuri.

Nina ndoa yangu kwa miaka sita sasa tuna mtoto mmoja na tunategemea mwingine Mungu akijaalia mwaka huu. Baada ya uja uzito wa kwanza tumbo la mke wangu halikurudi katika hali ya mwanzo, yaani alikuwa na kitumbo kinamna fulani. Lilipungua lakini si katika hali ya mwanzo au tuseme ya kawaida.Tumejaribu kutafuta tight ya tumbo lakini haikusaidia, ingawa labda haikuwa nzuri sana.

Sasa tukafikiri na kuona labda kabla hajajifungua safari hii tujaribu kupata utaalamu wa jinsi gani tunaweza kupunguza na ikiwezekana kurudisha tumbo lake katika hali ya kawaida, maana hata yeye mwenyewe inamnyima raha kiaina. Sasa ni njia gani nzuri za kutumia zisizokuwa na madhara kwa afya? Nitafurahi mno kusikia ushauri na kama tutafanikiwa katika hili."
Jibu: Napata matumaini kuona kuwa wewe mwanaume unaungana na tatizo linalo mkera mkeo na kutafuta namna ya kumsaidia ili ajisikie anavutia tena baada ya kujifungua (wanawake wengi hujihisi kuwa hawavutii tena) kitu ambacho ni muhimu ili kumrudishia Mkeo kujiamini kwake akiwa mtupu hali itakayo pelekea ninyi wawili mfurahie miili yenu kwa uhuru zaidi.
Upangiliaji wa mlo (diet) na mazoezi kwa ruhusa ya Dakitari wake ni muhimu kutegemeana na alivyojifungua kwamba amejifungua kwa kawaida (asilia) au kwa upasuaji.
Pamoja na kuwa kufanya mazoezi kuna-sound rahisi mama wengi hushishwa kuyafanya kutokana na uchovu au kuwa na shughuli nyingi zinazohusiana na swala zima la kuwa mama.
Kabla hajaanza mazoezi ya kupunguza na kulikaza tumbo lake baada ya kujifungua atapaswa kulifunga (kiasili au kibongo-bongo) na vilevile kujitahidi kupunguza unene ulioongezeka kutokana na ujauzito na anaweza kufanya hivyo kwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kutembea haraka-haraka n.k alafu baada ya kupunguza unene ndio afanye mazoezi niliyoyaelezea kwenye topic hii Mazoezi ya tumbo. Kila la kheri ktk kumpokea mtoto mpya.

Tuesday

D'hicious.....a Year on!



Shukurani za dhati kwako wewe msomaji kwa ushirikiano wako, Rafiki zangu wote walioiweka D'hicious kwenye site zao kwa moyo mkunjufu na wenye furaha nasema Mungu awabariki sana kwa kuthamini mchango wangu ktk jamii ya Kitanzania "mtandaoni".

Katika safari hii ya miezi 12 nimekumbana na vishawishi vingi as you can imagine, nimekutana na kutengeneza mafariki wengi kutoka sehemu mbali mbali za Dunia, nimejifunza mengi kutoka kwa watu wengine na hata kukabiliana na "bullies".

Nisingekuwa nakiburi cha kuvuka miezi 12 na kusema nilichokisema leo hii bila ya Rafiki yangu mpenzi na wa Siku nyingi, Geeque aambae mimi huwa napenda kumuita "Jiikyuu" au GQ ambae siku zote usiku na mchana alikuwa pale kwa ajili yangu, huyu bwana ni kimbilio, nguzo na shujaa ktk maisha yangu "mtandaoni" ambayo time to time nilikuwa napata wakati mgumu kutokana na vitisho, abuse na vishawishi.

GQ unaja kabisa kuwa bila wewe D'hicious ingekuwa hadithi.......Asante kwa yote na Mungu akubariki sana.


Monday

Mam'mkwe hanipendi je niolewe?...Ushauri

kelly said..."Habarini za saa hizi wadau wote wa dinah.... mimi jamani nina jambo linanitatiza ningependa dinah na wadau wengine mnisaidie, kama nimetoka nje ya mada basi mnisamehe bure.... mimi nina mchumba uhusiano wetu mpk leo unamiaka minne,mwaka wa tatu nilivalishwa pete sasa tatizo ni kuwa mchumba wangu hataki nionane na mama yake kwa madai mama yake mkorofi ila ndugu wengine wote nawajua nawananijua na wanataka tuoane hata kesho,kwetu pia anajulikana.

Yeye anaishi kwao na mimi naishi kwetu na kila siku tunaonana na weekend tunashinda wote.... ila linapokuja swala la mama yake yupo sehemu fulani basi hatutaenda hiyo sehemu ili tu nisionane na mama yake.... sasa wadau kama jamaa anataka niwe mkewe itakuwaje hapo?


Nilishaambiwa na wifi zangu kuwa mama yake hanipendi,na yeye ndio kipenzi cha mama yake,siku moja nilimwambia kama mama yako akikataa tusioane itakuwaje akasema ooh atake asitake mimi nikishajipanga nakuoa yeye shauri yake.

Kwa upande wangu mimi sitaki kuoana nae kama mzazi wake huyo hatokuwa radhi na pia sikotayari kumpoteza kwa vile nampenda sana..... wadau na dinah naomba msaada wenu wa mawazo kama nitakuwa sijaeleweka niulizeni nitawafafanulia pale ambapo hamjanielewa nawapenda wadau wote wa dinah "

Thursday

Utachumbiwa lini.......? Make him(II)

White Gold & Diamond!
4-Ni mwiko kuwa tegemezi, hakikisha unafanya kila uwezalo kuonyesha kuwa unaweza kufanya mambo yako kivyako bila kuomba-omba (vibomu) unless umekwama kweli kweli yaani malipo yamechelewa au biashara hajaenda vema mwezi huu na mwenye nyumba anatishia kukuweka nje, hakikisha tukio hilo halijirudii mara kwa mara.

Kumbuka kuzungumzia malengo yako ya baadae (sio ndoa) malengo yako kimaisha kwamba ungependa unatafuta kiwanja ili ujenge nyumba hata ya chumba kimoja Mungu akikujaalia, ungependa kununua shamba mahali na kufanya kilimo cha mboga-mboga n.k.

Sahau au usithubutu mambo ya kisistaduu uchwara ya ningependa kufungua duka la kuuza nguo, kufanya pati kubwa ya kuzaliwa kwangu au kununua Prado.....haitosaidia kwani ni kama vile unamwambia akupe mtaji.....zungumzia vitu vikubwa vya kudumu.....atakuona una akili ya kimaendeleo na unafaa kua wa milele Daima.


Sisemi kuwa usipokee zawadi au "mshiko" aki-offer si kajitolea bwana.....hiyo bomba lakini kale ka mchezo ka' kumfanya mpenzi wako kitega uchumi sio njema kwani kila mtu anamajukumu yake ujue! Mwanaume akionakuwa unaweza kujitegemea bila kuwa na kiburi (uswawa kwa sana)anakuwa na uhakika na maisha yenu ya baadae kama familia, na hivyo kusogeza swala la ichumbana ndoa karibu zaidi kuliko alivyopanga kuwa mpaka ajenge nyumba, kumiliki biashara kubwa n.k.


Kwani atajua wazi kuwa mtashirikiana na kufanikisha mambo haraka zaidi ikiwa mko pamoja kama mke na mume......ni kweli ukiwa mwenyewe kufikia malengo inachukua muda mrefu sana (kutokana na uzoefu wangu) lakini mkiwa wawili ktk ndoa malengo yanafikiwa chap-chap....kumbuka usemi usemao umoja ni nguvu na...........!

Hivyo mwanamke usibweteke fanya bidii ktk shughuli zako na onyesha kuwa unaweza kuweka tofauti ktk maisha yenu (ikiwa mtafunga ndoa) hali itakayomvuta mpenzi kutangaza ndoa.


5-Kamwe narudia tena kwamwe usiruhusu amalizie manii yake ndani hakikisha na ni mwiko kutumia madawa ya kuzuia mimba (kisa cha kubadili mwili/maumbile yako) kwa mwanaume ambae hajakuchumbia, hakikisha manatumia "condom".....Kwanza hurushisiwi kabisa kufanya ngono lakini kutokanana mfumo wa maisha wa sasa, wadada tunabaki shuleni kwa muda mrefu tofauti na miaka ile na kuizuia nature inakuwa ngumu hivyo inabidi tu ufanye ngono nje ya ndoa.

Sasa kama huruhusiwi kufanya Ngono b4 ndoa kwanini unamruhusu mwanaume akumwagie ndani wakati unajua kabisa uhusiano wenu sio "commited" kwa sasa....nina maana hakuna pete ya uchumba? Ukimimbika je?Kumbuka unafanya ngono kabla ya ndoa ili kufurahisha mwili na sio kujenga familia (which is the Main reason ya kukutanisha miili yetu kwamujibu wa Sayansi na Dini)......kama anakupenda kweli, yaani kafika mwisho wa Reli lakini unamzuia kumalizia ndani ni wazi kuwa ataharakisha mambo ya kutangaza ndoa ili apate uhuru.......wenyewe wanasema "kumiliki mwili wako nje na ndani".


Baada ya kufanya yote haya na mengine ya kumfurahsiha na kumridhisha kitandani na nje ya kitanda ktk mwaka mmoja na bado hajatangaza ndoa? Aaaah lazima kuna kipengele nimekiacha, sasa hebu niambie mpenzi wako anapenda nini zaidi yaani kama vipi anaweza hata ngono akaiweka pembeni ili amalize anachokipenda na ikiwa hakijaenda alivyotaka basi ngono inakuwa "out of the window".

Nikipata majibu yako then nitakupa Mbinu ya mwisho (nitaweka ktk mtindo wa Polls kulia kwa site hii) na baada ya hii (mbinu ya mwisho) ndoa haijatangazwa basi no matter how much you love the guy ujue you are not enough to be his wife acha kupoteza muda, tafuta ustaarabu mwingine, maisha mafupi atii!

Kila la kheri.

Friday

Hatubadiliki bali tunakua/pevuka

Sote huwa tunasikia kama sio wewe unauzoefu tayari wa kulalamikiwa na mpenzi kuwa tumebadilika. Utasikia mkizozana kidogo mwenza wako anasema "siku hizi umebadilika sana, zamani hukuwa hivi" anaweza hata akakupa mifano hai lakini wewe unaweza ukabisha kwa nguvu zote na kushangaa au kujiuliza umebadilika nini? Mbona uko vilevile tu kitabia na kimuonekanao.


Lakini katk hali halisi huwa kuna kuwa na mabadiliko makubwa sana(ukuaji), wewe huyaoni kwavile ni sehemu ya ukuaji wako hivyo unabadilika automatically bila wewe kutambua. Ukiangalia nyuma ulipokuwa teen ni tofauti na sasa ambapo uko kwenye early 20s na unapofikia late 20s utakuwa na tabia tofauti na hapo awali hali kadhalika unapofikia miaka 30, 40 na kuendelea.


Wenza wengi hugombana na kutofautiana kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa vile huwa wanategemea wapenzi wao waendelee kuwa vilevile walivyo kutana nao miaka 6 au 15 iliyopita. Hawajui kuwa inategemea zaidi umekutana nae akiwa na umri gani, ukikutana na mpenzi yuko kwenye late 20s au early 30s huwa hakuna mabadiliko......lakini kama ulioa/olewa nyote mkiwa watoto au mmoja wenu ni chini ya miaka 27 basi mimi hapo wala sina la kuongeza!

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo? Unanyongeza? basi nafasi ni yako.....

Mwisho mzuri wa wiki. XXX

Thursday

Vijana wa sasa wanaharaka sana

Tofauti na zamani vijana sasa wamekuwa wakihofia zaidi kukutana na "the one" mapema zaidi ktk maisha yao kuliko kufanya bidii na kuzingatia masomo ili ufike mahali fulani kielimu au kimaisha (kazi/biashara), natambua kufaulu mitihani sio kufaulu maisha na kufeli mitihani sio kufeli maisha ni wewe tu na mipangilio yako si ndio jamani au?


Sina hakika ni nini hasa kinapelekea mfumuko wa hawa Dogo wengi kutaka kufunga ndoa au kuwa na wapenzi ktk umri mdogo badala ya kuzingatia masomo au pengine kufurahia maisha yao kabla ya kuongeza majukumu mengine kabla hata miili na akili zao hazijakomaa.


Sio kwamba na pinga kuwa na mpenzi au kwamba huyo "the one" hayupo au hapatikani hapana, unastahili kuwa nampenzi kutokana na matakwa ya mwili wako lakini sio kwa kumsaka na kupoteza muda mwingi kwenye "sites" za kutafutia wenza, wachumba au mahusiano ya kimapenzi au maeneo ya vilabu vya usiku, hotels kubwa, maeneo mengine ya starehe.


Katika hali halisi penzi huwa halitafutwi bali hujitokeza lenyewe tu ikiwa moyo wako utampenda mhusika, sasa kitendo cha kuanza kwenda kujiandikisha kwenye hizo "sites" kutafuta wenza ktk umri wa miaka 17-24 mimi binafsi nahisi kuwa ni kujipotezea muda na kujiongezea "stress" ambazo sio za msingi kabisa kwenye maisha yako ktk umri huo mdogo.


Baadhi yao wanajitosa kwenye "dating sites" au "maeneo ya starehe ya wanaojiweza" ili kukutana na wanaume/wanawake ambao tayari wamejijenga ili yeye akiingia kwenye uhusiano huo aweze kutumia vile ambavyo mwenzake amevihangaikia na kuvitolea jasho ili mtaani wamkome, sisemi kuwa huna haki ya kutumia mali (nyumba, gari, pesa) ya mume/mke au mpenzi wako kama anakuruhusu kufanya hivyo lakini huitaji ku-focus kwenye kutafuta mpenzi mwenye aina fulani ya maisha kwani kwa kufanya hivyo sio haki.

Sasa imefikia hatua hapa nyumbani (bongo) kuwa na boyfriend au girlfriend ni lazima kama vile kula au kuoga kama sio kuvaa chupi, unakutana na vitoto vidogo ndio kwanza vimemaliza shule ya Sekondari vinahangaishana mtaani na kwenye kumbi za starehe kama sio online kutafuta "the one".

Achana na swala zima la kuhaha huku na kule kutafuta mpenzi ktk umri huo mdogo na badala yake zingatia kitabu au kazi, tunza mapato yako na furahia maisha yako na huyo "the one" muda ukifika utakutana nae tu.


Wewe unasemaje kuhusu hili?......karibu.

Pages