Tofauti na zamani vijana sasa wamekuwa wakihofia zaidi kukutana na "the one" mapema zaidi ktk maisha yao kuliko kufanya bidii na kuzingatia masomo ili ufike mahali fulani kielimu au kimaisha (kazi/biashara), natambua kufaulu mitihani sio kufaulu maisha na kufeli mitihani sio kufeli maisha ni wewe tu na mipangilio yako si ndio jamani au?
Sina hakika ni nini hasa kinapelekea mfumuko wa hawa Dogo wengi kutaka kufunga ndoa au kuwa na wapenzi ktk umri mdogo badala ya kuzingatia masomo au pengine kufurahia maisha yao kabla ya kuongeza majukumu mengine kabla hata miili na akili zao hazijakomaa.
Sio kwamba na pinga kuwa na mpenzi au kwamba huyo "the one" hayupo au hapatikani hapana, unastahili kuwa nampenzi kutokana na matakwa ya mwili wako lakini sio kwa kumsaka na kupoteza muda mwingi kwenye "sites" za kutafutia wenza, wachumba au mahusiano ya kimapenzi au maeneo ya vilabu vya usiku, hotels kubwa, maeneo mengine ya starehe.
Katika hali halisi penzi huwa halitafutwi bali hujitokeza lenyewe tu ikiwa moyo wako utampenda mhusika, sasa kitendo cha kuanza kwenda kujiandikisha kwenye hizo "sites" kutafuta wenza ktk umri wa miaka 17-24 mimi binafsi nahisi kuwa ni kujipotezea muda na kujiongezea "stress" ambazo sio za msingi kabisa kwenye maisha yako ktk umri huo mdogo.
Baadhi yao wanajitosa kwenye "dating sites" au "maeneo ya starehe ya wanaojiweza" ili kukutana na wanaume/wanawake ambao tayari wamejijenga ili yeye akiingia kwenye uhusiano huo aweze kutumia vile ambavyo mwenzake amevihangaikia na kuvitolea jasho ili mtaani wamkome, sisemi kuwa huna haki ya kutumia mali (nyumba, gari, pesa) ya mume/mke au mpenzi wako kama anakuruhusu kufanya hivyo lakini huitaji ku-focus kwenye kutafuta mpenzi mwenye aina fulani ya maisha kwani kwa kufanya hivyo sio haki.
Sasa imefikia hatua hapa nyumbani (bongo) kuwa na boyfriend au girlfriend ni lazima kama vile kula au kuoga kama sio kuvaa chupi, unakutana na vitoto vidogo ndio kwanza vimemaliza shule ya Sekondari vinahangaishana mtaani na kwenye kumbi za starehe kama sio online kutafuta "the one".
Achana na swala zima la kuhaha huku na kule kutafuta mpenzi ktk umri huo mdogo na badala yake zingatia kitabu au kazi, tunza mapato yako na furahia maisha yako na huyo "the one" muda ukifika utakutana nae tu.
Wewe unasemaje kuhusu hili?......karibu.
No comments:
Post a Comment