Monday

"Abnormalitie" ktk uhusino wa kimapenzi....Ushauri!

"Asante sana dada Dinah kwa kutoa Elimu kwa watanzania wenzako. Samahani mimi naomba nitoke nje ya maada kidogo. Naomba niongelee suala la abnomaralities katika miili yetu na madhara yake katika mapenzi.

Abnormalities zenyewe ni mfano mwanamke kuwa na ndevu, wasichana au wavulana kuwa na mvi katika umri mdogo au wanakuwa wamezaliwa nayo. Kidogo mvi watu hutumia dawa( dye) kuzuia mvi, ila ndefu kwa wanawake imekuwa vigumu.

Nataka kujua je wasichana wenye ndefu na ambao hawajaolewa, wanapata wachumba? Swala la pili ni mimi mwenyewe: Mimi ni mvulana wa miaka 27. Nina mvi kiasi kichwani.

Nimekuwa na tabia ya kuzipata rangi ili zisionekane. Lakini girlfriend wangu wa kwanza siku moja aninikuta nikipaka rangi nywele zangu, then nikamwambie sababu, tangu siku hiyo akasema niache kupata rangi kuwa yeye haoni tatizo na hizi mvi zangu, akasema tena zinanipendeza sana.

Nilikaa naye miaka 4 tukaachana. Sasa ninaye girlfriend mwingine. Nimekaa naye miaka 2 sasa lakini hajui kama nina mvi kichwani kwani huwa nazipaka rangi. Tunapendana sana na mwezi ujao nina mpango wa kumvisha pete ya ndoa. Je niache kuzipata rangi mvi zangu ili azione au nifanyeje? Naogopa labda huenda akapunguza upendo wake kwangu.

Kwa ujumla mimi sijui wasichana wanamchukuliaje mvulana au mwanaume mwenye mvi katika umri mdogo. Dada Dinah na wadau wengine naombeni ushauri."

No comments:

Pages