"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka thelathini na tano niimeachana na mpenzi wangu karibu miezi miwili sasa, kilichopelekea tuachane ni mimi kutokuwa karibu nae pia kutofanya nae mapenzi kwa vile sikuwa najisikia kufanya hivyo na nilikuwa naona kama Dunia imenilemea kutokana na kuondokewa na Baba yangu Mzazi. Tatizo nililonalo hivi sasa ni kwamba bado nampenda na ninataka turudiane nifanye nini?"
Jawabu: Pole sana kaka yangu ka hilo lililopelekea wewe kuniandikia mimi. Nimefurahishwa na uwazi wako ktk hili. Niliposoma maelezo yako nikahisi kwamba ulikuwa unasumbuliwa na mawazo mengi kutokana na kuondokewa na mmoja kati ya watu muhimu sana ktk maisha yako, hali hiyo ilipelekea wewe kuwa na aina yua "Depression".
Sasa kabla sijakushauri nini cha kufanya ningependa ufahamu kuwa hali hiyo sasa imekwisha yaani umebadilika au niseme umepona na umekuwa wewe kama hapo awali na ndio maana swala la kutaka kutafuta suluhisho au njia ya kurudioana na mpenzi wako limekujia na umetambua kuwa wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuondoka!
Ni wazi kuwa mpenzi wako hakujua kuwa wewe ulikuwa unasumbuliwa na "Depression" na kwa mawazo ya mwanamke wa kawaida ndani ya Bongo alihisi labda humpendi tena na ndio maana akaamua kujitoa kitu ambacho ktk hali halisi hakupaswa kukifanya na badala yake alipaswa kuwa mvumilivu, kukupa ushirikiano kwenye "nyanja" nyingine na sio ile ya kimwili tu.
Unajua watu tunapokea na kuchukulia matatizo kitofauti sana, kuna wale ambao wakikumbwa na tatizo kama lako huwa haliwapigi/shitua kama ilivyokutokea wewe, na hiyo inategemea zaidi na ukaribu/uhusiano kati yako na mpendwa wako ambae ni Mzee (baba'ko).
Ushauri wangu kwa kuanzia ni kujenga hali ya kujiamini tena kwa kuanza kujichanganya na marafiki (outing), jiunge "gym" au anza kufanya mazoezi ya viungo mepesi (kukimbia, push-ups n.k), soma sana vitabu vya "challenges", angalia funny movies (usiguse zinazohusu mapenzi au huzuni) au jishughulishe na mambo ya shamba, bustani hata kama ni ya maua, usafi n.k (kuwa-busy) na kamwe usipende kukaa peke yako ama kumtembelea mama yako kila wakati (atakurudisha nyuma yaani utakuwa na uzuni zaidi).
Ikitokea uko peke yako basi jitahidi kusikiliza muziki uliochangamka Mf ule wa Mr blue na Chillah wa "Nipo, nilikuwepo na nitakuwepo" au Fiesta wa Ray C au hata ule wa Ngoma zetu sijui kaimba nani au za Mr Ebbo kwanizitakuchekesha kimtindo......those kind of songs na kwa sauti ya juu (usisumbue majirani lakini).
Wakati unaendelea na utaratibu huo anza kwa kuwasiliana na mpenzi wako mara moja/mbili kwa siku (ni salamu najisni gani unamkosa na kumpenda, tafadhali usithubutu ukagusia tatizo lako) Kisha mambo yakiwa "swafi"(baada ya wiki mbili mpaka tatu utakuwa umerudisha kujiamini kwako) na hapo ongeza "gia".
Pendekeza kuwa ungependa kuonana nae kwa ajili ya kinywaji mahala fulani (sio nyumbani kwako/kwake) ikiwa ni mpenzi wa maua basi si vibaya "kuibuka" na "bunch" la maua tafadhali yasiwe ya "plastic" (wanawake wengi tunapenda maua lakini si wote tunathamini maua), ili ushinde basi nunua hereni nzuri kwa ajili yake.
Natambua kuwa mkikutana utapenda kumwambia "nakupenda sana na ninataka turudiane na tupendane kama zamani" ni maneno mazuri lakini sio mwanzo mzuri, nakushauri uzungumzie mambo ya kawaida tu kama siasa, movie, muziki, jamii n.k, mtegee aanze yeye.
Mpenzi wako akijaribu kugusia mambo fulani mliyokuwa mnafanya pamoja kama wapenzi, hapo ujue umeshinda na ndio atakuwa amefungua mlango wa wewe kuomba msamaha na kumueleza ni nini haswa kilikuwa kinakufanya uwe mbali na yeye hasa pale kunako uhondo (kitandani)!
Nakutakia kila la kheri na mafanikio katika safari hiyo ya kurudiana na Mpenzi wako umpendae
No comments:
Post a Comment