Hili Naomba Ushauri wako Dinah!!!Pole kwa majuku na juhudi zako za kutuhudumia sisi kama wana jamii. Nahitaji msaada wa usahauri na mawazo pia juu ya suala hili,
Mimi ninae mpenzi wangu kwa sasa tuna nae miaka mitatu tangu tuwe ndani ya uhususiano huko, pamoja na kuwa maisha yetu yako mbali kwa maana ya mikoa mimi huwa niko Dar kwa wazazi wangu naye Tanga ndio kwao kwa wazazi wake waliko jiwekeza.
Lakini mimi nafanya kazi mkoa wa Kilimanjaro na yeye sasa kamaliza chuo yuko kwao Tanga. Suala kuu hapa ni mimi kushindwa kumuelewa huyu mwenzangu, mara kwa mara huwa nahitaji kufika kwao tukajitambulishe kuwa mimi na yeye tuko katika hayo mahusiano naye na ambayo mategemeo yetu ni ndoa na kumaliza maisha yetu tukiwa pamoja inshallah.
Lakini kinachotokea hapo ni kwamba anakuwa kinyume na hilo na anasema ni vema tukienda kujifahamisha na tusikae mda mrefu then tufunge ndoa, muda ambao yeye aliokuwa anataka usizidi miezi 6, nikamwambia fine mimi niko tayari hata sasa, then hapo sasa akaingiza suala la kusoma.
Kusoma huko ni kuwa mwaka huu kamaliza Advance Diploma ya Accounts na anahitaji kufanya CPA sasa kwa plani na mipangilio tukakuta kuwa kama mungu atajalia na kuenda vema basi mwaka 2009 mwezi wa tano atakuwa kamaliza, nami nikamwambia kuwa sasa tukajifahamishe then Mipango yetu ya ndoa iwe mwezi Decembar 2009 baada ya kumaliza pepazako.
Well, kilichoibuka hapo ni kwamba anasema yeye atakuwa tayari kufanya ndoa mwaka 2010 june, sasa kwa kweli mimi simuelewi mtu huyu kwani naona kama ananichanganya na mimi suala la kuwa niko tu hamapaka huko 2010 bila ya hata japo kufahamika kwa wazazi niko nae siwezi.
Bust still nampenda sana mpenzi wangu sasa sifahamu:- ni kwamba napenda mahala nisipo pendeka au nini hasa!!??Kwani hata wakati yuko chuo nikiwa niko Dar nilikuwa nikienda huko chuoni kwao Arusha na kaa nae kwa cku mbili na kuondoka zangu na baadae nilipokuja pata kazi hapa Kilimanjaro cha ajabu ni kuwa kwa almost mwaka mmoja alikuja mara tatu tu, na some time alikuwa akipata likizo chuo anathubutu kupita hapa moshi bila kushuka na kwenda kwao Tanga same applied akirudi chuo bila kushuka Moshi kuja kwangu.
Kwa hayo naomba msaada wenu wa mawazo ili nami niondokane na utata wa mapenzi.
Jawabu: Pole sana kwa kuwekwa njia panda, nafikiri kinachohitajika hapo kuzingatia na kuifanyia kazi kuu mbili kati ya zile tamo za kuboresha uhusaino wa kimapenzi ambazo kuelewana/kusikilizana, kuheshimiana na kuwasiliano.
Mnahitaji kuwasiliana kwa maana kuzungumza kwa uwazi kitu gani mhakihitaji kwenye maisha yetu kama "pea" au wapenzi mnaopendana na wenye nia moja ya kuishi maisha yenu tote pamoja kama mke na mume na wakati huohuo kuelewana nini kifanyike sasa na kitu gani kisubiri na bila kusahau heshima kwa maana ya kuheshimu uwepo na hisia za mwenzio kwa kumhusisha kwenye maamuzi yako balada ya kuamua kwanza kisha unaenda kumjulisha nini kinaenda kufanyika bila kujali kama ataafikia au la.....kwani pamojana kuwa umemwambia na anajua lakini hatokuwa na nguvu ya kuzia kile ulichoanza kukifanya.
Kutokana na Utamaduni wetu wa kibongo (kwa familia zinazoheshimu na kufuata maadili) mtu kuwa mpenzi (bf) anakuwa hana uzito sana kwenye maisha ya msichana husika isipokuwa tu kama mpenzi huyo atakuwa amechumbia na hapo ndio utakuwa unahusishwa zaidi kwenye maamuzi ya maisha yake ya baadae.
Hii inaweza kuwa moja ya sababu, kwamba yeye anaamua kufanya maamuzi kwanza kisha anakuja kukuambia kitu gani ameamua kufanya kwa vile anachokiona hapo ni yeye na sio ninyi kama pea/wenza.
Sababu nyingine inaweza kuwa jinsi anavyochukulia swala zima la kuchumbiwa na kufunga ndoa, unajua wanawake tunatofautiana, kuna wale ambao kuolewa au kuchumbiwa wanadhani ni "deal au bahati hivyo jamaa akionyesha nia ya kutekereza hilo huwa hawachelewi kukuruhusu uendelee na mipango ya kwenda kujitambulisha.
Wapo wanawake wengine ambao wao swala la kuchumbiwa na kuolewa kabla hawajafikisha maleongo yao ya kimaisha/masomo wanadhani ni kuharibiana maisha hivyo siku zote hukwepa na pengine kuua uhusiano mara tu utakapotangaza ndoa.
Vilevile wapo wachache ambao wanakuwa hawana uhakika (kama ilivyo kwa wanaume) kama wako tayari kuchumbiwa na hatimae kufunga ndoa japo kuwa wanamapenzi ya kweli na dhati kabisa, lakini mioyoni mwao wanahisi mwanaume husika sio "type" ya mume ambae wangependa kuishi nae milele hivyo hujizunguusha.
Bila kusahau sehemu ndogo sana ya jamii ambayo wazazi wanataka binti yao aolewe na kijana mwenye aina fulani ya maisha hali inayoweza kusababisha binti kuhofia kwenda kukutambulisha kwako kwa vile anajua kabisa akifanya hivyo ndio utakuwa mwisho wenu, lakini kwa vile anakupenda na angependa kuwa na wewe basi huamua kukwepa bila kukuambia ukweli ambao unaweza kukuumiza hisia zako na hatimae kuua uhusiano wenu.
Natambua kabisa vitendo vya huyu binti kubadili msimamo kila mara, kutokuja kukutembelea pale anapokuwa likizo na kugoma kwenda kujitambulisha kunakukatisha tamaa na kukufanya uhisi kuwa huyu binti huenda anauhusiano na mtu mwingine.
Unachopaswa kufanya hapa ni kutafuta muda na kuzungumza nae ana kwa ana na kumwambia hofu yako juu ya uhusiano wenu, mwambie kuwa huna tatizo kufunga ndoa mwaka 2010 (kutoka 2009-2010 sio mbali) ila kitu kitakacho kufanya uendelee kusubiri ukiwa na amani moyoni ni wewe kuchumbia (ku-book)kwa maana ya kwenda kwao kujitambulisha, kumvalisha pete na kulipa mahali (kama itahitajika).
Unaweza kumtambulisha hapa na akapata nafasi ya kuongea na mimi moja kwa moja ili niweze kumuweka sawa.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment