Friday

Heshima hana tena, nimekosea wapi?-Ushauri!

"Habari za kazi dada Dinah. Mie nina langu moja ambalo naomba ushauri wako au wa wengine pia . Ni katika kupanuana mawazo.

Ni hivii… Mie ni mdada wa umri 26, sijaolewa. Hapo kabla nilikuwa na mpenzi ambaye nilidumu naye kwa miaka 4, naweza nikasema kuwa mapenzi yetu yalikuwa motomoto kipindi kama cha miaka miwili ya mwanzo. Nilikuwa nampenda sana jamaa, pia na yeye alikuwa ananipenda sana tu.

Tatizo lilikuja kuanza baadae, kwamba niliona kama ameanza kunidharau na kuwa haniogopi/heshimu tena. Hata inapotokea ugomvi mdogo anakuwa mwepesi kutamka.. ah unaweza kwenda kutafuta bwana mwingine!


Nikawahi kumuuliza rafiki yangu mmoja, kwamba kwa nini huyu mtu yuko hivi? Akanijibu kuwa NI KWA SABABU ULISHAMWONYESHA KWAMBA UNAMPENDA SANA! Kwamba nilichotakiwa kufanya ningeweka mapenzi yangu rohoni na kauka nayo, lakini nisingemwonyesha jamaa kiasi gani ninampenda!


Hivi sasa nimesha achana na jamaa mwenyewe. Na nimepata mwingine kama mwezi hivi umepita. Hatujafanya chochote zaidi ya kukutana na kuongea, kupeana ofa tu. Ninamwona ni mstaarabu na ninahisi anaanza kuniingia moyoni. Sasa swali langu ni kwamba je ni vibaya kumwonyesha/kumwambia jamaa kama unampenda sana?


Binafsi nahisi kwamba nikimwonyesha ninampenda sana na ninaridhika kuwa naye na sitamwacha (namaanisha ki ukweli na not pretending) ndio atazidi kunipenda zaidi. Je ni sign ya kuonyesha udhaifu wangu wa mapenzi kwake?

Na kwamba itamfanya yeye a-take advantage? Je kutokumwenyesha ni kiasi umemfia ni njia sahihi ya kumfanya mwanaume awe anakuheshimu? (Hapa namaanisha kwamba atakuwa anakuona hubabaiki, na yeye sio mwisho wa reli).

Naomba mawazo yenu wapendwa ili nijue jinsi gani ya kumfanya mpenzi wangu aniheshimu na anithamini."

Jawabu: Shukrani na pole kwa kuwa na mwanaume ambae alijenga kiburi baada ya kujua kuwa unampenda. Kabla sijaendelea naomba nikukumbushe kuwa kuna tofauti ua Kuogopa na kuheshimu, mtu anaekuogopa ziku zote hawezi kukuheshimu ila ataonyesha anakuheshimu kwa vile anakuogopa (heshima za uongo) na yule anae kuheshimu hata siku moja hawezi kukuogopa.


Unakumbuka usemi wa "mapenzi ni kikohozi hayafichiki"? basi ndio ukweliw enyewe huo. Ukijaribu kuficha wewe ndiye utakae kuwa unaumia kwa kujifanya kuwa mtu mwingine na sio wewe. Mapenzi ni zawadi pekee ya thamani unayoweza kumpa mtu na wewe kuipata kutoka kwake sawa sawa au ziadi.

Suala muhimu kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi ni kuweka hisia zako wazi kwa mwenzio na yeye afanye hivyo hali itakayowafanya muwe huru na karibu zaidi.

Ikiwa wewe unampenda na unadhani kuwa yeye ndio mwisho wa Reli yaani safari zako zote pale umefika na mabegi umeweka chini (nimekumbuka maneno ya Chid Benz hehehehe) hakuna haja ya kulificha hilo, mueleze ajue....sio useme yote kwa siku moja, hapana.

Kuna namna ya kumfikishia ujumbe mpenzi kama wewe umefika bei (unampenda sana au kupita kiasi) na wakati huohuo kuonyesha kuwa unajiamini kama mwanamke kwamba unampenda na unamtaka lakini humuhitaji kwa maana kuwa huwezi kufa au kulala njaa bila yeye lakini maisha yako yatakuwa bomba na yenye furaha mkiwa pamoja....sijui unanielewa?

Wanaume ni wawindaji hivyo kama mwanamke kamfia mwanaume hulion ahilo na hutambua kuwa unamtaka/penda japokuwa unapokuwa nae kwenye uhusiano anaweza kuhitaji kuhakikishiwa kuwa kweli unampenda kwa kumfanyia au kufanyiana mambo tofauti tofauti.

Huyo jamaa najua kabisa hisia zako hivyo wewe kama vipi ruhusu tu uhusiano uendelee na wewe nenda na flow bila ya kujiwekea "kigingi" au hofu za Ex.

NB: wanaume wengine hawajui kuonyesha mapenzi kwa maneno bali vitendo na wengine ni kinyume chake hivyo kuwa mvumilivu mpaka hapo mtakapo zoeana na kuwa "comfortable" kwenye uhusiano wenu ndio umuelekeze mwenzio........

No comments:

Pages