Monday

Hakukua na m'naume maishani mwake, kajenga chuki!-Ushauri




" Kwangu mimi dinah na wadau wote ni kua mimi ni Mwanaume nilikutana na Mwanamke na tukatokea kupendana sana, shida kwake yeye ni kwamba alikwisha athirika Kisaikolojia kutokana na wanaume.


Kwa maelezo yake kwangu ni kua, aliwahi kuwa na Mwanaume hapo awali na alimpenda sana, baadae alikuja kuachwa na huyo Mwanaume kwa ajili ya Mwanamke mwingine ambae alikuwa ni rafiki yake.


Kitu ambacho kilimuumiza sana mpaka kufikia kuwachukia wanamme wote kuwa si watu wa kuwaamini au kuwa nao kwenye mahusiano. Japokuwa hivi sasa tuko pamoja nilipata taabu kubwa ya kumshawishi mpaka akakubali.


Vilevile huyu mpenzi wangu alishuhudia uhusiano mbaya kati ya Mama na Baba yake baada ya baba'ke kumuacha mama'ke alipokuwa mdogo akisoma hivyo amelelewa na mama peke yake mpaka sasa anafanya kazi akiwa bado chini ya mama yake.


Mambo kama hayo anayajumuisha katika kuwachukia wanamme kitu ambacho simlaumu kwani kwa namna moja au nyingine naona yuko sawa. Sasa je? Mtu kama huyu ni kitu gani hasa naweza kufanya kwenye uhusiano wetu ili ile hali ya kisilani na hasira kwa wanamme iweze kumtoka au kupungua?


Kwasababu mim ini binaadamu kama wengine kwamba naweza kukosea, na huwa nakosea wakati mwingine nakua na shughuli nyingi na ninahindwa hata kupata nafasi ya kumpigia Simu au kwenda kwao.


Hayo na mengine yamekua ni makosa yanayonijumuisha kule alikotoka wakati mimi siko hivyo. Matarajio yetu ni kuoana as soon as mungu atapenda kwa vile mimi mambo yangu bado hayajawa sawa sana ndiyo maana sijamuweka tayari na wala sijamwambia ni lini tutaoana.


Hatua za mwanzo tulikwisha pima ukimwi na kuwa tuko safi kwa kua mume na mke lakini kuhusu wazazi bado hatujaliweka jambo hili wazi. Hapo ndipo nauliza ni vipi niwe mwanaume bora/mwema kwa mtu kama huyu ili ajue nampenda na kwamba si lazima samaki mmoja akioza lazima waoze wote!

Nasubiri ushauri wako,wenu washika dau".



Jawabu: Hongera sana kwa kuwa na mpenzi muwazi (kukueleza past yake) na vilevile nafurahishwa na nia yako ya kutaka kumuonyesha kuwa wewe ni mwanaume bora na sio kama hao waliopita maishani mwake.



Napenda utambue tu kuwa kupima afya zenu ni wajibu (kila mtu anapaswa kupima kabla hajangonoka na mpenzi mpya) na sio hatua za mwanzo ya kwenda kufunga ndoa. Hatua ya mwanzo ya kutaka kufunga ndoa ni kuchumbia (kujitambulisha na kumaliza mambo ya Desturi na Mila kama yapo).


Mpenzi wako (kutokana na maelezo yako) hana kisirani na wanaume na ndio maana yuko na wewe hivi sasa, lakini inaweza ikawa binde litakapokuja suala la kufunga ndoa kwa vile hana imani tena na wanaume hivyo anaweza kuhofia kutokewa na kile kilichomtokea mama yake na kudhani ni heri kuwa na uhusiano ambao unampa uhuru kwa kuondoka atakapoona mambo yanakuwa sio mambo!



1-Kitu ambacho unatakiwa kukifanya kwa mtu kama huyo mpenzi wako ni kumuonyesha mapenzi ya kweli na yaliyo wazi, kuwa kwenye mawasiliano muda wote hata kama unashughuli nyingi (busy) haikufanyi ushindwe kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi (text).

Hakikisha unakuwa wazi na shughuli zako, Mf:-Unapotoka asubuhi kwenda kazini hakikisha unazungumza nae kwanza kabla hujatoka, ikiwezekana utakapofika mahali pa kazi pia sema umefika salama. Kuwa na maongezi ya kutosha kuhusu uhusiano wenu kabla hujaenda kulala hali itakayofanya ubaki kichwani mwake mpaka atakapopitiwa na usingizi.


Unapokuwa na nafasi katikati ya siku m-check anaendeleaje na umueleze hali yako kwa nusu siku hiyo. Kabla hujatoka pia wasiliana nae kuwa unatoka na ukifika nyumbani pia muambie kuwa umefika salama......hii ikiwa tabia yako itamfanya Kisaikolojia akuamini nakuhisi kuwa wewe uko tofauti, unamjali na kumpenda na baada ya muda atakuwa akifanya hivyo kwako.


2-Muambie mara kwa mara ni jinsi gani unampenda au unadhani yeye ni muhimu kiasi gani kwenye maisha yako....pamoja na kusemahivyo epuka kujifananisha na wanaume wengine wenye tabia mbaya ili uonekane wewe bora. Zingatia kuonyesha kwa vitendo wewe ni bora kisai gani na sio kwa kujifananisha na watu wengine kwa maneno tu.


3-Jitahidi kuwa nae kila mnapopata nafasi nakufanya hivyo, zungumza nae kuhusu mambo mengi tofauti hasa mipango yako ya baadae na unapofanya hivyo hakikisha unatumia uwingi kwa maana ya kuwa; badala ya kusema napenda baada ya miaka 3 nijenge nyumba, unasema napenda baada ya miaka mitatu tujenge nyumba n.k.


4-Mhusishe kwenye maamuzi yako, hofu yeyote kuhusu kazi, maisha n.k. hatakama unauhakika kabisa hawezi kukusaidia kimawazo (kutokana na upeo wake mdogo labda) lakini mhusishe hivyo-hivyo na wewe utakuwa na uamuzi wa kuyafanyia kazi maoni yake au kuyaacha palepale.


5-Kama mmejiingiza kwenye kufanya ngono/mapenzi, basi mnapofanya hakikisha wewe unafanya kwa mapenzi yako yote, onyesha jinsi gani una-admire umbo lake, ngozi yake, uzuri wake. Onyesha jinsi gani unashukuru kuwa yeye ni mpenzi wako mama wa watoto wako hapo baadae na kusahau mahitaji yako mpaka utakapokuwa na uhakika kuwa yeye ameridhika ndio sasa uhamishie hisia kwako. Au kwa kawaida anaweza kurudisha yote uliyomfanyia.



6-Ikitokea anatatizo/huzuni basi kuwa wa kwanza kuwepo au kuonyesha hali yakutaka kusaidia, hataka kama uwezo wako mdogo wa kusaidia lakini uwepo wako pale ni muhimu zaidi kuliko kuwa na uwezo wa kutatua jambo fulani. Unajua kumjali mtu sio kumpa vitu ambavyo ni "material", uwezo wako wa kumpa matumaini, kuwa ple kuzungumza nae, kumpa ushauri wa nini cha kufanya inatosha kabisa.


Nadhani haya na mengine ya wasomaji wangu yatakusaidia kuwa mwanaume bora kwa mpenzi wako.


Kila la kheri.





No comments:

Pages