Monday

Anataka nifanye Masters pia niwe msiri-Ushauri

"Mpendwa dada Dinah. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 naishi jijini DSM. Nimekuwa nikifuatilia na kusoma mambo mbalimbali na ushauri wako na comments za washirika tofautitofauti. Nimeona bora nije na hii yangu ambayo kwa ukweli inanichanganya kichwa.

Ninae boyfriend kwa hapa nitamwita X mwenye miaka 26, nimekutana nae chuoni mwaka 2006 nikiwa naingia mwaka wa kwanza na hadi sasa tumeshadumu miaka 3. Tulikuwa darasa moja huko chuoni ila yeye kwa sasa anaendelea na Masters ambapo kwa mimi plan ni next year ndiyo niisome hiyo masters kwani sikupenda kuunganisha.

Mwanzo alipoanza kunidate alikuwa mtu mzuri sana, muda wote alikuwa karibu na mimi na tulipoanza mahusiano mambo yalibadilika kidogo japo aliniambia kuwa yeye ni busy person. Tulikuwa tunaonana kwake siku za weekend tu tena mchana. Siku za kawaida na hata kama ni darasan ni salaam tu basi then kila mtu na muda wake.

Nilipomuuliza alinijibu kuwa yeye ni mtu anaependa privancy hasa kwenye mambo yake ya binafsi kama mahusiano. Tuliendelea hivyo japokuwa alinitambulisha kwa baadhi ya marafiki zake wa chuoni na hata wa kazini kwake akiwemo Boss wake. Kitu ambacho kilinishangaza katika usiri wake ambao ulikuwa ni chuoni tu, kwani tukishatoka chuoni alijitahidi kuwa close na mimi.

Mara moja moja tulipokuwa darasani alikuwa anakuja kukaa na mimi na mda mwingine hapana, japokuwa darasa zima lilikuwa likikujua kuwa tunadate na walikuwa wanatushangaa tunavyoact kama hatujuani.


Hapo ndipo mambo mengine yakaanza, akaniambia anataka watu wachanganyikiwe kwamba wasiwe na uhakika kama tunadate kweli au la. Akawa akiulizwa "mkewako mzima?" anawajibu "sina mke mimi" na baada a hapo anawaacha kwenye mataa na kuondoka.


Kitu kingine ambacho kiliniuma sana ni kuwa hata kwenye party za chuo kama za darasa ambazo ni za usiku alikuwa haongozani na mimi, bali na marafiki zake 3 wa kiume na msichana mmoja. Ndani ya party anakaa na hao watu ila mda mwingi anatoka nje na kurudi


Wakati party inaendelea msg zake kwangu haziishi kutumwa kuwa nisijali nivumilie na niact kiutu uzima. Ukicheza mziki na mkaka anakuja kukutoa na kuniambia nijiandae tunarudi nyumbani. Kwa maana hiyo party ndio inaishia hapo.


Siku zilienda mara nyingine alikuwa na mikutano ya kikazi mpaka saa sita za usiku ndio anaweza kuniambia anatoka kikaoni, nilikuwa najiuliza ni kazi gani usiku? Nijuacho mimi ni kuwa anafanya kazi kwenye makampuni 2 ambayo kote kuwili alinipeleka.

Hatimae nikaja kusikia tetesi kwa watu wengi wa darasani kuwa X anafanya kazi ya upelelezi, tena na hivi alikuwa anasafiri sana kwenda nchi tofauti na hamna anayemuaga zaidi ya mimi tu basi mi ndio nikawa nasumbuliwa "vipi mumeo kaenda kufanya upelelezi?" na maswalimengine mengi.

Siku moja nikamuuliza, akaniambia "kazi zangu zote mbili unazijua haya ya upelelezi sijawahi kukuambia na wala siyajui ndio mana nikakwambia watu wambea sana wanaongea mno, wewe nisikilize mimi na si wao".

Kwa kweli haya yote yalinisumbua sana kichwa changu na mara kwa mara niliongea nae ila jibu lake ni kuwa eti nahitaji kumwelewa na tupeleke mahusiano kiutu uzima na si kitoto. Basi kwa vile nilimpenda nikaka kimya.

Ilimradi mapenzi niliyapata, nikiumwa yupo,nikiwa na shida ananisaidia, akiwa less busy naenda kwake na hata nikitaka kulala huko yeye sawa tu, pia yeye alikuwa anakuja kunitembelea nilikokuwa naishi na wakati mwingine analala. Marafiki zangu walimjua na aliwajua vizuri japo alikuwa ananiambia nisiongee nao kila kitu kuhusu mapenzi yetu kwani hataki umbea.


Siku moja nikamuuliza hivi una mpango gani na mimi wa mbeleni? akanijibu "nataka usome hadi masters mana kamwe sitaoa mwanamke asie na masters" na akaniambia kwa yeye ana plan ya kumaliza masters na kuendelea kusoma na ana mpango wa kuoa mwaka 2015 ila kwa sasa nijue tu kuwa sisi ni wapenzi mungu akipenda basi tutafika mbali.


Ila akaniambia ukitaka tuwe wapenzi zaidi inabidi ujifunze kuwa privancy person hiyo ndiyo sheria yangu,ukianza kuongeaongea sana mambo yetu na mengineyo tutaishia hapo.

Kwa saa tupo mbalimbali na huwa nafunga safari kumfuata chuoni na ninakaa nae siku tatu au mbili kisha narudi kazini. Mambo si rahisi kwa huu umbali ila najitahidi kumtembelea na hata mapenzi ya simu yanachukua nafasi kubwa zaidi kama nikiwa nimekosa kisingizio cha kuomba ruhusa kazini, maana kazi nazo si kila mara uombe ruhusa.

Basi mara nyingi mimi ndio nikawa nampigia simu kila siku jioni, inaweza kupita hata siku mbili kama sijapiga basi tena. Siku moja nikamwambia sipendi hiyo tabia kwa nini hapigi simu?akanijibu kuwa huwa anasahau kuweka credit basi nikamwambia "kama hunipendi uniambie kuliko kunipotezea muda".Tukaagana.

Kesho yake yeye akapiga simu ila sikuchangamka kama siku nyingine.Siku iliyofuata usiku akanitext "hujambo umeshindaje?usiku mwema", mimi nikamwendea hewani tukaongea vizuri tu mwisho nikamwambia "i love u",akanijibu "me too".


Nikamuliza "una uhakika?" akanijibu "sina budi ya kurudia kitu kwa miaka yote 3 tuliyokuwa pamoja hujakua tu?kua basi tuwe na mapenzi ya kiutu uzima" na akaniambia "kusema i love u kila siku haimaanishi ndo unapendwa naweza nikakuambia hivyo na bado nisimaanishi. Kwa kweli sikumwelewa, akaniambia mwisho tukagombana bure na yeye hataki hilo litokee bora tulale,basi tukaagana.

Huyu ndie mwanaume ambae ninae dada Dinah kwa miaka 3 sijapata jibu ni mwanaume wa aina gani huyu na kama kweli ananipenda na ana mpango na mimi. TAFADHALI NAOMBA UNISAIDIE KWA USHAURI NIFANYAJE.
Na washiriki wengine nahitaji maoni yenu tafadhali.

Ni mimi dada F"

Dinah anasema: Dada F, shukrani kwa ushirikiano na uvumilivu wako as nachukua muda mrefu kujibu kutokana na uwingi wa majukumu mengine ya kikazi na maisha. Nimefurahishwa na maelezo yako ya kina na kumfanya yeyote kuelewa picha nzima bila kuwa na maswali.....hongera kwa hilo.

Suala la Ushushushu sio muhimu sana as long as wewe unajua kazini kwake, na akitoweka siku zote huwa anakuambia kuwa anasafiri hivyo huitaji kujipa hofu na mimi binafsi sina uzoefu na masuala ya wapelelezi. Nitakupa maelezo kuhusiana na issue ya uhusiano wenu wa kimapenzi ambayo naamini yatafungua macho yako kwa kiasi fulani.

Mimi binafsi ninaamini kuwa sisi wanadamu lazima tupitie hatua sita za maisha ya kimapenzi na mahusinao. Ila tatizo la wengi huwa tunakurupuka na kutaka/kutegemea jambo fulani kabla ya wakati.

-Uzoefu/kutambua ujinsia wako kwanza (hapa unakuwa kwenye umri mdogo so jaribu kufurahia maisha na kupata uzoefu zaidi wa kimaisha na wakti huohuo unazingatia masomo/kazi, sio lazima ungonoke).

Pili:-Unapenda na ku-commit (hapa utakuwa mkubwa kiumri na umetulia kiakili).

Tatu:-Chumbia na Ndoa (kuwa na uhakika wa kuishi na huyo mmoja tu maisha yako yote).

Nne:-Familia(Uamuzi au kukubaliana kuzaa).

Tano:-Kufanya uhusiano wenu wa kimapenzi na ndoa kusimama Imara.

Mf-ninyi wawili bado wadogo, mnapendana sana tu (kutokana na maelezo yako bado mko hatua ya kwanza)...ila wewe unategea au unataka zaidi ya unachokipata kutoka kwenye uhusiano wenu, huenda ungependa siku moja ufunge ndoa na huyo mpenzi X hasa ukizingatia kuwa owte mnafanya kazi na mmeshakuwa pamoja kwa muda mrefu. Lakini yeye hayuko tayari kufanya hivyo kwani anachotaka yeye kwa sasa ni kurekebisha maisha yake na wakati huohuo kuongeza Elimu.

Kitu ambacho sisi wanawake huwa tunakikosea ni kuharakisha mambo, labda kutokana na " msukumo" kutoka kwa jamii inayotuzunguuka kuwa ukiwa kwenye uhusiano baada ya muda fulani basi lazima uolewe au hata kuzaa.

Lakini katika hali halisi tunatakiwa kujua nini hasa wapenzi wetu (wanaume) wanakitaka kutoka kwenye uhusiano husika na je ni hatua gani hivi sasa uhusiano wetu upo? kabla hatujaanza kurukia/harakisha hatua inayofuata kama sio kuziruka zote na kwenda hatua ya mwisho.

Sasa ninachokiona hapa ni wewe kutaka commitment na kuhakikishiwa nafasi yako, wakati yeye bado anajaribu ku-have fun. Kweli anakupenda lakini hiyo hamfanyi yeye kuwa na uhakika kwa 100% kuwa wewe ndio mke wake.......anahitaji muda.

Kwenye suala la wewe kuwa msiri, mimi sioni tatizo kwani naelewa kuwa kuna baadhi ya watu wanaaibu sana yanapokuja masuala yao ya kimapenzi.....yaani hawapendi kujionyesha wa watu wengine kuwa wao ni wapenzi. Sasa kwa vile mpenzi X ni mmoja kati ya hao watu ni vema wewe kuheshimu takwa lake hilo.

Nini cha kufanya: Jiulize nini hasa unataka out of the relationship with X, mawasiliano yenu yako bomba kama wapenzi, unapewa mapenzi yake yote, mnaonana kila mnapohitajiana, anakujali, kila mtu yuko huru kwenda kwa mwenzie, mnaoneana wivu (which ni dalili nzuri) X anaonyesha ameji-commit kwako.......nini kingine unataka?

Kama ni ndoa ndio utakayo ni wazi hutompata kwa sasa kwani yeye anadhania takuwa tayari akiwa na miaka 31 (2015) which wanaume wengi ndio hupenda kujipangia hivyo kuanzia 31-36 wawe wamefunga ndoa, huamini by that time wanakuwa somehow wamekamilisha "mipango" yao kimaisha.

Hivyo hapo kuna maamuzi 3 tofauti;
(1)-Endela na uhusiano huku ukimsubiri tumia muda huo kwenda kufanya hiyo Master yako au

(2)- Endela na uhusiano, furahia maisha yako na chukulia kila siku kama inavyokujia (mkifunga ndoa poa isipotokea ndoa poa).

(3)-Toka kwenye uhusiano ili kupata utakacho kwenye uhusiano mwingine (kama unaharaka sana na maisha ya wawili).

Nakutakia kila la kheri.

No comments:

Pages