Naomba unishauri kitu, mimi nina boyfriend wangu ambaye ametoka kwenye mahusiano na msichana waliedumu naye miaka 4.Hofu yangu je atanidis na mimi kama alivyomuacha huyo mwingine baada ya muda mrefu?
Sasa hivi simuelewi-elewi kwani anapenda sana kushika simu yangu na kusoma sms zangu tena wakati mwingine sms inaingia hata mimi sijaisoma tayari yeye anasoma.
Juzi nilienda kulala kwake lakini hakuonyesha kunijali, je ni dalili kuwa atakuwa na mwingine? je niachane nae? au niendelee nae lakini nisiwe naenda kwake?
Nilijaribu kumuuliza kama anamalengo yeyote na mimi,akasema ndioa anamalengo mazuri. Hiyo juzi nilipokwenda kwake nilimfulia nguo na kwa bahati mbaya zikaibiwa.
Nimemtumia sms lakini hajanibu hadi this time, je na mimi nikae kimya au nimtafute? Nitashukuru nikipata ushauri wako dada na nitaufanyia kazi ushauri wako.Please usiniweke kibarazani.
Kazi njema, be blessed"
Dinah anasema:Asante sana kwa mail yako, namshukuru Mungu ananipa nguvu kila siku.
Wengi wetu tunapoingia kwenye mahusiano mapya ni wazi tumeacha au tumeachwa. Kuachwa kwa mtu hakukuhusu wewe,japokuwa ni muhumu kujua nini kilitokea au kusababisha mpaka wakaachana ili ikusaidie wewe kuepuka au kujua namna ya kukabiliana na same tatizo kama litajitokeza.
Kwa kawaida humchukua mtu yeyote muda mrefu kuwa tayari kupenda tena na kujenga uhusiano mpya baada yakutoka kwenye uhusiano wa zamani.
Sina hakika mpenzi wako amekuwa na wewe baada ya muda gani tangu aachane na huyo mpenzi wake wa awali, lakini kutokana na ulichokisema hapa(vitendo vyake) inaonyesha jamaa bado hajapona maumivu ya mapenzi aliyopata kabla yako.
Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa unaharaka ya kufunga ndoa na wakati huohuo unaogopa kuachwa ukiamini kuwa "kama aliacha yule, hatamimi ataniacha". Sio lazima iwe hivyo.
Unapoingia kwenye uhusiano unatakiwa kuzingatia nini utawekeza kwenye uhusiano ili uhusiano na mpenzi wako kuwa Imara na uliotawaliwa na mapenzi. Huitaji kuishi kwenye hofu ya kuachwa au kufikiria maisha yake kabla yako!
Kosa dogo ulilofanya ni kuanza kwenda nyumbani kwake na kumfanyia shughuli kama vile wewe ni mchumba/mkewe, mwanaume hafuliwi wala kupikiwa mara kwa mara ikiwa uhusiano bado ni mchanga, unaweza kumsaidia vijishughuli kwa mapenzi lakini isiwe kila weekend, utakuwa unamugopesha na atakudhania kuwa unataka kufanya nyumbani kwake ni kwako.....hii can scare him off.
Vilevile hukupaswa kumuuliza malengo yake kwako na badala yake ungetumia mbinu nyingine ili kujua msimamo wake juu ya uhusiano wenu kama wapenzi, kumbuka uhusiano unajengwa na watu wawili.
Hawezi kuwa na malengo kwako kwani wewe sio mwanae bali ni mpenzi wake, lakini anaweza kuwa na malengo fulani juu ya uhusiano wenu na wewe unapaswa kuwa na malengo fulani kwenye uhusiano huo ila nina uhakika yeye hajawahi kukuuliza unamalengo gani kwake....has he?
Huyu mwanaume inaonyesha kuwa aliachwa(wanaume wengi hawapendi kusema waliacha kwa vile ni aibu kwao)kutokana na kitendo chake cha ku-withdraw na kuangalia-angalia simu yako ni dalili tosha kuwa jamaa alitendwa au niseme alikuwa cheated na hivyo inakuwa ngumu kukuamini na ndio maana anafuatilia sana SMS na simu ili asije umizwa tena.
Kitendo cha yeye kutokukujali ulipokuwa kwake inawezekana alikuwa amechoka au anamawazo(kama ulikuwa unataka ngono), na mwanaume anapokuwa ktk hali hiyo huwa ngumu sana kungonoka lakini kwa kumsaidia (kuzungumza nae na kumpa matumaini, kumpoza, kumliwaza n.k.)anaweza kuwa sawa na tendo likafanyika.
Nini cha Kufanya: Mtumie ujumbe au mpigie simu na kumuomba msamaha kwa kusababisha nguo zake kuibiwa. Najua kosa sio lako lakini omba radhi kwa hilo, kwani anaweza kuwa na hasira kuwa usingezifua zisingeibiwa hasa kama uliamua kufua bila yeye kutaka ufanye hivyo....hilo moja.
Pili, mdogo wangu punguza safari za kwenda kwake na badala yake mpigie zungumza nae kwa simu na kupanga mihadi ya kukutana mahali au kwenda kutembea sehemu na ikitokea anakualika kwenda kwake baada ya matembezi au chakula then nenda kwake lakini usilale unless anaomba ufanye hivyo.
Unapokuwa huko kwa Jamaa usijipe shughuli kama vile wewe ni mchumba/mkewe tayari. Unaweza kuandaa labda Chai asubuhi na kutandika kitanda kwa vile mmekitumia, pia unaweza kusafisha vifaa ulivyotumia lakini sio unafanya usafi nyumba nzima na kumfulia juu.
Muonyeshe mapenzi ya dhati ulionayo bila kuhoji malengo yake, hakikisha unampatia ile hali ya kukuamini kuongeza mawasiliano Mf:kwa kumueleza mipango yako ya siku na kuomba yeye akueleze mipangilio yake ya wiki au siku na hivyo kujua lini mtakutana tena kama wapenzi n.k
Mfanyie mambo yakingono na ya kimapenzi (nje ya kitanda) na kitabia ambayo unauhakika hakuna mtu amewahi kumfanyia.....njia rahisi yakujua ni kuwa wazi kwake na kumhoji kimahaba na yeye atakuambia anapenda Binti mwenye tabia gani, nini hawaji kufanya lakini angependa kujaribu/kukifanya kingono n.k.
Acha kuwa na haraka za kuolewa, furahia uhusiano wako kama ulivyo na hakikisha unafanya mambo ya kimapenzi ili atangaze ndoa yeye mwenyewe bila kusukumwa na maswali yako kuhusu malengo yake.
Kumbuka ndoa nzuri ni ile inayotokana na uamuzi wa watu wawili wanaopendana kwa dhati na wenye lengo la kuishi pamoja maisha yao yote yaliyobaki.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment