"Da Dinah pole na majukumu, mimi nina tatizo kidogo na boyfriend wangu wa miaka 34. Tumefahamiaka kwa muda wa miaka 3 na tumekuwa wapenzi kwa miezi 8.
Kipindi chote hicho sijawahai kufika kwake wala kukutana na ndugu yake mmoja, mawasiliano ni ya tabu hata nikianza kumshirikisha jambo langu huonyesha kama vile hana interest. Kwa kifupi I dont feel secured with him.
Je! nifanye nini kuimarisha uhusiano wetu kama kuna hiyo nafasi? Maana nikimwambia kuhusu tabia yake hiyo huwa anasisitiza kwa kusema kuwa ananipenda no matter what na atajirekebisha.
Kweli huwa anabadilika lakini mabadiliko hayo hayadumu muda mrefu, je napaswa kufanya nini?"
Dinah anasema: Asante kwa mail, Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa mpenzi wako anaendesha maisha mengine ambayo hayuko tayari kukushirikisha kwa sasa na pengine kutokukushirikisha kabisa ikiwa utomwambia au kuonyesha nia ya kutaka kujua anapoishi (sio lazima ufike/uende).
Mabadiliko hayo ya muda mfupi ni ya kukusikiliza, kuonyesha interest kwenye issues zako na mawasiliano sio? Kama anaweza kubadilika kwa muda fulani basi ni wazi kuwa anajua kosa lake na anajitahidi kujirekebisha. Lakini hiyo isikufaye u-relax kwani huyo ni mpenzi wako wa miezi 8 na una haki ya kujua anapoishi japokuwa sio lazima uende nyumbani kwake mapaka mwenyewe awe tayari.
Huwezi juwa huenda anaishi na wazazi wake na hivyo sio heshima kukupeleka wewe nyumbani kwako, vilevile isije kuwa mpenzi wako anafamilia (miaka 34 kibongo-bongo wengi huwa tayari wanawake na watoto), ni vema kama utafanya uchunguzi kimya-kimya ili kujua ukweli kuliko kuendelea kupoteza muda na mtu ambae anaku-treat kama Kimada na sio mpenzi wake.
Ukipata ukweli kuwa jamaa hana familia (mke na watoto au mpenzi mwingine), basi hakikisha unamuweka chini na kuzungumza nae kuhusu uhusiano wenu na kuweka wazi kero zako, umuhimu wake kwenye maisha yako na mengine yote yalioujaza moyo wako na wote kwa pamoja kutatua tatizo kama wapenzi(ikiwa tu hana mtu mwingine).
Lakini kama ukigundua kuwa jamaa anamaisha mengine basi ni vema kuachana nae na wewe kupata nafasi ya kupenda na kupendwa na mkaka mwingine asie na "mzigo", Mkaka atakae weka akili yako na moyo wake wote kwako, Mkaka atakae jali hisia zako na kukusikiliza, mkaka ambae anajua umuhimu wa wewe kujua wapi anaishi....kwa kifupi ni makaka atakae kupenda kwa dhati na mwenye kuthamini uhusiano wa kimapenzi.
Kila la kheri!