"Habari da Dinah? I hope wee mzima na unaendelea na shughuli nzito ya uelimishaji wa jamii. Am greatful topics zako nyingi zimenisaidia. Mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 24, nina ujauzito wa miezi sita na nusu sasa.
Niliposhika mimba nilipata taabu ya kutapika na kushindwa kula kwa miezi kama 4 hivi. Mpenzi wangu alivumilia sana kwani nilimfanyia visa sana ingawa haikuwa makusudi.
Sasa shida ya kwanza ni kwamba anataka tufanye mapenzi lakini mimi nashindwa kwani uchafu umezidi kutoka na ni mwingi mno mpaka inakera, imefikia hatua navaa pantyliners kila siku.
Hii hali inanifanya nihisi kama vile mpenzi wangu hatosikia raha na mimi sipendi kuwa weti hivyo kwani nasikia kichefuchefu lakini wakati huohuo sitaki mpenzi wangu anaitelekeze.
Pili Sehemu zangu za siri zimebadilika rangi na kuwa nyeusi wakati rangi yangu ya ngozi ni lighter kiasi, pia nikinyoa natokwa na vipele vidogo vidogo, sasa sitaki mpenzi wangu anione nikiwa hivyo, je nitaondoaje vipele na kurudisha rangi yangu ya awali?
Nilikwenda kwa Gyno wangu kuangaliwa na sikuwa na maambukizo yeyote
Je kuna dawa asilia ambayo naweza kuitumia? maana hizi dawa za kizungu nyingi hazifai kutumiwa wakati wa ujauzito.
Tatu Matiti yangu yanauma na kuwasha sana, basi huwa najikuna mpaka najikwaruza ili kupoza napaka mild steroid lakini wapi!! Sasa how will we have sex when matiti yako hivyo?
Nne Mpenzi wangu hupenda mwili wangu ukiwa bonge kiasi, sasa kpindi cha miezi 4 nilipokuwa naumwa na kushindwa kula nimepungua sana, yaani na tumbo langu kubwa bado sijafikia mwili wangu kabla ya ujauzito kwani nilikuwa a bit kibonge.
Mpenzi kaniletea Dada zake waje kunisaidia kupika ili nile na kuwa na afya lakini wapi! alafu mbaya zaidi ni kuwa nikikonda naonekana so terrible na I really feel unattractive na i think nikikubali kumvulia nguo hatoniona navutia tena. Sitaki kumpoteza mpenzi wangu.
Kila siku natoa sababu za kuumwa, tafadhali naomba ufumbuzi wa haraka kwani mpenzi ameanza kuwa bitter and unhappy ninapomkwepa kwani anasema anataka kuwa karibu na mimi."