"Dada Dinah na wachangiaji wote, tafadhali naomba ushauri au mawazo kwani nipo kwenye kipindi cha kufanya maamuzi magumu.
Nina mchumba wangu ambae tunataka kufunga ndoa, lakini nitakapofunga ndoa nitalazimika kuhama kutoka Nchi moja kwenda nyingine na kuacha ajira yangu.
Kinachonichanganya hasa ni suala la kuacha kazi, yaani mawazo juu ya hilo hunipa maumivu ya tumbo na huonga huniingia.
Naomba ushauri kutoka kwa yeyote aliyepitia hii hali katika maisha yake, asanteni"
No comments:
Post a Comment