Sunday

Ndani ya Wiki mbili kesha "move on" na jamaa kwenye WhatsApp!

Habari yako dada Dinah,

Mimi ni kijana Mtanzania, nina jambo ambalo ningependa ushauri wako. Jambo lenyewe ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye tuligombana na tukakaa kama wiki mbili hivi hatuelewani...ndani ya hizo wiki mbili akafanya ngono na mwanaume mwingine.


Sasa baadae, baada ya hizo wiki mbili tulikuja kuelewana tukasameheana yale yaliyotugombanisha. Hapo bado sikuwa najua kama alifanya ngono na mtu huyo mwingine.


Sasa baada ya hapo tukarudiana na kuendelea na uhusiano kama mwanzo, Mpenzi alikuwa anatumia simu ya Blackberry ambayo baadae alinipa mimi niitumie kwasababu yeye tayari alishapata simu nyingine ambayo sio Blackberry lakini anaipenda zaidi. Nikaichukua ile simu nikaweka line yangu ya vodacom.

Cha kushangaza, baada ya siku kama mbili tatu hivi napokea Message kutoka kwa mtu ambaye walikuwa wakiwasiliana kupitia WhatsApp, hiyo message ilikuwa ya kimapenzi...then muda mfupi nikapokea picha mbili ambazo huyo jamaa alizituma.

Hizo picha zilionyesha walipiga wakiwa wote, moja wamelaliana yeye mpenzi akiwa amejifunga khanga moja tu, na nyingine wanakipeana busu yeye akiwa amemkalia huyo jamaa...


Nikaamua kumuuliza taratibu kwanza kabla hata ya kumuonyesha hizo picha, nikamuuliza kama anazijua namba za huyo jamaa nilimuonyesha maana kwenye whatsApp namba ya alietuma inaonekana, akasema anamjua.


Nikamuuliza wakoje naye, akasema ni rafiki tu japokuwa jamaa anamfuatilia mara nyingi kwani amekuwa akimtaka...akakataa kabisa kusema ukweli.


Baadae nikawa mkali na kumwambia tuachane kabisaa aendelee na huyo jamaa yake! Akawa mkali, hapo bado sijamuonyesha zile picha, akawa analia machozi kabisa kila siku ananibembeleza nimsamehe kwakuwa hakuwahi kuniambia kuwa huyo jamaa huwa wanatongozana japo bado hajamkubali.


Ndio siku moja nikamwambia upo tayari kusema ukweli ili nikusamehe?..akasema ndio! basi nikamwambia tukutane sehemu tuongee....ukweli ni kwamba hakuna alichokisema kipya zaidi ya kusisitizia kuwa huyo jamaa yeye ndiyo anaemfuatili (kumtongoza) lakini yeye hamtaki na wala hawajawahi kukaa au kukutana faragha popote.

Nikamuuliza je? nikikuonyesha ushahidi kwamba yule ni bwana yako, nimfanye nini?...akanijibu niachane naye nisimsikilize tena na akasema yeye atakuwa Malaya na hafai...


Mmh nikaguna kidogo, nikamuuliza tena kama kuna jambo ambalo amefanya nae halafu hajaniambia basi aseme lakini wapi...akang'ang'ania msimamo wake.


Ndipo nikamuonyesha hizo picha mbili. Alitahamaki, akaanza kulia na kuoba msamaha tena kwa kunipigia magoti, ila moyo wangu ulishakufa ganzi nilipomuona anajiamini baada ya kupinga maswali yote niliomuuliza wakati ni uongo ambao hata yeye alikuwa akiujua kuwa ni uongo.


Kwasababu baada ya kumuonyesha zile picha tu alianza kulia na kuomba samahani nisifanye yale aliyojiapiza, wakati nilitegemea angezikana zile picha au angalau abishe bishe kidogo lakini alizikubali pale pale na kuanza kulia na kuomba samahani akinisihi nisifanye yale aliyojiapiza...


Hapo mimi nilinyanyuka na kuondoka zangu nikimwambia tusijuane tena...aendelee na huyo jamaa yake...


Hivi ninavyoongea mpaka sasa bado hatuna mawasiliano mazuri, mimi ndio sitaki kuwa naye tena japo roho inaniuma lakini nikimuangalia nasikia hasira sana.


Nimejaribu kumuuliza maswali kadha wa kadha kwamba kwanini na ilikuwaje ndani ya muda mfupi vile alifikia umbali wote huo wa kufanya ngono na mtu mwingine?


Akanijibu eti frustration tu..ndio zimemchanganya akajikuta kafanya hivyo...Mh akilini kweli mimi hainiiingii...Frustration?...Sasa swali langu mimi kwako na hata wadau wengine wanisaidie mawazo.

Je! sio kwamba huyo mtu alikuwa naye muda mrefu tu?...au ni kweli inawezekana ndani ya hizo wiki mbili ndio wamekubaliana na kutiana kweli?...

Na je! ni vyema mimi kumkubali na kumsamehe turudiane kama mwanzo?....je! Inawezekana ndio tabia yake?, kwasababu nijuavyo mimi, mwanamke yeyote anaweza akatongozwa karibu kila siku na watu tofauti, lakini kukubali ndani ya muda mfupi hivyo kumvulia mtu chupi na kufanya naye mapenzi sio rahisi tena ukiwa katika kipindi kibaya umegombana na mpenzi wako ambaye leo au kesho unaomba akusamehe ili mrudiane?


Pamoja na maswali hayo ukweli ni kwamba nimemchukia sana yule dada.

Sasa dada Dinah na Wadau wengine naombeni ushauri...nini cha kufanya hapo?

Natanguliza shukrani zangu, Ahsanteni"

------------------

No comments:

Pages