Kwa kawaida Wanawake tunadondoka kimapenzi haraka zaidi kuliko wenzetu. Huenda Mwanaume akawa amevutiwa na Muonekano wako, Uzuri, Uwezo kiakili, Sauti, Utembeavyo n.k. Mkaanza au mkakubaliana kutoka kama wapenzi. Hiyo hamfanyi yeye kukupenda wewe!
Enzi za Bibi yangu ilikuwa ni kawaida kwa Binti kuolewa bila kumpenda Mwanaume, kwamba kila kitu kinatayarishwa na familia mbili na wewe kama Binti unaambiwa tu utaolewa na Bwana fulani Mtoto wa Familia/Ukoo fulani.
Kabla ya kuchumbiwa Binti unakuwa tayari umefundwa kuhusianana mambo mengi tu kuhusu Mapenzi, Ndoa, Uzazi na Mabadiliko yatakayoendelea kujitokeza kwenye maisha yenu kama Wazazi na Wapenzi.
Ikiwa kwa bahati nzuri unamfahamu “Mchumba” na pengine ulikuwa unapendezwa nae basi unahitaji kumfanya akupende(baada ya ndoa) na ikiwa bahati akakupenda ghafla basi unapaswa kumfanya akupende zaidi, yaani umkae moyoni na kichwani(akilini).
Kipindi hicho Wanaume wengi walikuwa wanafunga Ndoa ili kuendeleza Ukoo(kuzaa) na kujiwekea heshima kwenye Jamii sio kwa mapenzi kama ilivyo sasa kwa baadhi yetu. Wachache sana walifunga Ndoa kwa vile waliwapenda Wanawake waliochaguliwa.
Hii bado inaendelea hadi sasa kwa baadhi ya wanaume wa “kisasa” na Wasomi, kwamba “anatafuta” Mke ili amzalie watoto na kuwalea, ampikie na kufanya shughuli zote za ndani.
**Kutokana na “Maendeleo” au sijui ni mambo ya Usawa siku hizi nasikia kuna Wanawake wanafunga Ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi (hii ni topic nyingine).....tumalizie hii kwanza.
Changamoto:
Kutoa changamoto ni tofauti kabisa na kutokuwa msikivu au kutokuwa na heshima kwake. Wanaume hawakuzaliwa wakiwa wanajua kila kitu na ndio maana tukaumbwa sisi kama wasaidizi wao, kwamba kuna wakati wanahitaji kuwekwa sawa kiakili, kiutendaji(kitandani included), Sio kila asemacho wewe ni "ndio Bwana" hata kwenye suala ambalo halihitaji "ndio".
Mapishi:
Ukiachilia mbali suala la Kuridhishana na kufurahisha Mwili, kujua kupika aina mbali mbali za vyakula ni muhimu pia. Unapofundwa unaambiwa “ kamwe usiruhusu Mpenzi wako kula chakula cha mwanamke mwingine hata kama dada ni dada yake.
Kwa kawaida Wanaume wengi husifia na kupenda mapishi ya mama zao, sasa hapa ndio muhimu kujenga uhusiano mzuri na Mama mkwe nakuhakikisha unajifunza ili ukampikie mwanae nyumbani kwako.
Usafi wa nguo:
Najua wanawake wengi wa “kisasa” wanapinga sana hili lakini sie tuliofundwa na wa kisasa tunachanganya yote ili “kushinda” hihihihi....Kamwe usivundike nguo mpaka anaishiwa ya kuvaa, ni vema kuhakikisha nguo ni safi na zimenyooshwa vyema.
Maendeleo:
Hata kama huna kipato sio mbaya kuchangia maendeleo kwa kutoa mawazo mazuri na endelevu, na hata kuchangia katika utafutaji wa “info” kuhusiana na mfano Ujenzi, upatikanaji wa Mbegu za mazao fulani au Bidhaa kwa ajili ya mradi fulani n.k.
Kujali:
Zamani hakukuwa na urahisi wa mawasiliano hivyo ilikuwa muhimu kumpokea mpenzi na kumpa pole, kumkumbatia anapofika nyumbani, unakaa nae na kuulizia hali yake na siku ilivyokwenda.
Siku hizi ni rahisi kimawasiliano hivyo basi sio mbaya kama utaulizia anavyoendelea huko aliko....ni mpenzi wako tayari hivyo huwezi kuonekana “needy” ikiwa uta-check anaendeleaje akiwa kwenye mishughuliko yake badala ya kusubiri yeye ndio akupigie au akutumie ujumbe.
Jipende Kimwili:
Enzi zile ilikuwa ni Usafi, valia Khanga Mbili na kujifukiza Udi....inategema na ufanyacho ili kujipenda kimwili(kuvaa vizuri, kunyoa vinyweleo, kufanya mazoezi, n.k) aili mradi tu kinakufanya ujisikie vizuri na kukuongezea hali ya kujiamini na kuwa tayari kwa lolote(namaanisha Tendo)....siol azimalitokee lakini pia sio mbaya kama ukiwa tayari wakati wote.
Tunza Haiba ya Uanamke wako:
Pamoja na usomi wako au kuishi kwako sana na Wazungu, usisahau kuwa wewe ni mwanamke wa Kiafrika kwenye maadili (inategemea na kabila) fulani ambayo hao wa “kisasa” hawana na hiyo inakufanya wewe uwe tofauti na wanawake wengine wengi Duniani.
Pamoja na kusema hivyo haina maana uvumilie unyanyaswaji kwa vile tu kikwenu kunyanyaswa ni sehemu ya Maadili, chukua maadili mazuri na yenye manufaa kwako na kwa mpenzi wako.
Jitegemee:
Hupaswi kusubiri yeye afanye manunuzi fulani bali wewe kama mwanamke mwenye kipato unapaswa kuangalia nini kinahitajika/kosekana ndani na kurekebisha mambo. Natambua baadhi ya wanawake wenye kipato lakini hutegemea wanaume wawafanyie kila kitu wakiamini kuwa kufanya hivyo kutamzuia mwanaume huyo kuhonga nje ya uhusiano wake.
Unapoonyesha kuwa unajitegemea unamjengea mpenzi wako imani kuwa hata mkiwa na watoto na yeyekupoteza kipato au hata kufa wewe kama mwanamke utaweza kutunza watotowenu bila tatizo lolote. Ikiwa huna kipato basi sio mbaya kama utakuwa unamkumbusha mpenzi pale panapokuwa na mapungufu ya vitu ndani ya nyumba yenu.
Kidokezo: Vitu vidogo kwenye ambavyo pengine wewe unadhani havina umuhimu ndio hivyo hivyo vinavyoweza kuharibu uhusiano wenu.
Mf: Nguo zote chafu hivyo inabidi avae nguo ambayo haipendi na hivyo kuwa “uncomfortable” huko kazini, ikiwa kachekwa ni wazi hatokuwa na furaha hata akirudi nyumbani na hali hiyo ikiendelea ni wazi kuwa uhusiano wenu utakuwa Mashakani.
Ahsante kwa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment