"Hi, dada Dinah, Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi.
Wednesday
Nilihisi, nikahakiki na kupoteza mapenzi-Ushuhuda!
"Hi, dada Dinah, Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi.
Ushuhuda wa aliyehisi, akahakiki na kupoteza mapenzi!
Tuesday
Nahisi naibiwa-Ushauri.
Dada Dinah samahani mimi ni mwanaume nina miaka 28, na nakaribia kuoa kama Mungu akipenda mwishoni mwa 2010 au mwanzoni 2011.Tatizo lililo nileta hapa ni kuuliza vitu 61. Kwanini Girlfrend wangu kila akiwa kwenye siku anakuwa mgonjwa kabisa, anatapika haswa, maumivu ya tumbo ndio usiseme huwa anajigaragaza tu chini na dawa ya kutuliza kama diclofenac kameza?
Pia nilimshawishi amuone Doctor kwa hilo anasema ni mara kwa mara kauliza wanasema akizaa mara ya kwanza hilo tatizo linaisha kuna ukweli hapo??
2.Kuna kipindi hakupata siku zake miezi kwa miezi miwili lakini mwezi wa tatu ulipoanza ali-bleed kidogo sana ,mwezi wa nne pia then akaja akaugua vichomi akapelekwa Hospitali yeye anasema Doctor kasema ile damu ya bleed iliganda so akapewa dawa akapona lakini rafiki zake wameni dokeza kuwa katoa mimba nielewe lipi hapa na kama ilikuwa yangu kwanini atoe yaani sielewi kabisa ila yeye akiulizwa anakataa kutoa mimba na anasema hajawahi fanya mapenzi bila kinga. Mimi ni wa kwanza baada ya kupima, yaani sielewi lipi ni lipi!
3. Simu yake mara nyingine hataki niishike, sina kawaida yakuiangalia napenda uhuru ila yangu ruksa sina hiyana. Kuna siku sasa msg iliingia yaani kama machale hivi nikasema huyo lazima atakuwa mwizi wangu ngoja niifungue, kufungua lahaula! ni kama maneno yangu, yaani ni full dear, sijui honey sasa lini tunaonana, nina njaa na vitu kama hivyo.
Siku nyingine msg dear leo nipo Kibaha njoo tulale huku msg hazina majina ni namba tu, nilipo muuliza ni nani akajibu ni jamaa tu anamtongoza ila yeye hamtaki, lakini siku zote nilimwambia nahisi kama naibiwa hivi ila yeye akasema nisiwe na presha wala hana mtu zaidi yangu na kunisifia eti hawezi kumpa penzi mtu mwingine kwani hakuna mwanume kamfikisha kama mimi.
Ila kwa kweli nililazimika kubadili namba yake ya simu aliyokuwa akitumia nikaichukua nikaiweka hewani nilishangaa siku kama 3 simu inaita saa nane au kumi usiku nikipokea anakata nilimpelekea ile namba nikauliza ni ya nani akasema ya baba yake, nilishangaa kwanini baba apige simu muda huo?!
4.Kuna siku alienda kwa shangazi mtu ambako alitakiwa kuangalia watoto wakati shangazi yusafari, aliniambia kuwa uncle mme wa shangazi alimtaka. Mara kuna siku alisahau kufunga mlango wa chumbani uncle kaja na pensi imetuna mboo akimkumbushia kumtaka.
Mimi nikamwambia awe mwangalifu pia amwambie shangazi kuwa kuna hilo limetokea, hakumwambia. Siku nyingine akasema anaumwa akaenda Hospital peke yake uncle akiwa home akatibiwa akarudi.
Si muda mrefu akadai anaumwa tena hiyo siku uncle akampeleka hospital saa 5 asubuhi ,mimi nilipiga simu saa tisa akadai bado wapo hospital?!! saa kumi wapo tangi bovu na huyo huyo uncle wanakula nyama choma yeye akidai mgonjwa!!!?!,vile vile amesema uncle alijituma sana kumletea zawadi hapo home.
Siku nyingine mimi nilikuwa na wasi sana na hilo so nilikuwa napiga simu kila mara. Kuna siku nilipiga simu kuanzia saba usiku mpaka 2 asubuhi hola, haipokelewi, saa nne hivi nakuja kupiga anapokea nikamuuliza hajaona miscalls zangu nyingi nilimpigia akasema hajaona lakini hazikuwa less than 40 na kudai pengine mtoto aliyelala naye kazifuta kwani pengine alishituka usiku na kuchezea simu????!!!!!..
5. Wakati anatoka huko kwa shangazi siku mbili baada ya ile siku nilopiga simu kuanzia saba usiku hadi asubuhi hakupokea, nilimuomba ngono alikubali round ya kwanza tu niliona hahimili kabisa, na mimi nilitaka ku-prove kama niliibiwa au laa na kawaida huwa naunga sometime bao 2 za kwanza kama round moja, siku hiyo ya kwanza ilikuwa kama 7min,nika unga dakika kama ya 10/13 hivi alilalamika anaumia na kuomba apumzike kitu ambacho sijawahi kukiona ni mwaka na miezi kadha sasa tangu tumekuwa pamoja.
Huwa anahimili round zote vizuri 3-6, sasa hapa nina doubt kuibiwa hii kuchoka round ya 2 tena fupi kabisa! aidha kwa mujibu wa marafiki zake huyo uncle alikuwa anamnunulia hadi pad akiwa period sasa hapa jamani ni sahihi kweli hakunakitu kweli hapa? Yeye nikimuuliza anasema hakuna hawezi share na aunt yake!!!?!
6. Na mwisho kabisa dada D ni kuhusu marafiki,anao wengi wakiume, nikimuuliza oooh nilisoma nao, ndugu, sasa hutaki niongee na wanaume!,aaah wivu umekujaa, kwanza watoto wadogo mimi siwataki unanitosha, unanitafutia visa unataka kuniacha lakini kuna wengine mimi nampunguzia credit halafu yeye anawapunguzia ile nilomtumianaomba msaada wa ufafanuzi wa haya mimi naona hapa kama hakuna kitu ingawa yeye anadai kunipenda sana au ni ya kawaida? nitashukuru
by mdau Baraka.M DSM"
Jawabu:Baraka asante kwa kuungana nasi mahali hapa, baadhi ya watu mnapitia mambo mazito kwenye safari hii ya mahusiano ya kimapenzi lakini mnauvumilivu wa ajabu sana au sijui niseme mapenzi ya dhati!
1-Tatizo la kuumwa tumbo wakati wa hedhi kwa baadhi yetu wanawake ni la kawaida, kwa wengine kama ulivyosema hapo hali hiyo huambatana na dalilizote ambazo mwanamke anakuwa nazo anaposhika mimba(sio wanawake wote wakiwa na mimba wanapitia hatu ahii), lakini vilevile wanawake wengine linaweza kuwa sio tatizo la kawaida la hedhi bali tatizo lingine ambalo labda linaweza likahitaji matibabu au hata upasuaji kutokana na ushauri wa Daktari.
2-Mpenzi anapokuwa mchoyo wa simu yake (wengine wanaweka na password kabisa0 au hata neno la siri la barua pepe yake mara zote huwa kuna kitu anaficha na asingependa wewe ujue. Kwa kawaida wapenzi walio kwenye uhusiano "serious" unaoelekea kwenye kufunga ndoa huwa hakuna sababu ya kutokuwa huru mwenzako ashike au kuangalia simu yako. Hata kama huna tabia hiyo bado mpenzi anatakiwa kutohofia kama wewe utaifungua simu yake n.k.
3-Sasa kutokana na tabia ya mpenzio nadhani ulipoteza ile hali ya kumuamini na ukaamua kufanya ulichofanya na kukutana na kile ambacho ulikuwa ukitegemea kukikuta simuni mwake. Kutokana na mapenzi yako ukabadili namba yake ili kuzuia mawasiliano na huyo "mwizi wako" ktk hali halisi angekuwa mwanaume mwingine angemtibua huyo binti kwa ku-cheat!
Kama hiyo haitosho binti huyo alidiliki kuigawa ile namba mpya kwa mpenzi wake wa nje ya uhusiano wenu, wanasema "a cheater will always be a cheater" na hii imethibitishwa na mpenzi wako huyo baada ya kuwa akipigiwa simu na "baba" usiku wa manane.
4-Watoto wa shangazi yake (binamu) wanaishi na baba yako ambae kutokana na maelezo yako nahisi kuwa ndio "baba" na ndio mwizi mkuu wa mpenzi wako. Sababu ya yeye kuwa kule kwa Shangazi kuangalia watoto haimpi ruhusa kulala kuho huko kwani baba yako anakuwepo usiku. Hivyo ktk hali halisi huyu Mpenzi wako alipaswa kutumia akili akisaidiwa na wewe kimawazo kuwa akae na watoto during the day nakurudi kwake/kwenu usiku badala ya kulala huko huko.
Baada ya kuja tuhuma kuwa Mjomba anamtokea, yeye kama binti muaminifu alipaswa kutumia akili na kutokuwepo pale nyumbani usiku (asilale pale), yule ni mjomba ambae hana uhusiano kidamu na mpenzi wako hivyo attraction inaweza kabisa kujitokeza na watu wakapendana......watu wataamua kutoendelea kwa sababu ya kuheshima kuwa ni mume wa shangazi ambae ni dada wa baba......(kwenye jamii nyingine wapwa ni marufuku kuwa karibu na wajomba walio oa dada wa baba yako).
Badala ya kumuambua awe muangalifu ulitakiwa kumshauri asiwe akilala pale kwa mjomba kama nilivyoeleza hapo juu. Nasikitika kusema kuwa kisingizio cha kutokupokea simu na kupokea baadae na kudai kuwa "labda mtoto alichezea" hakina nguvu ya kushawishi ukweli ndani yake.
Kuhusu swala la yeye kuumwa mara kwa mara linatia wasiwasi, hebu mshauri akaangalie afya yake kwa ujumla na zaidi VVU, pia wewe mwenyewe kaangaliwe afya ili ufahamu mapema kama uko huru dhidi ya VVU na kama ni matibabu yaanze haraka na vilevile suala zima la kubadili mtindo wako wa maisha(Lishe, matumizi ya madawa, kuwa muangalifu zaidi kuhusu swala zima la ngono inategemeana na majibu).
5-Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa siku hiyo ya mwisho walikuwa wakifanya "kamuagano" nahuenda alichoka sio kutokana na ngono ya mjomba bali pia hali yake ya kuumwa (natumaini ulitumia kinga siku hiyo).....ila na wewe una moyo wa ajabu!!
Kununuliwa pads sio kitu cha ajabu, hata baba/kaka anaweza kukununulia pads kwani anajua kabisa kuwa unazihitaji kama mwanamke hasa kama huna kipato (hufanyi kazi).
6-Hata kama ingekuwa mimi nisingeweza kuamini rafiki zake wengine wenye jinsia tofauti na yeye. Maelezo yako yameweka wazi tabia halisi ya mpenzi wako kuwa sio muaminifu, sio kwamba unahisi tu bali ushahidi unao kuwa "anachezea hisia zako" kwamba hajatulia hivyo ni ngumu sana kuamini chochote anachosema au kukuambia.
Nini cha kufanya-Nenda kaangalie afya kujua kama una VVU au huna. Majibu utakayoyapata yachukulie kuwa ni ufunguo wa wewe kuanza maisha mapya. Baada ya majibu yako, mshauri na yeye akafanye hivyo (ikiwezekana muende pamoja ili kusiwe na rushwa, mana'ke wengine hulipa ili majibu yabadilishwe).
Ikiwa wote mko safi kiafya au mmeathirika na unahisi kumpenda na unaamini kuwa atabadilika kitabia basi zungumzieni yote na hofu yako juu ya uhusiano wenu, jaribu kuhoji kitu gani anakitaka kutoka kwako ambacho anakwenda kutafuta huko kwa "mjomba". Mawasiliano hayo yatakusaidia wewe kujua mapungufu yako wapi na kuyarekebisha.
Baada ya kukubaliana kuwa mjaribu tena uhusiano wenu basi ni vema kuweka miiko/sheria/rules ndani ua uhusiano wenu na itekelezwe na ninyi wote (mf. kuwa huru kutumia simu zenu, kutokwenda kwa "mjomba" peke yake, kupunguza marafiki wa kiume ambao sio muhimu kwake,n.k.) kisha mpe muda (trial) wa kubadilika bila kuharakisha ndoa.
Vinginevyo (ukihisi hutaki tenakuendelea nae) wewe endelea tu na maisha yako na siku moja utakutana na binti mzuri, mwenye haiba ya kike na mwenye kuthamini penzi.
Heri ya mwaka mpya na kila la kheri!
Sunday
Waume za watu wananisumbua-Ushauri
Mimi tatizo langu ambalo lilisababisha kutengana na baba watoto lilikuwa ni uhuni wake, na nikaamua kumwacha ili tusije tukafa na UKIMWI na kuacha watoto. Na nikaapa sitakaa nitoke na mtu aliyeoa au sitakaa niharibu ndoa ya mtu kwa kuingilia penzi.
Sasa tatizo lilikuja hivi, mara nyingi sana mahali ninapofanya kazi waume za watu wanajaribu kunitongoza, na msimamo wangu nimekuwa sitaki kusikia mume wa mtu manake na mimi niliyaonja nilipokuwa kwenye ndoa yangu.
Sasa basi siku isiyoliwa kitu, kuna baba mmoja mume wa mtu kazini amekuwa akinisumbua zaidi ya wanaume wote ili niwe naye kimapenzi. Sasa siku moja tulikuwa na cocktail party na akaja na ushamba wake wa kunitaka kimahusiano, nami(jamani sijui kinywaji kilishaniingia) au ni shetani gani lilonifanya nifungue mdomo.
Nikamwambia kuwa mimi msimamo wangu ni ule ule 'sitaki kuwa naye' lakini kama anataka nimtafutie mtu basi nitafanya hivyo, he took up on the offer na kutokana nilikuwa na rafiki yangu wa kike ambaye ni single nikamwi-introduce.
Na baada ya wiki moja yule rafiki yangu niliyomwi-introduce akaniambia jamaa amenunulia sofa set, halafu mara wanafanya party ' na mara nyingi naona huyu jamaa ndio ana-finance' wananialika na zaidi ya yote inaonekana wamekuwa quite close katika uhusiano wao.
Mimi kama mwanamke ambaye nilishawahi kuolewa najisikia vibaya sana, yaani naji-picture kama mke wa huyu jamaa, naona kweli huyu baba ananyima familia yake upendo na anatoka nje na mimi ndie niliyefanya connection - yaani nimeshajilaaumu saaanaaa, najisikia vibaya kweli, hata kama ndugu wasomaji mkinitukana - kweli I deserve it - lakini yaani sijui jinsi gani yaku-reverse jambo hili. Sasa nimekuwa mbali na wote wawili, wakinialika kwenye party au kutoka nawapa excuse.
Mimi naomba......mnisaidie jinsi ya kufanya, japokuwa najua naweza kutoeleweka ( I risk to be misunderstood) wakadhania labda ni wivu etc, lakini ki ukweli ni kwamba - kujisikia kwangu vibaya ni kwa sababu nilikuwa kisaidizi kikuu kwa kuwakutanisha, na upweke wa mke wa huyu baba (wakati mume anajivinjari na kurudi nyumbani usiku, na uongo anaomwambia ili kuficha kinachoendelea) najua na naona ndio nimeusababisha - mimi naumia sana na mawazo.
Da Dinah - nimeandika kwa ajili ya kutaka tu ushauri wa hali yoyote.
Nitashukuru sana."
Jawabu: Shukurani kwa kuniandikia. Kuna umri fulani mwanamke ukifikia wanaume wanaokutokea wengi wanakuwa tayari wamekwisha oa hiyo haina maana kuwa hakuna wanaume ambao hawana wake/wapenzi la hasha!
Wanawake wengi tunakutana na majaribu hayo. Mimi mwenyewe nakutana sana na vishawishi vya namna hiyo lakini as for me natumia nafasi hiyo kutaka kujua kwanini hasa huyo mume anataka kutoka na mimi hili hali anamke na watoto nyumbani, najitahidi kutafuta namna ya kujua ukweli wa nini anakikosa huko kwake na kutaka huku nje?......akiwa wazi nampa ushauri na ile kunitaka mimi kunabadilika na kuwa rafiki na mara mambo yakiwa mazuri unajikuta unatambulishwa kwa mkewe kama mtu uliyesaidia na sio "the other woman".
Ni kweli ulifanya kosa kubwa sana kuunganisha mume wa mtu kwa mwanamke mwingine ukijua wazi kuwa mwanaume huyo ana mke na watoto. Kama mwanamke mwenye maadili mema na mwenye kujali maisha bora kwa mwanamke mwenzio na watoto (ukizingatia kuwa wewe ni mama na sidhani kama ungependa watoto wako siku moja wateseke) ungemshauri mume huyo kutulia na mkewe.
Wakati mwingine unaweza kuokoa ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kutoa ushauri kwa mwanaume anaekutaka au kumwambia mkewe kwa namna yeyote ile hata kama ni ku-form urafiki wa kizushi (sio kwenda na kudai mumewe anakutaka, hapana) bali kumtahadhalisha kuwa awe muangalifu na mwenendo wa mume wake na kama kuna kitu kinakosekana ndani ya nyumba kama vile romance,amani, upendo, ngono, n.k. basi ajaribu ku-restore vinginevyo ataletewa magonjwa, ikiwezekana mfundishe, muelekeze nini cha kufanya......najua mwanamke mjinga-mjinga atadhani unataka kumuibia mumewe lakini mwanamke muelevu atakuelewa na kukushukuru.
Kwa bahati mbaya umechelewa na hakuna kitu unachoweza kukifanya ili rafiki yako na mfanyakazi mwenzio ambae katika hali halisi ni Fuska ili waachane bila kukudhani kuwa wewe unawaonea wivu kutokana na wanavyopendana nakufanyiana mambo ambayo wewe umeona ni muhimu na kuyataja kama vile party, vifaa vya ndani n.k.
Nini cha kufanya-Kaa chini na rafiki yako na mueleze ukweli kuhusu huyo Baba (mfanya kazi mwenzio) kuwa ametelekeza familia yake kwa ajili ya huyo rafiki uliyemuunganishia......unaweza kusema ulimsakizia kwa vile wewe hukutaka kuendelea kusumbuliwa na huyo mwanaume lakini hukutegemea kama wangeanzisha uhusiano nakufikia hatua ya huyo jamaa kutelekeza mke na watoto wake.
Kwa vile unauzoefu na ndoa, familia yenye watoto uliowazaa mwenyewe na Talaka unajua wazi maumivu anayopata mke ikiwa atagundua mumewe anatoka nje ya ndoa, hofu ya watoto kuishi bila baba yao....hivyo pamoja na maelezo mengine muhimu tumia uzoefu wako huo kufikisha ujumbe kwa rafiki yako juu ya kutembea na mume wa mtu.....omba radhi kwa kuwaunganisha ikiwezekana.
Itakuwa ngumu na itamchukua muda mrefu kwa rafiki yako kuachia ngazi ikiwa amejenga mapenzi ya kweli na huyo mwanaume, inawezekana kabisa akamshawishi jamaa amuache mkewe ili amuoe yeye na hapo ndio utakapojisikia vibaya zaidi. Kwani itakuwa sio tu umesababbisha wawe wapenzi bali pia watakuwa mke na mume na wakati huohuo utajisikia unahatia kuwa umevunja ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kumrusha mume wa mtu na rafiki yako.
Baada ya kuweka wazi kwa rafiki yako achana nao waendelee na mambo yao, Yeye kama mtu mzima atakuelewa, atatafakari na kufanya uamuzi wa busara. Endelea na maisha yako na watoto wako bila kuonyesha chuki juu ya uhusiano wao ambao sio halali.
Mungu akubariki na kila lililo jema!
Wednesday
Hana shukrani na a'niponda tu kwa Marafiki-Ushauri
Tabia ya mke wangu ni kuchukua mambo ya ndani na kuyapeleka nje, na amekua mtu wa kulalamika everyday, Najitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha anapata kila anachohitaji lakini imekua kazi bure.
Kutokana na kipato changu hua nikipata pesa nanunua kila kitu ambacho ni muhimu kwa matumizi ya nyumbani kuanzia chakula na mahitaji yake mengine muhimu yaani kwa kifupi everything needed I give to her, lakini kwake yeye ni complaint tu.
Na kitu kina choniumiza zaidi ni pale anapokuwa either with my friends or her friends, yaani hakuna stori nyingine isipokuwa ni kuniponda na kusema namtesa, na mnyanyasa sasa sielewi kama kweli ana mapenzi ya dhati na mimi au la.
Na nikimwambia kama vipi akapumzike home hataki anasema nikimpeleka nyumbani nimpe na Talaka. So dada nahitaji ushauri wako nini nifanye? na je ananipenda au hanipendi kwa hali hii?"
Jawabu:Asante kwa kuniandikia. Mkeo ama hana mapenzi na wewe au hapati kile ambacho anakitaka au alitegemea kukipata kutoka kwako mara baada ya kufunga nae ndoa pamoja na kusema hivyo inawezekana huyu binti alilelewa kwenye mazingira ya kutokujua na kuheshimu miiko ya nyumbani kwako, kwamba kinachotokea kwenu kinabaki palepale kwenu, kwa kifupi hana heshima....utoto pia unaweza kuchangia yeye kuendelea kuwa na katabia hako kabaya kabisa.
Kutokana na maelezo yako umesema kuwa unahakikisha kuwa anapata kila kitu anachotaka na unampa mahitaji yake muhimu ndani ya nyumba, hakuna mahali umeelezea kuhusu kumpa mapenzi ya kutosha.....maisha yenu ya kingono yakoje? Unadhani kuwa unamridhisha linapokuja suala la mahitaji yake ya mwili na hisia?
Tatizo la baadhi yenu wanaume mnadhani kuwa mwanamke ukimpa kila kitu in terms of material things na chakula cha kumwaga basi karidhishwa huyo......kuna mahitaji mengine ambayo kwa baadhi yetu wanawake ni muhimu lakini kwenu wanaume hayana umuhimu kwavile ni madogo.
Ninyi mmefunga ndoa mkiwa wadogo sana (ukilinganisha na maisha tunayishi hivi sasa) hivyo mnatakiwa kufanya mambo kama "young couple" more like bf and gf kuliko baba na mama......have fun!
Kitu kama kujenga urafiki kati yako wewe na mkeo hii itasaidia kuwa karibu zaidi na wewe na kukuambia yaliyomsibu au nini hakimfurahishi ndani ya ndoa yenu. Kumuonyesha mapenzi kwa vitendo sio kufanya hivyo only unapotaka kufanya ngono bali fanya hivyo kila unapopata muda....vitu vidogo kama kumshika, kumbatia wakati mnaangalia Tv, kutoka kwa ajili ya matembezi, kumbusu kila unapokuwa karibu yake.
Akikatiza mbele yako kuelekea jikoni mvute na mpe busu mate, mshike tako na vitu kama hivyo, kumuonyesha kuwa unavutiwa nae na unampenda, msaidie kufanya vijishughuli ndani ya nyumba ukipata nafasi sio kila kitu afanye yeye kwa vile tu umeoa n.k.
Hakikisha mnapofanya mapenzi anaridhika kwanza alafu ndio wewe unamalizia, hakikisha unajua uwezo wake wa kungonoka badala ya kuwa unafanya nae kila siku wakati yeye ni twice a week type(hapo lazima atahisi kuteswa ofcoz) au kama yeye ni wale wanaotaka kila siku na wewe ni mtu wa once a week ofcoz utakuwa unamtesa.
Nini cha kufanya-Kaeni chini na mzungumzie tofauti zenu, weka wazi kuwa hupenzi tabia yake ya kwenda kueleza watu maisha yenu binafsi, mwambie kama kuna tatizo lolote au kuna kitu hakifurahii ungependa akuambie wewe moja kwa moja ili ujirekebishe.
Anza kwa kumuambia akueleze kwa uwazi vitu gani unafanya havipendi tangu mmekuwa pamoja, akivisema basi hakikisha unajirekebisha na kuwa mume bora kwake. Mawasiliano ndio ufunguo wa kurekebisha mambo na kuondoa tofauti ndani ya uhusiano wowote wa kimapenzi kwani ni njia pekee itakufanya wewe na yeye kujua tatizo liko wapi na lilekebishwe vipi.
Mwambie yeye ndio mama mwenye nyumba na yeye ndio anaweza kuibomoa au kuijenga nyumba yenu na kuwa bora zaidi na mfano kwa wanandoa wadogo wengine.
Shirikianeni ili muweze kuishi kwa amani na upendo, kwani mnasafari ndefu sana ya kuendelea kuishi pamoja since wote ni wadogo ndani ya ndoa. Kumbuka ili ndoa iwe bora inahitaji kufanyiwa kazi, Uhusiano wa kimapenzi sio lelemama ni hard work.
Kila la kheri!
***Dinah anawatakia usherekeaji mzuri wa sikukuu ya Noeli, nawapa pole wale wote wanaouguliwa na wale waliofiwa, Mungu awapeuponaji wa haraka wagonjwa na kuwapa moyo wa uvumilivu wafiwa kipindi hiki......Mungu awe nanyi!
Monday
Alinitega, sasa anataka urafiki wa karibu-Ushauri
Maana haijawahi kutokea maishani mwangu. Hivi majuzi nikiwa Nairobi nilikutana na mrembo mmoja ambaye nilikuwa nafahamiana nae kwa muda mrefu (lakini sio mahusiano ya karibu sana). Sasa huyu dada alinichangamkia na akawa ananipa company pale ninapokuwa free kwenye shughuli zangu nilizoenda kufanya hapo Nairobi.
Labda niwaeleze pia kuwa nilikaa Nairobi kwa muda wa wiki mbili tu. Sasa siku moja nilitoka nae(huyo dada) out na tulipokuwa katikati ya maongezi yetu aliniambia kuwa hana hamu ya kulala kwake. So nikamchomekea kuwa aje kulala kwangu.
Kwa maajabu akakubali. Basi ilipofika mida ya usiku kama unavyojua tena kidume majaribu yakanizidia. Hivyo nikaamua kumtokea. Kwa kweli huyo dada alikataa kata kata kunipa mchezo. Alikubali nimguse baadhi ya maeneo ya mwili lakini sio sehemu zote.
Na pia wakati tumelala alivaa suruali na blouse. So you can imagine jinsi alivyoziba direct access kwenye mwili wake. Nilipojaribu kumbembeleza alikataa na kusema kuwa hayuko tayari kufanya kitendo na pia yeye haitaji kuwa na mtu kwa sasa.
Hivyo nikaamua kuheshimu matakwa yake ingawa kwa shingo upande. Sasa je dada dinah na wanablog wengine. Hembu niambieni huyu dada alikuja kunichezea akili tu au alikuwa anataka nini?
Je ningetumia nguvu kidogo na kumvua nguo na kutombana nae ningekuwa nimefanya makosa?? Mpaka leo ananisalimia na anainsist close friendship. Nipeni ushauri wakuu. Maana hili ni kasheshe sijawahi kukutana nalo.
Wenu mdau.....David"
Jawabu:David nashukuru kwa kuniandikia. Natumaini wasomaji wangu wamekupa majibu yaliyosaidia kuelewa kwanini hasa huyu binti aligoma kungonoka na wewe siku hiyo. Ila nakupa hongera sana, na hapo naweza kukuamini kuwa kweli unampenda huyo binti, angekuwa mwanaume mwingine mjinga-mjinga angebaka.
Wanawake hatutongozi wanaume kama wanaume mnavyotongoza, wanawake huwa tunatumia uanamke wetu kutuma ujumbe kuwa "tumekuzimikia", lakini kama hujaona au unajifanya kudharau (play hard to get) mwanamke anaweza kukata tamaa au anaweza kutumia mbinu nyingine anayoona inaweza kufikisha ujumbe na wakati huohuo kujua kama mwanaume huyo anahisia kama zake.
Sasa kutokana na maelezo yako huyu binti ni wazi anakutaka wewe kama mpenzi lakini hukuliona hilo hapo awali mlipokijuana na kitendo cha yeye kusema kachoka kulala kwake na kukubali offer ya kwenda kulala kwako ni wazi alikuwa anataka kujua msimamo wako wa kihisia....kwa kifupi alikutongoza.
Huyu binti anataka uhusiano "serious" na wewe na kutokana na "mawazo" ya wanawake wengi ni kuwa kufanya ngono siku ya kwanza ni kujidharaulisha na pengine kuna weza kum-put off mwanaume na kukudhania wewe ni "maharage ya mbeya" yaani rahisi, kama tumengonoka mara tu baada ya kukutana utakuwa umengonoka na watu wangapi kabla yangu.....mwanaume atajiuliza.
Lakini ktk hali halisi kufanya ngono ni makubaliano yenu ninyi watu wawili ambayo yanategemea zaidi mmefahamiana kwa muda gani, unajisikia comfy kiasi gani mbele ya mtu huyo, nguvu za hisia zenu na Chemistry itakayojitokeza pale miili yenu itakapokuwa zero distance. Kufanya ngono siku ya kwanza haina uhusiano na tabia ya mtu au sio kigezo kuwa mtu huyo ni mlala ovyo(Malaya).
Huyu binti inawezekana kabisa kuwa anakupenda na ndio maana alikubali kabisa kubadilishana mate na wewe nakushikana hapa na pale ila anataka muwe na uhusiano mzuri na wakudumu sio ule wa kungonoana kila mnapokuwa na hamu (casul).
Nini cha kufanya- Kubali kuwa na urafiki nae wa karibu kama kweli unampenda na sio kwamba unataka ngono tu kutoka kwake. Utakapo kuwa kwenye uhusiano ambao ni urafiki itakuwa rahisi zaidi kuwa na uhusiano madhubuti ambao utakuwa umejengwa ktk misingi ya urafiki.
Nenda taratibu na kama kuna "kemikali" zinazoendana kati yenu basi mambo yatakuwa mambo before you know it.
Kila la kheri.
Sunday
Ndoa imekuwa Ndoano,nimechoka!-Ushauri
Tendo la ndoa atake yeye ukitaka wewe hataki tena kwa maneno machafu na kuhama chumba hali hiyo imeni-affect kiasi kwamba akitaka nampa lakini silalamiki simsifii wala mguno wa aina yeyote ile kwani nahisi anadhurumu nafsi yangu.
Sipendi kutoka nje ya ndoa hivyo niliamua kujipiga punyeto wakati nikihitaji na na-enjoy kuliko hata anavyonifanya kwani ni mchoyo akikojoa yeye basi, kwasasa amenitia mimba[miezi 5] nayo kama imetumwa nyege kibao.
Kupiga nyeto Daktari anashauri sio nzuri ukiwa na mimba hivyo nikamueleza mwenzangu akanijibu nifute akilini hawezi nisaidia na tunaenda kwa week mara 1 au mara 2 kwa mwezi. Mimi sasa akitaka namnyima kwa hasira lakini wakati huohuo nina nyege, roho inauma sana.
Kingine sio mtu wa kulea kutokana na hali ya mjamzito anataka nini anaona kama najifanyisha nikimwambia najisikia vibaya,nikitaka matunda napigwa Calender nikimwomba kuichuachua kidogo miguu kwani inailekea kuvimba hataki, yaani sio wa kunisikiliza kwa lolote hatukai tukashauriana anachoamua yeye ndio hichohhicho kiujumla hakuna mapenzi.
Lakini nikimwambia nipe talaka yangu hataki nimechoka kuishi ndoa isiyo na upendo heri nikae mwenyewe, haijawahi kutoke siku akanisifia sifa zote za ubaya ninazo mimi naitwa jeuri, mbishi mchoyo, mchafu.
Wakati mwingine nasema kama ningejua nisingeolewa na tayari tuna mtoto 1 na huyu wa pili na ni wadogo nikae nilee watoto wakue eti wapate malezi ya baba na mama huku kila nikimwona au kusikia sauti yake hasira zinapanda au nikae mwenyewe nilee wanangu kama nitapata tutakae endana nae uongo dhambi nitaishi nae nina miaka 29 tu.
Nitashukuru kwa ushauri wenu na Kiongozi wetu mwana wa Nkibi"
Jawabu:Aisee ni kweli kabisa kuwa ukisoma tatizo la mwenzio unaweza kupata ahueni kuwa lako sio kitu. Lakini ukweli unabaki pale pale sote yunahitaji kuwa na furaha ndani ya mahusiano yetu ya kimapenzi hasa ndoa.
Kabla sijaanza ningependa ufahamu kitu kimoja ambacho wengi huwa hatukitilii maanani pale tunapokwenda kufunga ndoa. Mtu anapotaka kufunga ndoa huwa kuna sababu kwanini anataka kufunga ndoa na wewe haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
1-Kutokana na Imani ya Dini tunafunga ndoa kwa vile tumeambiwa kuwa tendo la ndoa kabla ya ndoa ni dhambi, hivyo ni kama vile tunafunga ndoa ili kungonoana kihalali (usininukuu), hapa inawezekana kukawa na mapenzi au matamanio.
2-Kutokana na Imani hizo za Dini pia tunafunga ndoa ili kujenga familia bora inawezekana kusiwe na mapenzi.
3-Tunafunga ndoa ili kuwa na heshima mbele ya jamii (Africa zaidi) au kuondoa mkosi, hapa tutafunga ndoa bila mapenzi.
4-Tunafunga ndoa kwa vile tunalazimika kufanya hivyo kutokana umri, hapa vilevile mapenzi hakuna.
5-Tunafunga ndoa kwa vile tumeelewana kuwa kwenye uhusiano na kugundua tunapendana na kutaka kuishi maisha yetu yote pamoja (Kisasa).
6-Tunafunga ndoa kwa vile wazazi wanataka ufanye hivyo, hapa utafunga ndoa na yeyote atakaejitokeza bila mapenzi, nasikitika kusema tena kuwa hapa mapenzi hayapo.
7-Tunafunga ndoa kwa ajili ya kupata sifa, umeoa/olewa na mtu kutoka kabila/nchi fulani, mtoto wa fulani, mzuri, maarufu n.k. mapenzi hakuna.
8-Tunafunga ndoa kwa vile marafiki zetu wote wamefanya hivyo na wewe unahisi kuwa nio pekee umebaki bila mume/mke, hakuna mapenzi.
9-Tunafunga ndoa ili kupata msaidizi, iwe ni kupikiwa au kujikimu kutokana na ugumu wa maisha, hapa mapenzi ni sufuri,......kama kunamengine unaweza kuongeza.
Ili ndoa iwe nzuri, yenye amani na upendo inatakiwa ijengwe kwenye misingi ya mambo mengi (inategemeana na ninyi wenyewe) lakini muhimu zaidi ni mapenzi mliyonayo kati yenu ninyi watu wawili.
Sina uhakika ( hujanipa maelezo) ya uhusaiano wenu ulivyokuwa kabla hamjaamua kufunga ndoa, mlikuwa kwenye uhusiano kwa muda gani kabla ya kufunga ndoa na vilevile ngono ilikuwaje?......
Sasa pale uliposema kuwa wewe ni "mtoto wa kitanga" ni wazi kuwa ulimaanisha ni mjuzi wa mambo ya kuridhisha, liwaza na kufurahisha mpenzi si ndio? lakini pamoja na ujuzi wako na bidii kwa mumeo huyo hakuna kilichobadilika na badala yake hali inazidi kuwa mbaya na yeye kukutenga.
Inawezekana kabisa kuwa "maujizi" unayompa sio yale ambayo yeye anataka kutoka kwako, sasa badala ya kumfanya afurahie unamfanya ajisikie ovyo na huenda anashindwa kukuambia kwa vile anaogopa kukukatisha tamaa kama sio kukudhania kuwa wewe ni "mwingi wa khabari" (Malaya) kwamba unajua mengi ukilinganisha na umri wako.....si unajua baadhi ya wanaume wa kibongo? Bado wanamavumbi (not open minded)
Lakini kitendo cha yeye kufanya ngono anapotaka na kuhama chumba ikiwa wewe unataka ngono inanifanya nihisi kuwa huyu bwana (mumeo) hana mapenzi kabisa na wewe na anapongonoka na wewe ni kwa vile anahitaji kupunguza nyege yaani unatumiwa kama "chombo" cha kumalizia tamaa zake za mwili au kama wanavyosema "kiburudisho".
Ikiwa huyu bwana hana mapenzi na wewe ni wazi kuwa hawezi kukulea, bembeleza wala kujali hisia zako, chochote utakachohitaji kwake itakuwa ni usumbufu.
Kama unampenda (najua umechoka lakini.....) kuomba Talaka kabla hujajua tatizo linasababishwa na nini na kujaribu kulitatua sio jambo la busara, Suluhisho ni kuzungumza nae (Wasiliana) na wewe kama mwanamke kuchukua jukumu la kumfanya mwanaume huyo akupende au awe na mapenzi na wewe kwani mwanamke ndio mtu pekee anaeweza kujenga maisha bora na mazuri ya ndoa au kuyabomoa.
Wanaume kama mume (samahani Kaka zangu) huwa wanadai kuwa wao ni kama watoto wanahitaji kubembelezwa wakati mwingine, sio kubembelezwa tu bali kufundishwa, kuelekezwa, kuambiwa na kuongozwa na anaeweza kufanikisha hayo yote sio mama yake bali ni wewe mkewe. Kama unamapenzi ya kweli kwake basi pigania penzi lako, sio unaachia kirahisi hivyo wakati uwezo wa kuweka sawa mambo uko mikononi mwako.
Baada ya kujaribu hayo na kushindikana hapo ndio linapokuja suala la kutafuta "ustaarabu mwingine" iweni ni kumpa nafasi (kutengana) au kuchukua kilichochako (Talaka)...
Nini cha kufanya-Muonyeshe mapenzi ya hisia na sio ya mwili, jitahidi kuwa karibu nae na kuzungumza nae kwa kumuangalia machoni (ana kwa ana) kuhusiana na unavyojisikia juu yamapenzi yako kwake (sio kulalamika), Muulize kama alipofunga ndoa na wewe hakuwa tayari au hakuwa na mapenzi ya dhati juu yako.
Sema wazi kuwa kama alikuoa kwa sababu nyingine na sio kwa mapenzi unaelewa anavyojisikia na hata kama ingekuwa wewe ungejisikia hivyo ajisikiavyo yeye......lakini wewe unampenda sana, (hapa mmwagie misifa zinazokaribia na ukweli)........sio kumuambia yeye mzuri hapana, sifa kutokana na utendaji wake kitandani, uongeaji wake, muonekano wake, busu zake, mwendo, misuli yake ya kiume n.k tena fanya hivyo ukionyesha ashiki lakini usipitilize, kumbuka unaonyesha mapenzi ya hisia na sio ya mwili hapa.
Hoji kwa upole na upendo kama kuna tatizo lolote ambalo labda wewe hulijui akueleze na mtafute suruhisho kwa pamoja kama familia, husisha watoto kwenye maongezi hayo, kuwa wanahitaji kukua kwenye mazingira ya upendo na amani utokao kwa wazazi wao ambao ni wewe na yeye.
Mawasiliano hayo yatasaidia kumfanya awe huru kutoa yaliyouaza moyo wake (inategemea na utakavyo muanza na jinsi utakavyo m-bembeleza na kumshawishi kwa mapenzi ya hisia, wanawake tuna uwezo huo)......ikiwa alikuoa wewe bila mapenzi yake anaweza kueleza hilo, kama ni "maujuzi yako" yanam-put off atasema (kumbuka unatafuta suluhisho), sasa hata akikuku-offend wewe chukulia kawaida.
Baada ya hapo utakuwa umejua ukweli kwanini amekuwa na tabia ya ajabu, hapo atakuwa amekupa mwanga wa kuweka mikakati madhubuti kurekebisha mambo. Usimtenge, endelea kumuonyesha mapenzi ya dhati. Siku akitaka ngono mmpe kwa mapenzi yako yote na wewe i-tune akili yako kuwa unafanya mapenzi na mumeo ili uweze kufurahia.
Ikitokea wewe unataka usimuambie moja kwa moja kuwa unataka kutiwa na badala yake fanya vitendo vitakavyomfanya awe-relaxed......kabla hujalianzisha, na unapolianzisha sio unakimbilia kufungua zipu na kumnyonya "abdala kipara" na badala yake cheza na zile kona za kumnyegesha mwanaume kwa kutumia ulimi au mikono na vidole.
Nasikitika kusema kuwa mwanaume anapokuambia mambo fulani na kuyarudia mara kwa mara tambua kuwa kati ya hayo moja au mawili ni kweli, hivyo ni wajibu wako kufanya mabadiliko. Sasa angalia kwa undani haya yafuatayo ambayo nitayafafanua ili unielewe vema.
Ujeuri-Kutokana na kukosa ngono ipasavyo ni wazi kuwa huna raha na inakusababishia hasira hivyo chochote mumeo atakacho kuuliza au kukuambia unaweza kumjibu kijeuri, pengine sio yeye tu bali kila mtu aliye karibu na wewe. Badilika.
Uchafu-Pamoja na kujiswafi kwako na kuoga, huenda manukato unayotumia (waoga maji ya hiriki au marumba-rumba, wajifukiza udi, mafuta uzuri yatokanayo na mkaratusi etc) ambayo Bibi alikuambia humvutia mwanaume huyu mumeo yanamchefua.
Unajua harufu za manukato (hata kama ni Oganza) zikijichanganya na harufu asilia ya mwili inaweza kutoa harufu mbaya mmno na harufu ya mwili ni bonge la pu-off. Vilevile inawezekana jinsi unavyoiweka nyuma, iweke nyumba ionenkane kuna mwanamke, jipende, badilisha mpangilio wa vitu kila baada ya miezi 3-6, ipambe lakini isiwe too much.
Pia isije kuwa jinsi unavyovyaa.....mwanamke kujipenda na kuvutia, hivyo sio unatilia mavazi mazuri ukienda harusini tu bali mvalie mumeo vizuri ili avutiwe na wewe. Badilisha mtindo wako wa kimavazi na jinsi unavyoiweka nyumba yako.
Uchoyo-Kutokana na hasira, kutokuwa na furaha, inawezekana unapika chakula cha aina moja au hupiki kabisa kumkomoa au kutuma ujumbe kuwa wewe ni muhimu, lakini yeye halioni hilo bali anakudhania kuwa wewe ni mchoyo. Vilevile inawezekana anapokuja na wageni na wewe huonyeshi kufurahi (kutokana na matatizo yako ya ndoa), lakini wageni hao na mumeo wanahisi kuwa hupendi waje kwako kula, ukidhani wanakuja kula n.k.
Ubishi-Unayokumbana nayo kwenye uhusiano wako yanaweza kuwa ni matokeo ya wewe kujaribu kupigania haki yako, mumeo anapokuambia kitu au kuomba kitu unabisha kukifanya kwa vile yeye huwa hafanyi lolote unapohitaji. Kumbuka nimekuambia onyesha mapenzi ya hisia, basi acha ubishi.
Baada ya yote haya mumeo haonyeshi kubadilika hata robo? Girl go for the Talaka, tunafunga ndoa ili kuwa na furaha, kupata ushirikiano ktk nyanja zote lakini wewe huzipati, kisa cha kuwa single mum with a husband??
Kila la kheri!
Thursday
M3 on Washenga!
Hiki ni moja ya visa vinavyoharibu uhusiano na mapenzi ya kweli katika jamii, sio hadithi au riwaya. Kuna hawa watu wanaoitwa `washenga’ na kuna kundi jingine linaitwa `makuwadi’. Tukio hili linahusu washenga.
Kuna tofauti kubwa ya washenga ambao wanafanya jambo halali katika uchumba kwenda kwenye ndoa. Lakini lipo kundi jingine la makuwadi wao wanafanya kazi ya kuwatafutia watu wengine wanaume au wanawake kwa minajili ya starehe tu, bila kujali ni nani unayemtafutia au madhara gani yatakayotokea baadaye.
Kisa hiki kimetokea maeneo ya kwetu, na kuiva hivi karibuni. Mwanzoni nilifikiri ni hadithi tu, mpaka vurugu hii ilipotokea nikaamini ni kweli. Jamaa aliyefanya tendo hili amerejea na kimwana wake na kusababisha tafrani iliyopelekea kuumizana vibaya hutaamini.
Ilikuwa hivi, kijana mmoja alirejea toka Ulaya hivi karibuni, akaona atafute mchumba. Hakutaka ile ya kuzungukazunguka, aliona aoe moja kwa moja. Jirani yake kuna binti mmoja mrembo kwelikweli lakini wa geti kali. Akampenda, akatafuta kila mbinu wakaonana, wakakubaliana.
Hili swala likapelekwa kwa wazazi na wao wakaridhia. Kiutaratibu mkishakubaliana kuwa wachumba na mkawa katika harakati za maandalizi ya harusi wewe muoaji huwa huruhusiwi kuonana moja kwa moja na binti wa watu analindwa ile mbaya, inagawaje sasa mambo haya yanafifia.
Lakini wapo wale ambao wanafuata taratibu hizi hadi leo. Sio mbaya, ila wanadamu ndio wabaya. Jamaa huyu huko Ughaibuni alikuwa na best friend wake mcheshi saana, basi yeye akaona amtumie kama mshenga wake.
Hili ni kosa kubwa, kwani washenga ni vyema wawe watu walio-oa, kama sikosei. Tusipende kuwachukua vijana, marafiki zetu ambao ni mabachela. Mawasiliano kati ya binti na jamaa yetu huyu yakawa kupitia kwa mshenga yule na wazazi wa pande zote mbili walimuamini sana huyu jamaa.
Lakini kilichokuwa kinaendelea katikati hapa watu walikuwa hawajui. Walijua baadaye.Kukawa na visa na matukio ya kuahirisha ahirisha hii ndoa kwa muda, mara bwana harusi kafiwa,mara binti harusi anaumwa , mara hili au lile. Matukio haya yalikuwa mazito yakusababisha harusi icheleweshwe na kusogezwa mbele kila tukio linapotokea.
Siku isiyojulikana binti akayeyuka. Hutaamini, wazee wa pande zote mbili walihaha huku na kule, kwanza walimficha bwana harusi lakini baadaye ilibidi aambiwe kuwa binti ametoroka nyumbani na haijulikani alipo.
Bwana harusi akachanganyikiwa, unajua kuchanganyikiwa, huyu jamaa alichanganyikiwa, akawa hali vizuri ana mawazo, akajikuta anakonda kwa kipindi kifupi. Kwanini ilitokea hivyo, kwanini alimfanyia hivyo kwanini, ikawa kwanini…Cha ajabu huyu mshenga aliondoka naye, lakini yeye aliaga kuwa amepatwa na dharura atarejea karibuni, kwahiyo hamna mtu aliyemdhania vibaya.
Na huku alikoenda akawa anawasiliana na jamaa huku akimpa moyo kuwa asikate tama. Siku zikayoyoma jamaa akasalimu amri kuwa `hiyo siyo ridhiki’ na bahati nzuri akasafiri kidogo huko majuu. Alirudi hapa karibuni na mikakati ya kutafuta mchumba mwingine.
Wakati yupo kwenye pilikapilika za kuchuja huyu au yule,mara yule mchumba wake wa zamani akareja. Na amereja na mzigo. Na mzigo huo sio mwingine ni mimba, ujauzito. Inavyoonekana wazazi wa binti walishajua nini kinaendelea, lakini wakawa wameficha, kwani vinginevyo wangeenda polisi, kuwa binti yao kapotea, hii ni hisia yangu.
Siku moja jamaa akawafuma `live’ binti yule akiwa ameongozana na mshenga wake wakitokea kiliniki. Jamaa akashindwa kuvumilia, ikawa vurugu kweli. Jamaa anasema nia sio kumgombea yule binti ila yeye alitaka kumfundisha adabu yule mshenga ambae ni rafiki yake, kwanini alimfanyia kitendo kile, baada ya kukiri kuwa yule sasa ni mkewe.
Ni vizuri kuwa waangalifu na watu hawa, na uwe na uhakika na unayetaka kumuoa kuwa kweli anakupenda kwa dhati au ni babaisha bwege. Wenu emu-three"
Wednesday
Hivi huyu anampango na mimi au myeyushaji tu-Ushauri!
Kipindi chote hicho mwenzangu hakuwa tayari kwa ndoa na mimi sababu kubwa ikiwa haniamini juu ya mahusiano ya mapenzi niliyokuwa nayo zamani kabla ya kukutana naye. Hapo nyuma niliwahi kuwa na relationships na watu wengine, ila tangu nilipokuwa nae sijawahi kuwa na wengine.
Ila wakati wa mwanzo kabisa wa uhusiano wetu aliwahi kukuta message kwenye simu yangu kutoka kwa ex boyfriend japo haikuwa ya mapenzi. All my ex boyfriends hatukugombana na kuachana kwa shari so huwa tunaweza wasiliana kama casual friends.
Alinieleza kuwa hapendi na mimi nikaacha. Ila nadhani hakunisamehe kwa hilo toka moyoni. Tumekaa na akatafuta access kwenye email yangu na kusoma mails zangu akakuta email toka kwa ex boy friend ikinipa hongera ya kuwa na mtoto, alikasirika sana na sasa akaamua kuwa uhusiano wetu ufe kabisa.
Ila mimi sababu nampenda sana nikamuomba afikirie upya uamuzi wake, mwanzo alikataa kabisa. Baadae akakubali nimpe muda japo wakati huo aliweka masharti juu ya uhusiano wetu, kuwa mawasialiano naye yawe juu ya mtoto tu.
Niliamua kujifunga mkanda na kuvumilia kipindi hiki, ni kama miezi miwili sasa tangu kianze, mwanzo nilikuwa nalia sana ila sasa nimeizoea hali, na pia hata yeye sasa anaonekana anapenda tuanze kuwa karibu, imeshatokea hata mara kadhaa tumefanya mapenzi.
Niliamua kubadili emails na hata kubadili namba ya simu ili kupunguza namna ya watu kuweza kunipata au kuwasiliana na mimi. Tatizo langu ni kwamba, sielewi kichwani kwake kweli anamapenzi gani na mimi na ana mpango gani na mimi.
Je ananiadhibu ili nijifunze somo au ananikomoa au anataka nikate tamaa sielewi. Amenifanya uwezo wangu kikazi na hata mahusiano yangu na marafiki na ndugu na hata watu wengine kuwa magumu na bado anasema anahitaji muda kuendelea kufikiri, je niendelee kusubiri au? maana kumpenda nampenda sana, kuishi bila yeye itawezanigharimu hata kuhama nchi. Naomba ushauri"
Jawabu:Pole kwa kuwekwa njia panda na baba wa mtoto wako.Kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi, pamoja na mambo mengine muhimu kuna nguzo kuu tano za kufanya uhusiano huo kuwa bora. Nguzo muhimu ambayo wengi huisahau au kutoilia maanani ni "mawasiliano".
Mawasiliano ninayozungumzia sio yale ya kuulizana hali zenu,mtoto au jinsi gani mnapendana kama sio matatizo uliyokumbana nayo kazini bali ni kuelezana na kupeana habari kuhusiana na mambo muhimu kwenye uhusiano wenu, kuweka wazi nini kinakukera, kuhoji uhusiano wenu unapokwenda, msimamo wenu na uhakika na hisia zenu, kuweka sawa mipango ya maisha yenu ya baadae (je ipo au haipo) n.k.
Asilimia kubwa ya wanadamu tunapokutana, kupendana na kukubaliana kuanzisha uhusiano huwa tunakuwa na mzigo wa maisha yetu ya awali ya kimapenzi kabla hatujakutana na wapenzi wa sasa. Hii inapaswa kutambulika na niwajibu wenu ninyi kama wapenzi kutambua kuwa ile "Past" ni sehemu ya historia ya maisha yako na haiwezi kufutika kamwe!
Hivyo wote mnapaswa kujua namna ya kukabiliana na "maisha ya awali" mnapokuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi. Sio wapenzi wote wanaoachana kwa vita na chuki, kuna wengine wanaamua kuachana tu kwa vile mmoja anataka ndoa mwingine hayuko tayari kuolewa au kuoa, wapo wanaoachana kwa vile hawaridhishana kingono, wengine wanaachana kwa vile wamegundua penzi halipo n.k.
Hizo sababu nilizozitaja haziwezi kuwafanya watu hawa walio-share sehemu ya maisha yao pamoja kuachana 4 good, wengi wetu huwa tunapaenda kubaki marafiki mpaka mmoja wetu anapokuwa na mpenzi hapo ndio huwa tunapunguza ukaribu na tunabakiza salamu tu zile za kujuliana hali kama unauhakika mpenzi wako mpya atakubali hilo liwepo n.k.
Ni kweli wewe (muomba Ushauri) unampenda mzazi mwenzako na ndio maana umekua radhi kufanya yote ambayo alitaka ufanye ikiwa ni pamoja na kupoteza marafiki zako, kubadili nambari ya simu na anuani yako ya barua pepe, lakini huyo mpenzi wako bado halioni hilo kutokana na ubinafsi alionao.
Kuna matatizo machache ninayaona kwenye uhusiano wenu (kutokana na maelezo yako)kama nilivyodokeza hapo juu ni kuwa hakukuwa na hakuna mawasiliano, mpenzi wako hajiamini hali inayopelekea yeye kuwa "control freak" na mwisho kabisa ni kuwa hana uhakika na hisia zake juu yako.
Kitendo cha yeye kuonyesha anataka kurudiana na wewe mimi nadhani ni kwavile unampa ngono, isijekuwa anakuja hapo kwa ajili ya mwili wako lakini hana mpango na wewe kama mpenzi wake wa kudumu.
Kuona ujumbe wa kukupa Hongera ya kujifungua kutoka kwa Ex sio kosa kubwa la kumfanya ahitaji muda wa kufikiri, anafikiri nini kisichofikirika kwa muda wa miezi zaidi ya miwili? Ingekuwa amekukuta na mwanaume mwingine ningeelewa kuwa nahitaji muda hata wa miezi sita kufikiri na kujitahidi kukusamehe na kusahau lakini barua pepe tu!.....anawalakini huyo.
Nini cha kufanya-Sitisha uhusiano wa kingono na yeye tangu anahitaji muda kufikiri basi aendelee kufikiri na akimaliza nakuamua kurudiana na wewe moja kwa moja ndio Ngono itapatikana. Muambie kuwa huwezi kufanya ngono nje ya uhusiano kwa vile unahofia afya yako na ya mtoto kwani hakuna sababu ya kupewa mapenzi ya mwili wakati yeye hakupi mapenzi wala amani moyoni, vilevile hujui anafanya nini huko anakotumia muda wake kufikiri. Hilo mosi.
Pili, Rudisha uhusiano kwa marafiki na ndugu zako na tumia muda wako mwingi na watu hao hali itakayokusiaidia kuondokana na mawazo juu ya mwanaume asiye muelevu na wala hajui kuthamini hisia za mtu anaempenda kwa dhati ambae ni wewe mama wa mtoto wake.
Kitendo cha kuwa karibu na watu hao (ndugu na marafiki zako) kama ilivyokuwa zamani itasaidia kuboresha utendaji wako wa kazi nakuongeza furaha kwenye maisha yako, kumbuka kuwa unajukumu lingine ambalo ni mtoto. Hakikisha huruhusu matatizo yako ya kimapenzi kuathiri utendaji wako wa kazi ili usije fukuzwa kazi.
Jitahidi kutumia muda wako mwingi na watu hao pale unapopata nafasi, ikiwezekana badilisha kabisa mtindo wa maisha yako na mtindo wa kimavazi na jinsi unavyokuwa ukijiweka wakati uko na huyo "mzee wa kufikiri". Kumbuka wewe bado Kijana, Mzuri, unapendeza na kuvutiaa sasa muonyeshe kuwa unamtaka kwa vile unampenda lakini humuhitaji (Unaweza kuishi bila yeye) ikiwa hana mpango na wewe......hapo humuambii unamuonyesha kwa vitendo, kutokana na utakavyokuwa ukijiweka, sawa?
Tatu, Ji-keep busy na mambo yako na mtoto, lakini siku akitaka kuja kumuona mtoto usimkatalie lakini hakikisha kuna kuwa na "limit" ya yeye kuwepo hapo kwako na vilevile anapokuwa na mtoto wewe endelea na shughuli zako nyingine, yaani usimpe muda wa kuongea na wewe au kulianzisha zali la kutaka ngono.
Ukiendelea kumsubiri utakuwa unajipotezea muda, unajinyima amani na uhuru wa kuwa karibu na ndugu, jamaa na marafiki na vilevile kukataa wanaume wengine wanaokutokea na wanakupenda kwa kudhani kuwa baba mtoto wako anafikiria na siku moja atarudi. Siku hazitokusubiri wewe, zinasonga mbele kama ifuatavyo.......
Nne,(ukifikia hatua hii kama anakupenda kweli na anampango nawe, ataomba mzungumze), akiomba mazungumzo na wewe usikubali haraka haraka, mpe muda......mwambie leo unashughuli nyingi hivyo muonane keshokutwa na siku ya siku ikifika usisahau kujiweka ktk hali ya kupendeza na kuvutia kwa maana ya "sexy".
......na kabla hajaanza muwahi na muambie jinsi gani umejitahidi kufanya yale yote ambayo alitaka uyafanye, ulijiweka mbali na marafiki, ndugu na jamaa kwa ajili yake, umebadili nambari ya simu na anuani ya barua pepe ili Ex wako asiwasiliane na wewe kwa vile hukutaka kumuumiza hisia zake.
Kisha muambie msimamo wako na unachokitaka kutoka kwake, iwe ni commitment au unataka kujua uhusiano wenu na mtoto unakwenda wapi na mengine unayodhani ni muhimu na unayataka kutoka kwenye uhusiano wenu huo......alafu mpe nafasi aseme alichotaka kusema!
***Lakini baada ya kufanya yote hayo bado hajaonyesha dalili ya kutaka mazungumzo ili kurudisha "majeshi", basi ujue alikuwa anakutumia kwa ngono kila anapokuja kumuona mtoto wake. Achana nae na keep sexy, keep happy, work hard na siku moja utakutana na mwanaume anaejiamini, atakae kupenda kwa dhati na kukuthamini.
Wewe bado mdada mdogo na kumbuka penzi halilazimishwi.
Kila la kheri.
Friday
Rafiki kaua ndoa ya mshikaji'ke, afanye nini-Ushauri!
Mim ni mwanaume, kuna lafiki yangu ambaye ni mtu mzima amabe ana mke na watoto. Huyu rafiki yangu ana rafiki yake kipenzi na wamekua kama familia moja, kibaya zaidi huyu jamaa (rafiki yangu) amefanya kitendo kibaya sana cha kumtongoza mke wa rafiki yake na hatimaye kufanya naye vitendo ngono.
Mie nikiwa kama msiri wake mkubwa aliponiambia mambo yale nilimkatalia kabisa na kumwambia ache mambo hayo kwani yatakuja mletea shida baadae lakini hakusikia na kuendelea na mambo yale.
Sasa kilicho kuja kutokea ni mume wa huyo mwanamke Rafiki yake) kuja kujua huo mchezo wao mchafu,alipobanwa mwanamke alikili kuwepo ukweli wa jambo hilo na uadui kuanzia hapo baina ya mumewe na huyu jamaa yangu ambae pia alikuwa rafiki yake.
Kibaya zaidi huyo jamaa kamwacha mke wake kwa sababu hiyo na kumtaalifu mshikaji kuwa amemwacha mke kwa sababu yake. Sasa amenirudia mimi nimsaidie,binafsi sijui nini cha kumshauri na kwa sababu nilimkataza mambo hayo mapema hana cha kunilaumu.
Sijui Dinah na watu wangu mna nini cha kusema juu ya hili. "
Jawabu:Hata mimi sijui cha kumshauri honestly! Rafiki yako hana utu hata kidogo, alijua ni mke wa rafiki yake na bado akatongoza na mpaka kufanya nae ngono, huyo mwanamke ambae ni mke wa rafiki yake pia ni mshenzi na hafai kuwa ktk jamii tena hana hulka kabisa. Kitu gani hasa kilimfanya akubali kutoka na rafiki ya mume wake akiwa ndani ya ndoa?
Natambua wanawake wakati mwingine tunapenda "attention", ukijua kuwa kuna wanaume wengine wanakutamani na kuku-chat up unajisikia raha na mwenye nguvu fulani kama mwanamke, kutongozwa ni kawaida kwa baadhi yetu, kwani kuolewa haina maana kuwa hatutamaniwi na wanaume wengine.
Lakini hiyo haina maana kuwa umkubali kila anaekutongoza na kuanzisha uhusiano ukijua uko ndani ya uhusiano mwingine na mtu unaempenda na ulieahidi kuishi nae maisha yako yote!
Uhusiano wa rafiki yako na mke wa rafiki yake ukoje? bado wanaendelea baada ya mwenye mke kuacha? Je wanadhani kuwa wanapendana?......kama uhusiano wao mzuri basi waendelee lakini kama jamaa alikuwa anataka kuharibu ndoa ya mwenzie kutokana na tamaa au wivu basi akamuombe rafiki yake msamaha alafu ajitenge nae (yaani urafiki ufe), asijaribu kuendeleza urafiki na jamaa baada yakumtombea mkewe.
Ushauri wangu ni wewe kumaliza urafiki na huyo mharibifu wa ndoa ya watu kwani ni wazi kabisa na wewe ukioa ataweza kufanya exactly alichokifanya kwa rafiki yake nakusababisha ndoa yako kufa.
Watu kama hawa, wanapaswa kutengwa na jamii, kwani wanasababisha watu hasa vijana kuhofia suala zima la kufunga ndoa, wanaifanya ndoa kutokuwa na thamani tena.
Kila lililojema!
Tuesday
Nilihisi, nikahakiki, akabisha sasa nimepoteza mapenzi?-Ushauri
Mimi ni msichana wa miaka 28 nimeolewa na nina watoto waili. Tatizo langu ni kwamba nilihisi mume wangu anatoka nje ya ndoa wakati nikiwa mjamzito wa mtoto wa pili, baada ya kuona anapokea simu za ajabu ajabu na kutwa simu zake alikuwa anaziweka silent au simu zinakaa kwenye suruali tu au kwenye gari.
Siku moja usiku kama saa 4 hivi ilipigwa simu alikua anaoga cha ajabu simu ilikuwa inawaka taa tuu kwa namba hiyo ila kwa namba zingine zinaita kwa sauti ila kwa namba hiyo ndio inawaka taa tu tena bila hata vibration, mi kuona hivyo nikapokea hiyo simu na kukutana na mwanadada bila hata kujua ni mie nikasikia mambo darling, nikamwambia Darling wako anaoga una ujumbe akija nimpe?
Akakata simu mie nikachukua ile namba nikasave kwenye simu yangu na darling wake alipotoka siku mwambia kama alipigiwa simu. Mara tukiwa mezani na watoto tunakula ikapigwa simu ileile akapokea akaanza kubabaika, kidogo kaacha chakula kasema kaitwa na ndugu yake ana matatizo na mie nikamwambia ni bora twende wote maana kama ndugu yake na mie ni wangu pia akakataa na mie nikamwambia hutoki nje ya nyumba hii usiku huu bila mie nikachukua funguo zote za gari nikakaa nazo na nikamwambia ukitoa mguu hapa utajuta.
Basi akaenda chumbani kupiga simu na mie nilijua tuu nikaenda mlangoni nikawa namsikiliza eti anasema naweza kuja ila sina uhakika ila usitegemee sana. Sasa mie kwa hasira Asubuhi nikampigia huyo dem wake kwa private akapokea nilivyokuwa naongea nae akanishtukia akampa mwanaume aongee.
Jioni nikauliza hii namba ni ya nani akaniambia ni ya rafiki yake nikamuuliza mbona sijawahi kusikia kama una rafiki kama huyo nikamwambia mbona ni mwanamke akaniambia kuwa huwa wanashare na mumewe simu nikajua lazima atakuwa kamwambia kuwa nimepiga simu leo.
Nikamwambia huo ni uongo, Basi baada ya hapo nikawa na stress za ajabu mpaka nikapata na matatizo sana mpaka nikaandikiwa Bedrest na ninashukuru Mungu kanijaalia nikazaa salama salmini.
Baada ya kuona nina matatizo akaniambia kuwa huyo dem ni mke wa rafiki yake na anamtaka yeye hana mpango nae na hana tena mawasiliano nao kabisa na sitakaa nisikie simu wala nione sms toka namba hiyo.
Mara akaumbuka ilipoingia sms inamuuliza Vipi leo utakuja??? Mi nikaijibu nikasema siji then nikamwambia kuna msg yako hapa imekuja na nishakujibia, Nikamwambia kama kweli huna mpango nae mpigie simu umwambie amkomeshe na mie nikisikia kama kweli akasema ooh haina haja sijui nini akajitetea na kusema kwakua ndio nilikuwa nimetokakujifungua hata mwezi haujaisha.
Nikaachachana nae nikalala nikaogopa kujipa stress nikakosa Maziwa ya mtoto bure, Asubuhi nikapiga simu ili niongee na yule dada kwa amani yule dada lipogundua ni mimi aliniporomoshea mitusi hata kabla sijaongea nilichotaka kuongea.
Jioni nikamwambia bwana'ake(mume wangu) nikajibiwa sasa na wewe unapigiapigia simu tu watu usiowajua unategemea nini? Sikuamini kama nimejibiwa hivyo nikasema poa nimekoma. Na toka siku izo nikawa sina mapenzi na yeye nikawa namwangalia tuu, niko na watoto wangu tu ila yeye sina stori nae zaidi ya salamu na siku nyingine hata simsalimii ila naumia sana.
Nikakaa kimya nikawa sina mpango nae tuko tuu kama kaka na dada nikiongea nae sawa nisipoongea nae poa, Siku moja nikaamua kumtisha nikamwambia sasa nishamaliza meternity leave namaanisha kuwa mtoto ni mkubwa vya kutosha na sasa na mie naweza kutafuta mtu wa kunipooza moyo niondokane na mawazo nikae na mie na amani moyoni tuwe Ngoma droo.
Maana kama yeye kaoa na anatongoza basi na mie nimeolewa na nitatongozwa na akijaribu tu namkubali hata kama sijampenda ilimradi na mie nipoze moyo .Kumbe ilimuiingia na akajua naweza kufanya kweli akaanza kujidai anarudisha mapenzi kwa kasi kubwa mara ananiongelesha hata kama sitaki kuongeleshwa mara hivi mara vile.
Ila mie nikawa tu kama jiwe sijali ndo kwanza najidai simwoni niko Busy na simu kutwa nachat na rafiki zangu nacheka yani hata nikiwa na rafiki zake au ndugu zake mie busy na simu yangu tuu wala siwaoni.
Siku moja nilikuwa nimelala akaniamsha eti naomba kuongea na wewe nikamsikiliza akaniambia eti kuwa vile nilivyokuwa navihisi ni kweli alikuwa na mahusiano na huyo dem ila ni mahusiano tu kama rafiki yake tu wa kuongea nae tuu na kunywa tuu lakini hajawahi kufanya nae chochote hata kiss hajawahi miezi yote zaidi ya 7.
So mie nikitaka kufanya nitalipiza itakuwa ni kuwaumiza watoto tu cha kufanya tuelewane na tupendane kama zamani maana yeye hajafanya chochote cha ajabu ni kukaa tu na kuongea na huyo dada.
Nikamuuliza kama kweli kwanini ulishindwa hata kuniambia kama una rafiki wa design hiyo? Na kwanini siku aliyonitukana kama ni rafiki wa kawaida kwanini asimchukulie hatua yeyote au kwanini huyo dada anitukane kama hatembei na mume wangu??
Mi nikamsikiliza alivyomaliza nikamwambia haya nimekusikia nikaendelea kulala maana nilijionea ananizingua tuu mie nausingizi na nasubiri niamke kumnyonyesha mtoto ye ananiletea habari zake za kijinga ambazo mie zimegoma kaminika na kichwa changu.
Sasa naomba mniambie kwa story hiyo ni kweli kua hajawahi kufanya chochote au kaamua tu kuniambia hivyo kwakuwa nimemtishia na mie kutoka nje ya ndoa au kurudisha amani ndani?
Mie bado nipo vilevile kama jiwe vile simjali kwa chochote najijua mie na wanangu tuu yeye namwona kama picha ya ukutani tuu."
Jawabu: Asante sana kwa ku-share tatizo lako mahali hapa, nakupa pole kwa yote unayokabiliana nayo lakini wakati huohuo nakupa hongera kwa kusimama Imara dhidi ya emotional "abuse" kutoka kwa mumeo.
Hili ni tatizo sugu kwa wanaume wengi wa Kiafrika, mwanamke anapokuwa mjamzito au kujifungua wanadhani wamepatiwa nafasi ya kwenda kutembeza "viungo" vyao nje ya ndoa zao. Kutokana na maelezo haya ni wazi kuwa mumeo hakuwa akikuthamnini na wala hana haeshimu ndoa yake.
Hawajui kuwa Mwanamke anahitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa mume mara baada ya kujifungua, sio kuanza kusumbuliwa kiakili na kihisia.
Mumeo ameongopa ili wewe usiende kufanya kama alivyofanya yeye(Mkuki kwa Nguruwe) lakini ukweli (kutokana na maelezo yako) amefanya mambo ya kimapenzi mengi tu na huyo "rafiki yake".
Kinachoshangaza nikuwa, pamoja na kukubali urafiki ulikuwepo bado hajaonyesha kuwa anajutia makosa yake kwani hajakuomba msamaha, kitu kinachonifanya mimi (Dinah) nihisi kuwa mumeo huyu anakiburi, anajivunia alichokifanya na hana mpango wa kubadili hiyo tabia yake chafu.
Naelewa kabisa uamuzi wako wa kumtenga mumeo na itachukua muda mrefu sana mpaka utakapomuamini tena, kumtamani tena, kumtaka tena na kujisikia kutaka kufanya nae mapenzi.
Inawezekana kila ukiwa nae karibu au anapokufanyia jambo/mambo fulani picha ya yeye kumfanyia yule mwanamke mwingine inaweza kukujia na kuua "mood", yaani hata kama ulikuwa na hamu inakuishia ghafla.
Nini cha kufanya-Kama tangu umejifungua hujafanya mapenzi na mumeo itakuwa vema akienda kuangaliwa kama yuko salama kutoka VVU, lakini kama ulikuwa ukifanya mapenzi wakati unahisi kuwa "anatereza" nje basi ni vema kama wewe, yeye na mtoto mkaenda kuangaliwa damu ili mjue kama mko salama kutoka VVU.
Pamoja na kuwa mumeo anaonyesha mapenzi kuliko mlivyokutana hapo mwanzo, hakikisha hu-give in mpaka aombe msamaha na kuahidi kutorudia tena kosa alilolifanya (msamaha maana yake ni mabadiliko kwa vitendo), hivyo hiyo itakuwa nafasi yake pekee ya kubadilika.
Kamwe usimwambie ukweli kuwa ulikuwa unamtishia kuwa utaenda kulalwa nje ya ndoa yako, iache kama ilivyo.......najua siku moja atataka umhakikishie kama kweli ulikuwa na mpango huo au hata kama tayari umelala na mwanaume mwingine (hapo alipo linamuuma kweli kweli sema hana jinsi ya kuliweka wazi......hakuna mwanaume anapenda kutombewa mwanamke wake, hasa yule mwenye tabia hiyo.
Akitaka kujua muambie ukweli kuwa hukufanya lakini ulikuwa ukisukumwa kufanya hivyo kutokana na tabia yake ya kwenda nje ya ndoa yenu...kwa maana nyingine ni kuwa, huwezi ku-cheat ikiwa yeye hato-cheat, aki-cheat anakuhamasiha na wewe kufanya hivyo. Hii itakuwa adhabu tosha kwake japokuwa wewe unajua moyoni huwezi ukafanya hivyo bali ulikuwa ukimtishia tu.
Kitu kingingine ambacho ni muhimu sana ni kuwekeana Sheria, ni mume wako, mnapokuwa pamoja inamaana mnaunda ushirika fulani ambao unapaswa kufuata Sheria fulani na ni mwiko kabisa kuzivunja.
Kwa Mf-Simu yake ni yako, rafiki zako awafahamu na wewe uwafahamu wake, Namba zote ziwe-saved kwa majina unayoyajua kutokana na ulivyotambulishwa, kama kuna shughuli za kifamilia wote 2 mnashiriki, hakuna safari za usiku unless mnatoka wote, kuambizana kwa uwazi kama kuna kitu kimepungua kwenye uhusiano wenu na kupeana mikakati ya kukirudisha, kuwa na muda wenu kama wapenzi na sio kama baba na mama, kutumia kinga dhidi ya VVU mpaka utakapo hisi kumuamini tena (kama utaamua kufanya mapenzi na mumeo).
Kumbuka kwenye ndoa yenu kuna watu wadogo wawili hivyo ni muhimu kuwafikiria watoto wenu zaidi na maisha yao ya baadae kuliko kujifikiria ninyi zaidi. Hawa watoto wanahitaji mapenzi yenu nyote wawili, baba na mama mliopendana hapo mwanzo na kufunga ndoa.....hivyo ni vema kuonyesha mapenzi mbele ya watoto wenu na tofauti zenu kuziweka pembeni machoni mwao.
Ukiona unashindwa ku-recover kutokana na "Emotional abuse" basi unaweza kwenda kupata msaada kwa wataalamu, kama nilivyosema itakuchukua muda mrefu lakini kutokana na ushirikiano wa mumeo (kubadili tabia) utakuwa sawa na kufurahia ndoa yako.
Wewe ni mwanamke tofauti kabisa na wale tuliowazoea hapa Bongo akina "ndio bwana", ni mfano wa kuingwa na wanawake wengine, kisa chako kinaonyesha kuwa huitaji mwanume bali unamtaka mwanaume.........Safi sana.
Mimi na wachangiaji wengine tunakutakia kila la kheri.
Monday
Nimebamba msg za mapenzi kutoka kwa Ex ?-Ushauri
Hope ya doing fine with ya great work that ya doing of advicing us people who are confused with these love affairs.
Am a girl 23yrs old, now I have a boyfriend whom we have kinda long relationship we have been together for a year now. But what gives me headache is his Ex girfriend. Last week when I was at his place I tried to send a msg by using his phone i was so saprised when he rushed into me and took the phone by force without even know what i wanted it for.
Sis dinah thats is what gave me suspecious of what can be in that phone so after a while I pretented to go to a waah room and took his phone with me when I opened the inbox I found alot of msgs from his EX I was so heartbroked and i couldn't ask him nothing since he didnt know I took his phone.
The msg where like they are still love eachother and they wanna ge back together I really wanted to ask him but i was so afraid so I decided to just ask and if they would be I would just sufer the consequences.
So I ask him and what he told me is that the girl wants him back but he doesn't want to go back to her that's why there are msgs in his phone and he didn't want me to see them coz he didn't want me to suffer.
Should I truest him or he just lieing to me to get me out the way?He said if I didnt trust him we can call the girl and ask her. But i can't do that coz I will seem to be unsecured of his love.What can I really do my dear I do still love him and I did trust him B4 the msgz.
Thanks Dinah and may good bless u with all the gratfull of the world"
Sunday
Ananiacha kwavile tu mimi sio kabila lake!-Ushauri
Habari yenyewe inaanza mwaka 1998 Novemba baada ya kuhamia Arusha tukitokea DSM baada ya baba yangu aliyekuwa Askari jeshi kuteuliwa kuwa Katibu Tarafa mkoani Arusha na kuhamishia makazi huku.
Kwenye nyumba tuliyofikia alikuwa akiishi msichana moja anaitwa Agness Meliyo(Totoo)kabila ni Muarusha alikuwa akiishi na mama moja aliyeamua kumsomesha msichana huyo na kumsaidia kazi ndogondogo baada ya kutoka shuleni, sasa kipindi hicho mimi nilihamia nikiwa darasa la sita na kuhamia shule hiyo aliyokuwa akisoma msichana huyo yeye akiwa darasa la nne.
Kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemtamkia mwenzake kuwa anampenda kwa kuwa bado tulikuwa shule ya msingi mwaka 1999 baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba wao walihama katika kitongoji cha Sakina na kuhamia katika Kitongoji cha Majengo kwa kuwa mama huyo aliyekuwa akimlea alikuwa akinipenda nilimsaidia kuhamisha baadhi ya vitu na kuniomba nikalale kwake alipohamia nilifanya hivyo na kipindi hicho ndicho tulianza rasmi mapenzi yetu na Agness.
Baada ya kukubaliana nakuona kila moja mwenzake anampenda tulianza mahusiano naye mwaka 1999 Desemba nikiwa mimi tayari nimemaliza darasa la saba na nikajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2000 nikiwa kidato cha pili baada ya miaka miwili kuanza shule yeye akiwa darasa la sita tulishirikiana kingono na kwa kweli nilimkuta na usichana wake ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kukaa miaka miwili pamoja.
Kwa kweli mapenzi yetu yalikuwa ni mazuri huku kila moja akijitahidi kumpenda mwenzake kwa nia ya siku moja kuoana na uhusiano wetu ulikuwa ukijulikana na wazazi wake wa kumzaa ambao nao tunaishi nao hatua chache kutoka tunapoishi sisi pamoja na mama yake mlezi.
Baada ya mimi kumaliza kidato cha nne mwaka 2003 nilisoma baadhi ya kozi hapa Arusha na mwaka 2005-2007 nilikuwa DSM nikisome katika chuo cha Rayol college of Tanzania nikisomea Uhandishi wa habari muda wote tulikuwa tukiwasiliana na kupeana ahadi nyingi ya baadaye kuja kuishi pamoja,na kipindi chote alikuwa anakuja nyumbani na anamsaidia mama yangu kudeki,kupika na kuosha vyombo yani kila mtu alikuwa akielewa uhusiano wetu.
TATIZO LENYEWE.
Baada ya kumaliza kidato cha nne mchumba wangu huyo aliamua kusome Ualimu wa awali(chekechea)kwa muda wa miaka miwili na kipindi fulani akikaribia kumaliza chuo alikuwa akidaiwa Ada jumla ya Tsh.Laki moja na mama yake mlezi alimweleza kuwa kipindi hiki yeye hana fedha kwa hiyo amfuate mama yake mzazi amlipie Ada hiyo naye mama yake hakuwa nayo ikabidi amweleze mama yangu ambaye alimpatia fedha hiyo na kwenda kulipa Ada hiyo na kufanikiwa kumaliza lakini hivi sasa ndio wapo kwenye mitihani ya mwisho huku akiwa amepata field katika moja ya shule mkoani Kilimanjaro.
Msichana huyu kwa kweli ndugu zangu nilikuwa nampenda sana ni ilikuwa kuanzia mwakani tuanze kuishi pamoja kwa sababu ndio alikuwa amemaliza masomo yake.
Tumeishi na msichana huyo tangu mwaka 1999 akiwa ni mwanafunzi wa darasa la nne hadi leo 2008 Novemba eti ndio ananieleza niachane nae kisa ni hivi.
Msichana huyo yeye ni Muarusha na kabila hilo huwa halitaki kuoana na kabila tofauti eti mama yake amemtishia kumlaani ili aweze kuachana na mimi wakati tangu muda mrefu wazazi wake walikuwa wakipinga na yeye alisema hawasikilizi.
Baada ya kupata nafasi ya field huko Moshi alikuja nyumbani siku moja nikijaribu kuongea naye anakuwa na hasira hakutaka kuongea na mimi kabisa sasa kuna rafiki yake ambaye hupenda kumueleza mambo yake na yangu hata yale ya siri,nikawa nimestuka hali hiyo nilimweleza dada huyo ambaye huuza pombe katika kibanda na nyama ya nguruwe kuwa anayoyataka yatatimia kwa kuwa alikuwa akiongea baadhi ya mambo kinyume nyume kinachohusiana mimi na mchumba wangu tena mambo yenyewe yakiwa ni siri kati ya mchumba wangu na mimi.
Basi siku moja alikuja kutoka Moshi akamweleza rafiki yake huyo ambaye mimi nahisi ndiye mnafiki kuwa eti ana mazungumzo na mimi nilimfuta nyumbani kwao saa za jioni akaniambia ni kweli anataka kuongea na mimi lakini kwa muda huo alikuwa akitoka akielekea Ngaramtoni kwa rafiki yake nikaachana nae nikarudi kwa huyo dada na kumuuliza ni kitu gani anachiotaka kuongea.
Agness akaniambia kuwa eti anataka kuachana na mimi na alishamweleza kila kitu dada huyo na kesho yake aliporudi kweli akanielezea kusudio lake na nilipomuuliza sababu yeye alisema kuwa ameamua tu na kwa sababu ya mama yake kumkataza eti jamani baada ya miaka tisa nikiwa naye tena nilianza naye akiwa ni mtoto kabisa.
Lakini siwezi kuwaficha kitu chochote juu ya huyo binti ila nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilimuita msichana huyo chumbani kwangu ni ilikuwa ni kujaribu vipi kuhusu ahadi yake na mimi baada ya mambozii fulani nilimweleza kuwa nilikuwa nataka kuachana naye kwa kweli alistuka sana na aliponiuliza ni kwa sababu gani sikumweleza kitu chochote na akaamua kuondoka chumbani kwangu.
Asubuhi ilipofika alinitumia barua kwa mdogo wake na ndani ya barua hiyo alikuwa amesema kuwa hawezi kuishi bila yangu hivyo ameamua kujinyonga na akasema tukio hilo atakwenda kulifanyia chumbani kwangu kwa kweli nilimsihi sana asifanye hivyo na akanielewa baada ya kumwita na kuongea naye kuwa nilikuwa nataka kujua msimamo wake katika uhusiano wetu na alinielewa tukarudia kama zamani tena kwa upendo zaidi hadi kilichotokea hivi ajuzi.
Hivyo ndugu zangu wadau naomba ushauri wenu maana nimeshindwa kuvumilia kwa sababu ninampenda sana na tumeishi naye kwa muda mrefu tangu wote naweza kusema tulikuwa wadogo maana mimi nilikuwa ndio nimemaliza darasa la Saba na yeye akiwa darasa la Tano mwaka 1999 mpaka leo ameamua kuachana na mimi je? nifanyaje."
Wednesday
Nampenda mume wangu lakini hani-apreciate!-Ushauri
"Dada dinah mimi sijui hata nifanye nini kwani kila siku najikuta sina raha na mume wangu ndani ya nyumba. Nimeolewa miaka mitatu sasa na nimevumilia wee sasa nimechoka kabisa na tabia yake ambayo mimi sijaizoea. Siokwamba hatuzungumzi mambo ambayo hayatufurahisi, tunaongea sana tu lakini inaonyesha kuwa hawezi kujirekebisha.
Tatizo lenyewe ni hili, mume wangu hajawahi kusema asante nikimfanyia jambo au kitu. Yaani hata baada ya kula asante huwa hamitoki anaishia kusema nimeshiba au chakula kilikuwa kitamu, ile shukurani haipo, hata kama amekinunua yeye si bado jamani anatakiwa kunishukuru mimi kwa kumpikia kama ninavyomshukuru mimi akinipa pesa za matumizi au akija na chakula nyumbani huwa namwambia asante kwa kununua kitu fulani.
Kitu kingine ambacho sina uhakika naomba wewe unisaidie kutokana na uzoefu wako ni hivi, eti kumfulia na kumpigia basi mume wangu ni wajibu wangu wa ndoa? na je nikimfanyia hivyo anatakiwa kunishukuru au inakuwaje hapo.
Alafu tukifanya mapenzi na kumaliza nani anatakiwa kumshukuru mwenzie? na je unamshukuruje mpenzi wako baada ya kufika kileleni?
Dada dinah wengine tuliolewa bila kuwa na bahati kama uliyokuwa nayo wewe, tuliolewa tukijua kusema asante na samahani mengine tunajifunzia humo humo na wakati mwingine unaishia kukasirika tu kwa vile unahisi mpenzi wako hakujali wewe wala yale madogo umfanyiayo.
Nifanye nini ili na mimi nijisikie spesho ndani ya ndoa yangu?"
Jawabu: Kweli umevumilia sana kwa miaka yote mitatu kuishi na mtu ambae unahisi haku-apreciate, kwa kweli inaumiza sana kwa mtu ambae anaelewa umuhimu na thamani ya kuonyeshwa kuwa uko-valued kwenye uhusiano wako na kuwa-appreciated hata kwa kile kidogo unachokifanya.
Nafurahi sana kuwa umelileta hili mahali hapa ili wale ambao labda walikuwa hawajui ni jinsi gani baadhi yetu huwa tunajisikia ikiwa wenza wetu hawaonyeshi shukurani kwa uwepo wetu achilia mbali vile vidogo tufanyavyo.
Mimi binafsi kama Dinah sipendezwi na tabia ya baadhi ya watu na kukufanya wewe ujisikie "unppreciated" ni kama vile unajipendekeza au mpenzi hana habari na wewe (huenda anakujali and all that lakini haisaidii ikiwa sioni, hunionyeshi kuwa unashukuru, unani-value n.k), Kitu kidogo kama kumuambia mpenzi wako "nakupenda" bila kupata ile "nakupenda pia" inaweza kukufanya ujione "msaidizi" badala ya mpenzi wake.
Unatambua, kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) wanapokuwa na wewe kama mpenzi/mke wanahisi kukumiliki hivyo chochote unachokifanya kwa ajili yao ni haki yao na "actualy" unapaswa kufanya hivyo kwani wamekuoa au umewaoa kitu ambacho sio kweli na kama ni Imani basi ni potofu kuliko maana halisi ya neno lenyewe.
Kuna wanandoa waliwahi kuja kwangu wakitaka ushuri, nilipozungumza nao niligundua kuwa hawafanyi vile vitu vidogo ambavyo wengi tunavidharau bila kujua umuhimu wake kwenye maisha yetu kama wapenzi, Mume alikuwa anadai kuwa anahisi kuwa hamridhishi mkewe kitandani kwavile mkewe huyo hajwahi kuonyesha shukurani kila wanapofanya mapenzi........sasa unaweza kugundua umuhimu wa shukurani kwa baadhi ya watu.
Mtu kama wewe (muuliza swali) asante kwako ni muhimu na inakufanya ukose amani ndani ya ndoa yako(this is serious), si ajabu unajihisi mpweke wakati mwingine kwa vile unahisi kuwa mumeo haku-appreciate.
Wengi tunatofautiana kimalezi kwani tumlelewa ktk mazingira tofauti, baadhi yetu tulifundishwa umuhimu wa kuomba msamaha, kuomba ikiwa unahitaji kitu na kushukuru unapopewa au fanyiwa jambo lakini wapo ambao vitu kama hivyo havikuwepo kabisa (msome m3 kwenye Comment).
1)-Kweli kabisa mumeo anapaswa kushukuru kwa kumpikia na kumuandalia chakula hata kama yeye kakinunua, unapompikia mume wako mara nyingi unapika kwa mapenzi yako yote, utamu wa chakula au uchaguzi wa nini kiliwe siku hiyo unatoka moyoni mwako na unafanya hivyo ili mume wako akirudi nyumbani afurahie chakula hicho. Sasa asiposema kuwa kakipenda na kushukuru kwa kweli inakatisha tamaa na inauma mno.
Kule kwetu tunaambiwa/fundwa kuwa hakikisha mumeo hali chakula cha mwanamke mwingine(hata kama ni mama yake), ikiwa anapenda kula kwa mama'ke au kwa rafiki yake (mkewe kapika) au Hotelini basi hakikisha unajifunza mapishi hayo......got the point eeh?
2)-Kitu chochote unachokifanya ndani ya ndoa yako kwa ajili ya mpenzi wako sio wajibu wako wa ndoa ni mapenzi yako juu yake, kumjali na kuhakikisha kuwa anakuwa msafi na anapendeza wakati wote bila kusahau kumsaidia labda kutokana na shughuli zake nyingi za kikazi. Lakini kama wote mnafanya kazi basi mnapaswa kufua pamoja au mmoja wenu kufanya hivyo akipata nafasi......ndoa ni ushirika hivyo mnatakiw akushirikiana na kusaidiana ktk kila jambo ndani ya nyumba yenu.
Bila shaka ikiwa atakuta nguo zake zimefuliwa na akunyooshwa basi anapaswa kuonyesha kuwa ameona hili na anashukuru kwa kufanya hivyo....."mke wangu asante kwa udobi" sio sentensi ngumu na wala hulipii kodi japokuwa kwa mwanamke inathamani kubwa sana.
3)-Ku-appreciate baada ya kufanya mapenzi au hata wakati mchezo unaendelea inategemea na wahusika wenyewe, unaweza ukawa unasema jina lake na kumwambia kiasi gani unapenda anachokifanya na mengine yatakayokujia wakati huo unaposikia raha/utamu.
Vilevile unaweza ukamkumbatia kwa nguvu na kwa mapenzi yako yote na kumbusu kabla "hajang'atuka" mwilini mwako, pia unaweza ukasema asante na kumuambia jinsi ulivyofurahia "the moment" na kama amekufanya ktk mtindo tofauti au leo umehisi kichw akikubwa zaidi kuliko jana mwambie......na yeye akafanya hivyo kwako.
Ufanye nini basi ili aanze ku-appriciate-Ondoa hasira na anza kuwa unamshukuru kila anapokufanyia kitu hata kama ni kukukata ukucha, mwambie asante na mpe kibusu shavuni au mshike kuonyesha shukurani yako. Hilo mosi.
Pili, Mwambie ukweli tu jinsi unavyojisikia, mwambie kwa upole na kwa upendo kuwa unahisi "unappreciated" na inakunyima amani kabisa moyoni mwako.
Mueleze kuwa unapompikia chakula huwa unakipika kwa mapenzi yako yote, na huwa unasikia raha ikiwa anaonyesha kukipenda lakini unahisi "special" zaidi ikiwa atasema asante kwa chakula kitamu n.k
Ni mumeo na hakika anakupenda, ikiwa alikuwa hajui kuwa "shukurani" ni muhimu sana kwako basi atataka kujua zaidi vitu gani akifanya unahisi kuwa na wewe ni "special wife" kwake na ataanzia hapo, taratibu lakini surely na atazoea na maisha yako ya ndoa yatakuwa mazuri na kwa vile utakuwa na unahisi spesho kama ulivyosema na vilevile hutokuwa na hasira tena.
Mungu ailinde ndoa yenu, kila la kheri!
Nakuja......
Monday
Miaka 5 na mume wa mtu, Hamkunielewa-Ushauri.
Kifupi ni kwamba huyu bwana yuko tayari kumpa talaka mkewe ila mimi siko tayari kwahilo. Pili kuhusu kuolewa yuko tayari mda na siku yoyote hata leo ila dini zetu zinaleta pingamizi nami naliona gumu pia kwani siwezi kuwa muislam na yeye alishambadilisha mkewe dini na kumpeleka uislam hivo hawezi kuja ukristo amwache mkewe huko.
Naombeni tena mnisaidie nitumie mbinu gani nitumie katika kuachana na huyu bwana na ni mda gani muafaka wa kutumia katika kulizungumzia hili kwani kila nikijaribu kumtajia hilo tu ni ugomvi na inakuwa kama ndo nimemwambia ahamie kwangu kwani atalala kwangu mwezi mzima bila kwenda kwake.
Kunitambulisha ameshanitambulisha kwao ndugu,wazazi, mkewe, watoto wote wananijua na wamenikubali ila kwangu naona sio kitu hilo kwani siko kwenye nafsi zao hivo uenda ni unafiki au ni ukweli.
Nashukuru sana kwa watakaonisaidia kutatua hili na sio kuniponda.
Kazi na siku njema wote Asanteni. "
Jawabu: Pole kwa kukwazika. Wasomaji wangu ni wazi walipatwa na hasira kwa sababu wasingependa kitu kama hicho kiwatokee wao au hata wanawake wenzao kwa imani kuwa wanawake tunapaswa kushirikiana na sio kuharibiana ndoa.
Mume/mke wa mtu akikutokea mkatae akizidi kukufuata fuata basi nenda kamwambie mkewe hali itakayofanya mke huyo kuwa awear na tabia chafu ya mume/mke wake....hapo utakuwa umesaidia kuokoa ndoa yao, maisha ya watoto wao (ni vema watoto kukua ndani ya ndoa wakiw ana wazazi wote 2) na kuongeza amani kwenye nyumba yao.
Majibu ya wengi yaliegemea kutokana na maelezo yako ambayo sasa umegundua kuwa hayakuwa yamejitosheleza au hayakuwa wazi kwenye points muhimu ambazo ni hizi:-
1-Kumbe jamaa ni Muislamu hivyo anahaki kabisa ya kuoa mke wa pili kwa mujibu wa Imani yake as long as anauwezo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.
2-Wewe hauko na haukuwa tayari kufunga nae ndoa ya kiislamu(hutaki kubadili Dini), which tells me kuwa wazazi wako hawamkubali jamaa kwa vile Dini yake ni tofauti na sio kwa vile ni mume wa mtu.
3-Mkewe, watoto, ndugu na jamaa zake wamekukubali kama mke wa pili lakini wewe ndio unasita kutokana na Imani zenu za Dini kuwa tofauti.
Ungeweka wazi yote haya ingesaidia wasomaji wangu kukupa ushauri tofauti na walivyokushauri mwanzo.*********************************************
Nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kutoka kwenye uhusiano huo kama ambavyo wengi walikushauri, kwani ukikubali kuolewa ni wazi kuwa utakuwa umechangia kwa kiasi fulani kuharibu maisha ya watoto ambao tayari wamezaliwa kama matunda ya ndoa hiyo(haijalishi kama dini inaruhusu au la) suala muhimu ni kutokuwa wabinafsi na kuwafikiria watoto hao na maisha yao ya baadae.
Nasema hivyo kwa vile, watoto hao siku zote watakuwa wakichukulia au kuamini kuwa wewe umechukua nafasi ya mama yao na maisha hayatakuwa the same kwao kitu ambacho wengi huwa tunajaribu kukiepuka.
Watoto hao watalazimika kukupa heshima ya uoga (kwa vile baba anataka iwe hivyo), lakini mioyoni mwao hautokuwepo kabisa (jaribu kujiweka wewe kwenye their shoes.....ungejisikiaje?).
Hawatokupa upendo sawa na ule walionao kwa mama yao mzazi, hawatokuthamini kama vile wanavyofanya kwa mama yao mzazi hali itakayokufanya utamani kuzaa watoto wako mwenywe kitu ambacho kitaongeza idadi ya watoto na hivyo maisha yanaweza kubadilika kwani huwezi kujua nini kitatokea in 10yrs time.
Kama hao watoto hawatopata matunzo muhimu labda baada ya mama yako kuachika na wakaamua kwenda kuishi na mama (watoto wengi huenda na mama, mama are the best, we have strong bonds na we love mamas) au kushindwa kuendelea na masomo baada ya baba yao (mungu apishe mbali) kuodoka Duniani lawama zote zitakuangukia wewe, labda usingeolewa na baba yao na kuongeza Idadi ya watoto maisha yangekuwa tofauti hata kama Mzee hayupo.....si unajua mambo ya urithi!
Kujitoa kwako kwenye uhusiano na mume wa mtu kutakuwa kumeokoa ndoa ya mwanamke mwenzio, kuokoa maisha ya baadae ya watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na pengine litakuwa fundisho kwa mwanaume huyo na hivyo itakuwa mwisho wa kuwa na kimada.
Kuna mchangiaji mmoja kagusia kuhama mji, hiyo ndio njia nzuri na ya pekee ambayo inaweza kuua uhusiano haraka na kukusaidia kuanza maisha upya mkoa/kijiji/kitongoji/mji mwingine. Wakati unaendelea na mipango yako ya kuhama "nchi" humuambii mtu, ukikamilisha wewe unatoweka tu lakini julisha ndungu zako na hakikisha hawamuambii jamaa uko wapi.
Ili basi kumsaidia huyo jamaa, muandikie walaka wa kwanini umeamua kuua uhusiano wenu (usiseme unahamia wapi) na weka points muhimu wazi, Points muhimu ni kuhusu ndoa yake(onyesha kuwa hauko tayari kuharibu ndoa ya mwanamke mwenzio, usigusie suala la utofauti wa dini zenu), watoto na maisha yao ya baade(onyesha unajali maisha ya watoto hao kama vile ambavyo ungejali maisha yako wewe ulipokuwa mtoto).
Mungu atakubariki kwa kuokoa ndoa ya mwenzio na vilevile atakujaalia na utakutana na kijana kama wewe, mwenye nia moja kuwa na wewe kama mke wake.
Sio mwisho wa maisha kum-buti mpenzi, bali ni mwanzo wa maisha yako mapya.
Kila la kheri!