Kipindi chote hicho mwenzangu hakuwa tayari kwa ndoa na mimi sababu kubwa ikiwa haniamini juu ya mahusiano ya mapenzi niliyokuwa nayo zamani kabla ya kukutana naye. Hapo nyuma niliwahi kuwa na relationships na watu wengine, ila tangu nilipokuwa nae sijawahi kuwa na wengine.
Ila wakati wa mwanzo kabisa wa uhusiano wetu aliwahi kukuta message kwenye simu yangu kutoka kwa ex boyfriend japo haikuwa ya mapenzi. All my ex boyfriends hatukugombana na kuachana kwa shari so huwa tunaweza wasiliana kama casual friends.
Alinieleza kuwa hapendi na mimi nikaacha. Ila nadhani hakunisamehe kwa hilo toka moyoni. Tumekaa na akatafuta access kwenye email yangu na kusoma mails zangu akakuta email toka kwa ex boy friend ikinipa hongera ya kuwa na mtoto, alikasirika sana na sasa akaamua kuwa uhusiano wetu ufe kabisa.
Ila mimi sababu nampenda sana nikamuomba afikirie upya uamuzi wake, mwanzo alikataa kabisa. Baadae akakubali nimpe muda japo wakati huo aliweka masharti juu ya uhusiano wetu, kuwa mawasialiano naye yawe juu ya mtoto tu.
Niliamua kujifunga mkanda na kuvumilia kipindi hiki, ni kama miezi miwili sasa tangu kianze, mwanzo nilikuwa nalia sana ila sasa nimeizoea hali, na pia hata yeye sasa anaonekana anapenda tuanze kuwa karibu, imeshatokea hata mara kadhaa tumefanya mapenzi.
Niliamua kubadili emails na hata kubadili namba ya simu ili kupunguza namna ya watu kuweza kunipata au kuwasiliana na mimi. Tatizo langu ni kwamba, sielewi kichwani kwake kweli anamapenzi gani na mimi na ana mpango gani na mimi.
Je ananiadhibu ili nijifunze somo au ananikomoa au anataka nikate tamaa sielewi. Amenifanya uwezo wangu kikazi na hata mahusiano yangu na marafiki na ndugu na hata watu wengine kuwa magumu na bado anasema anahitaji muda kuendelea kufikiri, je niendelee kusubiri au? maana kumpenda nampenda sana, kuishi bila yeye itawezanigharimu hata kuhama nchi. Naomba ushauri"
Jawabu:Pole kwa kuwekwa njia panda na baba wa mtoto wako.Kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi, pamoja na mambo mengine muhimu kuna nguzo kuu tano za kufanya uhusiano huo kuwa bora. Nguzo muhimu ambayo wengi huisahau au kutoilia maanani ni "mawasiliano".
Mawasiliano ninayozungumzia sio yale ya kuulizana hali zenu,mtoto au jinsi gani mnapendana kama sio matatizo uliyokumbana nayo kazini bali ni kuelezana na kupeana habari kuhusiana na mambo muhimu kwenye uhusiano wenu, kuweka wazi nini kinakukera, kuhoji uhusiano wenu unapokwenda, msimamo wenu na uhakika na hisia zenu, kuweka sawa mipango ya maisha yenu ya baadae (je ipo au haipo) n.k.
Asilimia kubwa ya wanadamu tunapokutana, kupendana na kukubaliana kuanzisha uhusiano huwa tunakuwa na mzigo wa maisha yetu ya awali ya kimapenzi kabla hatujakutana na wapenzi wa sasa. Hii inapaswa kutambulika na niwajibu wenu ninyi kama wapenzi kutambua kuwa ile "Past" ni sehemu ya historia ya maisha yako na haiwezi kufutika kamwe!
Hivyo wote mnapaswa kujua namna ya kukabiliana na "maisha ya awali" mnapokuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi. Sio wapenzi wote wanaoachana kwa vita na chuki, kuna wengine wanaamua kuachana tu kwa vile mmoja anataka ndoa mwingine hayuko tayari kuolewa au kuoa, wapo wanaoachana kwa vile hawaridhishana kingono, wengine wanaachana kwa vile wamegundua penzi halipo n.k.
Hizo sababu nilizozitaja haziwezi kuwafanya watu hawa walio-share sehemu ya maisha yao pamoja kuachana 4 good, wengi wetu huwa tunapaenda kubaki marafiki mpaka mmoja wetu anapokuwa na mpenzi hapo ndio huwa tunapunguza ukaribu na tunabakiza salamu tu zile za kujuliana hali kama unauhakika mpenzi wako mpya atakubali hilo liwepo n.k.
Ni kweli wewe (muomba Ushauri) unampenda mzazi mwenzako na ndio maana umekua radhi kufanya yote ambayo alitaka ufanye ikiwa ni pamoja na kupoteza marafiki zako, kubadili nambari ya simu na anuani yako ya barua pepe, lakini huyo mpenzi wako bado halioni hilo kutokana na ubinafsi alionao.
Kuna matatizo machache ninayaona kwenye uhusiano wenu (kutokana na maelezo yako)kama nilivyodokeza hapo juu ni kuwa hakukuwa na hakuna mawasiliano, mpenzi wako hajiamini hali inayopelekea yeye kuwa "control freak" na mwisho kabisa ni kuwa hana uhakika na hisia zake juu yako.
Kitendo cha yeye kuonyesha anataka kurudiana na wewe mimi nadhani ni kwavile unampa ngono, isijekuwa anakuja hapo kwa ajili ya mwili wako lakini hana mpango na wewe kama mpenzi wake wa kudumu.
Kuona ujumbe wa kukupa Hongera ya kujifungua kutoka kwa Ex sio kosa kubwa la kumfanya ahitaji muda wa kufikiri, anafikiri nini kisichofikirika kwa muda wa miezi zaidi ya miwili? Ingekuwa amekukuta na mwanaume mwingine ningeelewa kuwa nahitaji muda hata wa miezi sita kufikiri na kujitahidi kukusamehe na kusahau lakini barua pepe tu!.....anawalakini huyo.
Nini cha kufanya-Sitisha uhusiano wa kingono na yeye tangu anahitaji muda kufikiri basi aendelee kufikiri na akimaliza nakuamua kurudiana na wewe moja kwa moja ndio Ngono itapatikana. Muambie kuwa huwezi kufanya ngono nje ya uhusiano kwa vile unahofia afya yako na ya mtoto kwani hakuna sababu ya kupewa mapenzi ya mwili wakati yeye hakupi mapenzi wala amani moyoni, vilevile hujui anafanya nini huko anakotumia muda wake kufikiri. Hilo mosi.
Pili, Rudisha uhusiano kwa marafiki na ndugu zako na tumia muda wako mwingi na watu hao hali itakayokusiaidia kuondokana na mawazo juu ya mwanaume asiye muelevu na wala hajui kuthamini hisia za mtu anaempenda kwa dhati ambae ni wewe mama wa mtoto wake.
Kitendo cha kuwa karibu na watu hao (ndugu na marafiki zako) kama ilivyokuwa zamani itasaidia kuboresha utendaji wako wa kazi nakuongeza furaha kwenye maisha yako, kumbuka kuwa unajukumu lingine ambalo ni mtoto. Hakikisha huruhusu matatizo yako ya kimapenzi kuathiri utendaji wako wa kazi ili usije fukuzwa kazi.
Jitahidi kutumia muda wako mwingi na watu hao pale unapopata nafasi, ikiwezekana badilisha kabisa mtindo wa maisha yako na mtindo wa kimavazi na jinsi unavyokuwa ukijiweka wakati uko na huyo "mzee wa kufikiri". Kumbuka wewe bado Kijana, Mzuri, unapendeza na kuvutiaa sasa muonyeshe kuwa unamtaka kwa vile unampenda lakini humuhitaji (Unaweza kuishi bila yeye) ikiwa hana mpango na wewe......hapo humuambii unamuonyesha kwa vitendo, kutokana na utakavyokuwa ukijiweka, sawa?
Tatu, Ji-keep busy na mambo yako na mtoto, lakini siku akitaka kuja kumuona mtoto usimkatalie lakini hakikisha kuna kuwa na "limit" ya yeye kuwepo hapo kwako na vilevile anapokuwa na mtoto wewe endelea na shughuli zako nyingine, yaani usimpe muda wa kuongea na wewe au kulianzisha zali la kutaka ngono.
Ukiendelea kumsubiri utakuwa unajipotezea muda, unajinyima amani na uhuru wa kuwa karibu na ndugu, jamaa na marafiki na vilevile kukataa wanaume wengine wanaokutokea na wanakupenda kwa kudhani kuwa baba mtoto wako anafikiria na siku moja atarudi. Siku hazitokusubiri wewe, zinasonga mbele kama ifuatavyo.......
Nne,(ukifikia hatua hii kama anakupenda kweli na anampango nawe, ataomba mzungumze), akiomba mazungumzo na wewe usikubali haraka haraka, mpe muda......mwambie leo unashughuli nyingi hivyo muonane keshokutwa na siku ya siku ikifika usisahau kujiweka ktk hali ya kupendeza na kuvutia kwa maana ya "sexy".
......na kabla hajaanza muwahi na muambie jinsi gani umejitahidi kufanya yale yote ambayo alitaka uyafanye, ulijiweka mbali na marafiki, ndugu na jamaa kwa ajili yake, umebadili nambari ya simu na anuani ya barua pepe ili Ex wako asiwasiliane na wewe kwa vile hukutaka kumuumiza hisia zake.
Kisha muambie msimamo wako na unachokitaka kutoka kwake, iwe ni commitment au unataka kujua uhusiano wenu na mtoto unakwenda wapi na mengine unayodhani ni muhimu na unayataka kutoka kwenye uhusiano wenu huo......alafu mpe nafasi aseme alichotaka kusema!
***Lakini baada ya kufanya yote hayo bado hajaonyesha dalili ya kutaka mazungumzo ili kurudisha "majeshi", basi ujue alikuwa anakutumia kwa ngono kila anapokuja kumuona mtoto wake. Achana nae na keep sexy, keep happy, work hard na siku moja utakutana na mwanaume anaejiamini, atakae kupenda kwa dhati na kukuthamini.
Wewe bado mdada mdogo na kumbuka penzi halilazimishwi.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment