Wednesday

Nampenda mume wangu lakini hani-apreciate!-Ushauri






"Dada dinah mimi sijui hata nifanye nini kwani kila siku najikuta sina raha na mume wangu ndani ya nyumba. Nimeolewa miaka mitatu sasa na nimevumilia wee sasa nimechoka kabisa na tabia yake ambayo mimi sijaizoea. Siokwamba hatuzungumzi mambo ambayo hayatufurahisi, tunaongea sana tu lakini inaonyesha kuwa hawezi kujirekebisha.




Tatizo lenyewe ni hili, mume wangu hajawahi kusema asante nikimfanyia jambo au kitu. Yaani hata baada ya kula asante huwa hamitoki anaishia kusema nimeshiba au chakula kilikuwa kitamu, ile shukurani haipo, hata kama amekinunua yeye si bado jamani anatakiwa kunishukuru mimi kwa kumpikia kama ninavyomshukuru mimi akinipa pesa za matumizi au akija na chakula nyumbani huwa namwambia asante kwa kununua kitu fulani.



Kitu kingine ambacho sina uhakika naomba wewe unisaidie kutokana na uzoefu wako ni hivi, eti kumfulia na kumpigia basi mume wangu ni wajibu wangu wa ndoa? na je nikimfanyia hivyo anatakiwa kunishukuru au inakuwaje hapo.



Alafu tukifanya mapenzi na kumaliza nani anatakiwa kumshukuru mwenzie? na je unamshukuruje mpenzi wako baada ya kufika kileleni?



Dada dinah wengine tuliolewa bila kuwa na bahati kama uliyokuwa nayo wewe, tuliolewa tukijua kusema asante na samahani mengine tunajifunzia humo humo na wakati mwingine unaishia kukasirika tu kwa vile unahisi mpenzi wako hakujali wewe wala yale madogo umfanyiayo.



Nifanye nini ili na mimi nijisikie spesho ndani ya ndoa yangu?"


Jawabu: Kweli umevumilia sana kwa miaka yote mitatu kuishi na mtu ambae unahisi haku-apreciate, kwa kweli inaumiza sana kwa mtu ambae anaelewa umuhimu na thamani ya kuonyeshwa kuwa uko-valued kwenye uhusiano wako na kuwa-appreciated hata kwa kile kidogo unachokifanya.


Nafurahi sana kuwa umelileta hili mahali hapa ili wale ambao labda walikuwa hawajui ni jinsi gani baadhi yetu huwa tunajisikia ikiwa wenza wetu hawaonyeshi shukurani kwa uwepo wetu achilia mbali vile vidogo tufanyavyo.


Mimi binafsi kama Dinah sipendezwi na tabia ya baadhi ya watu na kukufanya wewe ujisikie "unppreciated" ni kama vile unajipendekeza au mpenzi hana habari na wewe (huenda anakujali and all that lakini haisaidii ikiwa sioni, hunionyeshi kuwa unashukuru, unani-value n.k), Kitu kidogo kama kumuambia mpenzi wako "nakupenda" bila kupata ile "nakupenda pia" inaweza kukufanya ujione "msaidizi" badala ya mpenzi wake.


Unatambua, kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) wanapokuwa na wewe kama mpenzi/mke wanahisi kukumiliki hivyo chochote unachokifanya kwa ajili yao ni haki yao na "actualy" unapaswa kufanya hivyo kwani wamekuoa au umewaoa kitu ambacho sio kweli na kama ni Imani basi ni potofu kuliko maana halisi ya neno lenyewe.

Kuna wanandoa waliwahi kuja kwangu wakitaka ushuri, nilipozungumza nao niligundua kuwa hawafanyi vile vitu vidogo ambavyo wengi tunavidharau bila kujua umuhimu wake kwenye maisha yetu kama wapenzi, Mume alikuwa anadai kuwa anahisi kuwa hamridhishi mkewe kitandani kwavile mkewe huyo hajwahi kuonyesha shukurani kila wanapofanya mapenzi........sasa unaweza kugundua umuhimu wa shukurani kwa baadhi ya watu.

Mtu kama wewe (muuliza swali) asante kwako ni muhimu na inakufanya ukose amani ndani ya ndoa yako(this is serious), si ajabu unajihisi mpweke wakati mwingine kwa vile unahisi kuwa mumeo haku-appreciate.

Wengi tunatofautiana kimalezi kwani tumlelewa ktk mazingira tofauti, baadhi yetu tulifundishwa umuhimu wa kuomba msamaha, kuomba ikiwa unahitaji kitu na kushukuru unapopewa au fanyiwa jambo lakini wapo ambao vitu kama hivyo havikuwepo kabisa (msome m3 kwenye Comment).

1)-Kweli kabisa mumeo anapaswa kushukuru kwa kumpikia na kumuandalia chakula hata kama yeye kakinunua, unapompikia mume wako mara nyingi unapika kwa mapenzi yako yote, utamu wa chakula au uchaguzi wa nini kiliwe siku hiyo unatoka moyoni mwako na unafanya hivyo ili mume wako akirudi nyumbani afurahie chakula hicho. Sasa asiposema kuwa kakipenda na kushukuru kwa kweli inakatisha tamaa na inauma mno.

Kule kwetu tunaambiwa/fundwa kuwa hakikisha mumeo hali chakula cha mwanamke mwingine(hata kama ni mama yake), ikiwa anapenda kula kwa mama'ke au kwa rafiki yake (mkewe kapika) au Hotelini basi hakikisha unajifunza mapishi hayo......got the point eeh?

2)-Kitu chochote unachokifanya ndani ya ndoa yako kwa ajili ya mpenzi wako sio wajibu wako wa ndoa ni mapenzi yako juu yake, kumjali na kuhakikisha kuwa anakuwa msafi na anapendeza wakati wote bila kusahau kumsaidia labda kutokana na shughuli zake nyingi za kikazi. Lakini kama wote mnafanya kazi basi mnapaswa kufua pamoja au mmoja wenu kufanya hivyo akipata nafasi......ndoa ni ushirika hivyo mnatakiw akushirikiana na kusaidiana ktk kila jambo ndani ya nyumba yenu.

Bila shaka ikiwa atakuta nguo zake zimefuliwa na akunyooshwa basi anapaswa kuonyesha kuwa ameona hili na anashukuru kwa kufanya hivyo....."mke wangu asante kwa udobi" sio sentensi ngumu na wala hulipii kodi japokuwa kwa mwanamke inathamani kubwa sana.

3)-Ku-appreciate baada ya kufanya mapenzi au hata wakati mchezo unaendelea inategemea na wahusika wenyewe, unaweza ukawa unasema jina lake na kumwambia kiasi gani unapenda anachokifanya na mengine yatakayokujia wakati huo unaposikia raha/utamu.

Vilevile unaweza ukamkumbatia kwa nguvu na kwa mapenzi yako yote na kumbusu kabla "hajang'atuka" mwilini mwako, pia unaweza ukasema asante na kumuambia jinsi ulivyofurahia "the moment" na kama amekufanya ktk mtindo tofauti au leo umehisi kichw akikubwa zaidi kuliko jana mwambie......na yeye akafanya hivyo kwako.

Ufanye nini basi ili aanze ku-appriciate-Ondoa hasira na anza kuwa unamshukuru kila anapokufanyia kitu hata kama ni kukukata ukucha, mwambie asante na mpe kibusu shavuni au mshike kuonyesha shukurani yako. Hilo mosi.

Pili, Mwambie ukweli tu jinsi unavyojisikia, mwambie kwa upole na kwa upendo kuwa unahisi "unappreciated" na inakunyima amani kabisa moyoni mwako.

Mueleze kuwa unapompikia chakula huwa unakipika kwa mapenzi yako yote, na huwa unasikia raha ikiwa anaonyesha kukipenda lakini unahisi "special" zaidi ikiwa atasema asante kwa chakula kitamu n.k

Ni mumeo na hakika anakupenda, ikiwa alikuwa hajui kuwa "shukurani" ni muhimu sana kwako basi atataka kujua zaidi vitu gani akifanya unahisi kuwa na wewe ni "special wife" kwake na ataanzia hapo, taratibu lakini surely na atazoea na maisha yako ya ndoa yatakuwa mazuri na kwa vile utakuwa na unahisi spesho kama ulivyosema na vilevile hutokuwa na hasira tena.

Mungu ailinde ndoa yenu, kila la kheri!

Nakuja......

No comments:

Pages