Friday

Mume Cheated, sasa anadai tupeane nafasi-Ushauri

"Hi, wadau mwenzenu nina shida, mnajua toka mume wangu acheat wakati nina mimba, sijamsamehe. Tunaongea vizuri na tunalea familia vizuri, ila tatizo nikikumbuka maudhi ya mume wangu basi naacha huduma zote na chumba nahama.

Nakaa hata wiki then tunaongea narudi, najaribu kumsamehe na kusahau nashindwa, nakuwa jeuri sana siwajibiki chochote kuhusu mume. Na hii jeuri inakuwepo muda mwingi zaidi kuliko amani.

Sasa eti kaja na solution, eti we need space from each other so mimi nirudi kwetu kwa atleast 3 weeks or 1 month.. Nikamwambia "mie siendi popote coz siwezi kuacha watoto wangu na I dont need any space. Kama he needs hata yeye ana kwao aende tu. Mi mi kama nitaondoka ni 4 good na naondoka na TALAKA yangu mkononi". Akasema hatuachani ila tunarekebishana. Hapo wadau nisaidieni kuna cha kurekebishana au ana yake?"

Dinah anasema:Pole sana Mdada kwa unayokabiliana nayo, watu hawaelewi ni namna gani kuwa cheated on inauma na ni ngumu kiasi gani kusahau. Unaweza kusamehe vema kabisa , well ukadhani umesamehe (huwezi kusamehe kama huwezi kusahau) na ukawa unazungumza na mumeo lakini uhusiano wenu ninyi wawili hautakuwa the same again unless huyo aliyekosa (kwa case yako Mumeo) afanye kazi ya ziada ili wewe uweze kumuamini tena na hatimae kusahau aliyokutenda......hebu bofya hapa kwa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kiasi fulani.

Sio kwamba unakiburi bali unahasira kutokana na kitendo chake kichafu na hujafanikiwa kusamehe kama ulivyodai mwenyewe kitu ambacho kinaongeza ugumu zaidi kwenye kusahau na kuganga ya mbele. Ingekuwa yeye ndio katendwa yaani kama wewe ndio ungekuwa ume-cheat on him sidhani kama angekuwa na wewe by this time.....angekutwanga TALAKA siku hiyo hiyo.

Nimekutana na watu wachache wenye tatizo kama lako na niliwasaidia na wakafanikiwa na sasa wako pamoja wakiendelea na ndoa zao, na huko ndiko nilikopatia uzoefu na hivyo kujiamini ktk kulielezea hili suala la cheating.

Kwa mtu ambae hajawahi kukutwa na tatizo hili ningumu sana kwake kujua ugumu na maumivu yake na hivyo kudhani kuwa wewe unakiburi tu na unachezea shilingi chooni, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa, unampenda mumeo, unataka sana kuendelea kuwa kwenye ndoa lakini hujui how to 4get and move on, kwasababu 1)-huji kwanini alifanya hivyo(cheat), 2)-Je umenusurika dhini ya maambukizo? 3)- Kwanini yeye hana habari na anachukulia kawaida (kwa vile hajaomba msamaha) na maswali mengine lundo.

Wewe kuwa mjamzito ni moja ya sababu kati ya zile nyingi ambazo wanaume huzitumia kama sababu kwa nini hutereza nje a.k.a cheat,.

Tatizo lililopo hivi sasa si yeye ku-cheat japokuwa ndio sababu, ninachokiona hapo ni mume wako kuwa na Majivuno (proud of himself) kwa vile tu yeye ni mwanaume na wewe kuwa needy na muoga kudai haki yako. Kingine ni ukosefu wa maswalisiliano baina yenu.

Mwanaume yeyote ambae hana majivuno na anathamini ndoa yake hawezi kukaa ziku zote hizo bila kuomba msamaha kuhusiana na tabia yake chafu, unless huna uhakika na unahisi tu kitu ambacho kitakufanya ushindwe kuwakilisha hoja.

Kama mgewasiliana kuhusu tukio lililotokea wakati wewe mjamzito na unauhakika kweli alikusaliti ni wazi kuwa angeomba msamaha na kuahidi kuacha hiyo tabia na kubadilika kuwa a loving hubby kwako na a great father kwa watoto wenu.

Cheating sio kitu kizuri na ni sawasawa kabisa na yule muuaji(inategemea na reaction ya mhusika), lakini haina maana kuwa ndio mwisho wa ndoa yenu au mwisho wa uhusiano wenu. Inawezekana kabisa kutokana na tukio hilo mkawa the best couple (am not asking u to cheat on ur lover ili kuwa best...hapana), ila kwa bahati mbaya ikitokea na uko kwenye ndoa kuna hatua za kufuata na kuna njia ya kukabiliana na hilo.

Nini cha kufanya:Kwanza kabisa unatakiwa kujua umesimama wapi na unataka nini out of ndoa yako?
1)- Je unampenda mumeo na ungependa ku-work things aout na mumeo ili ndoa iendelee kuwepo na iwe yenye amani na upendo?(Kuna mengi ya kufanyia kazi ili kufanikisha hilo)

2)-Je Penzi limepauka/chujuka ila unamheshimukwa vile ni baba wa watoto wenu na unahofia watoto wenu wasilelewe na mzazi mmoja ikiwa utatoka ndoani?(Mkiweka mipangilio mizuri watoto watalelewa na ninyi wote, lakini kujilazimisha kukaa kwenye ndoa wakati huna furaha sio afya kwako)

3)-Unahitaji muda zaidi kuponyeka kabla hujafanya uamuzi wa busara? (hapa utahitaji kutengana nae kwa muda ili ku-sort our ur feelings and ur head).

Sasa kutokana na kitendo chake cha kukusaliti unadhani kuwa ukiondoka na kwenda nyumbani yeye atahamishia makazi kwa huyo mwanamke mwingine si ndio? Vipi ikiwa yeye ataondoka nakukuacha hapo nyumbani? Unauhakikahuko aendako ni nyumbani kweli na je itakuwaje kama atabeba na huyo msaliti mwenzie kwenda huko wote? Mana'ke kuna nyumba za wageni na wanaweza kutumia.........

Sulihusho hapa ni kupeana nafasi (kama alivyodai mwenyewe) ili kuona kama kweli bado mnapendana na mnataka ndoa yenu iendelee kuwepo lakini kutokana na hali halisi ya uhusiano wenu itakuwa ngumu kwa vile wewe humuamini tena mumeo.

Mimi nashauri wote wawili msafiri na kwenda mahali ambako hakuna ndugu wala jamaa, mkakae hotelini na huko muende kujaribu kurekebisha mambo baina yenu, kitendo cha kukaa ninyi wawili pakeenu na kuwatumia muda wote pamoja kufanya mambo tofauti ya kufurahi (msihusihe ngono) itasaidia kujua hisia zenu na namna gani mnahitajiana ktk maisha yenu.

Pia itasaidia ninyi wawili kutaka kuzungumza kuhusu maisha yenu, kumbuka siku zote naamini kuwa mwanamke ndio mtu pekee anaweza kubomboa au kujenga ndoa yake......hivyo basi jukumu hili liko mikononi mwako kwahiyo ni wewe pekee ndio uko upande wa kulianzisha na kulizungumzia tatizo lililopo kwenye ndoa yenu hivi sasa.

Lakini je utamuanzaje ili akubali?-Ili kumpata kwanza kabisa muombe msamaha kwa kumtamkia Talaka na kubishia wazo lake la kutengana kwa muda. Mwambie kwa uwazi na kwa upole kuwa hudhani kama ni idea nzuri kutengana na unadhani kuwa mnahitaji kutumia muda mwingi peke yanu bila ndugu, watoto na marafiki ili kusort things out.

Sema kuwa, ikiwa yeye au wewe utasafiri na kuwa mbali mbali itaongeza matatizo badala ya kuyamaliza. Mueleze kuwa mnahitaji muda wa kutosha ili kuzungumza na kurudisha the romance kwenye ndoa yenu kwani unahisi imetoweka ghafla na unadhani inawezekana kabisa ni kutokana na vitendo vyako ambavyo unavifanya kutokana na sababu ambayo utamueleza muda ukifika (hii itampa hamu ya kutaka kujua), na kama kweli alikusaliti atang'amua then na kama hakukusaliti basi atasubiri au anaweza ku-demand umwambie....

Wewe usimwambie mpaka mtakapo safiri nje ya mji au mkoa mwingine.....Kama mnaishi Tz basi Morogoro pale pametulia, Arusha pia kuzuri, Bagamoyo, Kigamboni kule kuna Hotel moja bomba kabisa kwa ajili ya kupumzikia mwisho wa wiki....lakini kuzuri kabisa nadhani ni kwenye Mbuga za wanyama kutokana na asilia ya nchi itawasaidia muwe na mood nzuri zaidi....


Weka wazi hisia zako zilizoumizwa ili mumeo aelewe kuwa bado linakuuma na huwezi kabisaa kusahau (ikiwa unauhakika na usaliti wake). Unajitahidi kusamehe lakini msamaha haukamiliki ikiwa yeye mumeo hajakubali kuwa alikosa na kukuomba msamaha.....kama mwanamke natambua unafanya vyote hivyo kwa kudhani kuwa yeye mumeo atang'amua unataka nini kutoka kwake.

Kwa bahati mbaya hawezi kusoma via vitendo vyako wala hawezi kujua yaliyokichwani mwako isipokuwa pale utakapoamua kuliweka wazi ktk mtindo wa kuwasiliana. Ukiendelea hivyo ataamua kwenda kutafuta amani sehemu nyingine na wewe utabaki unaumia even more.

Ikiwa hunauhakika na usaliti wake pia mueleze kuwa ulipokuwa mjamzito ulikuwa unahisi au kama uliambiwa bsi sema wazi kuwa kuna watu walikuambia kuwa mumeo anatoka na mtu fulani na tangu siku hiyo imani nae mumeo imekutoka na hunashindwa kumuamini tena.

Kama akikana kutokana na tuhuma hizo (ikiwa huna uhakika) then inabidi kuwekeana rules kama inawezekana ili kukuongezea au kukurudishia wewe ile hali ya uaminifu juu yake mume(kwamba uanze kumuamini tena).

Ndoa ni ngumu sana kama hakuna mawasiliano ya kutosha au hujui namna ya kuwasiliana na mwenza wako, ndoa ni ngumu kama hakuna uaminifu baina yenu, ndoa ni ngumu kama hakuna maelewano wala masikilizano, ndoa inaweza kuwa ndoano kama hakuna amani ndani ya nyumba yenu.

Ndoa ni our third job kwa wale wote wenye kazi, watoto na waume/wake pia ni our second job kwa wale wote ambao bado hamjazaa lakini mna wake/waume na kazi. Hivyo tukitaka ndoa zetu ziwe Imara, bora, nzuri, zenye furaha na amani hatuna budi kuwajibika na kuzifanyia kazi kila siku iendayo kwa Mungu kama vile unavyokwenda kazini kila siku ili kulipwa mshahara lakini tofauti ya ndoa ni kuwa haina mwisho wa wiki wala likizo ila malipo yake ni zaidi ya Mshahara ikiwa utawajibika vema.

Nakutakia kila la kheri ktk kurudisha ndoa yake kwenye track kama kweli unataka kuendelea kuwa ndani yake.

Ubarikiwe!

No comments:

Pages