"Hakika wewe ni mwanamke jasiri..
Mimi ni msichina wa umri wa miaka 28 nimekuwa ktk uhusiano wa kimapenzi huu mwaka wa tano sasa, lakini sielewi nini cha kufanya mpaka sasa. Mpenzi wangu ni mchanganyiko wa rangi kati ya mweusi na mwarabu kwa baba.
Tunapendana tena sana tu, wazazi wake wanamwambia kuwa muda wa kuoa umefika atafute msichana aoe lakini si msichana aliyekuwa nae, thats means mimi, Alipopata habari hizo aliniambia japo roho yangu iliniuma sana lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kumwachia yeye aamue..
Ndipo baada ya mwezi mmoja aliponiomba kuwa anataka kuwa na mtoto na mimi, nilifurahi kwani napenda niwe na mtoto naye pengine hata awe mume wangu, akadai kuwa tutakapokuwa na mtoto itakuwa rahisi yeye kuwa karibu na mimi siku zote na pengine kuwa wote kabisa na hata kama ataoa ni kwa kuwaridhisha wazazi wake tu kwani yeye chaguo lake hasa ni mimi. Nikamuambia naomba muda nifikirie kwanza ili kama kufanya maamuzi yawe sahihi
Dinah sasa hapo ndio sijui nini cha kufanya:
Nafikiri niachane naye tu lakini nampenda na roho inauma sana hata ukizingatia tumevumiliana kwa mengi na pia huwa sipendi kubadili mahusiano hadi hapo inapobidi. Nahofia pindi atakapo oa, je ni kweli ataweza kuwa karibu na mimi?
Hasa atakapokuwa na huyo mkewe? Au ndio nitaishia kupata tabu na mwanangu tu? Maana si unajua mtu akishakuwa na mke tena hasa hawa wenzetu waarabu bila shaka huyo mkewe atakuwa mwarabu pia. Naomba ushauri wako ambao utanitoa hapa kigazini nilipo."
Dinah anasema: Pole kwa unayokabiliana nayo. Haya hutokea sana kwenye jamii nyingi tu za Kiafrika na sio Waarabu peke yao. Kabla sijaendelea naomba nikuulize swali.....hao wazazi wake wanajua kuwa wewe ni mpenzi wake?
Unayokumbana husababisha wanaume wengi kuamua kuoa mara mbili, ndoa ya kwanza kulidhisha wazazi na ya pili ni kwa mapenzi yake na hufanya siri bila wazazi wao kujua. Hapo hutafuta visa kama vile kunyima tendo la ndoa, kutorudi nyumbani mapema, kutokua chakula kipikwacho nyumbani, kutoongea nao, kutotembea nao n.k.
Hali inayopelekea mke huyo aliyechaguliwa kuomba Talaka, na hili likitokea Bwana anakuwa huru kutangaza ndoa nyingine ambayo tayari alikuwa ameshafunga sambamba na ile ya mke wa "kutafutiwa" na wazazi.
Huyu bwana inaelekea hata yeye amechanganyikiwa kama wewe ulivyochanganyikiwa na kweli anakupenda ndio maana anatumia njia ya kuzaa na wewe ili usijekuwa na mtu mwingine na akakukosa. Lakini, pamoja na nia yake njema bado utakuwa umezaa nae nje ya ndoa pia utakuwa ni Kimada na sio Mke pamoja na kuwa wewe ndio ulikuwa wa kwanza kuwa nae ktk uhusiano wa imapenzi.
Wewe hukupaswa kumuachia mzigo wote yeye peke yake ili afanya uamuzi (kosa kubwa ulifanya hapa), Wote wawili mlipaswa kulijadili suala hilo zito na kufanya maamuzi ya busara hasa ukizingatia mmekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.
Kitendo ulichokifanya kimemrahisishia yeye kufanya uamuzi logically zaidi na si kihisia na ndio maana akaja na suala la kukumimba ili aendelee kuwakaribu na wewe bila kuangalia hiyo itakuathiri vipi wewe Kihisia, Kimwili na Kisaikolojia.
Natambua ulipomuachia jukumu hilo ulitegemea yeye kukuambia kuwa hajali wazazi wake wanataka nini, atakachofanya ni kufunga ndoa na wewe, hata ikiwezekana kuhama mahali hapo na kupotea kabisa lakini awe na wewe............mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na mwenye kujali hisia za mpenzi wake hakika angefanya hivyo na sio kuja na suala la kuzaa na wewe lakini kuoa anaoa mtu mwingine.
Nakubaliana na ufikiriavyo, kwamba ni heri muachane tu. Ikiwa hili ndio utakalo basi fanya haraka iwezekanavyo kabla hujapoteza muda zaidi. Natambua inauma sana......maumivu hayo ni ya kawaida kwa yeyote anaeachana na mpenzi wake ampendae, iwe kwa kugombana au kwa kuelewana bado maumivu ni yale yale lakini kutokana na tofauti zenu kubwa inabidi iwe hivyo.
Kuzaa nae ni sawa sawa na kuzuia baraka na bahati kutoka kwa wanaume wengine wazuri out there, sio wanaume wote watakuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine na si dhani kama huyo bwana ataendelea kuwa karibu nawe the way anaahidi sasa. Kama kweli anataka kuzaa na wewe basi mfunge ndoa as simple as that!
Ukimuacha kabla yeye hajafanya hivyo itakuwa vema kwani utamuonyesha kuwa wewe ni mwanamke mwenye msimamo, unajiamini na unajua unataka nini maishani mwako. Unataka kuendesha maisha yenye amani na furaha, unataka kuthaminiwa, kushehimiwa, kupendwa na siku moja kuolewa na kuwa mama, sio kuwa mama na wakati huo huo Kimada.
Miaka 28 bado unamuda mzuri tu wa kukutana mwanaume mwenye kujali hisia zako, atakaepigana kwa ajili yako bila kujali ni nani hasa anataka kujiingiza kwenye maisha yenu ya kimapenzi.
Mungu akujaalie ktk maisha yako na siku moja utafunga ndoa na mwanaume mwenye kufuata Moyo na kufanya uamuzi yeye kama mwanaume kamili na sio kuamuliwa na Wazazi wake.......
Kila la kheri!
No comments:
Post a Comment