"Nina msichana wangu nasoma naye chuo kimoja nje ya nchi na tumekuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka miwili sasa. Nampenda na yeye anaonyesha dalili zote za kunipenda mimi. Kila kitu nikimwambia huwa ananielewa haraka kitu ambacho ni muhimu sana kwangu.
Mwezi huu wa Tisa amepata likizo ya kurudi Tanzania, ndipo nikachukuwa nafasi hiyo kutaka uchumba wangu ujulikane kwa wazazi hivyo nikamuelekeza kwetu na akafika. Mimi nikawatambulisha wazazi wangu kwa njia ya simu kuwa huyo ndie chaguo langu yaani ndie atakuwa mke wangu baadaye.
Wazazi waliniunga mkono!! ila kuna kitu nashindwa kukielewa naomba ushauri wenu, tangu mpenzi amefika kuna line ya simu anaitumia ambayo ina tatizo la kutopiga huku nilipo hata kutuma message. Yaani akitaka kupiga au kutuma message hadi atumie namba ya mama yake au ya dada yake sasa sometime ikitokea watu hao wanakuwa na shughuli zao au hawapo ndio hatuwasiliani kabisa hadi mimi nimpigie.
Nilimwambia mchumba abadilishe hiyo line akaniambia atabadilisha, sasa ni Mwezi umepita line bado anayo ileile na sidhani kwamba hana hela. Je hapa kulikoni? naomba ushauri wenu wadau."
Dinah anasema: Hongera sana kwa kuchumbia! Asante kwa mail na uvumilivu wako pia. Tatizo lako ni kutojiamini hali inayopelekea wewe kushindwa kumuamini mwenzio. Natambua ugumu wa kuwa na mpenzi mbali na wewe, lakini ukiwa na ukosefu wa kujiamini inakuwa even harder!
Ni kweli mawasiliano kwa baadhi Network Bongo huwa magumu kwani ni lazima vyombo hivyo vya mawasiliano kuwa na "ubia" na vyombo vya mawasiliano vya nchi husika ambayo wewe unaishi ili kufanikisha mawasiliano(nilipata usumbufu huo nilipokuwa nawasiliana na mtu aliyekuwa akitumia Zantel). Hivyo hili lisikupe hofu sana au hata kumfikiria mwenzio mabaya.
Huenda suala la yeye kubadilisha mtandao/line ni rahisi sana kulifikiria, lakini tambua kuwa huyu Binti kaenda nyumbani kuonda ndugu zake baada ya muda mrefu kuwa mbali nao, wewe ulikuwa nae kila siku na baada ya muda huo mfupi utaendelea kuwa nae.
Kibongo-bongo, unapokwenda nyumbani kila mtu anapenda ku-spend muda na wewe kwa vile hawajakuona kwa muda mrefu hivyo inatokea kuwa unakuwa busy sana na shughuli za kifamilia na suala la kubadili nambari ya simu ili kukuondoa hofu wewe mpenzi linakuwa la mwisho kwani anajua moyoni anakupenda na anawasiliana na wewe kupitia Mama na ndugu zake wengine, ktk hali halisi hii ingekufanya uwe na Amani myoni kuwa yupo na watu unaweza kuwaamini, imagine angekuwa anawasiliana na wewe Via rafiki au kibanda cha Simu?
Ni matumaini yangu ulifanyia kazi vema maelezo ya wasomaji wangu. Naamini Mpenzi sasa amerudi na kila kitu kiko sawa, nawatakia maisha mema yenye amani na furaha na Mungu awajaalie mfunge ndoa na kuishi maishamarefu ya ndoa.
Pamoja na mambo mengine mengi Uamininifu ni nguzo muhimu ili kuwa na uhusiano bora wenye kuzaa ndoa thabiti.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment