Tuesday

SMS kwa jina la kike mhusika Dume-Ushauri!

"DEAR,
MImi ni kijana mwenye umri wa miaka 24, nina mpenzi ambaye hadi sasa nimekuwa nae kwa mda wa mwaka mmoja. Mpenzi wangu huyu ni msiri sana linapokuja suala la matumizi ya simu. Kwenye simu yake inaonyesha anamtu mwingine ambae anaishi Mtwara na huwa wanawasiliiana mara kwa mara, lakini kila nikimuuliza ni nani huyo? yeye anasema kuwa ni rafiki yake na ni mwanamke.

Lakini katika uchunguzi nilioufanya nimegundu mtu huyu ambaye ni rafiki yake ni Mwanaume kwani amekuwa wanawasiliana kwa sms, akitumiwa tu sms husoma na kuzifuta haraka sana. Sasa tarehe 16/9/2009, Tulitoka na kwenda Biashara Club kwa ajili ya msosi, Mpenzi akatoka kidogo na kwa bahati mbaya akawa ameissahau simu yake mezani.


Mara sms ikaingia, kwa sababu nilikuwa na wasiwasi na mawasiliano yake ya mara kwa mara nikaamua kuisoma ile sms ikisema wakutane mda wa saa mbili usiku, wakati ujumbe umeingia ilikuwa ni saa mmoja usiku.


Namba ya huyo mtuma ujumbe imetunzwa kwenye simu kwa jina la MASA, kutokana na sms niliyo soma na kupata uhakika zaidi ambao nilikuwa nautafuta niliamua kumwambia mpenzi kuwa na hitajika nyumbani kwani kuna tatizo, sikuweza kuendelea kuwepo pale, sasa ili nijue ukweli wake nifanye nini?
Naomba ushauri wako dada.
it's me Hassan"

Dinah anasema: Hassan, pole kwa mkasa huo. Hiyo ni tabia ya watu wengi ambao sio waaminifu, wanakuwa na wapenzi nje ya mahusiano yao na kutunza mawasiliano ya simu kwa majina ya ambayo sio halisi. Mf- Kamani mwanamke watatunza kwa jina la kiume na kama ni wa Kiume basi jina litakuwa la kike.

Jambo muhimu ni kwenda kufanya vipimo ili kujua kama uko huru kutoka HIV! Kwani hali ni mbaya sana na inatisha.

Katika hali halisi unapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huitaji kuwa na siri, kila kitu unachodhani ni muhimu mwenzako kujua basi utaweka wazi jambo husika, hata kama mtu huyo anampenzi mwingine kwa sababu nyingine labda za kimapenzi au kiuchumi (wapo watu wanakuwa na wapenzi 2, mmoja wa kimapenzi na mwingine kwa ajili ya pesa) pia unatakiwa kuweka wazi hilo ili huyo anaetaka uhusiano na wewe aweze kufanya uamuzi wa busara.

Nasikitika kusema kuwa mpenzi wako sio mwaminifu na kuna uwezekano mkubwa anakuchanganya wewe na mwanaume mwingine. Ni vema kama utamueleza mpenzi wako ukweli wa nini kilichokufanya uondoke usiku ule mlipokuwa nje kwa ajili ya chakula, muulize kuhusu huyo Jamaa anaewasiliana nae na kama wanangonoana n.k.

Kisha msikilize anasemaje na umwambie uwazi kuhusu msimamo wako Mf- hutaki kum-share yeye na mwanume mwingine, hupendezwi na tabia yake ya usiri. Sasa kama hakuna kinachoendelea na huyo jamaa wa SMS (mana'ke inawezekana njemba inamtaka tu lakini hajafanya nayo ngono)....mwambie Demu abadilishe tabia yake ili uweze kumuamini.

Kama walikwisha ngonoka, ni wazi kuwa mdada huyo hakufai hivyo basi achana nae na subiri kupata binti mwingine atakaejiheshimu nakuheshimu uhusiano wenu na kukuthamini wewe kama mwanadamu.

Kila la kheri!

No comments:

Pages