Saturday

Mume ataja jina la binti yetu wakati wa Tendo!-Ni kawaida?

"Dada dinah habari ya mwaka mpya natumaini mwaka umeuanza vizuri. Mimi ndio mara yangu ya kwanza kutuma swali langu lakini ni mpenzi wa blog yako.


Mimi nimeolewa na ndoa yetu imejaaliwa mtoto moja wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, mimi na mme wangu tumekuwa pamoja kwa miaka mitano sasa. Jana (1/01/10 ndio ilikwa mwaka mpya hatukutoka tulikuwa tu home kwavile nchi tuliyopo ni baridi sana na snow kwa kwingi sana.


Hivyo tuliamua kukaa home na fungua mwaka mpya home, ilipofika saa sita kufunga mwaka na kufungua mwaka tulifungua champagne na kunywa kwa furaha tukakaa mpaka saa saba usiku ndio tukaanza kufanya mapenzi, yaani mwanzo ilikuwa poa sana mara katikati ya mapenzi ndio mme wangu akataja jina la mwanangu badala ya jina langu katikati ya mapenzi.


Tulivyo maliza mavitunzi ndio nikamuliza kuhusu kuita jina la mwanangu katikati ya mavituzi, akasema amezoea kuita hilo jina all the time ndio maana amejisahu na kuita hilo jina. Dada dinah naomba uniambie kama hii ni kawaina na kama imewahi kutokea kwa watu wengine hapa.
Naombeni michango yenu.
Ni mimi Samatha"

Dinah anasema: Samatha asante kwa email yako, lakini naomba kuuliza kidogo kabla sijakupa maelezo na pengine itasaidia watu wengine kukupa michango ya uhakika zaidi. Je hilo jina la mtoto ni nani alichagua? Mumeo na wewe ukakubali au wewe na yeye akalikubali? Je jina la mtoto na lako linafanana kwa mbali Mfano Dinah na Daniela, Maria na Marian/Mariam n.k....inawezekana ni jina la Ex n.k.

Huenda alitaka kukuita mama____(jina la mtoto) na akaishia jina la mtoto akasahau "mama".

Asante Samatha kwa nyongeza ya maelezo (nenda kwenye comments), naungana na mchangiaji aliyehoji Uraia/Makuzi ya mumeo, hakika sio ubaguzi lakini sio watu wa mataifa mengine tu wanawarudi watoto wao. Hapa Tanzania wapo wengi tu lakini kutokana na kulinda "heshima ya familia" watu hukaa kimya nakutunza siri.


Natambua inaumiza kumfikiria mumeo jinsi ambavyo watu wengine wanamdhania, lakini mimi nakuomba ufanye ushunguzi bila kumuuliza binti wala baba yake. Kuwa karibu zaidi na binti yako ili kuondoa wasi wasi. Samahani kama maelezo hayo yatakuwa yamekukwaza. Inawezekana hajawahi kumuingizia wala hana mpango huo ila huwa anamchezea-chezea.


Ujue watoto wa kike huwa tunakuwa karibu sana na baba zetu, lakini kutokana na mazingira yetu hapa Bongo inakuwa ngumu sana kuwa that karibu na baba, yaani baba hapewi nafasi ya kubadili nepi ya mtoto wa kike achilia mbali kumuogesha.

Lakini kwa watoto wa nje ya Tanzania huwa karibu zaidi kutokana na mazingira baba hulazimika ku-baby sit wakati mama anaenda kazini n.k. hivyoinawezekana kabisa mtu akaibua a sick tabia ya kumchezea mwanae wa kike ktk harakati za kutafuta namna ya kumbembeleza n.k.

Kuna babaz wanawazoesha kuwachezea watoto wao wa kike na kuwapandikiza imani kuwa "baba anakupenda ndio maana anafanya hivi". Wengine wanaimani za kishirikina, ili kufanikiw abasi mudi mwanao, baadhi hulazimika kuwarudi watoto wao kama sehemu ya Mila....wenyewe wanaita Suna!

***************************MUNGU APISHE MBALI!

Tendo la ndoa ni tamu, ni takatifu linawafanya wote wawili kuwakaribu zaidi in a way mtu mwingine yeyote hawezi kujua achilia mbali kuhusika. The moment na utamu wake, mihemo na sauti za mahaba, harufu za majimaji ya miili yenu na namna mnashikana n.k hakika HUWEZI kabisa kulopoka jina la mwanao au la mtu mwingine yeyote unless otherwise umewahi ku-share the momet like that with au u r willing to do so!


Haijalishi unapata utamu kiasi gani au wewe mwanamke ni mlopokaji kiasi gani, huwezi kabisa-kabisa kumtaja baba yako au mtoto wako wa kiume. Katika hali halisi wanaume ni wagumu sana kulopoka-lopoka wakati wa tendo na wanapofanya hivyo ni wazi kuna uhusiano mkubwa kati ya jina na tendo (amewahi/anafanya ngono na mtu mwenye jina hilo).


Kama jamaa ni mbongo na anakuita mama nanihii time 2 time ni wazi alikusudia kukuita hivyo il akasahau neno "mama", pia inawezekana kabisa kuna mtu alimkaa sana kichwani (alimpenda kupita kiasi) na utamu alioupata siku hiyo ulimkumbusha huyo mtu mwenye jina linalofanana na mtoto wenu.

Kutokana na uzoefu wangu, wanaume wanatabia ya kuita binti zao majina the last Ex b4 mke aliemuoa hasa kama walipendana sana enzi zao ila mmoja hakuwa tayari kuendelea mbele. Kuna Njemba moja iliwahi kuniambia "Dinah hata kama tukiachana, nikioa nakubalikiwa kuzaa mtoto wa kike lazima nimuite Dinah"......which kafanya hivyo!


Pia inawezekana ni character kwenye Porn movies ambayo mumeo anaipenda namlipokuwa mkifanya akili yake ilikuwa ikimfikiria huyo mtu wa kwenye Kideo, lakini ktk kujitetea ikabidi aseme kuwa alimtaja mtoto kwa vile anamuita na kumtaja kila wakati ili kulinda hisia zako.

Sasa Samatha, kama ni jina la Ex au Porn star basi let it go kwa sasa, akirudia tena kutaja jina hilo ni wazi mtahitaji kuzungumza kuhusu hilo Jina kwa undani zaidi.

Amos, amegusia kitu muhimu sana kwa jamii yetuya Kibongo, baba kuchagua jina la mtoto wa kiume na mama kuchagua jina la mtoto wa kike.

Kila la kheri mdada.

No comments:

Pages