"Naitwa Michael miaka 25 ni mara yangu ya kwanza kwenye libeneke kuomba ushauri. Kuna binti anaitwa Joy ana miaka 23 ambaye ningependa awemchumba wangu, lakini nakuwa katika wakati mgumu kutokana na majibu anayonipa nikiwasiliana naye kupitia simu. Wakati huu hatukuwa karibu.
Majibu anayonipa hasa kwenye story za kawaida tunazopiga yanaonyesha uelekeo wa yeye kunikubali lakini nikimuuliza kuhusu mimi na yeye kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ananiambia muda wake wa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi bado, na nikimuuliza lini atakuwa tayari kasema "ni katika kipindi cha miaka 3 ijayo".
Nilimuahidi kumsubiri lakini akakataa kwa kisingizio kuwa asingependa kuniumiza wala mimi kumuumiza yeye.Tumekuwa karibu sana katika kipindi cha miezi 3 ya mawasiliano kupitia simu kiasi cha yeye kuniambia mambo mengi kuhusu familia yake na mengine yangehitaji mtu wa karibu sana kuyajua.
Mambo kuhusu boyfriend wake wa kwanza na jinsi walivyoachana, sifa za mume ambaye anamhitaji na zote ziliniangukia.Nilipomuuliza kama ananipenda na kunihtaji alisema ananipenda lakini kunihitaji hakuwa na jibu kamili.
Sasa wakati mgumu nilionao ni je niendelee kumbembeleza au nimuache? nikitaka kufanya hivyo roho yangu inasita kwani kwa jinsi anavyokuwa mgumu ndio nazidi kumpenda. Nifanyeje? Michael"
Dinah anasema:Mike hebu kuwa mkweli, unauhakika ktk umri wa miaka 25 uko tayari kumuoa huyo binti au ni gia tu ya kumpata kimapenzi? Kama kweli unauhakika na unania ya kumchumbia na kuja kufunga nae ndoa nasikitika kusema kuwa yeye kwa sasa hayuko tayari kwa ajili hiyo na amekuwa wazi kwako, kuwa anakupenda lakini hayuko tayari labda baada ya miaka 3...hapo uamuzi ni wako ku-take risk na kumsubiri au kuendelea na maisha yako.
Uamuzi wa kumsubiri unaweza kukupa matokeo mawili tofauti moja ni chanya au hasi, kwamba akawa nawe kama mpenzi/mchumba au akawa na mtu mwingine....ndio maana nikasema take risk.
Kitendo cha huyu binti kukuambia vitu vingi ambavyo wewe unadhani anapaswa kuambiwa mtu wa karibu zaidi kama vile mpenzi, ni kwa sababu anakuamini kama rafiki yake. Inawezekana kabisa hata upendo alionao ni wa kirafiki na sio wa kimapenzi na ndio maana anakosa jibu unapomuuliza suala la yeye kukuhitaji wewe kama mpenzi.
Katika hali halisi ni Binti mdogo ambae tayari amewahi kuwa kwenye uhusiano, kama mpenzi aliyekuwa nae alikuwa ndio mpenzi wake wa mwanzo ni wazi kuwa itamchukua muda mrefu kidogo kama hajaingia kwenye uhusiano mpya na mwanaume yeyote sio wewe tu.
Kutokana na maelezo yako nahisi kuwa huyu binti bado anahisia na yule ex, hisia zinazomfanya ashindwe kufanya uamuzi kwa vile hana uhakika kama bado anampenda yule au la! Inawezekana pia kajiwekea hiyo miaka mitatu kuweza kujua hisia zake ziko wapi.
Kitu ambacho kimepelekea yeye kukuambia kuwa asingependa kukuumiza au wewe kumuumiza, pale ulipoahidi kumsubiri ndani ya miaka mitatu ambayo kwa mujibu wake ndio atakuwa tayari kuingia kwenye uhusiano.
Nimependezwa na uwazi wa huyu Binti, kajaribu kuwa mkweli ili kukusaidia wewe kufanya uamuzi na kuendelea na maisha yako lakini wakati huohuo uendelee kuwa rafiki na mtu wake wa karibu.
Mimi nakushauri umuache (kwani kubembeleza kukizidi huwa kunaudhi sana) lakini endelea kuwa pale kama rafiki, msikilize, mshauri, msaidie na yote muhimu kwa marafiki. Ukionyesha kuwa umeheshimu "msimamo" wake lakini bado unaendeleza urafiki ni wazi atakuwa comfortable na wewe na pengine baada ya hiyo miaka mitatu wewe ukawa the one.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment