Wednesday

Sitaki kuudhi mke na Familia yangu, nitaachaje?-Ushauri

"Habari dada Dinah, Mimi nijiite Elly. Umri wangu sasa ni 34yrs, naishi scandinavia countries.
Leo ndio mara yangu ya kwanza kuandika humu japo kwa suala la kupitia mana nyingine najikuta nimerudi kama mara mbili kwa siku kuona kama kuna jipya.

Ni ukweli nisiouficha kuwa nimekuwa nikijifunza mengi kupitia hapa.
Nimeona niandike humu kwani naamini kwa ushuri wanaopewa waliopitia hapa kuomba ushauri kwa kweli naona wanasaidiwa. Kwani wengi wa watembeleji wa humu ni watu wazima.

Kifupi Dinah, mie nimekuwalia mazingira ya dukani tangu nikiwa Primary hadi Secondary, kipindi hicho chote cha kuuza duka kuna wateja hasa Arusha , Mererani na Mbeya ambako nimeuza duka nyakati tofaui (sio yangu ni ya kaka zangu) wakinunua sigara basi wana kuambia "niwashie" na mimi kuwawashia kama kawaida. Tangu kipindi hicho basi ndio mwanzo wa kujua sigara.

Sikuwa mvutaji yule wa viile, Ila pale ninapohitaji kuchangamka kama wanywa pombe ama wala ndumu, mie steam zangu ni sigara moja nachangamka.Tabia hii nimekuwa nayo kwa miaka 17 sasa. Miaka sita iliopia nilifunga ndoa na tumejaliwa mtoto mmoja ambae nilimuacha Bongo kwa miaka 3 sasa na mwanetu ana 4yrs.


Wakati wa kudate na ma wife hakuwahi gundua kuwa mara nyingine huwa navuta sigara, nasema mara nyingine maana kama nilivyotangulia kusema mie nilikuwa sivuti kila siku.
Pamoja na kutokujua ila kati yetu kuna kipindi fulani tuliambiana what I like and don't.

Yeye cha kwanza ni uvutaji na pombe, katu hatopenda wala kutamani mwenzie atumie. Pombe kweli Sijawahi kutumia kwani ladha yake tu inatosha kuninyima raha ya kunywa. Tabu yangu tangu nimekuwa huku Ughaibuni, Unajua tena kutimiza ndoto kwanza naona sio kama nilivyotarajia.

Maana nilitegemea ningeweza kuileta family huku ktk kipindi cha 1 year kitu ambacho kinaonekana ni kigumu hivyo napigana pengine kupata mtaji nirudi ku-join family ama kama yeye atapaa skuli basi aje. Ila hili sio ilionileta hapa ktk blog.


Sasa kipindi chote cha 3years nimekuwa nikivua takriban sigara 10 kwa siku, ila cha ajabu siwezi vuta waziwazi hadi nikiwa mwenyewe hivyo hata marafiki hili nao hawajui. Dinah sigara siipendi na sipendi kuwa mvuaji bali najikuta tu navuta.

Nimejaribu kuacha nimeshindwa, najua hata wife akijua japo nitajitutumua ka kidume ila ukweli hili litanipunguzia heshima nilionayo kwa mke wangu na jamii ya kwatu ambao hakuna hata mmoja mvutaji, sijui nimetokea wapi maana huu si utoto tena kwa umri huu.


Tafadhali msinishambulie jamani bali mnipe ushauri kama kuna mwenye kujua mbinu yoyote ya kuepukana na sigara.
Shukrani sana kwa ushauri mtakao nipa maana nitaufanyia kazi"

Dinah anasema: Elly asante sana kwa ushirikiano wako pia uvumilivu. Inapendeza kuona watu wamechangia uzoefu wao kuhusu matumizi ya sigara, mimi binafsi nitakupa ushauri wa uhakika wa kuacha "habit" yeyote mbaya inaweza kuwa kujichua, kutokuoga, ngono na watu tofauti kila siku (ngono zembe) kula sana, uvivu, kujamba, kutumia psa ovyo, kunywa pombe n.k

Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa mtu anaweza kuzoea kitu fulani na kukitumia kitu hicho kama "kiondoa" mawazo au kwa case yako kukuchangamsha, mazoea hayo yanaweza kujenga tabia na tabia ikazaa tatizo liitwalo addiction kwa kitaalam.

Kama huko Ughaibuni ni pande za Uingereza, basi nafurahi kukuhabarisha kuwa NHS wanatoa huduma ya bure na baadhi hupewa malipo fulani ili waache kuvuta sigara, hivyo basi unaweza kufanya mawasiliano na wahusika ili kupata msaada wa kitaalam zaidi na support ili uache kabisa kuvuta Sigara.

Vinginevyo ni kujiwekea mikakati mwenyewe ya kujaribu kuacha tabia ya uvutaji, natambua kuwa ni ngumu sana kuacha kufanya jambo ambalo umelizoea ghafla, hivyo ni vema ukaanza kupunguza kiwango unachovuta kwa siku.

Mfano badala ya kuvuta kumi kwa siku kama ilivyo sasa, jitahidi na uvute mbili, jinsi ambavo siku zinakwenda unazidi kupunguza siku za uvutaji...Mf; umeweza kuvuta kila siku sigara mbili sasa anza kuvuta sigara moja kila baada ya siku mbili, endelea kubadilisha the habit, na sasa punguza na vuta moja kila baada ya siku nne.

Utajikuta unavuta moja kila baada ya wiki na baadae itakuwa moja kila baada ya wiki 2, alafu utajikuta unavuta moja kila baada ya mwezi na hatimae utasahau kama umevuta au laa!...haina maana ukaitafute bali jipongeze kwa kufanikiwa.

Hii haitochukua siku mbili au mwezi mmoja bali ni miezi kadhaa hivyo kuwa mvumilivu na kuwa commited kwenye mkakati utakaojiwekea, kumbuka ni wewe pekee mwenye uwezo wa kujizuia kuvuta sigara.

Wakati unaendelea na mkakati wako wa kuacha kuvuta sigara, jaribu kubuni kitu mbadala utakachokuwa unakitumia kujiliwaza au kuondoa mawazo kila unapojisikia mpweke, mwenye huzuni, unapoikumbuka familia yako.....unaweza ukatumia senti unayonunulia sigara kumi kununua kadi ya simu/muda wa kutosha ili kuzungumza na watu ambao ni muhimu kwako au kwenye shughuli zako au zile unazotaka kwenda kuzifanya Nyumbani.

Kwa vile uko mwenyewe huko Ulaya ni wazi kuna wakati unapata upweke sio wa kimapenzi tu bali hata ule wa marafiki, ndugu na jamaa, maisha ya Ughaibuni ni tofauti sana na hapa nyumbani kutokana na Tamaduni zetu kutofautiana.

Unaweza ukajikuta unaishi ili kufanya kazi badala ya kufanya kazi ili uishi, yaani yanakuwa ya upweke sana kwa vile hakuna ile " kujichanganya" kama hapa bongo, kwamba ukitoka kazini kila mtu anakwenda kwake na maisha yake kivyake.

Ni matumaini yangu utachukua ushauri wa waungwana wengine na sehemu ya maelezo yangu na kufanyia kazi kamaulivyo ahidi.

Kila lililojema.

No comments:

Pages