Monday

Mchumba ana UTI isiyoisha-Ushauri!

"Pole na kazi dada Dinah
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 sasa na nina mahusiano na nataka sasa nifanye maamuzi hasa kwenye maisha ili niweze kuoa, maana nafikiri kila kitu nimemaliza kwani nimeshapata elimu kwa kiwango cha degree moja na nimepata kazi nzuri .

Kwa sasa nimeshatoka nyumbani najitegemea na nimeshafikiria maamuzi ya kuoa, ila tatizo kubwa linaloniumiza kichwa ni huyu mpenzi wangu karibu kila baada ya miezi 2-3 lazima atalalamika kuwa tumbo linamuuma sana na akienda hospital anaambiwa kuwa ana UTI sasa mimi nashindwa kuelewa.

Tunakaa pamoja na nyumba ina choo cha kuflash na sasa ni zaidi ya mara 5 amepatwa na huo ugonjwa, napata wasi wasi sana japokuwa nilipomwambia tukapime HIV alikubali na wote tulikuwa safi, sasa najiuliza maswali haya

1.Huu ugonjwa ukiachilia uchafu wa chooni tatizo lingine linasababishwa na nini?

Dinah anasema: Maambukizo kwenye njia/mfumo wa Mkojo unasababisha na wadudu wanaoishi sehemu ya kutolea haja kubwa na sio uchafu wa chooni, japokuwa uchafu chooni unaweza kusababisha maambukizo mengine ukeni.

Mgonjwa akipata UTI na kuanza matibabu ni lazima amalize Dozi aliyoandikiwa na wakati akiendelea na unywaji wa dawa lakini akawa mzembe kunywa maji kwa wingi tatizo hilo litaendelea kujitokeza mara kwa mara kwa vile wakati alipokuwa akitumiia dawa alipaswa kunywa maji kwa wingi ili kusafisha njia yake ya mkojo kwa kukojoa mara nyingi.


Msemaji aliyesema kuwa UTI ni kichocho sio kweli, kichocho ni maambukizo mengine ambayo husababishwa na wadudu wanaishi kwenye maji yaliyotuwama/simama. Mtu mwenye kichocho hukojoa mkojo wa damu wakati mtu mwenye UTI anakojoa mkojo wenye rangi ya kama brauni hivi....yaani mkojo wake sio msafi na huto aharufu mbaya na kali sana.

2.Je akifanya ngono tatizo hili alimuathiri ?

Dinah anasema: Mhusika napopatawa na UTI hata kama ni mwanaume, unatakiwa kutumia Condom wakati wa kufanya ngono ili kuepuka maambukizo. Lakini ni vema kutofanya ngono mpaka mgonjwa amalize Dozi na kuponakabisa. Utajua umepona baada ya kwenda kumuona Daktari kwa vipimo vingine na pia mkojo kuwa msafi (unatakiwa kuwa kama maji).

3.Kwanini hiyo UTI inamtokea mara kwa mara?

Dinah anasema: Kuna sababu chache ambazo nimezigusia hapo juu na nyingine ni kwa vile anaendelea kungonoka wakati wewe ambae nadhani utakuwa umeambukizwa. Mlipaswa wote kupimwa na kutumia dawa za kutibu UTI.....ugonjwa huu sio kwa wanawake tu, bali hata wanaume.

4.Ni njia zipi zinaweza kuchukuliwa ili asipate tena ?

Dinah anasema: Kuhakikisha anapimwa tena, anatumia dawa na kumaliza Dozi yote bila kuruka siku, masaa. Kujenga tabia ya kunywa maji kwa wingi kila siku, kujifunza kuwa msafi na kujua namna yakujisafisha sehemu zake nyeti.

Kutokubana mkojo kwa muda mrefu, wanawake tunauwezo wa kubana mkojo kwa zaidi yamasaa manne na huwa tunajisifu sana kwa hilo lakini kama umewahikuwa na UTI hakikisha ukibanwa tu mkojo unaenda kukojoa haraka.

Vilevile kukojoa kila baada ya kufanya ngono ( ni muhimu kunywa kimiminika) sio uji, Soda wala pombe bali juisi iliyochanganywa na maji mfano maji ya Ukwaju, Ubuyu, Squash (hii lazima uzimue na maji) au aina yeyote ya kinywaji ambayo inachanganywa na maji asilia. Yote kwa yote maji ni mazuri zaidi ya vimiminika vingine.

Anapojisafisha baada ya kunya asijisafishe mpaka ukeni kwa wakati mmoja. Kama amekojoa wakati anakunya na anataka kujisafisha "kwa mpigo" ni vema kuanza kujiswafi uke na kumalizia sehemu ya kunyea kwama viungo viwili vinavyojitegemea kwamwe asisafishe kwa wakati mmoja. Pia kuepuka kuchangia vyombo/vifaa/sehemu za kuongea au kujisafishia nyeti zake.

Ikitokea amjemaliza kujisaidia (kunya) kisha akaenda kuoga (baada ya kuchamba) ahakikishe kuwa amesafisha mikono yake kwa sabuni kabla hajagusa uke wake nakujisafika ukeni (kuondoa utoko).

5.Madhara gani makubwa yanaweza kutokea baadae?

Dinah anasema: Kama ataendelea kutumia aina ya Antibaotics kutibu UTI kwa muda mrefu, inasemekana dawa hizo husababisha tatizo lingine la kiafya, pia kama UTI itafikia kwenye kiwango cha mgonjwa kukojoa mkojo mzito (uliochanganyikana na usaa) au usaa kuteremka wenyewe kama Utoko basi ni wazi kuwa mrija wake wa mkojo unaweza kuzima na hivyo kushindwa kutoa mkojo kawaida.....unabanwa mkojo lakini huwezi kukojoa.

Ikifikia hatua hii mhusika tahitaji kufanyiwa upasuaji ili asafishe na pengine kuwekewa Catheter (mrija wa mpira) kwenye Kibofu cha mkojo nahivyo kutumia Mfuko wa nje wa kutunzia mkojo.

Nitashukuru sana nikipata majibu kutoka kwako hili nitoe wasiwasi wangu
Ni mimi nduguyo Jm."

Dinah anasema: Asante sana JM kwa uwazi na ushirikiano. Ni matumaini yangu maelezo ya wachangiaji na haya yangu niliyo ongezea yatasaida wewe na mpenzi wako kwa pamoja kwenda kwa Daktari ili kupata matibabu na kutibu tatizo.

Kila la kheri.

No comments:

Pages