"Dada Dinah na wasomaji wote, Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22, nina mchumba wangu tunapendana sana na hivi karibuni tunatarajia kuoana.
Tatizo langu kubwa ni hivi, kabla ya huyu mchumba wangu nilikuwa na boyfriend ambaye nae mwanzo tulipendana sana ikaja kutokea hitilafu katika mapenzi yetu kwani alikuwa na mahusiano na mwanafunzi nje ya uhusiano wetu. Kabla ya kuchukua uamuzi nilijaribu kukaa nae nikamweleza ni jinsi gani naumia juu ya tabia yake aliyoianza.
Ilionyesha kuwa alinielewa na tukaendelea na mapenzi yetu kama kawaida, baada ya muda tena nikaja kuona sms ya yule yule mwanafunzi aliekuwa akitembea nae akimtaka aende kwake, kwakweli nilishindwa kuvumilia.
Nikaongea na Dada zake kwani yeye hana baba wala mama hao dada zake na kaka zake ndio walezi wake, japo kua mama yake mzazi amefariki hivi karibuni akiwa ananitambua kama mkwe wake mtarajiwa.
Dada zake walikaa Ex wangu na kuongea nae kwa kirefu zaidi, akawa kama ameelewa lakini baada ya mda mfupi mambo yakawa yale yale, basi dada zake wakaniambia kua wamejaribu kumuonya lakini hawaoni msimamo wake ni upi! Basi nikajitahidi kwenda nae hivyo hivyo, baadae nikachoka nikaamua kumwacha aendelee na mambo yake.
Sasa huyu Mchumba wangu ambaye nimeamini kuwa ananipenda labda aje abadilike hapo baadae nami nampenda pia lakini kila nikikutana nae njiani yule Ex ananiambia kua anaomba turudiane kwani amejifunza na amejua umuhimu wangu.
Anadai kila mwanamke atakae mpata anakuwa nae siku chache tu baada ya kugundua kua anamwanaume mwingine, na mimi nashindwa kumsahau kabisa na kila nimwonapo huyu Ex mwili wangu wote unasisimka.
Sijajua nifanye nini ili niweze kumsahau kabisa japokuwa alinitenda lakini nahisi kama kuna hisia zimebaki, naombeni ushauri wenu wadau japo kua najua wengine wataniponda hilo sinto jali zaidi nahitaji ushauri ili nijue njia ya kumsahau huyo Ex ili niweze kufunga ndoa kwa amani na Mchumba wangu wa sasa.
Asanteni
Mwanablog"
Dinah anasema: Hey asante sana kwa mail yako. Kutokana na maelezo yako inaelekea kuwa wewe umeingia kwenye uhusiano mpya muda mfupi tu baada ya kuachana na Ex wako hali inayosababishwa wewe kushindwa kuelewa hisia zako.
Ikiwa tayari umechumbiwa na mwanaume unaempenda na yeye anakupenda kwanini upoteze muda na huyo mwanaume ambae anakuja kwako kwa vile tu kila mwanamke anaekua nae anakuwa sijui na nini? Mwanaume anakuja kwako na kutaka mrudiane kwa vile anakupenda sio kwa vile wanawake wengine anaokua nao wanakuwa na tatizo fulani!!! hii ni sababu tosha ya wewe kuhama mtaa kabisa achilia mbali kubadili njia ili usikutane nae.
Nini cha kufanya ili umsahau Ex: Kama inawezekana basi hamisha makazi, ikiwa haiwezekani basi tafuta namna ya kumkwepa kama ulivyofanya mara tu baada ya kuachana. Hilo Mosi.
Pili, hakikisha unapotoka unakuwa na mchumba wako au mtu yeyote anaejua uchumba wenu kwa sababu za "kiusalama" kwamba jamaa likikuona na mtu mwingine halitopata nafasi ya kuongea nawe kuhusiana na hisia za kale.
Tatu, epuka kukaa mwenyewe kwani kunaweza kukufanya uanze kukumbuka yaliyopita, hakikisha akili yako inafanya kazi kila wakati kwa kufikiria mambo mengine muhimu kama vile kazi/masomo, maisha yako ya baadae na nini ungependa kufanya baada ya kuolewa, mipango ya ndoa yenu, aina gani ya gauni, rangi, ukumbi, wageni n.k.
Nne, jitahidi kuzungumza na mpenzi wako kwa njia ya simu kila siku kabla hujalala hii itasaidia kutokuwaza Ex, ukizungumza nampenzi wak kuhusu hisia zenu za kimapenzi na jinsi mnavyopendana ndio yatakayotawala akili yako mpaka utakapo pitiwa na usingizi.
Nakutakia kila la kheri kwenye kumsahau Ex na hatimae kufunga ndoa namchumba wako.
1 comment:
Jina langu ni Lilian N.Hii ni siku ya furaha sana ya maisha yangu kwa sababu ya msaada wa Dragaguru amenipatia kwa kunisaidia kupata mume wangu wa zamani na uchawi na kupenda. Nilikuwa nimeolewa kwa miaka 6 na ilikuwa ni ya kutisha sana kwa sababu mume wangu alikuwa anajaribu kudanganya juu yangu na alikuwa akitafuta talaka lakini nilipoona barua pepe ya Dr.saguru kwenye mtandao juu ya jinsi amewasaidia watu wengi kupata zamani yao na kusaidia kurekebisha uhusiano. na kuwafanya watu wawe na furaha katika uhusiano wao. Nilimfafanua hali yangu na kisha nikitafuta msaada wake lakini kwa kushangaza kwangu zaidi, aliniambia kwamba ataniunga mkono na kesi yangu na hapa ninaadhimisha sasa kwa sababu Mume wangu amebadilisha kabisa kwa mema. Daima anataka kuwa na mimi na hawezi kufanya chochote bila ya sasa. Ninafurahia sana ndoa yangu, ni sherehe kubwa. Nitaendelea kutoa ushuhuda kwenye mtandao kwa sababu Dragaguru ni kweli harufu halisi ya spell. Je, unahitaji kupasa kuwasiliana na mkurugenzi SAGURU sasa VIA EMAIL: drsagurusolutions@gmail.com au Whatsapp +2349037545183 Yeye ndiye jibu pekee kwa tatizo lako na hufanya uwe na furaha katika uhusiano wako.
1 wapenzi SPELL
2 WIN EX BACK
3 FRUIT YA WOMB
4 PROMOTION SPELL
5 SPOTE YA KUJIBU
6 BUSINESS SPELL
7 JODA YA KIENDA
8 LOTTERY SPELL na COURT CASE SPELL.
Post a Comment