Tuesday

Miaka 10 kwenye uhusiano na mtoto moja bila ndoa, je nimuache?

"Habari dada Dinah,
Pole kwa majukumu na hongera kwa kuelimisha jamii. Mimi ni mdada nina miaka 32 toka Arusha. Nina uhusiano na mwanaume kwa muda wa miaka 10 na nimezaa naye mtoto mmoja.

Kabla ya kuwa na mimi huyu mwanaume alishawahi kuwa na wanawake tofauti na amezaa watoto wawili kila mmoja na mama yake.Katika uhusiano wetu tumefanikiwa kununua nyumba moja yeye alichangia hela nyingi kuliko mimi ila mimi niliifanyia ukarabati mkubwa, hati nilisaini mimi na alinikabidhi.

Nyumba hiyo ninaishi mimi na mtoto wangu, yeye anaishi nyumba nyingine na watoto wake hao wawili na huwa nafika hapo ila hajawahi kunikaribisha ndani wala kunitambulisha kwa watoto wake.

Alishawahi kunitambulisha kwa baadhi ya ndugu na rafiki zake na kwa staff wenzie ofisini. Huyu mwanaume amekuwa msaada sana kwangu na familia yangu, kwetu wanamfahamu kama baba wa mtoto wangu.

Mimi nataka kuachana na huyu mwanaume kwa sababu naona ananipotezea muda pamoja na kwamba ananisaidia. Ila kuna ndugu zangu wananishauri nisimuache. Mimi binafsi naona hayupo serious kwani angekuwa serious na mimi au kuwa na mpango na mimi sidhani kama angekaa nyumba tofauti na mimi.

Pili, muda wa miaka kumi ni mrefu sana kama angekuwa na mpango na mimi nadhani angenioa. Nimejaribu kuongea naye mara nyingi takribani miaka 6 sasa kuhusu suala la ndoa lakini kila siku jibu lake kuwa ana mipango anaikamilisha kwanza lakini haniweki wazi ni mipango gani hiyo.

Tatu, Pamoja na kwamba huwa anakuja kwangu na tunafanya mapenzi lakini si kivile na mara nyingi huwa nakuwa mpweke, kwa kifupi huwa anakuja anavyotaka yeye so nakuwa sipo uhuru na mapenzi.

Nne hakuna relation yeyote kati ya mtoto wangu na watoto wake yaani kwa kifupi mambo yake mengi haniweki wazi hizo ndio sababu ambazo zinanifanya niamue kuachana naye pamoja na kwamba ananihudumia kwa kila kitu.

Binafsi bado nampenda sana, tena kwa dhati ila kwa kweli nimechemsha kwa hilo. Nilishawahi kumwambia kuwa nimechoka na ninataka tuachane, aliumwa presha mpaka akalazwa. Toka nimekuwa na uhusiano naye sijawahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya uhusiano wetu na nilishawakataa wengi kwa ajili yake lakini kwa sasa nimechoka.

Hofu yangu ni kuwa baada ya kuachana itabidi tuuze hiyo nyumba na nitahangaika na makazi mimi na mwanangu. Pia nahofia usalama wake maana bado atabaki kuwa baba wa mtoto wangu.

Ninaomba wana-blog wenzangu mnishauri katika hili ili niweze kuchukua maamuzi sahihi. Samahanini sana kwa maelezo yangu marefu, Madada wa Arusha".

No comments:

Pages