Sunday

Kitu kidogo tu anitishia kuachana, nimuache kweli au?-Ushauri

"Habari yako dada Dinah???
I hope upo pouwa sana and well, thanks for everything you have been taught us and may God Bless u always...

My name is (dinah kahifadhi jina) am Tanzanian but currently am in Malaysia studying, I am having a problem with my GirlLover and I completely dont understand her! My girllover lives in Tanzania and am here (in Malaysia). Every end of the year I go to Tanzania to see her, I have no other reasons for me to go there apart from seeing her.

Anapenda sana kunitishia kuniacha yaani kitu kidogo tu atanuna na kunitumia msg'z kama "maisha mema na usinipige simu wala kuni text" tena kwa kosa dogo sana ambalo liko juu ya uwezo wangu, kosa lenyewe ni kutopokea sms zake kwavile network ilikuwa inamatatizo.

Pia nikifanya kosa bahati mbaya basi atanuna wiki moja au mbili, yaani nisimsemeshe. Lakini yeye akifanya kosa kama nililofanya mimi na akiomba msamaha ni hapo hapo umsamehe na usimpomsamehe hapo on the spot ataanza kunitishia kuwa "basi kama huwezi kusamehe on the spot tuachane" na kosa hilo hilo nilikifanya mimi naweza kuomba msamaha kwa wiki mbili mfululizo lakini hanisamehei and it's annoying.

Nampenda sana na nimeshamtambulisha home na yeye ameshanitambulisha kwao na familia zetu ni friends lakini hii tabia yake inaniboa sana, pia hivi vitisho vyake vya "tuachane" vinanifanya nisisome kwa raha yaani performance inashuka.

Nampenda sana na I can't afford to loose her... sasa nifanye nini ili aache kunitishia hivo vitisho au njia ni kuachana nae na nikiongea nae sometimes anakubali kuendelea na mimi but kitu kidogo anarejea hiyo tabia.

Naomba ushauri jamaa, ni kuachana nae au njia ni ipi hasa?"

No comments:

Pages