"Thanxs dada dinah kwa ushauri unaotupa wanawake wenzio. Ila dada naomba ushauri wako pamoja na wachangiaji wengine. Mimi nina mahusiano na mume wa mtu na nampenda sana naye ananipenda sana na pia ndio mwanaume wa kwanza kwangu.
Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.
Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"
Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!
No comments:
Post a Comment