Tuesday

Nikisema sina hela ananuna, busu, kumbatio ni tatizo, nimbadilishe vipi?

"Hi da Dinah

Pole na hongera kwa kutoa elimu kwa vijana wa kitanzania. Mimi ni kijana wa miaka 23 na ni muajiliwa wa kampuni moja hapa Tanzania, tatizo langu ni kutopata mpenzi anayejali na kuthamini hisia zangu .



Natamani kuwa na mpenzi anayeendana na mitazayamo yangu ya kimaisha, kwa sasa ninae mpenzi lakini ni mtu anayependa pesa zaidi, siku ukimwambia huna basi atanuna na wakati mwingine anasema kuwa anahisi humpendi.



Na mbaya zaidi huwa hapendi kutoka na mimi ila marafiki zake its okay na hata hugs and kisses huwa kwake ni tatizo.Niini nifanye niweze kumbadilisha au niachane nae na kupata yule anayeendana na hisia nizitakazo? kwamba tupendane na tuendane kwenye masuala ya kimaisha?



Kwasababu wakati mwingine nahisi kuwa labda nina mkosi na sitokuja pata chaguo la moyo wangu nitakae mpenda na yeye anipende na sio kupenda pesa zangu."



No comments:

Pages