"Mimi ni mwanamke ambae niko kwenye ndoa miaka minne sasa. Ila ninatatizo naomba mnipe maoni na ushauri. Mume wangu ambae nilimpenda kupitiliza nimegundua amekuwa akitoka nje ya ndoa yetu pale nilipoanza kumufatilia sana ingawa alikuwa mjanja sana.
Kinachoniuma saaana huyo mwanamke aliekuwa akitoknae nilianza kumuhisia kipindi hatujafungandoa, kila siku nilikuwa nikiona msg zake akimtukana mtu fulani ila nikijaribu kumuuliza mume wangu anasema kuwa ni mambo tu ya kazini. Lakini kila nilipokuwa nikiona msg nahisi kusutwa!
Hivi sasa tuna watoto wawili na nilikuwa muamini zaidi mume wangu nakila ninapo shitukia ishu kuwa labda anatoka kusaliti ndoa yetu na kumhoji kama ni kweli, mume wangu anakasirika na kuniomba nipige magoti nisali na kuomba Msamaha.
Nilikuwa nikifanya hivyo na hata yeye kuomba pamoja nami huku maombezi yake yakiwa Mungu atupe tuweze kuaminiana. Hajawahi kupunguza mapenzi kwangu wala kuonyesha ila siku moja nimekamata msg nyingine nikajifanya mimi ni mume wangu na hapo ndipo nilipogundua mwanamke huyo anavyo enjoy na mume wangu.
Kinachoniumiza sana alikuwa akitumia rafiki yake huku mara nyingi nyingi kujifanya kuwa ni mgonjwa anahitaji kwenda hospitoli anadai asindikizwe na mume wangu kumbe ilikuwa njia yakumtoa tu. Akitoka asubuhi kusaliti ndoa yetu anahubiri Kanisani kama kawaida na huku akisukuma Injili.
Yaani nikifikiria hapo nahisi kumchukia, hata mida mingine sijisikii kumpikia kutokana na ahadi nyingi tele tele na huku akionya watu wengi kuhusu ndoa. Naombeni jamani mniambie nifanye nini kumsamehe sijamsamehe ila aliishaomba msamaha nakunieleza kuwa kila nililoligundua ni ukweli! ninaumia sana.
Nilimwambia asubiri nitampa jibu. Sasa mawazoni mwangu najiandaa na nikipata kazi nitamuacha kwani nikifanya uamzi mapema naweza kuumia sijuwi niko sahihi au nakosea?
Hii yote ni kwasababu hakuna njia nyingine ya kumuamini hasa pale anaponiambia yote "tumkabizi Mungu" nahisi hata hilo jina asiwe analitaja. Nikiwa mbali na yeye ninajihisi kufurahi nikimuona nahisi kujinyonga sasa jamani mnasemaje hapo naombeni ushauri wenu. Asante"
No comments:
Post a Comment