Monday
Dalili za Utasa kwa Mwanaume!
Habari za kazi Doctor. Nimekua nikifwatilia mada zenu nami nina maswali yafuatayo naomba unisaidie. Swali langu la 1 ni je? kuna dalili zozote za mwanaume ambaye ni Tasa? Mfano kwa kuangalia rangi ya shahawa ama kujua shahawa zilizokomaa zinakua na rangi gani?
Dinah anasema: Ayee! Mie sio Dakitari ila nina Elimu ya Awali ya Kiasili na kauzoefu tu kiasi , siku ni njema kabisa nashukuru kwa ushirikiano Ndugu yangu.
Hapana! Sidhani kuwa kuna dalili yeyote inayoashiria kuwa Mtu ni Tasa iwe ni mwanaume au mwanamke. Ukomavu wa Shahawa ni pale unapobalehe.....ukibalehe hata kama una miaka 7 bado utaweza "kusababisha" mimba na hatimae Mtoto ikiwa utafanya ngono bila kinga.
Isipokuwa kama una matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha tatizo la uzazi basi kutakuwa na dalili zinazohusiana na tatizo hilo la kiafya (Ugonjwa). Pamoja na kusema hivyo kuna dalili zinazoweza kusadiki Ugumba kutokana na Shahawa zako, kwamba hazina ubora/afya kutokana na rangi, harufu na uwingi/uchache, uzito/wepesi.
Japokuwa utahitaji vipimo Kitibabu ili kuhakiki Ugumba na kupata Ushauri yakinifu wa Kitaalam. Tambua kunatofauti ya Utasa (tatizo la kudumu) na Ugumba (tatizo la muda).
2. Ninaye mpenzi wangu, siku moja nilifanya nae mapenzi ambapo siku hiyo anadai Yai lilikua tayari then wakati nafanya nika-withdraw nje.Ila kwa bahati mbaya niliacha Shahawa kidogo sana ndani na nyingi nilimwaga nje, lakini hakupata Ujauzito je? Kuna uashiria wowote kua naweza kua Tasa?
Dinah anasema: Kujua kuwa Yai lipo tayari sio "business" rahisi ndio maana kuna Bidhaa maalumu za kukusaidia kujua kama upo tayari au la! Huenda alichanganya kukaribia siku zake na Yai kupevuka (kuwa tayari).
Pia kuna dalili za kimwili kama vile Ute mwepesi kuongezeka, joto kupanda na Nyege kuongeza....ila sio wakati wote mwanamke huwa sahihi kwenye hili. Unahitaji muda na kujua mahesabu ya Mzunguuko wa Hedhi kwa undani na ukaribu zaidi.
Kama alikuwa tayari kushika Mimba na hakushika basi Manii zilikuwa chache au zilisafiri taratibu na kufika wakati Yai limekwisha telemka. Pia ni vema utambue kuwa kwa mwanaume Kukojoa (kumwaga Shahawa) na kufika Kileleni ni vitu viwili tofauti.
Wakati mwingine mwanaume anaweza kukojoa bila Mbegu (Sperms)....Vilevile Kitaalam (huku niliko sijui kwa Bongo) mtu anahesabika Mgumba ikiwa kajaribu "kusababisha" au "kushika" Mimba kwa Miaka miwili.
Na hii ni kwa kufanya Mapenzi mara nyingi kila wiki bila Kinga kwa miaka hiyo 2.Baada ya hapo unafanyiwa Uchunguzi Kitibabu alafu mnajaribu tena, kama ni Mgumba utafanikiwa baada ya matibabu/kufuata ushauri.
Vinginevyo unafanyiwa uchunguzi zaidi ili kuhakikisha kuwa wewe ni kweli Tasa na kwanini.
3. Hivi karibuni nimekua nikikaa hata wiki moja bila kufanya mapenzi, nikienda kuoga wakati nakojoa mwanzoni huanza kutoka kalundo mfano kitu kama shahawa ila hakuna maumivu. Je? Naweza kuwa na tatizo lolote? Au ni hali ya kawaida?
Dinah anasema: Mwanaume mwenzio angekupa Jibu vizuri zaidi.....Inawezekana "Mfuko wa kuhifadhi Shahawa" umejaa, hebu jaribu kuzipunguza alafu uone inakuaje ndani ya siku chache.
Nikijibu swali lako, sidhani kama unatatizo lolote, ila unahofu ya Utasa hali inayopelekea kuwa na wasiwasi kila unapoona tofauti huko sehemu- sehemu.
4. Nimekukua nikijichua kwa muda wa miaka 10 sasa, mfano muda mwingine nikiwa mbali na mpenzi wangu huwa napiga punyeto je? Kuna madhara yoyote labda naweza nisipate mtoto hapo baadae?
Hayo ndiyo maswali yangu ambayo yamekua yakiniumiza kichwa na kunikosesha amani.Nitashkuru kwa majibu na kazi njema.
*************************************************
Dinah anasema: Kujipa Mkono kuna madhara Kisaikolojia ikiwa huwezi kujizuia au niseme ukiwa addicted. Nijuavyo mie kujichua mara 1-3 kwa wiki ni Afya na Salama kama huna Mpenzi au Mpenzi yupo mbali.
Punyeto haiwezi kukusababishia tatizo la kupata mtoto hapo baadae.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment