Mambo vip dada Dinah. Pole sana na shughuli za kila siku. Mimi ni
Mwanaume mwenye miaka 25 nipo mwanza.
Nimemaliza Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) mwaka jana (2013). Kwa sasa naishi na Kaka yangu, Shemeji (mke
wa kaka) pamoja na mdogo wake Shemeji, wa kike.
Kwa sasa tumetokea kupendana sana sana na Shemeji (mdogo wake Mke wa Kaka). Mapenzi yetu ni siri sana kwa sababu Kaka hajui wala Mke wake hajui chochote.
Tumeshapanga mambo mengi ambayo tutafanya hapo baadae. Naomba ushauri, hivi kuna tatizo nikimuoa shemej yangu?!
*************************
Dinah anasema: Ahsante na Shukurani kwa Ushirikiano. Well huyo Binti sio Shemeji yako bali ni Shemeji ya Kaka yako. Huyo Binti ni mdogo wa shemeji yako au niseme ni Shemeji ya Kaka yako. Huna uhusiano wowote hapo.
Kinachofanya Ndugu wa pande mbili tofauti zilizofunga ndoa kutopendana ni Heshima au Uoga (inategemea na Kabila na Mazingira).
Enzi za Bibi yangu, Mwanaume akiwa anajiweza kiuchumi na kuchumbia familia nyingine, Baba Mkwe alikuwa anatoa Binti yake mwingine kama zawadi/Nyongeza.
Hivyo Mwanaume anaoa Dada na Mdogo wake....hehehehe, My point is:- Hakuna tatizo lolote Kiimani na Kitamaduni kuoa Mdogo wa Shemeji yako.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
No comments:
Post a Comment