Habari gani Dada Dinah!
Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 40, nimekua kwenye maisha ya Ndoa na mke wangu kwa miaka 12 sasa lakini hatujabahatika kupata Mtoto. Tatizo kubwa lipo upande wa Mke wangu kwani anashika Mimba vizuri tu lakini baada ya Muda uharibika.
Tatizo hilo limeanza tangu mwaka wa pili wa ndoa yetu tulipoamua kuanzisha familia. Tumekwisha poteza mimba nyingi mpaka ikafikia mahali mimi nikagoma kuendelea kujaribu kutokana na huruma kwa Mke wangu. Lakini mke wangu alionyesha kutojali na anasisitiza tuendelee kujaribu na siku moja mimba itakuwa vizuri na tutapata watoto wetu.
Dada mie nimechoka kiakili, kihisia na umri wangu unakwenda, nikamshauri kuwa tujaribu Adoption. Mke wangu akakataa kata kata akisisitiza tuendelee kujaribu tutafanikiwa.
Sielewi kwanini mwenzangu anang'ang'ania tuendelee wakati yeye ndio anaetaabika Kimwili!! Naomba ushauri, nifanye nini ili nimshawishi Mke wangu akubali kuadopt?
Asante Dada.
*******************************
Dinah anasema: Poleni sana kwa tatizo mnalokabiliana nalo, tatizo hili ni sensitive sana, huwa nakimbia kulizungumzia kwani nahofia kuumiza hisia za waathirika. Mimba/Mtoto ni jambo la Neema kwa Wanandoa kwavile "tumeaminishwa" kuwa ndoa ni mwanzo mzuri wa kuanzisha familia Bora, hivyo tunapofunga ndoa mara zote kinachofuata ni Mtoto/Watoto (kwa baadhi).
Ukiachilia mbali hilo pia kuna Pressure kwenye jamii na familia kwa Mwanamke kuzaa, kwamba Wanawake wengi Tanzania "wamejiaminisha" kuwa kuzaa ndio "UANAMKE"...."huwezi kuwa mwanamke kamili kama hujazaa"...."Mwanamke ameumbwa kuzaa".
Sasa wanawake wengi hufanya kila njia ili kuthibitisha kuwa wao ni "kamili", wengine hupitiliza na kubeba Mimba za Uongo(kuigiza) ili tu ionekane na wao walishika mimba hivyo ni "kamili".
Hivyo nahisi ameng'ang'ania kuendelea kujaribu kwa sababu hizo hapo juu. Katika hali halisi uanamke sio Mimba wala Kuzaa, na kuzaa sio Mafanikio ya mwanamke kimaisha.
Kuna mengi mwanamke anaweza kufanya kuthibitisha kuwa yeye ni kamili na kafanikiwa. Unaweza usizae kutokana na Matatizo lakini uka-Asili (Adopt) kichanga na kumkuza, kumtunza, kumpenda na kumtimizia mahitaji yake kama watoto wengine katika jamii.
Nadhani Mkeo anahitaji msaada Kisaikolojia, anahitaji uondoa dhana ya "mwanamke kaumbwa kuzaa" na kukubali kuwa kama wanandoa mnatatizo na tatizo lenu halitoi guarantee kuwa siku moja litatoweka na litawapa watoto.
Zungumza nae tena kwa Upendo na umuambie kuwa pamoja na kuasili Mtoto mtaendelea kujaribu tena mara Kichanga wenu (mtakae asili) akifikia umri fulani....labda mwaka na nusu au miaka miwili na mkifanikiwa mtakuwa na watoto wawili badala ya mmoja.
Mhakikishie kuwa tatizo lenu halipunguzi mapenzi yako kwake, unampenda na utaendelea kumpenda akiwa mama wa watoto wenu wote iwe ni wa damu au wa kuasiliwa. Ukiona analeta mizinguo na kutumbukizia "emotions", ongeza Mkwara lakini kwa upole na upendo.....
Chomekea Mkwara kwa kusema....usingependa kupoteza miaka 10 ya mapenzi na ndoa yenu na usingependa mpoteza bahati ya kulea na kupenda mtoto wa kuasili mkiwa kama mke na Mume.
Mpe muda, usirudie issue hii mpaka mwenyewe ailete tena Mezani, natumaini akiirudisha itakuwa CHANYA.
Nawatakia kila la kheri kwa yote mawili.
Mapendo tele kwako...
No comments:
Post a Comment