Monday

Ananipenda au ananizingua?

Habari dada,
pole na hongera kwa kazi ya kuelimisha jamii. Mimi ni msichana na nipo kwenye uhusuano na mpenzi wangu kwa
miaka miwili sasa.

Mwanzo wa uhusiano tuliishi vizuri japo tulikuwa mbali mbali kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu yeye alikuwa anaishi Dar (akiwa
Chuoni) na mimi nilikuwa Singida (Shuleni-form6).

Mwaka jana mwishoni nilijiunga na Chuo fulani hapo Dar ndipo tukawa karibu. Miezi ya kwanza
alinijali kwa kila kitu lakini sasa hivi kabadilika yaani anaweza kukaa zaidi ya Wiki 2 asinitafute kwa Simu.



Kila nikimpigia Simu anakata na hata
Meseji hajibu, yale mambo aliyokuwa ananifanyia kama kunitembelea
ninapokaa hayapo tena. Siku akijisikia kunipigia simu haniulizi kama mimi
mzima au la! Ila anataka tukutane kwa ajili ya sex tu.

Nikimuuliza kwanini hapokei Simu zangu anasema eti nisimuwaze sana kwasababu yuko busy
na maisha yake. Hivi sasa wiki 3 zimepita hajanitafuta, sasa nashindwa
kuelewa nipo kwenye mapenzi ya aina gani?

Nisaidie dada yangu.


************


Dinah anasema: Habari ni njema tu, ahsante! Shukurani kwa Ushirikiano.

Sijui mlimudu vipi Uhusiano wenu kipindi cha mwaka mmoja mlipokuwa mnaishi Mikoa tofauti, ila nahisi umbali huo ndio uliomaliza Uhusiano wenu.


Mlichokuwa nacho pale ulipohamia Dar na kuwa karibu ni "Mazoea" na kufidia kipindi mlichokosana huku mwenzio akijaribu kuangalia kama hisia ni zilezile au hazipo tena.....wewe ukapata matumaini tofauti na kilichokuwa kichwani mwake.


Sioni Uhusiano hapo ila Jamaa anakutumia kwa Ngono pale anapojisikia, na wewe unakubali ukidhani unaomsogeza karibu kama mpenzi.

Mpaka kafikia mahali anakuambia usimuwaze sana kwani yupo busy na maisha yake...ujue haupo kwenye mipango yake na kwake wewe ni "kipoozeo" kwamba anakutafuta akibanwa na Nyege tu.

Anafanya hivyo kwasababu hayupo tayari kuwa na Uhusiano mpya na hataki kuwa na Uhusiano na wewe lakini ni rahisi kufanya Ngono na wewe anaekujua na amekuzoea kuliko mwanamke mwingine mpya....sijui unanielewa Mrembo?!!


Sasa hebu Mchunie, kwamba usimtafute na usipokee simu zake wala kujibu Meseji(ikiwezekana poteza mawasiliano yake).


Kuwa Imara kama mwanamke na anza maisha mapya bila yeye. Wanaume wapo wengi tu, muda ukifika utakutana na mwingine mwema.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages