Thursday

Nakuwa Moody na Mkali kwa Mpenzi...

Naomba ushauri kuhusu haya mambo nifanyaje ili niweze kuyabadilisha
kwasababu mpenzi wangu hajaridhishwa nayo.


Ni kwamba huwana change mood
ghafla na pia huwa nakuwa mkali asa sijajua nifanyaje nahitaji msaada
wenu.

***************

Dinah akauliza: G (Sio jina kamili),

Nahitaji maelezo zaidi ya hayo ili iwe rahisi kwangu kujua kama unahitaji Ushauri wa Kitibabu au Ushauri wa Kibinaadam.

Unabadili Mood ghafla na unakuwa mkali wakati gani hasa?


Unadhani ni kitu gani kinapelekea wewe kuhisi hasira, na kubadilisha mood huko hukutokea wakati gani?....nini hasa kina- triger?

***********

G(Si jina kamili) akajibu: ninapoona hali ya utofauti kwa mpenzi wangu au nikiona sms za mwaume mwingne au ataponijibu tofauti tu nabadilika mood na kuwa na hasira.

Dinah anasema: Ahsante kwa ushirikiano.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha wote mnamatatizo ya kitabia na wote mnapaswa kujirekebisha na kuelewana ili kila mmoja wenu aepuke "kumtuma" mwenzie kuwa au kufanya afanyavyo.


Kitu gani hasa kinamfanya mpenzi wako afanye mawasiliano na wanaume wengine ambayo yanakukera? Umewahi kujiuliza?


Huenda humpatii mahitaji kihisia, kimapenzi au labda hakuna commitment anayoitaka na hivyo ameacha "mlango" wazi ili kuona kwa watu wengine kuna offer nini?.

Kumbuka mahitaji hayo yanaweza kupatikana kutoka kwa mwanaume mwingine via sms au njia nyingine ya Mawasiliano, na hufikia mahali mtu anahisi kupenda/vutiwa hali inayoweza kusababisha Usaliti kimapenzi.

Hasira au kubadilisha Mood kwako kunasababishwa na vitendo(tabia) ya mpenzi wako, sina uhakika kama anajua kuwa mawasiliano yake na wanaume wengine au majibu yake kwako ndio sababu kuu ya wewe kukasirika au kuwa na Mood mbaya.


Kwenye uhusiano wowote wenye matatizo ni muhimu kujua chanzo cha tatizo na kujaribu kurekebisha kwa kumshirikisha mwenza wako kabla hujaomba ushauri nje ya Uhusiano wenu.


Umesema mpenzio haridhishwi na tabia yako ya kuwa Moody na Hasira, ni wazi hajui sababu ni ipi hasa inapelekea wewe kuwa hivyo.


Sasa rudi kwake na mkae chini na kuzungumzia issue yenu kwa upendo bila kubishana wala kulaumiana na wote kwa pamoja mkubaline kufanya mabadiliko.


Maisha ya mahusiano ya kimapenzi ni kama Bustani ya Maua, ukitaka Maua yaonekane na afya na yaendelee kunawiri basi utahakikisha unamwagilia maji na kuweka Mbolea kila inapohitajika.

Kila siku unayatazama mauwa yako unafurahi kutokana na kunawiri kwake, unasogea karibu ili kuona kama kuna Gugu (majani ambayo sio sehemu ya maua yako)....unatafuta chanzo chake na kukiteketeza ili Bustani ya Maua yako isiharibike.


Nadhani umenielewa,

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages