Sunday

Ignorant kwenye Hasara,Faida,umuhimu wa ndoa.


Ignorant, mchango wako umenifurahisha sana.

"Kwanza kabisa, pamoja na sababu ya mada hii kupata... Kwanza kabisa, pamoja na sababu ya mada hii kupata wachangiaji wachache kama ilivyotolewa na M3, nadhani urefu wa maelezo ya DL nayo pia ni inachangia kupata wachangiaji wachache.


Sidhani kama watu wengi wanaoingia hapa wamesoma post yote, na kama ndiyo, wachache wanaweza pata wazo la kuchangia baada ya kusoma post ndefu kama hii. Ok, nirudi katika mada yenyewe.Kwa mtazamo wangu, maelezo ya wachingiaji hapo juu yana-reflect jinsi tulivyokuzwa kuamini ngono ni mbaya.


Mbali na hilo, maelezo mengi yanachanganya madhumuni ya ngono na ndoa kuwa kitu kimoja. Nitaeleza haya.Tukiweka imani za kidini pembeni, (kwani mambo mengi ya kidini huwa hayajadiliki kutokana na kuwepo kitu utakatifu na hivyo kutompa binadamu yeyote uwezo wa kukosoa au kujadili uhalali wake).


Kwa mtazamo wangu, ngono ni kitu tofauti kabisa na ndoa. Ngono ni tendo la kukutanisha sehemu kike na kiume ilhali ndoa ni makubaliano ya watu wawili kuishi pamoja na inatarajiwa watu hawa kua jinsia tofauti (ingawa siku hizi kumeingia aina mpya ya ndoa). Kwa mtazamo huu, hailazimishi vitu hivi viwili kuendana kwa pamoja au kuuliza kipi kianze na kingine kifuate ingawa inajulikana kua katika ndoa kutakua na ngono.


Kutokana na makuzi yetu, mambo haya mawili yamewekwa pamoja na hivyo kuzua utata katika kutambua kila kimoja wapo. Kuchanganya kwa madhumuni ya kingono na ndoa ndiyo yanasababisha wanawake wengi kudhani wamedanganywa na wanaume pindi wanaposhindwa kuolewa ilhali wameshangonoana na hao wanaume (same men).


Kwa upande mwingine, wanaume nao wanakua waongo kwa kuahidi ndoa kwa wanawake/wapenzi wao ili wapate ngono. Kama ngono na ndoa vingeeleweka kua ni vitu viwili tofauti, maumivu na uongo huu usingetokea. Suala la kudhalilisha utu/ubinadamu kwa kuonyesha uchi/utupu linahitaji mjadala zaidi.


Suala la kudhalilika kwa kuonyesha utupu linategemea sana jinsi mtu alivyokuzwa kama sio utamaduni. Napenda nipingane na maelezo kua ngono hudhalilisha mtu kwa kua anaifanya akiwa mtupu, tunaweza kusema nini kwa wale madaktari walio na mwanya wa kuona utupu wa wagonjwa wao? Vp udaktari nao unadhalilisha utu?Kwa kumalizia, naomba tusome alama za nyakati.

Tuangalie ni nini kinawezekana kwa nyakati hizi na pengine kutambua mabaya na mazuri yake na jinsi ya kupunguza athari za hayo mabaya. Suala la kujadili ngono kabla ya ndoa ni bora au la ni la msingi, hata hivyo kwa kuangalia kinachoendelea katika jamii, ni vizuri tukafikiri zaidi ya swali hili. Sidhani kama watu wanaofanya ngono kabla ya ngono hawafahamu faida na hasara zake.

Tujadili yale tunayoweza kuyafanyia kazi."

No comments:

Pages