"Dada Dinah, hili la leo ni dukuduku la kijana mmoja, mwenye umri wa miaka 19. Kijana huyu analalamika kwani wazee wake `hawamtendei haki' kama alivyodai.
`Kijana kamtunuku `kikongwe'' kauli zimezagaa mitaani.
Sio kikongwe kwa umri, ila vijana wenzake mitaani wameamua kukuza, kwani `limama' analolitaka limemzidi karibu mara mbili. Samahani kwa kumuita huyu mama `limama' ila nimenogeza kwasababu umejazia sio mchezo! 'Unajua wazazi wangu hawaelewi kwanini nimempendea yule `mother', mimi sikubali mpaka nimuweke ndani' alilalamika huyu kijana.
Sasa Dinah, sijui tutamsaidiaje huyu kijana, kwani huenda anakile kinachoitwa `infatuation' au kimuhemuhe cha mapenzi, au ndio kama walivyovumisha ndugu zake kuwa huenda ametengenezwa. Na huenda kayapata mapenzi ambayo anahisi hayawezi kuyapata kwa mwanamke mwingine, au kweli kampenda, huwezi jua!
Je kuna madhara yoyote kwa kijana kama huyu kumuoa mama aliyemzidi umri karibu mara mbili ya umri wake? Kwa wanaume inawezekana, hiyo ipo dhahiri! Lakini nashangaa kwa wanawake inakuwa `issue'
Nikilipeleka swali hili kiutu uzima zaidi, je ipo raha gani kijana kama huyu ataipata kwa mama huyu, tukizingatia kuwa jinsi umri unavyokwenda ndivyo hali hasa ya `uke' inavyokwisha! Sijui kama nimekosea hapa! Na kwa mfano ndio wameoana, jinsi gani `wafanye' ili wasipishane kimalovu.
Ahsanteni
Emu-three".
Jawabu: M3 asante kwa kulileta swali lako mahali hapa,nafikiri neno Jimama (sifa) lingependeza zaidi kuliko limama (kashfa). Kama ulivyosema kwa wanaume inawezekana lakini inashangaza kwanini kwa wanawake inakuwa "big deal" hii inawezekana kabisa kuwa ule mfumo dume unamizizi miongoni mwa wanajamii sio wa Bongo tu bali Duniani kote.
Kisheria (Tz) na Kimila kijana anaruhusiwa kuoa akiwa na miaka 18 hivyo huyu bwana mdogo anapaswa kufuata moyo wake na kutosahau akili yake (kuwa makini na uhakika wa kile anachotaka kukifanya).
Kama wazazi na ndugu wa karibu wanapaswa kumshauri na kumtahadharisha lakini sio kumtisha au kumlazimisha ili kuachana/ua uhusiano kwa vile tu mtu anaempenda ni mkubwa sana kwake.
Mapenzi ni hisia alizo nazo mtu juu ya mtu mwingine na hazina uhusiano wowote na umri, muonekano, mali, umbile na vitu vingine ambavyo watu wengi huvihusisha na mapenzi kimakosa. Penzi hujitokeza mahali popote na wakati wowote juu yamtu yeyote, hakuna mtu anapenda kumpenda fulani bali inatokea tu kuwa "umefika bei" na kama ni Reli yakati basi umefika mwisho Kigoma!
Kuhusiana na swala la Umri na ngono kama ulivyogusia M3 kwenye kipengele cha mwisho pia halina uhusiano na mapenzi, Ngono ni tendo linalowafanya wapenzi kuwa karibu zaidi na kujuana kiundani zaidi ukiachilia mbali suala zima la kumfanya mmoja wao kujisikia "safii" kiakili na kimwili bila kusahau kuijaza Dunia(Uzazi).
Uke wa mwanamke haubadiliki sana akizeeka (umbile) kinachotokea kwa wengi(sio wote) ni ukavu kuongezeka na hiyo huwatokea wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 50 au wale ambao wanaanza kukoma hedhi mapema which inaweza kuwa kwa wanawake wenye miaka 32-45(inategemea na maumbile).
Hivyo nina uhakika kabisa jamaa karidhika na alivyo jimama lake na pia inaonyesha kabisa anampenda au ni mara yake ya kwanza kupata hisia za kimapenzi (kutokana na umri wake).
Kitu pekee tunachoweza kumsaidia Dogo ni kumwambia aende taratibu (asifunge ndoa unless ni muislamu kwamba anaruhusiwa kutaliki) vinginevyo achukulie kila siku kama inavyomjia nakufurahia maisha yake ya kimapenzi na Jimama.
Atakapo kua sasa atafanya maamuzi yake ya busara na hakika akili itakuwa imetulia na kujua nini alikuwa kikifanya, anakifanya sasa na anakwenda kukifanya ktk maisha yake ya baadae.
Tuheshimu maamuzi yake na tuendelee kuwa pale kwa ajili yake atakapohitaji ushauri, tusimtupe kwa vile tu kapenda mtu mkubwa zaidi yake.
Kila la kheri!
No comments:
Post a Comment