Wednesday

Mume wangu ataka Ex awe mke wa Pili kwavile alizaa nae!

Dada Dinah pole kwa kazi ngumu ya kuelimisha na kutatua matatizo ya kijamii kwa kiasi kikubwa.

Binafsi nimepitia makala zako karibia zote only last month baada ya kupata link ya web yako nilipokuwa nasearch kitu fulani mtandaoni!

Nami leo nikaona ni vyema nitoe ya moyoni yanayonitatiza kwa muda mrefu na ambayo sijawahi kuomba ushauri kokote wewe ndio wa kwanza.

Mimi ni binti wa miaka 26, nimeolewa miaka 4 iliyopita ila bado sijabahatika kupata mtoto kutokana na mipangilio ya Mungu na ya kimaisha.

Wakati naanza uhusiano na huyu mume wangu alinieleza kuwa ana watoto 2 kwa mama tofauti ila alishaachana nao wakiwa kwenye mazingira ya uchumba na those pregnancies were a mistake he regrates!

Na kwamba kutokana na hilo hatafuti tena girlfriend bali mke wa kuoa, na alinieleza mazingira yaliyopekekea kuachana nao na nikaridhika.

Ex wake wa kwanza alishaolewa ila huyo wa pili bado yupo single to date. Hao ma-ex siwafahamu zaidi ya kuwaona kwenye picha.

Wa kwanza yeye alikata mawasiliano kabisa ila huyu wa pili huwa wanawasiliana kwa ajili ya mtoto. Mwanzoni sikuwa na tatizo na hilo, ila baada ya mwaka tangu tuoane akaanza kusafiri kwenda huko kwa Ex ambaye anaishi Nje ya Mkoa kwa madai ya kumtembelea mtoto na ndipo tatizo lilipoanza kutokea.


Kwani baada ya kuwa anawatembelea mara kwa mara akaanza kusema kwamba hajisikii vizuri kutengana na huyo Ex kwani mtoto anakosa matunzo ya baba na mama hivyo anataka nayeye awe mke wa pili ili mtoto akue katika misingi mizuri.

Anadai kwamba mwanaume akishazaa au kutembea na  mwanamke basi huyo ni mke wake.

Mimi nilipinga vikali swala hilo na nikamwambia imani yangu ya kikristo hairuhusu ndoa za wake wengi kwani sote ni wakristo na kama ingekuwa mtu kuzaa na mwanamke ndio mkeo basi wanaume wote wangetakiwa kuwaoa maEx zao.

Naisitoshe kama ndo hivyo iweje unataka kuoa huyu wa pili tu mbona yule wa kwanza humzungumzii!

Nikamwambia ni heri ungeniambia hivyo wakati tuko wachumba mimi ningekupisha tu muendelee lakini sasa siwezi kwani mimi ni mkeo halali wa ndoa ambaye ulioa pasipo kulazimishwa.

Nikamwambia siku zote tulikuwa sawa ila tatizo lako hilo limeanza baada ya kuanza kwenda kumtembelea Ex hivyo kinachokusumbua siyo mapenzi ya dhati bali ni guiltiness unapokuwa mbele ya Ex so ni bora ukate mawasiliano.

Baada ya malumbano ya mda mrefu ambayo alikataa katakata tusishirikishe watu hasa kwa ushauri hatimaye akatulia kwa muda na kusitisha mawasiliano.

Baada ya kipindi kupita akaanza tena yaleyale but this time bila kwenda huko ila anadai anataka tu kujua maendeleo ya mtoto.

Kinachonishangaza ni kuwa huwa hafanyi mazungumzo na huyo ex nikiwepo kitu ambacho si kawaida yake kwa simu nyingine.

Kwakweli tangia matukio hayo yalipoanza sina amani kabisa na mume wangu kwani huwa nahisi kama kulikuwa na kitu kilichoendelaea kati yao wakati alipokuwa akiwatembelea.

Kwakweli kwa sasa sina amani tena na mume wangu kufanya mawasiliano na huyo Ex wake ambaye amezaa naye.


Nina mpenda pia sina shaka na upendo wake kwangu ila ninahisi kuna kitu kina mvuta arudishe mahusiano ya kimapenzi na huyo Ex, kwani nikishaongea nae hunielewa na kutulia then akiongea tu na huyo Ex ndio hayo mambo mengine ya kurudiana nae hutibuka so nashindwa kuelewa kuna nini nyuma ya pazia.

Ninaomba ushauri wako dada yangu nifanyeje ili kuwe na amani kwa wote! Maana hivi sasa akishataja tu jina la huyo mtoto nakosa amani ya roho kabisa na hata siwi tena comfy kuzungumza naye masuala ya watoto maana naona nakumbushia huko! asante.


*************


Dinah anasema: Ahsante kwa ushirikiano. Pole nawe kwa unayokabiliana nayo.


Enzi za Bibi zetu walikuwa wanawachukua watoto na kuishi nao pale inapojulikana mwanaume alizaa kabla ya Ndoa.


Hii ilikuwa inaondoa matatizo kama haya kwenye ndoa na inamfanya Ex asipate "matunzo" kwa kumtumia mtoto.

Hali hii iliwafanya Bibi zetu waonekane kuwa walikuwa na roho nzuri sana kwa vile wanakusanya watoto wa nje wa waume zao na kuishi nao nyumba moja. Nia ilikuwa kumuondoa Ex kwenye maisha yao ya ndoa zao....anyway!

Mumeo hakutaka mshirikishe watu wengine (mostly wazazi na aliewafungisha Ndoa) kwenye tatizo lenu kwa vile anajua wazi anachokifanya sio sahihi.

Maswali mengi yanajitokeza hapa:-

1)-Huyu bwana aliachana na Exes wake walipokuwa wachumba alafu Mimba zote zilikuwa mistake, well ya kwanza tukubali....na ya pili? Hakujifunza tu?


2)-Huyu Ex king'ang'anizi ni wa kwanza au wa Pili?


3)-Alafu kwanini anatunza picha za Ex zake? Umesema huwajui ila umewaona kwenye picha tu! Kuzaa nao sio sababu ya kutunza picha zao.

4)-Mtoto anaumri gani?


5)-Kwanini ulimruhusu aende peke yake kwa Ex?


6)-Kutokuzaa ni uamuzi kutokana na Maisha yenu yalivyo au mmejaribu lakini bado hamjafanikiwa?.....maana isijekuwa anaku-push makusudi ili uzae nae haraka.

Kama walifikia hatua ya Uchumba ni wazi kuwa walikuwa wakipendana tofauti na wale wa "usiku mmoja" baada ya pombe mara boom "nina mimba yako" sort of thing.

Naelewa Jina la mtoto likitajwa kwenye mazungumzo kinachokujia kichwani ni Ex na mumeo kama wapenzi in which inakufanya usitamani hata kulala kitanda kimoja na huyo Mumeo.

Nahisi Ex anatumia mtoto ili kurudiana na Mumeo au mtoto mwenyewe ndio anataka baba na Mama yake wawe pamoja na akamwambia baba yake live, baba akapata hatia.

Hakuna mtoto anaetaka wazazi wake wakae mbali-mbali, na mara nyingi mtoto hudhani "mke" wa baba wa sasa ndio aliesababisha mimi na mama kuachwa.


Sote tumewahi kuwa watoto na hakika hufurahi kuona baba na mama wakiishi pamoja.

Lakini mazingira ya upatikanaji wa baadhi ya watoto inakuwa ngumu kwa mama na baba zao kuishi na kuwalea pamoja kama familia.

Pamoja na kusema hivyo haina maana nakubaliana na uamuzi wa mke wa pili ila ni vema kuwa open kuishi na mtoto (ikiwa atakubali kuja ishi nanyi).


D'oh! Nimeenda kwa mtoto nimekusahau wewe....samahani!

Nini cha kufanya: Weka mumeo chini na mzungumze kwa upole lakini kuwa firm ili yamuingie na ajue wewe sio "ndio" bwana kind of a woman.

Mwambie unatambua umuhimu wake kama baba kwa mtoto na mtoto kwa baba yake na huna tatizo na hilo.

Mueleze kuwa nia yako ambayo ni amani kwa pande zote, Mtoto na ninyi kama wanandoa, Mama mtoto hausiki hapa.

Mkubaliane kama mawasiliano ni kuhusu mtoto basi yawe wazi na wewe kama mke hupaswi kufichwa.


Pia ongeza kuwa Ex asipige simu unless mtoto anamatatizo vinginevyo mumeo ndio apige kum-check mtoto na moja kwa moja aombe kuongea na Mtoto wake, hakuna stori na Ex baada ya salamu na hakuna Text.

Inategemea na umri wa mtoto, mkubaliane kwenda kumuona mtoto kila anapokuwa likizo (kama mdogo), ikiwa mtoto ni mkubwa basi awe anakuja kumtembelea baba yake hapo kwenu.

Ikiwa mtoto anamiaka 10 au zaidi basi Mumeo amnunulie Mtoto simu ambayo atakuwa akiwasiliana na mtoto wake mara kwa mara kabla ya ninyi kwenda kumuona.

Mnapokwenda kumuona hamfikii kwa Ex na wala Ex hapaswi kuambatana nanyi. Anakabidhi mtoto kisha anaishia kwa muda mliokubaliana kumrudisha mtoto.

Ni wewe, Mumeo na Mwanae.....nia na madhumuni hapa ni mtoto kuwa him/herself kwako na kuanza kukuzoea taratibu.

Usikubali kuitwa Mama Mdogo kwa vile Baba yake anataka hivyo, mwambie akuite jina lako. Mtoto akiwa comfy huko baadae mwenyewe ataamua kukuita anti au mama mdogo.

Usiahidi kuwa utampenda kama mwanao (wanaotoa ahadi hii kabla hawajaishi na mtoto huwa waongo) ila ahidi kuwa utam-treat kama mtoto anavyostahili kuwa treated.

Anza na haya, alafu tuone itakuaje.....kama hujanielewa tafadhali usisite kuni-check tena.

Tuone wengine watashauri namna gani.

Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages