Saturday

Nimeachana na Mume wangu bado nampenda.

Hi dada Dinah,
Ninaumri wa miaka 30 nina Watoto wawili niliolewa miaka mitano iliyopita.

Kiukweli mume wangu alikua na mapenzi makubwa sana kwangu hadi kufikia kuonewa wivu na majilani na baadhi ya ndugu hasa upande wa mumewangu.


Mimi na Mume wangu wote ni wafanyakazi, Matatizo yalianza baada ya mwaka mmoja kwenye ndoa baada ya mama mkwe na mawifi zangu walipokuja kututembelea na kukuta maisha ya amani na upendo tuliyokua tukiishi.


Kunakipindi mama mkwe alimwambia mwanae eti tuzae watoto wawili tu maana tayari kuna mtoto wa mdogo wake alishazaa so shuleni wamemuandikisha jina la mume wangu kama baba yake kwahiyo ni wetu na tumuweke kwenye mahesabu yetu.

Kwakweli sikukubaliana na hicho kitu, nikamshauri kuwa tutamsaidia kumsomesha na mambo mengine ila shwala la sisi kupunguza idadi ya watoto tuliopanga kuzaa hapana tukawa tumekubaliana.

*****************

Dinah anasema: What a bully Mkwe and Co! Kumsaidia mtu ni uamuzi wa Msaidizi (wewe na mumeo) na sio amri wala lazima hata kama msaidiwa ni Mdogo wako achilia mbali mtoto wake.

******************

Akamueleza mama yake, mama mkwe alibadilika kabisa na kudai eti mimi namnyanyasa mwanae  inakuje kila kitu anachoongea nae anieleze na kwanini hawezi kutoa maamuzi kama mwanaume hadi anishirikishe mimi.

Mwanzoni niliona kama utani mwisho ikawa majanga mume wangu akaanza tabia ambazo hakuanazo hapo nyuma, akawa anatoka nje ya Ndoa na wanawake tofauti tofauti.


Kukawa na kutokuelewana ndani ya nyumba, bila kujua chanzo ni mama mkwe nikawa namshitakia anamuonya mwanae na tabia hiyo inaisha nikamuamini sana mama mkwe nikidhani ndio mkombozi wangu kumbe ulikua ni mpango anaoufahamu vizuri na kukubaliana nao.

Nimejitaidi kuishi kwa mashaka hadi mwaka jana mume wangu alipo amua kuhama kabisa nyumbani na kuhamia kwa mwanamke mwingine.

Hakujua huku nyuma kaniacha na Ujauzito wa week moja baada ya week mbili nikajigundua ni mjamzito
nikamtalifu mama mkwe na shangazi yake nikijua kabisa watamtaarifu maana mume wangu alibadili namba ya simu nikawa sina mawasiliano nae.

Cha kushangaza mimba imefikisha
miezi sita mume wangu akanifuata Ofisini kwangu na kuanza kunieleza kwamba mimi nilimwambia dada yake kuwa ninamimba na mimba siyo ya mdogo wake, aliyenipa mimba yuko Dar.


Nikashangaa nikajaribu kumueleza hali halisi akagoma kabisa na akadai niwaambie kwetu waandae Mahali yake arudishiwe.


Miezi tisa baadae nikajifungua salama mtoto wa kiume  mtoto alifanana kila kitu na mume wangu nilifurahi nikijua suluhisho limepatikana.


Huwezi amini dada Dinah yule mwanamke anaeishi na mume wangu akajifungua pia mtoto wa kiume tarehe iliyofuata yani watoto wetu walipishana siku moja mimi nikianza yeye akifuata.


Siku zote hizo sikuwahi kujua kama yule mwanamke alikua ni Mjamzito baada ya week mbili mama mkwe alikuja kunisalimia  akakaa siku tano siku ya sita akaaga anaenda kijijini kwao.

Kumbe haikuwa kweli alikua anaenda kumsalimia mke mwenzangu na akakaa huko siku nne  akarudi kwangu bila kujua alivyokua huko alikutana
na watu wanao mfahamu na wananifahamu mimi maana alikua anakuja kila mara pale kwangu.

Alivyofika mimi sikutaka kumuonyesha kuwa najua alipokua nikamuuliza nyumbani hawajambo akasema hawajambo nilikuta kunawagonjwa huko ndio maana nikachelewa kurudi.

Mie uzalendo ukanishinda ikabidi nimuweke wazi kuwa najua kila kitu huko alikokua akabaki anajiuma uma tu na kesho yake wakaaga na kuondoka kwa aibu.

Baada ya hapo nilikuwa kama mwendawazimu nikizunguka kwa Waganga huku na huku na bila suluhisho cha zaidi niliambiwa mume wako anakupenda sana ila mbaya wako ni mama mkwe wako, amekutupia mkosi hadi mwanaume akahama nyumbani.


Siuamini kama kuna mzazi anayeweza kuharibu Mji wa mwanae, pamoja na majibu hayo lakini waganga wote hakuna aliyeweza kunisaidia.

Mwisho wa siku nimeamua  Kuokoka na ninampenda Yesu naamini mwisho wa matatizo yangu umefika nahitaji muungane na mimi katika maombi ili familia yangu irudi kama zamani.


Nafanyiwa maombi na Mchungaji  kunakitu aliniambia nikashangaa sana aliniambia "unajua kilichomtoa mume wako nyumbani?" Nikamwambia hapana mchungaji akaniambia
"nimefunuliwa wakati wa maombi ndugu wa mume wako walikukalia vikao sana hatimae wakafanikiwa kumgeuza akili mume wako ila Mungu ni Mwema muda si mrefu atarejea zidi kuomba na kufunga sana".


Kilichonifanya niandike haya ni kutaka kujua hivi ni kwanini wazazi hasa wa upande wa Kiume wanapenda kuharibu maisha ya watoto wao hasa  mama wakwe na mawifi?

Kwanini kama kunatatizo wasimueleze mtu hadi kufikia kumuendea kwa Waganga ili aachike ona sasa familia inavyotaabika.

Baba alishakataa kutoa matumizi na hataki kuwaona wala kuwasikia watoto wake kweli hii ni sahihi jamani?

Yaani huwezi amini kuanzia nimejifungua huyu mtoto baba mtu pamoja na kupata taarifa kafanana kila kitu lakini   hajawahi hata kujakumuona.

Naumia sana moyoni  nahitaji maombi yenu na ushauri wenu. Thanks dada Dinah.

****************

Dinah anasema: Gosh! mie nina Imani na Msimamo wangu kama mwanamke well kama Dinah.


Ndoa ni uvumilivu sawa, nakubali na nitavumilia magonjwa, nitavumilia ukosefu wa pesa, shida na matatizo ya kibinaadamu LAKINI kutoka Nje ya Ndoa hakuvumiliki.....am gone!

Pole mwaya kwa yote na usiumie sana kwani sio Mwisho wa maisha yako bali ni mwanzo mpya.....ngoja niende tu kwenye NUKTA.


Kwa kawaida Walokole hupeana matumaini na Moyo mpaka wakati mwingine wanakuwa wajinga na kupotezeana mida bila sababu ya Msingi.


Don't get me wrong, nina amini katika Yesu, Maombi ni sehemu kubwa ya maisha yangu ya kila siku, Mungu katendea mambo mengi ya ajabu na Mazuri maishani mwangu ila mimi sio Mlokole na siwaamini wanaojiita WALOKOLE.


Mumeo anakula raha huko na kijifamilia chake kipya, wewe unashupaa kujibana, kulia, kuwaza, kuhuzunika, kujiuliza kwanini nyingi, kukasirika n.k.


Hayo yote yanazuia bahati ya kukutana na mwanaume mwema ili ufurahie maisha kama mwanamke na kama mama kwa kuamini " siku moja mume wangu atarudi na tutakuwa na furaha".....mumeo sio Yesu....move on Mdada.


Baada ya yote aliyokufanyia yeye na familia yake + kumkataa mtoto bado unataka arudi kwako ili uendelee kuishi na mijitu ileile iso na Utu, Hekima, Heshima wala Ubinaadamu.


Kwa bahati nzuri unakazi yako, endelea kuangaliwa watoto wako wawili na kuwaonyesha upendo na furaha.

Piga kazi kwa bidii, ongeza Elimu ya Ujuzi kipindi hiki watoto bado wadogo ili uwe na uhakika wa kusimamia Elimu yao hapo baadae (upande Cheo au kupata kazi inayolipa zaidi).

Simama kama mwanamke ili wanao waje kujivunia Mama yao sio kwa kuwazaa(hukulazimishwa) bali kwa kuwalea vema, kuwatimizia mahitaji yao, kuwapenda na kutumia muda mwingi ukiwa nao.


Hii ni 2014 hatuhitaji wanaume bali tunawataka ili kufurahia maisha sasa kama ulienae hataki kuwa na wewe ili mfurahi pamoja basi songa mbele na utakutana na mwingine (ila usizae tena).

Najua hii inakwenda kinyume na Imani yako ya Kilokole but trust me, Mungu anajua kuwa umejaribu na imeshindikana na am sure atakubariki zaidi kama unafuraha na mwanaume mwingine iwe kwenye ndoa au uhusiano wa kudumu.

"Mambo ya Mume wangu atarudi tu"....."ni mwanaume wangu wa kwanza siwezi kuwa na mwingine"....."Penzi la kwanza haliishi" ni upuuzi.

Kuna watu wamepoteza (fiwa) Wenza wao wakiwa bado wanawapenda lakini baada ya kuomboleza na kukubali kuwa "ndio imetoka hiyo" huendelea na maisha yao kama ifuatavyo.....

Kumbuka maisha hayakusubiri wewe umalize kwanza kusononeka na kulalamika...maisha yanaendelea nawe huna budi kusonga nayo.

Watoto wakikua watamtafuta baba yao, usitieshaka wala kupoteza muda kufunga na kuomba Mumeo arudi kwako. Nani anataka ku-share mwanaume? ewww!

Piga kiberiti kila kitu kinachomuhusu huyo mwanaume, choma moto Kitanda na Godoro mlilokuwa mki-share.

Ikiwezekana hama nyumba, kama mlijenga basi fanya mpango wa kuiuza alafu uhamie kwingine(jenga kwingine).

Nenda Mahakamani kuomba kumtaliki Mumeo (Kisheria Tz inaruhusiwa mwanamke kumtaliki mwanaume)....

Kisha nenda Ustawi wa Jamii ili wakusaidie kuhusu matunzo ya watoto kutoka kwa Baba yao (sio lazima kama mwenyewe unajiweza kiuchumi).

Endelea kuomba ila maombi yasihusu mumeo kurudiana na wewe (wacha kuishi kwenye maisha yaliyokwisha pita) na badala yake ishi maisha uliyonayo sasa na yajayo.

Omba Mungu akupe mwanaume mwema, atakaekujali, kukupenda na kukuthamini.

Omba Mungu akupe afya njema ili uendelee ku-provide kwa watoto wako, awape afya njema watoto na uelewa ili wasikusumbue kuulizia habari za baba yao.

Omba ili Mungu akusaidie kufuta "emotions" zote kuhusu mumeo ili uweze kusonga mbele kiurahisi zaidi...Ni ngumu sana tena sana lakini utaweza tu.

Hilo la "Kwanini Mama Mkwe na Ndugu wa mwanaume huwa na roho mbaya au waharibifu wa maisha ya ndugu zao?"....fufanye iwe Topic siku zijazo.


Tuone wengine watasemaje....

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

1 comment:

. said...

Habari zenu. Ilikuwa ngumu sana kwangu wakati mpenzi wangu aliniacha kwa mwanamke mwingine. Niliharibiwa kihisia, nilivunjika moyo na sikujua la kufanya ili kumrudisha. Nilihangaika kwa miezi mingi na niliendelea kutafuta msaada kutoka kila mahali hadi nilipopata kujua kuhusu DR DAWN. Niliwasiliana naye na kumweleza shida zangu. Alikuwa tayari kunisaidia na kunisisitiza nifuate taratibu ili aweze kurejesha penzi kati yangu na mtu wangu na pia kuhakikisha tunarudiana wote wawili. Nilipata mahitaji yote na ilifanya kazi hiyo. Baada ya saa 48, nilipata ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu akiniuliza tarehe. Sasa tuko pamoja tena na shukrani zote kwa DR DAWN. Anaweza kukusaidia kumrudisha mpenzi wako,
Anaweza kukusaidia na uchawi wa ujauzito,

Anaweza kukusaidia kuponya aina yoyote ya ugonjwa.

ikiwa uko tayari kuamini na kubaki na matumaini. Watumie barua pepe tu kupitia: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159

Pages