Monday

Simpendi kihivyo na siwezi kumuacha kutokana na mapenzi yake!

Hello natumai hu mzima na afya tele.

Mie ni msichana nina mpenzi ambaye ananipenda sana yaani yupo tayari kufanya lolote kwa ajili yangu na ninaamini hivyo kwa sababu kasha nifnyia mengi.

Kiufupi ni nilikua natafuta mwanamme anipendaye na nimempata lakini hana sifa za nje ninazo zihitaji.  

Tuna miaka 2 katika mahusiano, nina hisia kwake lakini sio kama anavyonipenda yeye.


Ni mwanamme ambaye anajua kumjali mwanamke ambae kwa sasa sio rahisi kumpata kama yeye.

Natamani niachane nae but siwezi na hata kama nikimwambia hawezi kuniacha japo kashajua kuwa yeye si chaguo langu.


Nifanyeje? nisaidie.

***********

Dinah anasema: Mzima wa afya tele namshukuru Mungu, ahsante kwa ushirikiano.


Natambua unadhani nitakuambia "ng'ang'ania baraka za bwana" kwavile ni vigumu kupata mwanaume anaejali, penda na kufanya kila kitu kwa Mwanamke wake.

Siamini katika kuishi na mtu kwa vile ni vigumu kumpata kama yeye na sipendezwi na watu wanaopotezea wenzao muda na pengine bahati ya kukutana na watakaopendana nao kwa dhati.

Mimi naamini katika mapenzi ya kweli, kwamba kama humpendi anaekupenda ni vema kuachana nae ili umpe nafasi ya kukutana na mtu atakae mpenda.

Hakika huwezi kupendana na mtu kama kwa kiwango kimoja, lazima upande mmoja uwe zaidi....lakini bado kuna mapenzi kati yenu.

Kutokana na maelezo yako umesema una hisia kwake lakini sio kama anavyokupenda wewe, hujasema unampenda ila sio kama akupendavyo.

Huenda hizo hisia zinasababishwa na matendo mazuri na hali ya kukujaali na kukuheshimu kama mwanamke, yaani unapenda mambo anayokufanyia na unapendezwa na hisia unazozipata kutokana na mapenzi yake kwako.

Hakuna mtu anaekubali kuachwa lakini at the end huwa wanakubali kuwa hawatakiwi na hivyo wanaendelea na maisha yao.

Jinsi unavyozidi kumpotezea muda ndivyo unavyomzidishia machungu, sasa tangu unajua anavyojisikia juu yako kwa miaka yote miwili, anza kumuacha taratibu.

Ukimuacha ghafla kwa kumuambia inaweza ikagharimu maisha yako, maana Dunia ya sasa sio ile ya 1990.

Kama hamuishi pamoja, kwa nyakati tofauti punguza mawasiliano ya simu na ya ana kwa ana, badilisha makazi, mwambie badilisha mawasiliano.....


Ikiwa mnaishi pamoja, rudi nyumbani kwa muda alafu utafute chumba/nyumba kisha badilisha mawasiliano, badilisha kazi ama hama na usimwambie mtu yeyote anaemfahamu huyo jamaa yako.


Tafuta sababu ya kumfanya aelewe...well huna sababu ya kumuambia kwani hamjafunga ndoa. Mwambie tu nahitajika nyumbani hivyo nitakuwa huko kwa muda halafu anza kupunguza mawasiliano.

Muache mkaka wa watu ili apate nafasi ya kupenda na kupendwa kwa dhati na wewe upate nafasi ya kumpata atakae TICK mahitaji yako mengi iwe ya kiutu au kimuonekano.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages